ROHO MKONONI (7) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Alhamisi, 7 Julai 2022

ROHO MKONONI (7)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
Baada ya kuikamilisha akarejea nayo ofisini kwa mkuu wake na kumkabidhi...

Inspekta wa jeshi la polisi John Butu anapokea barua ya kuamishwa kazi,jambo hilo anapingana nalo na kuamua kuandika barua ya kuacha kazi kabisa je unadhani nini kitaendelea?!

KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI
πŸ‘‰GUSA HAPAπŸ‘ˆ

SASA ENDELEA...
Tayari akili yake ilishagubikwa na ukungu wa kukurupuka,

Akupenda hata kuchukua wasaa angalau dakika moja na ushee aidha kutafakari kile akifanyacho.

Tabia hii kila mara ndo ilo mfanya ajutie kile aamuacho kwanzia kumuua yule mwandishi,kumuua huyu alo mjua kama mr x na pia kuandika barua ya kuacha kazi,akaikabidhi kwa bosi wake,akuishia hapo akapiga

saluti muinuko,na kutoa kofia yake ya polisi akaiweka mezani,palepale akageuka na kuuendea mlango,hata mkuu wake alipo muita akuangaika kugeuka,alisha amua,na Butu kawaida yake akiamua kaamua huwa arudi nyuma.

Askari wenzake walishtuka kumuona katika hali ile,kengele ya hatari ikagonga katika vichwa vyao,ila hakuwa na muda wa kuwaeleza kilichotokea,akaingia ndani ya gari yake kuelekea kwake

Huku nyuma kamishna Nurdin alishika simu yake akapiga namba kadhaa akaweka simu masikioni simu ikaita...

"alooh!"

Upande wa pili ukapokea.

"Mkuu ni kwamba Butu kaacha kazi baada ya kumpa barua ya uamisho!"

"Ushawatangazia wenzake juu ya jambo hilo?!"

"Hapana mkuu!"

"Vizuri na usiwatangazie,haraka sana na kuitaji ofisini kwangu tujadili hili!"

"Sawa mkuu"

Palepale simu ikakatwa,

Pasina kupoteza muda kamishna akajinyanyua na kuelekea nje,ambapo aliingia ndani ya gari yake tayari kuelekea alipopajua yeye.
***
Katika jumba moja la kifahari,maeneo ya Tmk Vetenary,eneo aliloishi Inspekta Butu ilisimama pikipiki akashuka mtu ambapo baada ya kutoa element akavaa kofia la sweta lake lililo muwezesha kuficha sura yake akaanza kuliendea geti la nyumba ile alipofika akaingiza mkono wake ulovalishwa gloves katika mfuko wake wa jeans akatoka na funguo aina ya orlando akaziingiza katika kitasa cha geti akafungua haraka akazama ndani!

Alipofika mlango wa ndani akafanya vivyo hivyo,

Safari yake ikaanzia sebuleni alipopanda juu ya meza ya kioo,akuogopa kuivunja,akategesha kitu juu pembeni ya taa,kitu icho kidogo mfano wa kifungo ilikuwa ni ngumu kuonekana kwa urahisi!.

Alipomalika alishuka na kuelekea upeuni palikuwa pembeni kidogo na eneo lile la kupumzikia,eneo hili la kulia,akapanda juu ya meza kubwa ya mbao,pembeni ya taa akategesha kile kitu chake,sasa akashuka na kuelekea vyumbani,alifanya ivyo ivyo katika kila chumba pamoja na bafuni,sasa akarejea sebuleni peyuni,juu ya meza palikuwa na kompyuta mpakato alimaharufu kama laptop,akaiwasha, katika soketi,ikawaka sasa ikaitaji namba za siri,mtu yule akatabasamu akatoa flash na kuchomeka, akabonyeza bonyeza ajuavyo yeye laptop ile ikafunguka,akaanza kufanya alojua yeye,wakati akiendelea katu akujua nje mwenye nyumba aliwasili.

Alishtuka kukuta pikipiki nje ya nyumba yake,haraka akashuka na kuchomoa pistol yake,kwa mwendo wa haraka tena kwa uangalifu akaanza kunyata kulifata geti akafungua taratibu na kuzama ndani!,akaanza sasa kusonga mbele mpaka kwenye mlango wa nyumba ya ndani,akashika kitasa na kukikunja taratibu ghafla akaufungua na kuzama ndani!

Ile anaingia akapokewa na teke,kwa kuwa lilikuwa ni la ghafla lilimtupa pembeni pistol nayo ikamponyoka,

Mtu yule kwa haraka akauwai mlango na kutoka,

Butu akukubali kumuacha akainuka akaifata bastola yake akaiokota na kuuwai mlango akaufungua na kutoka nje,akaanza kurusha risasi ila mtu yule alikimbia kwa mwendo wa zig zag mpaka kulifikia geti,Butu bado alimmiminia risasi zilizo mkosa kosa,mtu yuld akafanikiwa kufungua mlango wa geti lile akaiendea pikipiki yake akavaa element na kuiondoa kwa kasi,Butu naye akukubali alipofika nje akapanda gari yake naye kuanza kuifukuzia ile pikipiki!.

Mfukuzano uliendelea ila mtu yule alikuja kumpotea makutano ya tazara,akumwona tena hata alipofika buguruni na kujaribu kuuliza akupata ushirikiano mwisho akaamua kurejea kwake,huku kichwani akiwa na mawazo mengi,je mtu yule ni nani!, ndo Mr x au mfuasi wake?,alikuwa anafanyaje kwenye kompyuta yake,aliwaza sana,kichwa kilimuuma kwa mawazo,alipofika kwake akaiendea kompyuta yake na kuifungua,akukuta cha zaidi,akaangaza angaza macho kule ndani pia akuona cha tofauti,akaiendea friji akatoa chupa kadhaa za bia akaweka mezani akachukua glasi na kuanza kuzigida,wakati akiendelea kunywa ghafla akapata wazo,haraka akajinyanyua na kuiendea pikipiki yake,akapanda na kuiondoa,safari yake iliishia katika duka liuzalo kamera za cctv,wakafanya maongezi akalipia,mafundi wakaingia kwenye gari yeye akaongoza mbele na pikipiki yake safari ya kuelekea kwake ikafatia,aliamua kwenda kufunga kamera za ulinzi!...

Inspkta John Butu ana amua kuacha kazi,ni baada ya kupewa barua ya uamisho,

Anarejea nyumbani,ila anashtuka kuikuta pikipiki nje ya nyumba yake kuingia anamkuta mtu akichezea kompyuta yake,mtu yule asiyemfahamu anafanikiwa kumponyoka,Butu anaamua kwenda katika duka la kamera anachukua mafundi na kuwaleta nyumbani wana anza kutegesha kamera za ulinzi katika jumba lile tusonge kujua kilichoendelea...

Watu wale wa cctv kamera walifanya kazi haraka haraka,wakiweka nje kwenye mlango kamera mbili sebuleni wakaweka ukutani na katika kila chumba,wakaunganisha na kompyuta zoezi lote likakamilika,awakuweza kuzitambua kamera zilizokuwa ndani ya kidude cha taa juu ya paa la nyumba ile

'Kazi sasa ishakamilika,boya yeyote atakayeingia humu nitamuona tu!'

Butu akawaza.
***
Upande mwingine zilipo ofisi za mkuu wa polisi 'igp' ili ingia gari,maeneo ya maegesho akashuka kamishna Nurdin,akaanza kupiga hatua kuelekea lilipo jengo la ofisi ya mkuu wake yule,njiani alipigiwa saluti.

"Mkuu yupo?!"

Alimuuliza katibu muhtasi wa mkuu wa polisi ambaye alitingisha kichwa kuafiki!

"Kasema ukija nikuruhusu ukamuone karibu kamishna".

Nurdin akujibu kitu akageuka na kuelekea upande ulipo mlango ambao juu kulikuwa na maandishi inspekta jenerali wa polisi 'I G P' alipofika akagonga,akashika kitasa akakizungusha na ku usukuma kidogo kwa ndani mlango akapata upenyo,akaingia,akaurudishia mlango kama alivyoukuta.

Alimpigia saluti mkuu wake,akampa ishara aketi Nurdin akamtwii!

"Lete habari,kijana kakataa uamisho?!"

Mkuu wa polisi alotambulika kwa jina la IGP STEVE jina lake kamili ni Julius Steven akauliza,kabla Butu ajajibu mlango ukafunguliwa na binti ambaye ni katibu muhtas wa Steve

Akaruhusiwa akaingia...

"Mkuu nikuletee nini?,chai,maziwa?!"

"Mletee Arabic ni mpenzi sana wa kahawa huyu jamaa,"

"Na kashata bila kusahau!".

Kamishna Nurdin akadakia wote wakaachia kicheko,

"Na wewe mkuu?!"

Binti akamgeukia bosi wake akamuhoji akimtupia tabasamu mwanana....

"Mi maziwa na bajia"

"Bajia,bagia?!"

Binti akamsahihisha...

"Ivyo hivyo ujuavyo binti!"

Igp akajibu kwa tabasamu binti yule

mrembo akageuka tayari kwa kuondoka.

Akapiga hatua kuufata mlango huku nyuma akisindikizwa na macho ya maafisa wale.

Baada ya kutoka ndipo maongezi yao yaliposhika hatamu.

"Yah,kijana kaacha kazi,kasema kuliko ahame Dar bora aache kazi bado anahitaji kulipiza kisasi!"

IGP akatingisha kichwa kwa masikitiko!

"Na vipi kuhusu upelelezi wa kesi yake?,ulo mkabidhi faili anasemaje?!"

"Amna chochote mkuu kesi ile ni ngumu tena inaonekana hao majamaa wana mtandao mkubwa sanaa"

"Kivipi iwe ngumu na mara ya mwisho ulinambia huyo 0759427653 mlimtia nguvuni?!"

"Mkuu nasikitika kukwambia yule mtu alikuwa siyo na Butu alimuua kimakosa hawa majamaa waliunganisha tu namba,"

"Unataka kunambia yule mlomkamata alikuwa ahusiki kwa chochote?"

Kabla CP Nurdin ajajibu mlango ukafunguliwa na binti yule akaingia mkononi akiwa na visahani viwili kimoja kikiwa na kashata kingine bagia,kashata akakiweka karibu na Nurdin kile cha bagia akakiweka karibu na Steve kisha akatoka.

Nurdin akaendelea....

"Yule mtu alikuwa ahusiki kwa chochote mkuu ni kosa tu lilitendeka na Butu ajui kama mimi najua hili!"

Igp Steve akashusha pumzi nzito,akakuna kichwa chake...

"Sasa nani atakuwa anahusika kwa haya yote?!"

Akamtupia swali,ikawa sasa zamu ya Nurdin kutafakari,kimya kikatanda baina yao,wakati kila mtu akiwaza lake mlango ukafunguliwa yule binti akaingia mkononi akiwa na vikombe viwili vya udongo,kimoja kikiwa na kahawa,kingine kikiwa kimejaa maziwa akaenda kuwaekea,

"Asante Muni kaendelee na kazi"

Igp akamshukuru mfanyakaz wake,

"Huyu kijana anapitia katika wakati mgumu sana,namuonea huruma kwa sasa tumuache afanye anachotaka zoezi zima likimalizika ndipo tumrejeshe kazini!"

Igp akatoa wazo lake,

"Sawa mkuu nitafanya ivyo,"

"Kingine mwambie huyo anayeisimamia kesi yake kila atakachogundua asisite kumwambia,mpaka hao washenzi walio iteketeza familia ya chombo cha dola waipate posho yao,iliniuma sana"

Hatimaye Igp alitoa ruksa kwa Butu kuendelea na kazi akiwa nje ya jeshi,japo Butu akutakiwa kuwambiwa chochote.

Ni wazi jeshi zima la polisi liliumizwa kwa alichofanyiwa.

SURA YA TATU
TEMEKE MIKOROSHINI: KATIKA JUMBA MOJA LA KIFAHARI
Katika chumba kimoja ndani walikwepo watu wa tatu,mwanamke mmoja ambaye anaweza fikia umri wa miaka 37 na wanaye wawili mmoja wa kike akiwa kama na miaka 17 huyu alionekana ndo mkubwa na wa pili wa kiume huyu miaka yake kumi na mbili,wote walikuwa katika hali ya majonzi,humo ndani walipokwepo hawakuwa huru!.

Walifungiwa!.

Chakula waliletewa na watu walojifunga nyuso zao,kutoruhusu sura zao zionekane,kuoga walioga humo humo,walitekwa na awakujua walitekewa nini,awakuambiwa chochote,siku ya tatu sasa ilishapita toka kutekwa kwao!

Awakujua wapo wapi kwani waliletwa wakiwa wamefungwa macho na walipofunguliwa wakajikuta katika chumba kile,hawakupewa mateso yoyote!...

Siku hii kama kawaida mlango ulifunguliwa,wakaingia watu wa tatu wote wakiwa wamefunika nyuso zao,ilikuwa ni mapande ya usiku!...

Kama saa moja na nusu hivi

"Leo mnarudi kwenu!"

Mmoja kati ya watekaji wale alizungumza,akawapa ishara wenzake wakawafunga vitambaa katika nyuso zao,wakawaswaga mpaka nje wakawaingiza kwenye gari safari ya kutoka katika jumba lile ikafatia...

Gari ile ilienda mwendo mfupi kabla ijaingia lami na kuchukua uelekeo wa tazara maghorofani,ikaelekea mpaka buguruni,safari yake ikaishia Tabata Matumbi ikaingia katika barabara ya vumbi na kuacha lami,ikakatiza mitaa kadhaa na mwisho ikasimama katika nyumba moja nzuri ya kifahari pia,watu wale wakafunguliwa vitamba usoni mwao,hawakuamini!,ni kweli mbele wali iyona nyumba yao,

"Mama tumewa achia huru atujawatesa wala kuwa ekea alama yoyote,usiripoti polisi kwa chochote juu ya utekaji huu na wala msiende polisi kuripoti chochote kama mnapenda kuendelea kuishi! Sawa?!"

USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE TAZAMA VIDEO HII KAMA MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA

KWA TELEGRAMπŸ‘‡BONYEZA HAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni