KITU MNATO (7) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatatu, 27 Februari 2023

KITU MNATO (7)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Jane Davis

SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
Basi baada kuridhika akauchomoa mtambo wake na kuufuta futa zile damu pamoja na kumfata mpz wake baada yapo akamlaza kiubavu na kuunyanyua mguu mmoja na kuichomeka tena antena ile wakazama katika ulimwengu ule wa mahaba.

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Purukushani zao zilimalizika Saa kumi jioni ambapo walienda kuoga pamoja na kuvaa

"Sasa mpz utatangulia nyumbani mi acha nikapate moja moto chukua hii itakusaidia katika swala zima La nauli"

Hakeem akatoa "misimbazi" mitatu na kumpa shemeji yake yule,wakatoka pamoja katika hoteli ile yenye gesti ndani walipofika nje kila mmoja akapita njia yake

Huo ndo ukawa mwendelezo wa usaliti wao,uliota mizizi kwanzia hapo

Shamimu furaha yote aliyokuwa nayo sasa ilitoweka,pindi alipomuhitaji mume wake mumewe aliishia kumwambia amechoka!

'Ni wapi lakini ninapokosea mimi'

wazo hilo likapita katika kichwa chake lakini hakulipatia jibu!

Taratibu akapeleka mkono wake kumpapasa,ilikuwa ni katikati ya usiku alipoamka hisia zake zilikuwa juu sana!,akalivua lile nguo la kulalia na kubakia na ch*pi tu

Akaupeleka ulimi wake katika masikio ya mumewe na kuanza kumuhemea, ghafla Hakeem akafungua macho yake!,akakutana na tabasamu mwanana la mke wake!

Hakeem akakunja sura!, Shamim hakujali akaupeleka mkono wake katika mkanda wa suruali kwa lengo la kuufungua!

"Alaf sipendezwi na hii tabia uliyoianzisha ya kulala na suruali mum…"

Kabla ajamalizia mkono wake ukashikwa,tena kwa nguvu na kutolewa eneo lile la suruali

"Nilishakwambia usifate maisha yangu hutaki kunisikia,hivi unanitafuta nini wewe mwanamke?!"

Hakeem akaongea kwa hasira akiwa kakunja mdomo….

Lakini kosa langu ni lipi mume wangu?!"

"huui?! Nakuuliza hujui?!"

"Basi kama nimekukosea naomba unsamehe mume wangu"

Hakeem hakujibu kitu akaishia kusonya na kugeukia upande wa pili, yani hamu na mke wake hakuwa nayo kabisa,

Shamimu hakupata hata lepe la usingizi,mawazo yakiutafuna ubongo wake,hisia Kali za wivu zikauchoma moyo wake akaazimia kuanza uchunguzi Mara moja

Ila kabla ya kuanza huo uchunguzi ilimlazimu akamuone somo wake aone atamshauri nini

SHERATON HOTEL

Ilikuwa ni hoteli ya watu wenye hela zao,Hakeem na Samira walikuwa katika meza wakipata chakula mdogo mdogo huku maongezi yao yakiyapa nafasi mahusiano yao.

Pembeni ya wapenzi wale aliketi mkaka mmoja wa kisomali ambaye kila dakika alikuwa akiweka simu yake katika masikio yake na kukunja sura!

Ni wazi Yule ampigiaye hakupatikana,hakuacha kuiangalia saa yake ya mkononi,wakati wote Samira kwa macho ya wizi alikuwa akimfatilia kaka yule!

Japo kimwili alikuwa na Hakeem pale lakini kimawazo alihama,

'mzoea goma kuacha ni ngoma'

Msemo huu ulitimia kwa Samira kwani alishazoea 'umalaya' hivyo kuacha kwake ilikuwa ni ngumu,alishamtamani msomali yule

'Alafu anaonekana ana hela'

Akazidi kuwaza akiweka tamaa mbele,hali ya kuwa hakuna kitu alichokihitaji kwa shemeji yake yule akakikosa!

ALISHAMPENDA MSOMALI

Pepo la ngono lilisha mpanda,ghafla macho ya Samera yakagongana na ya kaka yule!

Yule kaka akamkonyeza , Samera akatabasamu ambapo tabasamu lake lilikuwa ni sumu kwa kidume kile,sasa kilisahau simu,ghafla bila kutarajiwa nafasi ya dhahabu ikapatikana , ambayo jamaa yule "msomali" hakutaka kuichezea rafu na hatimaye aje aikose "golden" chance hiyo

Ni pale Hakeem alipoinuka na kuelekea toilet bila kuchelewa Kama mwanajeshi msomali yule akajinyanyua na kumfata Samera akampa simu ambapo bila kukawia

SAMERA AKAANDIKA NAMBA ZAKE KATIKA SIMU ILE!

Kama si yeye msomali akarudi katika kiti chake na kuketi dakika ile ile Hakeem akarejea na kuendelea na maongezi,

Baada ya kumaliza chakula Hakeem na SAMERA wakaondoka,samera akimuaga yule jamaa kwa siri!

"Ndo ivyo shoga yangu shemeji yako hashkiki hakamatiki sijui kwa nini kabadilika na miezi miwili sasa hajanipa haki yangu ya ndoa nikimuuliza anakuwa mkali"

Shamimu alikuwa akimuelezea "somo" wake ajulikanaye kwa jina la JANETH au maarufu kwa jina la "madam Jane"

"Kweli mdogo wangu hapo kuna matatizo mwezi?!,hebu nambie unafata mafundisho vizuri?!"

"Sijui nikwambieje somo yaani nyumba haina furaha kila siku ugomvi hanijali kama zamani!"

Shamim akaanza kulia!,Jane akaanza kumbembeleza

"Kulia si utatuzi wa tatizo mdogo wangu ushauri wangu onana na mshenga wake mzee ZUBERI atajua jinsi ya kukusaidia, kwa kuwa ni rafiki yake mkubwa lazima akikaa naye chini lazima atalijua tatizo"

Shamimu akashusha pumzi nzito,ushauri ule ulimwingia akilini…

"Sawa shoga yangu wacha niende nikalifanyie kazi na matokeo ntakwambia"

"Mmmh Dada wewe uje kwa somo uondoke hivi hivi hapana lazima nikupe darasa juu ya unyumba tofauti na ya mwanzo, mwanaume ni kama mtoto shoga weee anapaswa kulelewa kupewa vitu vipya vipya style mpya mpya….unafanyaga hivyo?! Au wewe unaishia vile vile vya zamani?!……….

"Basi shoga pita ndani hapa ni kwako wala hata usijali"

Madame Jane alimkaribisha Shamimu ndani kwake yaani chumbani kwani awali walikuwa nje!

Wakakaa kitandani!,na bila kupoteza muda Jane akaanza

"Ningependa NI kufundishe na stayle za mapenzi kama unaijua sawa na kama zitakuwa mpya kwako ndio fimbo ya awali ya kumchapia huyo mumeo shoga,pengine utakuwa una mlaumu mumeo bure kumbe tatizo unalo wewe jaribu hili ikishindikana ndio ukamuone mshenga wake sawa?!"

"Nakusikiliza shoga"

"OK nianze na Kitchen party nadhani unaifahamu hii ni juu ya mambo ya jikoni chakula umpikiacho mumeo je huwa anakula?! Na wewe ndio unapika au mfanyakazi?! Na kula kwake ni tofauti na zamani"

Jane akatupa swali!…

"Chakula mume wangu anakula vizuri tu na mfanyakazi ambaye ni mdogo wangu huwa anapika cha usiku ambacho ndio hula lakini mchana anakula kazini hivyo huwa mchana napika changu tu!"

FUNZO

Wanawake wengi hapa ndipo mnapokosea kuwaachia majukumu wasichana wa kazi pengine kupika yeye, kufua yeye , kupasi yeye na wengine hata bila aibu msichana wa kazi ndiyo anayefua nguo za mume au baba wa nyumba

Je mke kazi yako ni nini hapo nyumban!?! Kunyonyesha mtoto?! Maana wa mama wengine hata kulisha mtoto humwachia msichana wa kazi! ,ukija kuachwa akachukuliwa msichana huyo waanza kulalamika hooo mume wangu mbaya! Mume wangu msaliti, msaliti wewe usiyejua majukumu yako…

Jane akaendelea….

"Badilika kuanzia Leo shoga jikoni ingia wewe pika chakula kitamu mchuzi shata shata Nazi kwa roico mchuzi mixerr weka mazaga zaga yote mumeo ajing'ate lazima atashangaa mapishi hayo mapya na pengine atajua hata vya ndani vitakuwa na mabadiliko na hapo ndipo atakapo tamani kuonja na akikuonja tu amenasa kwa vitu nitakavyokufundisha!

Pili mavazi bibie! Unayo lalia nadhani wakati nilipokuwa nakufunda nilikwambia lala na kanga tupu si ndiyo?!

Shamimu akatingisha kichwa kuafiki!

" ndio hivyo hivyo ulalavyo?!"

"Ndiyo shostito,"

"Jiongeze bibie?! huoni kama mumeo amechoka badilika lala na ch*pi tu siku nyingine lala hivyo hivyo yule ni mumeo kingine shoga jinsi ya kulala penda kumkumbatia kama hataki vizia akiwa usingizini mkumbatie mwingizie miguu yako katikati ya miguu Yake akishtuka akutoe mwenyewe kama hana uwezo na atakuwa na lake jambo ila kama hana kigaloni basi lazima ashki zitampanda na atakushughulikia upo hapo bibie?!

Kingine lazima ujiongeze nunua pafyumu nzuri,pulizia chumbani akiingia aone utofauti fanya kazi zako haraka ukijua hii ni mida yake ya kutoka kazini kaoge jipare msubiri ukiwa msafi,

Siku nyingine vaa kimtego usichoke wala usimfokee akija amechoka mpe pole mpokee waiba waume za watu wanajua sana Ku " handle" ivyo kuokoa penzi lako lazima uwe juu ya huyo aliyemchanganya kama yupo upo hapo?!

Kitu kingine shosti jitahidi kuomba msamaha hata kama hujamkosea mume wako

Ni nini ninacho maanisha hapo?!

KUOMBA MSAMAHA KUNAWEZA KUZUIA UGOMVI

MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA KUKURAHISISHIA KUOMBA MSAMAHA IKIWA HAUNA KOSA

kwanza mfikirie mume wako shoga

Jaribu kukumbuka jinsi ulivyohisi vizuri ulipo ombwa msamaha na mtu Fulani kwa nini sasa usimfanye mumeo ahisi hivyo?! Hata kama ikiwa huamini kwamba ulikosea, unaweza kuomba msamaha kwa ajili ya maumivu ambayo mwenzii wako amepata au kwa sababu ya usumbufu wowote uliotokana na matendo yako upo hapo bibie?!

ZINGATIA NDOA YAKO

Ona kuomba msamaha kuwa ushindi katika ndoa yako si kushindwa,pia shoga yangu pindi uombapo msamaha unazuia kosa kuwa kikwazo kwa mumeo kuendelea kukukasirikia

ONESHA KWAMBA UNAKWAZIKA NA KOSA LAKO

Kutetea kosa lako si sawa na kuomba msamaha,wewe unatetea naye anakandamiza,unajenga mabishano ambayo ni sumu katika ndoa

Kusema kwa kejeli "samahani kwa kuwa naona unakwazika haraka kwa sababu ya jambo hilo" hii si njia sahihi ya kuomba msamaha hata kidogo , kubali kosa na utambue umemuumiza mume wako

Pia kuomba msamaha kunafanya iwe rahisi kwa mumeo kama ana mapenzi ya kwel juu yako kuwa rahisi naye kuomba msamaha

Na SHAMIMU tambua kila uombapo msamaha ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kufanya hivyo wakati mwingine lengo hasa la kuomba msamaha ni kurudisha amani na upendo uliyokwisha potea…."

"Sawa shoga nimekuelewa lakini mbona Mimi HAKEEM kila Mara namuomba msamaha ananiuliza kwa kosa gani tena kwa sauti yenye kiburi?!"

Swali zuri sana shoga yangu! Je ni wakati gani unapopaswa kuomba msamaha, na ni aina gani ya msamaha unao omba?!"

Ngoja nikufundishe kitu hapa shoga mfano! Nitaunda makosa mawili na jinsi ya kuyatatua kwa kuomba msamaha msamaha si lazima useme

"Nisamehe mume wangu, au samahani Mara kwa Mara mfano sasa….

Usiku wa Leo unahitaji tendo na mume wako kama ulivyonisimulia katika kumpapasa papasa kwako kule akaanza kugomba nawe usianze kumkoromea

Sijui umepata mwingine,kama umenichoka niambie Nina kwetu ati,Mara mwanaume si wewe tu! Unakosea shoga!

omba kwa unyenyekevu kwa kutumia sauti laini tamu

"Mume wangu sikujua kama kufanya hivi na kukwaza ila nami pia ni binadamu na hisia mwenzio kama si wewe wa kuzishusha ni nani sasa my husband nionee huruma mwenzio…

Ukiona anapandisha ukali basi Mwambie samahani kama nimekukwaza kisha geuka upande mwingine ulale!

Kwa nini asiwaze, kwa nini kisimuume shoga kama ana moyo lazima yatamuuma mapenzi si hasira shoga

Na mfano wa pili pengine karudi nyumbani kachelewa au kalewa umemuuliza kawa mkali kosa ni lake lakini je utafanyaje?! Mwambie kwa upole

"Mume wangu kwa nini umebadilika siku hizi unakuja nyumbani umechelewa huna hamu na Mimi tena,unaniacha mpweke nimekukosea nini mume wangu nisamehe kama nimekukosea mume sipendezwi na hivi tunavyoishi jua bado nakuhitaji HAKEEM

Je Shoga maneno haya hayatamuuma,lazima yamuume na akirudi mpe penzi shata shata akutamani tena na tena…."

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni