MUUZA CHIPS (16) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatatu, 22 Mei 2023

MUUZA CHIPS (16)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA...
Saumu alijua kweli alimuuzi chidi, hivyo hakutaka kubishana nae, aliondoka taratibu na kupanda daladala kwenda kwao,

Fatu alitoka kule kwenye stoo ya mkaa, na kuendela kukaa na chidi mana alijificha kwasababu ya saumu,

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"we nawe hilo domo lako lipoje"

"chidi, mpenzi wangu, nisamee"

"nani mpenzi wako tena"

"heeeeee yamekuwa hayo tena…. Sasa kama sio mpenzi wako mbona umeninyonya denda"

"aaahh hio ni salamu ya kizungu tu"

Chidi alikuwa akimchemsha fatu, na kujiona kama hapendi… Na fatu alikuwa ni mwembamba hivi ila alijaliwa kuwa na sura nzuri, pia alikuwa ana shindu laini iliomfanya chidi apagawe nae…

"basi kama ni salamu, ebu tusalimiane tena basi"

"subiri kidogo"

Tukija huku kwa kaka yake na chidi ambaye ni Ibrahim,… Akiwa yupo nyumbani kwa mke wake kama alivyoambiwa kuwa leo ni lazima akalale kwa mke wake huyo, japo hawajafunga ndoa lakini wanaitana mke na mume,..

Rehema ambae ndio mke wa Ibrahim alikuwa sio mkubwa wa kutisha, alikua ni mdogo tu wa wastani, ila alikuwa ni mzuri haswa, kitu kilichomfanya Ibrahim asiruke kwa jambo lolote lile,…

"leo nimekupikia wali samaki kwa ajili yako"

Aliongea rehema huku akimshika shika kidevu mume wake,..

"nakipenda sana hiki chakula, yani sijui ulijuaje jamani mke wangu"

Aliongea Ibrahim huku akitabasamu kwa mbali ili kumfurahisha mke wake,…

"eti eee"

"yes,… Afu vp mtoto wetu anaendeleaje hapo ndani"

Aliongea kijana Ibrahim huku akiliangalia tumbo la mke wake ambalo halikuwa likionyesha kama ana mimba, lakini inasemekana ana mimba ya miezi minne, sasa hatujui kiwa ni kweli mana kila mwanamke huumbwa na maumbile yake tofauti,…

"mume wangu, mchana si mtoto aligeuka mwenzio"

"weeeeeeeeee, sasa ikawaje"

"si nikaenda hospitali, akawekwa sawa, ila nilikopa elfu 50 pale hospitali"

"haaaaaa kwanini usingeniambia nikupeleke mke wangu"

"sikutaka kukusumbua mume wangu"

"mungu wangu eeee…. Lakini sasa hivi si upo salama"

"ndio… Ila lile deni sijalilipa bado"

Tukiachana na akina Ibrahim na mke wake, tunakuja huku kijijini, kwa akina chidi, maskini salma alikuwa kamaliza kale kapesa kalichobaki baada ya kununua dawa za kumuuguza baba mkwe wake,… Sasa hana jinsi na yeye ndio tegemezi,… Ikiwa ni usiku kama ilivyo kule mjini, salma alimtumia chidi wake tafadhali nipigie, na chidi hua hakawii kufanya hivyo…

Aliweka vocha kisha akampigia mke wake huyo ambae ni mama king,..

"haloo mama king mambo vp"

"poa mzima wewe"

"aahhh hali yangu ipo safi tu"

"ok.. Nashukuru kwakuwa umzima wa afya… Ila huku nyumbani hatuna kitu chidi, zile pesa zote tumemuuguza baba zimeisha"

"Mungu wangu eee…. Vp na kale nilichokupa si ukatumie tu"

"ndio iliishia mchana kununua dawa na unga…. Chidi mume wangu, hata hapa yenyewe nachambua majani ya kunde hayana mafuta wala kitunguu, Please nitumie hata elfu moja tupate hata mafuta tu"

Mara simu inakatwa na kijana chidi, huku fatuma akimuuliza

"chidi, kumbe ina mke"

"ndio… Ninae mke, kwani vp"

"kwanini uliwahi kuoa hivyo… Kwahio hapa kumbe nina mume wa mtu chidi"

"ndio… Hapa ulipo una mume wa mtu, lakini sipo nae hapa mjini"

"afu nimeskia kama una mtoto"

"ndio… Ana miezi sita sasa"

"mmmhhhh chidi basi we mkubwa eeti ee"

"wala ata mi sio mkubwa… Sema nilioa kwasababu nilimpa mwanafunzi mwenzangu mimba, hivyo kwakua nilikuwa nampenda, nikaambiwa nichague kuoa au kwenda jela,… Ikabidi nioe"

"huyo mtoto wako ni wa jinsia gani"

"dume haswaaa"

"kama wewe Eti eee"

"mmmmmhh yes"

"chidiiiiiiii"

"sema"

"nikuombe kitu"

"omba tu be free"

"nataka nikupe mtoto wa kike"

Fatu alichanganyikiwa na kijana chidi na kutaka kumzalia hata mtoto ingali bado mwanafunzi,

"kivipi sasa"

"naomba, nizae na wewe"

"sasa we si mwanafunzi wewe"

"si utakubali kama ulivyomkubali huyo mjinga wako huko kijijini"

"ati unasema nani wangu,…."

Chidi alitoa macho huku akimuuliza kwa umakini, kwa kile alichokisema fatu, chidi alikasirika, na fatu alijua kuwa kamuuzi fatu

"chidi, naomba unisamee mpenzi wangu, niliponyokwa tu na maneno"

"yaani ukirudia tena huo ujinga,.. Nitakuzaba vibao muda si mrefu"

"nisamehe, nipo chini ya miguu yako"

Tukija huku kwa Ibrahim akiwa na mke wake rehema,…

"ndio… Ila lile deni sijalilipa bado"

"umesema ni shilingi ngapi vile"

"mtoto alipogeuka, nilichukuwa taxi elfu 10, nilipofika kule nikatibiwa na mtoto akakaa vizuri,… Wakataka elfu 50 nikawa sina, nikamkopa rafiki yangu"

"kwahio ni elfu 60 si ndio"

"ndio…. "

"lakini mtoto si yupo salama mke wangu"

"usijali, mtoto wako yupo salama ila anapiga mateke huyooo"

"ukiona hivyo ujue atakua mcheza mpira huyo"

"akuuu mi staki mwanaume"

Ibrahim alikuwa akipenda apate mtoto, mana kitendo cha kusikia mdogo wake chidi ana mtoto hivyo nae akawa hima hima ili aitwe baba, mana umri unakwenda

Ibrahim alitoa pesa ya mtaji wa chipsi, shilingi elfu 60, akabakiwa na elfu 50 mfukoni, kana kwamba leo kauza sana, ila sema pesa zinatoka sana…

"hiii elfu 50, wacha ibaki ya kununulia viazi na nyama kidogo"

"sawa… Mtengenezee mwanao urithi mzuri eti"

Ibrahim alikuwa akifurahi sana pindi anaposikia swala la mtoto wake kuwa salama,…. Huku mke wake akiwa anachati kana kwamba kuna mtu alikuwa akichati nae,…

Tukija huku kwa kijana chidi, tunakuta ndio alikuwa anafunga kibanda cha chipsi kwani alikuwa kamaliza chipsi zote pamoja na nyama za mishkaki…

Hapo alikuwa ana faida nzuri tu, kwani alikuwa na kiasi cha shilingi elfu 80 mauzo ya leo tu, mana wanauza vitu vingi sana hapo bandani,…

Ghafla simu yake inaita, kuangalia jina alikuwa ni MY WIFE yaani mke wake wa kule kijijini, alipiga simu tena baada ya chidi kukata simu hio,…

"halooo"

"chidi mume wangu, mbona umekata simu, ina maana kukuomba hela nimekosea?… Basi nisamee mume wangu, nakutakia usiku mwema"

"salma mke wangu, simu ilikatika…"

Chidi aliiangalia ile pesa na kujishauri wacha atume shilingi elfu 40 ili iwaseidie huko nyumbani… Mana hio elfu 40 ni faida tu…. Abaki na hio 40

"ngoja nikutumie mke wangu, lakini hakikisha mzee azingatie dawa sawa mke wangu"

"sawa mume wangu, mbona haina shida"

Chidi alikata simu kisha akaenda tigo pesa na kuituma ele elfu 40 kule nyumbani,… Salma alijiskia raha na hata wazazi walifurahi sana kwa kitendo cha chidi kutuma pesa itakayowasukuma, kwa muda mrefu kiasi… Wazazi walimuombea kijana wao huyo….

Tukija huku kwa Ibrahim na mke wake rehema, ghafla simu ya rehema inaita, haikujulikana ni nani aliokuwa anapiga…

"haloo mamdogo shkamoo"

Rehema alimsalimia mamdogo wake

"marahaba ujambo mwanangu"

"sijambo hali yenu vp"

"we acha tu rehema… Mdogo wako kafariki dunia"

"unasemaje mamdogo…. Mungu wangu Uuiiiiiiiiiiii iiiii"

Rehema alianza kulia huku akimuangalia Ibrahim

"mke wangu kuna nini tena"

Ibrahim aliuliza huku akiwa na wasiwasi juu ya mke wake huyo

"kuna msiiiibaaaaa Uiiiiiiiiiiiiiiiiii"

Rehema alikuwa analia haswaaa,….

"basi nyamaza mke wangu,… "

"mamdogo, kunambia mdogo wangu kafariki dunia… Lakini mi staki kwenda nikuache mwenyewe"

"hapana mke wangu… Wacha twende tukazike wote, hata yeye ni ndugu yangu"

Ibrahim alitaka kwenda kuzika na mke wake huko kulikotokea msiba,…

"No, tutume tu pesa kwa ajili ya lambi lambi tu"

Maisha ni kutafuta na sio kutafutana, unashauriwa kuwa tafuta pesa kwa njia zako mwenyewe ila usiue ili upate pesa, na ukipata bwege wako kazana nae, maisha sio kuzubaa, mjini akili, nguvu peleka kijijini…

Kwa upande wa simulizi ya muuza chipsi, tunamuona mwanadada rehema ambae ni mke wa Ibrahim akiwa anachati na mtu tusimjua… Na haikupita muda rehema anapigiwa simu na kuupokea msiba wa mdogo wake kwa upande wa mamdogo wake, Ibrahim alikuwepo eneo hilo kwasababu siku hio aliambiwa akalalie kwa mke wake huyo na kwa bahati mbaya, kukatokea msiba…

"hapana mke wangu, wacha twende tukazike wote, hata yeye ni ndugu yangu"

Iliskika sauti ya Ibrahim ikimsihi rehema kuwa waende wakazike ndio itakuwa vizuri, lakini rehema hakuwa akitaka kwenda kwenye msiba, nia yake ni kutuma pesa,…

"No, tutume tu pesa kwa ajili ya lambi lambi tu"

"lakini mke wangu, tukionekana hata sisi sio mbaya, hata kama hatuna pesa lakini wacha tukaonekane"

"mi spendi nikuache"

"No, sio kuwa unaniacha.. Tunakwenda wote"

"mume wangu, kwanini tuiache nyumba peke etu, afu licha ya hivyo, Dokta aliniambia kuwa nisipende kumsumbua mtoto, sasa kwanini unakuwa hivyo"

"ok, nimekubali tufanye hivyo, ila ingelikuwa vizuri Twende kuzika"

Tukiachana na huku tuje huku kwa chidi ambae ndio alikuwa anapanda daladala akiwa sambamba na fatu,.. Mtoto kipotabo lakini ana sura haswa, afu chidi alimpenda kutokana na ngozi yake ilivyo laini, yaani ukimshika hata mkono tu, basi lazima kidume ubadirike, hivyo chidi ndio kitu alichompendea mtoto fatu,…

"chidi… "

"sema"

Wakiwa wapo ndani ya daladala wakielekea nyumbani,

"ivi huko kwako si kunafaa nilale mpaka asubuhi"

"ah ah, haiwezekani lazima utaondoka, coz tutakutwa na broo"

"heeeeeee kumbe upo na kaka yako"

"ndio, tunaishi pamoja ila leo hatolala nyumbani"

"sasa kama hatolala mi si nilale tu"

"akija usiku usiku"

"mmmhhhh we sema hutaki nilale kwako"

Fatu alikuwa akilazimisha kulala kwa kijana chidi, na sijui hawa wanafunzi wanaishi bipi huko majumbani mwao, kitu kinachowafanya walale kwa wanaume bila hata ya kuogopa wazazi wao.

Tukiachana na akina chidi waliokuwa wakibishana kwa kulala kwao,… Sasa tuje huku kwa akina miriam na sarah,… Marafiki wasiochokana, marafiki walioshibana haswaa,.. Leo walikuwa wakipiga stori za mapenzi mapenzi hivi ambazo wanazikumbuka sana walipokuwa shule

"sarah,… Unajua nimekumisi sana"

Alikuwa ni miriam ndio anamuuliza saraha kuwa kammisi sana, ila haijulikani kammisi kibipi,

"eeehhh mi mwenzio wala staki, nina mpenzi"

"saaaarah jamani, si unajua mi mwenzio sina mwanaume"

"mi staki bwana… Mtu mwenyewe hujawahi hata kuwa na mwanaume toka uzaliwe, ndio mana ukitongozwa unakataa miri… Hebu kuwa mwepesi, kwani wameumbiwa nani"

"sawa… Wameumbiwa sisi, lakini sijaona mwanaume wa kunishawishi yaani nitoe bikra yangu kwa mtu ambae hana maana akuu, bora nibaki hivi hivi"

"basi, kama hutaki wanaume nami staki, nina mwanaume tena nataka anioe"

"huyo jambazi au kuna mwingine"

"Jambazi… Alikuibia nini jamani Miri"

"jamani sarah, hebu tuyaache hayo, Please kifuani tu"

"sitakiiiiiiiii….tena leo silali na wewe…. Tongozwa mama ukubali, wameumbiwa sisi hao"

Sarah alitoka nje huku miriam akibaki chumbani peke yake,… Aliichukua simu yake na kuanza kuangalia video flani za 18+ only….

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni