MUUZA CHIPS (18) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatatu, 22 Mei 2023

MUUZA CHIPS (18)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
📖 KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
😂 VIDEO za KUCHEKESHA
📑 MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA KUMI NA NANE
ILIPOISHIA...
"Whaaaat?"

"ndio… Ukumbuke mara ya mwisho ulisahau kunanii nje"

"mungu weeeee….. Salma, sasa tutafanyeje na sisi bado ni wanafunzi eti"

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"chidi,.. Mi sijui tufanyeje"

"Kama vipi tuitoe"

"heeeeeeeeeee,.. Hapana chidi, utauwaje kiumbe cha mungu lakini"

"basi we unataka nifungwe si ndio ee, sawa leongo lako litatimia soon"

"sio hivyo chidi…. Subiri basi tuongee"

Chidi aliondoka bila kumsikiliza mpenzi wake ambae ni salma waliopeana mimba wakiwa shuleni,… Kuna afadhali ya mwanafunzi kwa mwanafunzi kuliko raia kwa mwanafunzi… 30 itakuhusu babaaa

Ikiwa ni siku nyingine tena, salma akiwa nyumbani kwao, alionekana kukimbilia uwani na kuanza kutapika, mama wa salma alimfuata mtoto wake, kisha akamuuliza

"wewe, una nini lakini… Unajua nilikuona jana unatapika nikahisi labda ulikula kitu kibaya, sasa na leo vipi mwanangu"

"mama, najiskia tu vibaya"

"wewe,… Niambie ukweli"

"mama, sina ukweli wowote najiskia tu vibaya"

"wewe una mimba ni kweli si kweli"

"Ah ah ah aha wala ata sina"

"sasa lazima Twende kituo cha afya"

Mama alimkokota salma mguu kwa mguu hadi kituo cha afya,. Na kufanyiwa vipimo, iligundulika ni kweli alikuwa ni mjamzito,..

Wakati huo chidi alikuwa shambani, kwani siku hio ilikuwa ni siku ya juma mosi, hivyo alikuwa akipiga kibarua mana hali ya maisha yao ilikuwa ni ngumu,.. Alikuwa akilima kwa hasira sana huku akikumbuka jana alipoenda hospitali na kuuliza gharama za kutoa mimba ni kiasi gani, hivyo kwakuwa hawana uwezo wa kumlipa dokta ili aifanye kazi hio… Hivyo alikuja huku mashambani na kuanza kulima kwa hasira, lakini anajua fika kuwa hapo anapolima hapawezi kutosha kulipia hospitali, hivyo kumbe kichwani alikuwa na nia nyingine tofauti ya kupata pesa,… Giza lilizidi kutanda akiwa bado analima

Kumbe kijana chidi alikuwa anategea kuiba mbuzi wa mzee mmoja hapo kijijini ili akauze na apate gharama za kulipia ili akatoe mimba aliokuwa nayo salma,.. Kweli mchungaji wa mbuzi alikuwa ana tabia ya kuchelewesha mbuzi hizo bila kujua kuwa kuna mtu anaziwinda.. Kawaida ya mchungaji wa mbuzi hukaa nyuma ya kundi la mbuzi, sasa chidi akajificha kwenye kichaka huku akiangalia mbuzi mnono mnono anauzika kwa haraka,.. Kagiza nako kalitanda.

"Enheeeee hili dume hapa ni babkubwa hili"

Aliongea chidi kimoyomoyo huku akilinyatia dume hilo,… Alianza kulishika mdomo kisha akalipiga mtama likatulia kimyaaa,… Muda huo yapa mida ya saa moja hivi usiku,… Alisubiri mpaka mchunga mbuzi kapita, tena akakaa kama dakika 10 hivi akiwa kamminya mbuzi pale chini, tena mbuzi wa haja…

Aliona kumetulia kimyaaaa

Chidi aliona pametulia sasa ni muda wa kuondoka,… Sasa akawa anamshika vizuri ili amweke begani tayari kwa kuuzwa… Sasa Cha ajabu na cha kushanaza kwa yule mbuzi,…

Chidi alijiskia raha sana baada ya kufanikiwa kuipata mbuzi hio kwa ajili ya kumuuza ili mimba ya salma itolewe mana mawazo ya kijana chidi yeye huogopa kwenda jela, mana umempa mimba mwanafunzi, tena salma alikuwa ana umbo dogo, na pia umria wake ulikuwa mdogo yapata kama miaka 17 hivi au 16,.. Chidi aliona kibarua hakiwezi kutoa ile mimba hivyo ndipo akaingia kwenye kundi la mbuzi na kuiba mbuzi mkubwa mbuzi mnono haswaaa,…

Lakini ukae na kujua kua kitu ambacho mungu hakipendi basi hakiwezi timia, Chidi alijiandaa kumbeba yule mbuzi amueke begani ili biasha ikafanyike,… Sasa cha ajabu na cha kushangaza kwa yule mbuzi,… Alikuwa kulegea tepe tepe, chidi kukagua vizuri, aligundua kuwa yule mbuzi alishakufa dakika chache zilizopita, chidia alianza kulia pale chidi huku akilaumu sana kwa kufa kwa kiumbe hicho, mana hakutaka kumuua… Sasa kumbe pale alipomshika mdomo yule mbuzi, alimshika na pua kwa nguvu ili asipige kelele, sasa mbuzi alivyokuwa anakata roho huku akirusha rusha miguu, chidi akajua ni usumbufu wa mbuzi huyo bila kujua kuwa alikuwa akikata roho,.. Mpaka hapo ni mungu kakataa mimba isitolewe, sema chidi hajui…

Hajakaa sawa mara kaskia sauti ya mtu anakuja mbele yake, na hapo alipo hata nguvu hana mana alichokitekemea hakikuwa kama kilivyotakiwa,…..

Alikuwa anaogopa sana kwa huyo mtu aliokuwa akija mbele yake,

"chidiiiiiiiiiiiiii"

Kumbe alikuwa ni salma kaja kumtafuta baada ya kuambiwa kaenda kibaruani kwenye shamba la mzee fulani, hivyo ndio mana akaja,

"nini wewe saa hizi"

Salma alishtuka kuskia sauti inatoka karibu yake mana alikuwa hajamuona kutokana na kiza kuwa kingi,…

"jamani chidi, kulima gani huku mpaka saa hizi jamani"

"we acha tu salma hali yangu mbaya"

"chidi… Mama angu kajua kuwa nina mimba"

"mungu wangu weeee umekuja kunipa presha wakati mi namwazia mbuzi wa watu"

"mbuzi… Mbuzi gani tena"

"salma,… Mi nataka tuitoe hio mimba"

"chidi…. Sitaki kuitoa hii mimba, nipo tayari kufa nayo lakini siitoi"

"salma mpenzi wangu, unataka nifungwe"

"wala sina maana hio"

"nimeuwa mbuzi wa watu kwa ajili yako, afu tena unajifanya hutaki kuitoa hio mimba"

"mimba sitoi.. Afu huyo mbuzi umemuua wapi"

"si huyu hapa nyuma yangu"

Salma alianza kumuangalia huyo mbuzi,

"sasa unasubiri nini hapa,.. Huyu mbuzi ni wa mzee malugwadu, na hawawezi kulala bila kumtafuta, sasa je wakikukuta nae hapa? Hebu amka uko"

Salma alimvuta kijana chidi na kumseidia jembe lake

"kile ni kiumbe cha kwanza umeshakiua, afu bado unatafuta kingine ukiue"

"nakuambia hivi, ni lazima itoke, mi sitaki kwenda jela, familia yangu itabaki vipi"

"mi sitoi, kwanza nilikuaga natamani sana kuzaa na wewe"

Salma alikuwa akimuuzi sana mpenzi wake kutokana na maneno aliokuwa akiyaongea,

Muda mchache tu walifika nyumbani kwa akina chidi, salma aliingiza jembe kule geto kwa chidi,…

Salma alitoka kisha akawa anasindikizwa na kijana chidi, mana ilikuwa yapata saa mbili usiku,…

Kesho yake ikiwa ni siku ya Jumapili mida ya saa tano hivi asubuhi, salma alikuja kwa akina chidi, na kuondoka nae

"tunaenda wapi we salma"

"we twende tu"

"salma, sema basi au tunaenda kuitoa"

"ndio.. Ila pesa anayo mama hivyo twende tukachukue"

"yaani hio pesa tukaichukue kwa mama yako si ndio ee"

"ndio…"

"basi nenda mwenyewe"

"sikia chidi… Mama yangu hana shida, na kanambia twende akakuone"

"weeeeeeeeeeeee, weeeeeee…. We kichaa kweli wewe, kwenda uko"

Chidi alikataa kwenda mana anajua ni msala,… Chidi alirudi nyumbani kwao, huku salma nae anamfuata tu,… Chidi alioofika nyumbani aliona bora amshirikishe mama ake kwanza, mana hata salma hataki mimba itolewe,.. Wakati huo salma ndio anafika na chidi yupo kwa uwani anaongea na mama yake

"mama….. Kuna kosa nimelifanya mama angu, naomba uniseidie"

"kosa gani tena mwanangu,…"

"mama usiseme kwa nguvu baba atasikia"

"wewe umefanya kosa gani mpaka hutaki baba ako asikie"

"mamaaa…. Salma"

"salma kafanyeje, si ulikuwa nae sasa hivi tu"

"tatizo sio hilo"

Mara salma katokea huku akimsalimia mama yake na chidi,

"shkamoo mama"

"marahaba mwanangu,.. Eti wewe umefanyeje"

Mama wa chidi alimuuliza salma kuwa kafanyeje, sasa salma kabla hajajibu, chidi akadakia juu juu

"mama huyu anatapika hovyo hovyo tu"

Sasa mama wa chidi kuskia hivyo, alishajua kuwa hapa ni nini kilikuwa kinaendelea

"haya toka hapa nenda zako geto huko"

Mama wa chidi alimtimua chidi kisha akamvuta salma kule uwani kwenye mkeka, mana alikuwa kakaa kwenye kamti hivi,..

"weeeee, unamaanisha una ujauzito"

"ndio mama"

"na una uhakika ni wa mtoto wangu"

"kabisa… Na yeye ndio nilianza nae.. Ila anataka nitoe"

"Ati nini… Huyu mtoto ni mshenzi sana huyu, yani mi nataka niitwe bibi halafu, mshenzi kabisa huyu.."

"lakini mama… Kwanini msiongee na wazazi wangu ili yaishe, mana chidi anaogopa kwenda jela"

"usijali mwanangu, ilimradi tu, hiki kiumbe kiwe damu yetu"

Salma alitoka hapo huku akiwa na furaha,

"chidi, mbona mama yako hana shida… Jamani chidi nakupenda, naomba unioe"

"ebu toa ujinga uko"

Wakati huo huku kwa mama wa chidi alikuwa akivaa vizuri sijui alikuwa akienda wapi,.. Alitoka na kuishia zake,.. Kumbe alikuwa anaenda kwa mama yake na salma, mana kule kijijini watu wanaishi kama ndugu, hata mtu wa mtaa wa pili huko anajuana na mtu wa mtaa wa saba huko, sio kama huku mjini, una miaka miwili ndani ya nyumba hata jirani humjui,..

Hivyo kwakuwa mama salma na mama wa chidi walikuwa wakijuana na hata salma alipomwambia kuwa kijana mwenyewe ni mtoto wa mzee kingazi, mama Salma alijua cha kufanya…

Sasa mama wa chidi ndio anafika nyumbani kwa akina salma, na kumkuta binti asumini kakaa kibarazani,…

"heeeeee yaani ndio nilikuwa nakuwaza sasa hivi"

Aliongea mama yake salma huku akimkaribisha aingie ndani.. Walikaa kisha wakaanza kuongea..

Wakati huo huku geto chidi na salma wanaingia katika matamanio ya kimapenzi,.

"salma"

"abeee"

"umevas chupi gani leo"

Sasa salma badala ya kusema kwa mdomo ni ngumu, akavua nguo na kumuonyesha rangi ya chupi alioivaa, kitu ambacho kilimsisimua chidi na kumvuta salma kitandani,.. Sauti za midomo ikibadirishana mate ziliskika huku chidi akiviminya vititi vya salma,…

Tukija huku kwa wamama watu wazima waliokuwa wakiongea wao kiutu uzima haswaa,

"unajua nini asumini,… Leo ndio nimezipata taarifa za mtoto wangu kwa mtoto wako, nikaona siwezi kukaa kimya tuje tuliongee"

"ni kweli, lakini na hii sheria ya sasa hivi itakuwaje mwenzangu, watoto wetu wenyewe ndio hawa"

"asumini, kwanini tusiongee vizuri na walimu, ili tuwaachie waowane"

"mimi juzi nilipomjua mwanangu, nilienda shuleni kwao, lakini nikaambiwa haiwezekani, hivyo wa kiume anaweza kuishia jela,.. Na ndio mana nilikuwa nafikiria kuja kwako"

"mmmhhh Aende jela"

"ni maelezo niliopewa na walimu.. Ila mwalimu mkuu alinipa njia moja tu ya kuwaseidia wote"

Unajua kule kijijini hua sio watu wa kuzingatia elimu, ni kama wanavyosema kuwa,.. Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe, na utajiri wa maskini ni watoto, kama ingelikuwa ni mjini hapa kingeshanuka kitambo tu,…

"njia gani hio binti asumini"

Binti asumini ni mama yake salma,…

"mkuu wa shule kaniambia hivi, kunatakiwa pesa ya kuuwa majina ya wawili hao, yaani majina yakafutwe kule wilayani, wajulikane wamekufa, hapo ndio itakua sawa, mana sheria ya kuchagua kuoa kwa sasa haipo, mana atachagua kuoa ili asiende jela hivyo hio sheria haipo kabisaaaaa"

"mungu wangu weeeee…. "

"sasa alisema kunahitajika kiasi gani"

"kwanza… Kule wilayani kunatakiwa laki moja, halafu huku shuleni kunatakiwa laki moja kwa ajili ya kuwafunga walimu midomo.. Na hii ya tatu, mtoto wangu alikuwa ni bikra, je nami mtaniangalia hata na ng'ombe dume"

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni