MUUZA CHIPS (21) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 23 Mei 2023

MUUZA CHIPS (21)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
📖 KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
😂 VIDEO za KUCHEKESHA
📑 MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Sasa ndio hivi vya mama miriam na mama sarah… Na ukaribu walionao mama sarah na mama miriam ndio ukaribu waliouanzisha miriam na sarah,.. Mama sarah na mama miriam walisoma wote kutoka shule ya msingi mpaka chuo,… Na akina miriam pia hivyo hivyo mpaka sasa wapo kama ndugu wa kuzaliwa kumbe ni marafiki tu,

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Mama Miriam alimkabidhi rafiki yake hoteli moja aimiliki yeye,.. Ila mauzo yanakuwa yanakwenda kwa boss,… Kama vile mtu aliokabidhiwa gari aendeshe atakavyo lakini jioni amletee pesa. Sasa ndio hivi vya mama miriam na mama sarah… Na ukaribu walionao mama sarah na mama miriam ndio ukaribu waliouanzisha miriam na sarah,.. Mama sarah na mama miriam walisoma wote kutoka shule ya msingi mpaka chuo,… Na akina miriam pia hivyo hivyo mpaka sasa wapo kama ndugu wa kuzaliwa kumbe ni marafiki tu,

KAMA UNATUMIA APP WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI
~>GUSA HAPA<~

SASA ENDELEA...

Tukija huku kwa chidi ikiwa ni mida ya saa 9 hivi, alikuwa akichoma kuku wa mteje,… Kulikuwa na mteja wa haja akiwa anasubiri kuku huyo,… Bonge la toto si haba mpaka chidi anamuangalia kwa chini chini,

Kabla hajamaliza kumpa mteja kuku wake mara kuna mteja mwingine aliosimamisha gari kalii, tena mteja wa maana, mpaka chidi akashtuka na kudhani labda hakuja hapo kwenye banda lake,..

"kijana habari yako"

Alikuwa ni mama mwenye umri wa makamo na alikuwa bonge la mama, yaani tukisema wale wamama wa mjini basi nae yumo, mana hata nguo zake alizovaa hazikuwa zikiendana na umri wake,…

"salama mama shkamoo"

"marahaba mwanangu ujambo"

"sijambo mama karibu uketi"

"hapana usijali,.. Aaahhh nilikuwa napita nikaona chipsi nzuri kweli, kijana unajua kupika chipsi vizuri sana"

Mama huyo alimsifia sana kijana chidi, kwa upikaji wake wa chipsi

"ndio mama, karibu sana mama"

Chidi aliendelea kuwa mkarimu kwa mama huyo akiwa kama mteja wake,

"za saa izi dada"

Mama huyo alimsalimia yule mteja anaesubiria kuku,

"salama hali yako"

"nzuri…. Naona unasubiri kuku"

"yeaaahh, napenda kula kuku wa hapa mana ni wasafi, afu pia wana chipsi zilizokauka vizuri"

"Ni kweli, kijana anapika chipsi vizuri sana, halafu ni kubwa kubwa tofauti na vibanda vingine"

"ndio, tena kuna mahoteli makubwa sana na hayapiki chipsi kama hizi"

"sio kuna… Mimi mwenyewe namiliki hoteli, lakini chipsi inayopikwa hapo siitamani hata kidogo.. Sasa nilipokuwa napita ndio nikaona hizi chipsi"

"aahhh kijana anajua kupika chipsi"

Basi kijana chidi alikuwa akijizolea sifa nyingi juu ya wateja hao, hata chidi alifurahi sana kuwa na wateja wakubwa wakubwa kama hao,.. Mana alijuwa wateja kama hao wanatakiwa wakale katika mahoteli makubwa makubwa, lakini wamekuja kwenye genge la chidi kitu ambacho ni cha kushangaza sana..

Mteja wa kuku alipewa kuku na akaondoka zake,

"mmmmhh sema mama angu nikiseidie nini"

"mi nataka unifungie chipsi nyama"

"sawa mama nipe dakika mbili"

Basi mama yule aliingia kwenye gari na kulipaki sawa sawa huku chidi akichoma nyama huku anageuza chipsi,….

Dakika 5 mbele kila kitu kikawa tayari, Chidi akafunga kila kitu na kumpelekea pale kwenye gari…

"hio nyama umeikata kata"

"hapana mama bado… Ngoja nichukie kisu tuikate kate"

Chidi alirudi kwa spidi na kuchukuwa kisu kisha akaingia ndani ya gari na kujigungia huko huku akikatakata nyama hio ziwe ndogo ndogo,… Sasa mimacho ya chidi ilivyo haina adabu, na kama nilivyosema kuwa, mama yule alivaa nguo ambazo haendani nazo kiumri,… Yaani alivaa suti, lakini sketi ya suti hio ilikuwa ni fupi mno, Sasa chidi akiwa anakata nyama,.. Kwa bahati mbaya jicho lake likapita kwenye paja la mama huyo,.. Chidi alianza kuhangaika pale alipo, si unajua zakaria akisimama inakuwaje,..

"una nini kijana"

"amna kitu mama, sema hua mgongo unakua unaniuma kidogo"

"ooohh pole"

Sasa chidi madala ya kukata nyama, alijikuta anatamani kuona tena pale alipoona mwanzo,… Sasa ile anapiga tu jicho, mama kamfumania chidi alipokuwa anaangali… Mama akalifuata lile jicho la chidi linaangalia wapi, akagundua kuwa kijana huyo alikuwa akiangalia paja lake…

"mmmhhh nyie watoto washenzi kweli, yaani baada uniambie nimekaa vibaya, kumbe unantolea macho"

"nisamehe mama angu"

Chidi alijuwa kafanya kosa lakini ukweli ni kwamba mama huyo alifurahi sana kuona kijana ambae, anaweza kustuka kwa kuona,…

"usiogope.. Kwani mimi na wewe nani mwenye kosa"

"ni mimi ndio mwenye makosa mama"

"hapana… Mimi ndio mwenye makosa…"

Lakini ghafla, walianza kubishana kuhusiana na makosa yao,… Lakini mama sijui ilikuaje katika mabishano,… Ila mwisho wa saa chidi anaona ile sketi imezidi kuwa fupi kuliko mwanzo, hapo chidi alishikwa na kigugumizi cha kuongea, na kutaka kutoka nje..

"sasa unaenda wapi,.. Mimi si ndio nina kosa"

"no mamy… Jifunge kanga kwanza"

"ina maana mfano nikikupa utaifunga kanga"

Heeeee chidi alishtuka kwa kuskia neno kama akipewa ataifunga kanga…. Chidi alikuwa aking'ata kucha kama demu, na hapo ndipo anaponiuzi hawezagi kumalizia sijui likoje hili ligosi….

Kiukweli mapenzi ni upofu na mapenzi hayajaribiwi, na hisia za mapenzi hazizuiliki hata kidogo bali kuzikontroo unaweza lakini kuzizuia huezi… Nikiwa na maana ya kwamba,.. Unapoona sehemu ya mwanamke ambayo kwako ni adimu kuiona, basi lazima mwili utetemeke, maana yake hapo umeshindwa kuzizuia, lakini jinsi ya kuzitumia unaweza kujizuia lakini ukiwa mwelewa ndio utaweza kuzikontroo hisia hizo,…

Ila kwa chidi aliokuwa mtoto wa kitanga, na sio yeye tu, bali kidume yeyote yule rijali, hawezi kukaukia ishu ya mapenzi hata iweje, na baadhi ya wanaume wengi wanashindwa kuingia kwenye uhusiano kwasababu ya udhaifu wa maisha, kana kwamba wanawake wa sasa hivi ni wapenda pesa, sasa na sisi wenyewe pesa ni za kulenga kwa manati…

Leo nikilala na wewe wataka elfu 20 au 30 au na zaidi, ndio maana wengi wetu tunaogopa kuwa na wapenzi,…

Chidi hakugikiria kabisa swala la kuwa na uhusiano na mama huyo, lakini kuyokana na maneno ya mama huyo, yalimfanya chidi agundue kitu katika hali hio…

"nimekuuliza, kwani nikikupa utaifunga kanga? Nijibu basi we MUUZA CHIPSI"

Chakushangaza mama alikuwa kama nae kalewa juu ya kijana chidi, kwani hata hilo neno aliliongea kwa pua

"samaani mama, naomba nikahudumie wateja"

"hhhhhmmmm ok, ni kiasi gani cha pesa unanidai"

"ni elfu 10 tu mama"

Mama alitoa pochi yake, na kihesabu peaa zaidi ya elfu 10, chidi kwa njaa yake ya fedha alijikuta akitoa macho katika ile pesa

"shika hii"

"lakini mama,.. Mbona sio pesa niliotaka"

"we mtoto wa mjini bwana mpaka nijishue sana ndio unielewe au"

Chidi alibaki kimya huku akisita sita kuipokea ile pesa,…

"chukuwa bwana,. Afu nipe namba yako ya simu ili nikitaka chipsi, nisije kusimama tu hapa, nitakuwa nakupigia simu kisha nakuja sawa"

Sasa chidi akakumbuka kuna kipindi walipigaga stori kule kijijini na marafiki zake, na walikuwa wakiongelea ishu za wamama kama hawa…. Sasa akawa ameelewa, kisha hapo hapo akachomekea na kingine…

"mi sina simu,.. Hii yenyewe haina maiki"

Chidi ndio anajua kuwa hawa ndio wale wamama wa mjini, wanaopenda watoto wadogo,

"haaaa yaani na ubora wako woote wa kuuza chipsi, kumbe unatumia kisimu cha ajabu hivyo"

"lakini ndio hali yangu sa nifanyeje"

"ok, usijali,… Nipe namba yako nitajua cha kufanya"

Chidi hakusita kumpa namba jimama hilo, huku mama huyo akimuangalia chidi katika sura, alikuwa akimvutia taswira ya sura yake,…

Chidi sura yake ilokuwa nzuri sana kutokana na moto anaouchezea kila siku katika hali ya kuchoma chipsi, hivyo kawa mweupe kiasi na kung'aa haswa,..

Mama aliandika namba kutoka kwa chidi huku chidi akiwa na furaha juu ya kuipata hio pesa, mana hua hapo kwenye banda haondoki hata na kumi kana kwamba hakuwa na asili ya kuiba, mana cha kaka yake ni chake hivyo hataki kuiba katika kazi yake,…

"watoto kama hawa ndio wa kuwalea… Mtoto akiona ngozi tu hoi, je akiona papuchi itakuwaje"

Mama huyo Alijisemea kimoyomoyo huku akiisevu namba ya chidi katika simu yake…

Chidi alishuka katika gari na mama huyo aliondoka zake, chidi aliingia ndani na kuanza kuzihesabu pesa zile

"moja, mbili, tatu, nne, tano, sita…. Heeee kwahio kanipa elfu 10 ya malipo, na hii elfu 50 ni yanini sasa…. Duuuu, hii naficha hata broo asiione"

Aliikunja pesa hio na kuificha katika bukta ya ndani, kisha akaendelea na kazi

Ilipofika mida ya saa 11 jioni kaka yake chidi katokea, mana alisema atakuja ili wafunge wote,.. Basi kazi ikawa nyepesi kwasababu walikuwa wawili chidi na kaka yake Ibrahim,…

Tukija huku hotelini kwa akina sarah na mama yake,… Mama huyo alionekana kurudi kutoka katika mishe zake, lakini ukweli ni kwamba mama yake sarah ndio yule aliokuwa na chidi kule ndani ya gari, sasa hapa sijui itakuaje mana mtoto na mama kama vile wanapita njia moja,…

"sarah"

"abee mama"

"njoo ule chipsi zenye akili… Sio hawa wakwetu wanaparua parua tu"

Mama huyo alimwita mtoto wake ili ale nae chipsi nyama ambazo ametoka nazo kwa chidi,

"mmmmhhhh mamy chipsi umetoa wapi"

"mi nakuamnia chipsi za mtaani ni tamu we acha tu"

"mmmhhhh maaaamaaaa, chipsi tamu hivi zimepikwa mtaani"

"tena zimepikwa na kijana haswa"

"kama ni msafi msafi mlete apikie hapa"

"mbona una haraka hivyo,… Subiri kila kitu ni taratibu"

"mama chipsi tamuu mama zimekauka kauuuuu, huyo mpika chipsi anapikia maeneo gani"

"kuleeee Sakina"

Mama alimdanganya mtoto wake kuwa mpika chipsi yupo sakina lakini sio kweli, chidi yupo pembezoni mwa mji, na ni karibu na shule,….

Mama alimficha mtoto wake huku akijisemea kuwa

"kale katoto kalivyo hensam, nikimuonyesha sarah, mmmmhh sijui itakuaje"

Aliongea hivyo kimoyomoyo huku sarah anasifia sana chipsi nyama hizo,…

"mama na kesho kalete tena"

"nyooooooo, kula hayo matapu tap yenu"

Tukija huku kwa kijana chidi akiwa na kaka yake, walikuwa wapo bize sana na kazi,…

Walifanya kazi sana kwa siku hio tena waliongeza chipsi zingine na walikaa hapo mpaka saa nne usiku….

Kesho yake ikiwa ni mida ya saa tano, chidi alikuwa kazini, lakini hakuwa na kaka yake, kwani jana waliingiza pesa nzuri iliofanya kuendeleza na lile banda lingine kule ambalo anamiliki Ibrahim,.. Ghafla saumu anakuja hapo na kuanza kuongea na kijana chidi

"chidi, nahisi utakuwa umekasirika"

Aliongea saumu huku akionekana kuomba msamaha kwa chidi,..

"skia saumu, mimi ni mwanaume na nina msimamo kama mwanaume"

"sawa chidi wangu, nakubali kosa lakini nisamehe chidi"

"niache wiki moja kwanza nifikirie"

"heeeeee chidi jamani, yaani wiki nzima jamani nateseka tu… Nisamehe mpenzi wangu"

"hapa yenyewe unafanya kosa"

"ok, basi wacha nivumilie tu hio wiki nisitibue vingine"

Saumu alikubaliana na neno la chidi huku akiondoka zake taratibu kabisa,…

Wakati huo tukija huku kwenye hoteli ya akina sarah na mama yake,

"saraaaa"

"abeeee mama"

"njoooo nikutume mjini"

Sarah alikuja kumsikiliza mama yake haraka, mama aliingiza mkono kwenye pochi na kutoa kiasi cha laki 8 na kumpa sarah,

"heeee mama yote hii ni ya nini"

"sikia… Nenda kaniletee Samsung S7"

"heeeee mama unataka ubadirishe simu"

"ndio, naona hii nimeichoka sana"

"ok..sawa"

Sarah aliondoka na kwenda kununua simu alioagizwa,..

Dakika 15 mbele sarah alirudi mana alienda na gari,..

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni