MUUZA CHIPS (20) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 23 Mei 2023

MUUZA CHIPS (20)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA ISHIRINI
ILIPOISHIA...
Alafu nakupa maximum ya pesa ninayotaka,.. Nataka kila siku uuze elfu 80, ole wako iwe chini ya hapo… Afu nimeshakugundua sasa hivi kule nyumbani kunanuka wanawake tu,… Mimi toka nije mjini ile nyumba haijawahi kuingiza mwanamke… Sasa Nasema hivi, Utahama mule ndani sio kwako, mshenzi wewe…"

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Ibrahim kumbe alijua kuwa mdogo wake alishaanza kuingiza mademu ndani, na hata leo katoka na demu,….. Lakini kitendo cha kaka yake kumtukana mama yake kilimuuma sana kijana chidi, yaani hakujiskia raha kabisa,….

Muda ulisogea sana na sasa ni saa 6 mchana, chidi na kaka yake wakiwa katka banda la zamani,.. Mana pesa haikutosha kuendeleza lile banda lingine, hivyo leo wapo pamoja huku wakiseidiana baadhi ya kazi, mmoja anahudumia na mwingine anageuza chipsi, walikuwa wakipendeza sana ndugu wawili kuwa pamoja lakini kila mmoja alikuwa na hasira za kivyake vyake,….

Tukija huku kwa mke wa Ibrahim, tunamuona anamshukuru sana rafiki yake kwa mchezo alioufanya,… Kumbe saa zile alipokuwa anachati, alikuwa anamwambia rafiki yake kuwa, ampigie simu aongee ishu ya msiba,.. Hivyo kumbe hakukua na msiba wala nini…. Rehema au mke wa Ibrahim alitoka na kwenda kwa wakala alie karibu nae kisha akaituma ile pesa yote aliopewa jana,.. Elfu 60 ya kulipia hospitali, na elfu 50 ya kutuma msibani, sasa hapa ndio kaituma,.. Baada ya kuituma akashika simu yake na kupiga…

"halooo mama… "

"Abeee mwanangu hujambo huko"

"sijambo shkamoo"

Rehema anaongea na mama yake hapo

"marahaba mwanangu… Vo hali"

"nzuri tu… Aaahhh juzi ulisema simenti imeisha"

"ndio… Halafu pia mchanga na kokoto zimeisha"

"nimetuma laki moja na kumi, hivyo utaangalia chenye umuhimu uanze nacho mama"

"sawa mwanangu… Fanya hima tuimalizie nyumba yetu"

"sawa mama mchana mwema"

Heeeeeeeeee kumbe akina rehema wanajenga nyumba, na ile pesa yote imetumwa ikanunulie matirio… Afu bado unajiita kidume wakati wenzako wanajenga na pesa yako, kwenu wanakufa njaa…kazana sana, na hii ni asilimia 60 ya wanawake wa mjini hata kama umemuoa, ni lazima afanye kitu kule kwao,… Ee mungu wajaalie wanaume wote wasiwe na akili kama za kaka wa chidi…

Tukija huku kwa chidi na kaka yake… Ibrahim alikua anahitaji kupumzika, hivyo alimuaga mdogo wake kuwa anaenda nyumbani kupumzika, mana hajiskii vizuri,

"chidi, sasa we endelea, wacha nikapumzike kidogo, ila jioni kama saa 11 hivi nitakuja ili tufunge wote, sawa"

"sawa broo we nenda tu kapumzike"

Ibrahim aliondoka huku akiangaza macho huku na huku kama atapata toyo impeleke nyumbani,.. Ila hakuwa amesimama bali aliona atembee taratibu kama akiona toyo sawa…

Dakika 5 mbele, ghafla fatu anatokea huku akiwa na hamu ya kuongea

"chidi leo kaka ako kakubana eee"

"kwanini useme hivyo"

"toka saa nne nilikuwa nataka nije nikuambie lakini nikawa namuogopa kaka ako"

"kwani ang'ata yule,… We ungekuja tu"

Walikuwa wakiongea huku wakitabasamiana…

"chidiiiii"

"sema… "

"jana ulinichetua, mmhhhh"

"aaaahhhh wapi, unanipaka mafuta kwa mgongo wa chupa"

"kweli vile…. Yaan mpaka nasahau chupi ulizani mchezo nini"

"Ati unasema umesahau nini"

Chidi alitoa jicho kuskia fatu kasahau chupi kule nyumbani,

"nimesahau chupi yangu kule kwenu"

"ivi fatu, unaongea kweli au unatania"

"njooo huku ndani nikuonyeshe, kama hujanikuta nipo uchi, hapa nina sketi tu, yaani nafanya kujizuia na begi mana ninavyotetemesha huku nyuma mmhh nahisi ntabakwa mwenzio"

Fatu alikua anachulia raha, lakini chidi tayari akili imeshavurugika,…

Aliikumbuka sauti ya kaka yake ikisema

"Mimi toka nije mjini ile nyumba haijawahi kuingiza mwanamke… Sasa Nasema hivi, Utahama mule ndani sio kwako mshenzi wewe…"

Alipomaliza kukumbuka hilo, akakumbuka na lingine la muda huo huo

"chidi, sasa we endelea, wacha nikapumzike kidogo, ila jioni kama saa 11 hivi nitakuja ili tufunge wote, sawa"

"sawa broo we nenda tu kapumzike"

Alipomaliza kukumbuka alimgeukia fatu na kumuuliza,

"ivi unakumbuka hio chupi uliiweka wapi"

"heeeee, wewe si ndio ulinivua mwenyewe pale kwenye kochi"

"muuungu wangu weee kumbe ip kwenye kochi…….. Ebu nisubiri hapo dakika mbili"

Chidi alitoka nje na kuangaza huku na kule kama ataona toyo,… Lakini hakukua na toyo wala nini,… Na muda alioondoka kaka yake atakuwa keshafika….

Chidi alipagawa haswa mana kaka yake akiiona ile chupi atamfukiza pale ndani, mana keshasema kuwa ile nyumba inanuka wanawake, lakini hajazibitisha kuwa ni kweli anaingiza wanawake au vipi,… Chidi alihaha huku na kule, na wakati huo baada ya kukosa pikipiki, aliamua kukimbia…. Lakini hakufika mbali, kwa bahati nzuri pikipiki hio hapo

"asee ebu kimbiza spidi ya mwisho"

Chidi alimuamuru dereva huyo ili awahi kabla ya kaka yake, na uzuri ni kwamba kila mtu ana funguo yake, hivyo kama Ibrahim hajawahi basi chidi akiwahi ataweza kuichukuwa,….

Wakati huo Ibrahim kumbe alikosa pikipiki, na hio ndio ilikuwa bahati kwa chidi, kwani kaka yake alikosa pikipiki hivyo aliamua kutembea taratibu, chidi alifika ndani ya dakika tano, mana pikipiki ilikuwa spidi kali mno,… Alifungua na kuichukua ile nguo, tena ilikuwa wazi mno kana kwamba kama angelifanikiwa kufika, basi ni lazima angeiona chupi hio

Chidi aliichukuwa na kuiweka mfukoni, kisha akatoka zake mpaka kibandani, na kumkuta fatu kakaa pale pale alipomuacha, chidi alikuwa akifikicha macho mana alikuwa akipulizwa na upepo katika pikipiki hio,…. Sasa alishindwa kumpa fatu chupi yake mana palikuwa na wateja hivyo alienda mpaka kwenye stoo ya mkaa na kuihifadhi mahali, afu akamfuata fatuma na kumwelekeza alipoiweka,..

Chidi alijipiga usafi vizuri kisha akaendelea na kazi, huku fatu akitoka katika stoo ya mkaa huku akiwa anaitengenezea vizuri nguo hio baada ya kuivaa,..

Hapo sasa chidi moyo wake ukawa umetulia,…

Lakini ghafla simu ya chidi inaita, kucheki jina alikuwa ni kaka yake,.. Alishtuka sana kuona jina la kaka yake,

"haloo broo"

Alipokea simu huku akiwa na wasiwasi juu ya simu hio, na fatu ndio alikuwa anatoka kwenda shule, hivyo kabla hajaongea kitu, chidi akamuuliza fatu huku simu ikiwa chini

"we fatu, hujaacha sidiria kule"

Chidi aliuliza kwa sauti ya chini sana, huku fatu akijibu

"akuuuuu toka lini nikavaa sidiria, kifua chenyewe ndio hiki cha kitoto hivi"

Na ni kweli chidi akiangalia hicho kifua cha fatu, hakikuwa tayari kwa kuvalishwa sidiria, ila sema chidi alimuuliza fatu kwa wenge la kupigiwa na kaka yake na kudhani labda kuna kitu kingine kimeachwa kule, lakini hakukuwa na kitu, hivyo chidi akairudishia simu sikioni na kusikia kaka yake anagomba mno,

"we vipi mbona unapokea simu afu huongei una akili wewe"

"broo nilikuwa na wateja,.. Sasa nimwache mteja afu niongee na simu"

"aahhhh Ok, basi poa… Sasa ikifika saa saba mchana, ebu nenda katume elfu 30 pale M-pesa sawa"

"heeeeee broo sasa elfu 30 tena na wakati inatakiwa kesho ufungue banda kule chini"

"hio pesa ni yako"

"ok, poa broo samaani lakini, nitakwenda kutuma"

Chidi alibidi akubaliane na kaka yake, kuwa akatume pesa kwa yule mtu wa siku ile,…

"saa saba juu ya alama, hakikisha hupotezi hata dakika moja"

"sawa broo, nitafanya hivyo"

Chidi alikata simu kisha akamgeukia fatu ambae alikuwa bado kasimama ili kuskia kuna nini kati ya kaka yake chidi,

"nenda shule wewe"

"sasa chidi"

"nini tena"

"leo nije tena"

"hapana, hapana, mtaniua fatu, mi stumii chuma eti, saumu mwenyewe akija hapa atataka niende nae,…"

"lakini si uliache hilo lisaumu, kwanza na litako lake lile anajua kukatika kama mimi yule?… Nakuuliza anajua"

"kwani kuna mwanamke asiojua kukatika?"

"wapo wengi tu, haswa huyo swaumu wako"

"wanawake wote wanajua kukatika sema Uvivu tu ndio unawakosti katika mapenzi"

"ok, lakini mi umenionaje chidi,… Kiuno changu kilaini eee?"

"waapi hata wewe mvivuuu"

"nyoooooooooo lione vile, ningelikuwa mvivu ungechoka vile, muone vile hata shukrani huna… Akaaa acha nienda zangu shule mimi"

Fatuma alitoka zake baada ya kuongea na kijana chidi, ndoto za Fatuma ni kufanikisha kuachwa kwa rafiki yake saumu, ili nafasi ya saumu aishike yeye peke yake,

Saa Saba juu ya alama kijana chidi anakwenda M-pesa, kutuma pesa kama alivyoambiwa na kaka yake

"haya broo inakuaje hapa"

Chidi alimsalimi mtu huyu ambaye ndio mtoa huduma hapo kwa wakala,..

"poa sana ndugu habari yako"

"nzuri…. Asee kuna hii elfu 30 hapa nimeagiziwa uitume kwenye ile namba"

"aaahhhhh ile namba ya Ibrahim"

"ndio"

"ok poa, hapo mambo yamekwisha, nitaituma shekhe"

Basi chidi aliondoka zake kisha akampigia kaka yake simu kuwa mtu huyo keshaipata au bado

"eehh broo, nimeshatuma, sasa sjui keshaipata"

"yes kaipata mana kanipigia sasa hivi…"

"ok poa broo"

Basi chidi alirudi kibandani kwake na kuendelea na kazi zake,..

Tukija huku kazini kwa akina sarah, tunamkuta mama yake sarah akiwa na mtoto wake,

"mwanangu sasa umekuwa ujue"

"yes, but what do you mean about your question"

"aahhh sijawahi kukuona hata ukiongelea swala la mchumba"

"sasa mama…. Wewe mwenyewe ndio unanibana, nilikuwa na mpenzi wangu nataka awe mchumba wangu, lakini ukanikataza"

"heeeeeeeeee huyo jambazi"

"mamaaaaa, unamsikiliza Miriam akisema jambazi, mamaaa huyo kaka ni hensam"

"mimi nataka ulete mtu mwenye kazi ya maana, sio jambazi bwana"

"mbona ana kazi tu,.. Sema miriam ananikandia tu na kumuita jambazi"

"sio hivyo, miri yupo sahihi mana kaniambia kuwa ulimkuta kachubukaa katoka kupigwa na wananchi wenye hasira kali"

"mungu wangu jamani mamaaa,.. Sema tu hutaki"

"ok, sawa… Ila kama hana kazi ya maana simtaki"

"usijali mama angu, unajua mi nataka niwe na mume sasa hivi, kama ni kusoma nimesoma na kazi ninayo, sasa kipi ambacho sina mama"

"mmmhhhh utajuwa mwenyewe… Ila sarah"

"abee mama"

"natoka kidogo hivyo kuwa makini"

"sawa mama, lakini si utarudi"

"ndio, lazima nirudi"

Sarah alifurahi kupewa uhuru kidogo na mama yake, huku mama akiwa kama boss katika hoteli hio na sarah akiwa kama meneja na keshia, yaani pesa yote ya mauzo ya hoteli hio yanamuangukia sarah, afu sarah anamkabidhi mama yake, na mama yake anamkabidhi mama yake miriam, kwahio wazazi wa miriam wana hoteli mbili na ndio wamiliki wa hoteli zote, ila kutokana na ukaribu wa mama sarah na mama miriam,.. Mama Miriam alimkabidhi rafiki yake hoteli moja aimiliki yeye,.. Ila mauzo yanakuwa yanakwenda kwa boss,… Kama vile mtu aliokabidhiwa gari aendeshe atakavyo lakini jioni amletee pesa. Sasa ndio hivi vya mama miriam na mama sarah… Na ukaribu walionao mama sarah na mama miriam ndio ukaribu waliouanzisha miriam na sarah,.. Mama sarah na mama miriam walisoma wote kutoka shule ya msingi mpaka chuo,… Na akina miriam pia hivyo hivyo mpaka sasa wapo kama ndugu wa kuzaliwa kumbe ni marafiki tu,

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni