MUUZA SUPU (14) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatatu, 8 Mei 2023

MUUZA SUPU (14)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Geofrey Malwa

SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
Hakuelewa kama pendo la kweli halishawishiwi kwa kufanya na mtu mapenzi mara nyingi au kuwa mjuzi sana kitandani
,,,Sonki kwanini unanichukia sana,,,
,,,sikuchukii lakini sihitaji kumpoteza Celline kwasababu nampenda,,,
,,,kwani yeye anakupa nini ambacho mimi sikupi,au anakuhonga pesa nyingi sana,,,?

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
,,,hapana mi nampenda tu,,,,
,,,naomba nikuombe kitu,,
,,,sema,,,
,,,jamani mbona kwa ukali hivyo,,,
,,,ongea nakusikiliza,,,
,,,naomba tuwe tunafanya hivi lakini Celline asijue,,,
,,,naomba iwe mwanzo na mwisho leo,tena ukiendelea mi nitakuhama nyumbani kwako,,,

Maongezi hayo yakiwa yanaendelea kati ya Sonki na Bosi wake Lina mara mlango wa chumba chake ulibishwa hodi,,Ngo,,ngo,,ngo,,!,,kidogo moyo wake Sonki ulishtuka,lakini akajua kabisa hakuna mtu mwingine zaidi ya Queen,,huyu atakuwa Queen tu si mwingine,na anataka nini sasahivi,,,aliongea hivyo Lina na kutaka kuinuka kwenda kufungua ,,,subiri kwanza Lina una uhakika ni yeye,,, alihoji Sonki huku akimshika mkono Lina kwa umzuia asiende kufungua mlango

,,ngo,, ngo,, ngo,,!, hodi Sonki,, mwili wa Sonki ulisisimka kusikia sauti hiyo ambapo hata Lin anaye alianza kutafuta mahali pa kujificha,,,kwavile sehemu ya kuingilia uvunguni kwenye kitanda hicho ni mdogo,Sonki alichokifanya alinyanyua kitanda kisha Lina akaingia chini ya uvungu na kujificha,,, Mungu wangu Celline sasahivi amekuja kufanya nini,,,?,, mbon aloe nimekwisha,, lakini nilimwambia huyu mwanamke hakuna siri hapa duniani itakuja kujulikana tu,,,akiwa anajiuliza maswali hayo kichwani mwake Sonki mara ujumbe mfupi uliingia kwenye simu yake,,,

,,,leo ndio utajieleza na nimeshamwambia Lin ayupo humo ndani,,,ujumbe uliandikwa hivyo ambapo aliyetuma alikuwa si mwingine ni Queen,,,Sonki aliona njia bora ya kuepuka tatizo kama hilo ni kujiamini mbele ya celline,,alikwenda na kufungua mlango ambapo kama alivyowaza alikuwa ni Celline kweli,,
,,mambo,,!
,,safi karibu,,,
,,nimekusapraizi eeh?,,
,,ni kweli,lakini nimefurahia ujio wako,,,

Waliongea hivyo Sonki na Celline ambapo Sonki alimpisha Celline akaingia ndani kisha na yeye akafuata,,,mmmh,Sonki,,,leo sina mengi ya kuongea na wewe lakini kaba ya sijaongea chochote naomba umtoe huyo uliyemficha,najua utashangaa sana kwa mimi kuja muda kama huu lakini leo nataka kujua ukweli wako,embu mtoe kwanza huyo Bosi wako,,,Celline aliongea hivyo huku akijiamini kanakwamba alikuwa anajua tukio zima,

Sonki alijawa na wasiwasi mwingi baada y akuyasikiliza maneno ya Celline kwa umakini,lakini moyo wake ulisita kumtoa Lina kwani alijua wazi pangeweza kutokea hatari kubwa kama wangeonana wawili hao,,,Sonki,mbona unachelewa kumtoa huyo Bosi wako,au unajua sijui alipojificha,humu ndani kuna sehemu mbili ambapo anaweza kujificha,moja ndani ya kabati na mbili ni chini ya uvungu wa kitanda,naomba unisikilize kwa makini,nimekupa uhuru wa kumtoa mwenyewe umeshindwa, nikimfuata mimi jua kwamba nitamuua,,, maneno ya awamu hii aliyoyatoa Celline yalimwingia Sonki akilini na kumzidisha hali ya wasiwasi

Lina akiwa chini ya uvungu kwavile hewa ilikuwa inamfikia kwa kiasi kidogo alijikuta akipumua kwa shida hali iliyomfanya ajulikane yuko wapi kwani alikuwa anahema kwa kasi huku akivuta hewa kwa nguvu,,kiukweli uhemaji wa Lina ulishamuumbua kwasababu alipoisikia Celline,hakukuwa tena na haja ya kumficha,basi Sonki aliinua kitanda kisha Lina akatoka,,,

Ilikuwa ni aibu kubwa kwa Lina ambaye muda wote alijifanya ni mstaharabu mbele ya Celline,,mmh,kaeni tu hapo,,aliongea Celline huku akionekana usoni mwake kutawaliwa na hasira sana,,,sawa nimeona maana ya upendo wako Sonki,pengine niliingilia penzi lenu wewe na Bosi wako,,kwaheri Sonki,,,aliongea hivyo Celline huku chozi likimtoka na kuwaacha kitandani hapo wameketi Sonki na Lina

Sonki alitulia kimya na kujaribu kumzuia Celline lakini haikuwezekana,Celline aliondoka nyumbani hapo kwa hasira,huku nyuma ndiko palitokea kizaazaa na vurugu la hatari,kwanza kabisa Sonki aliporusi ndani alimkuta Lina amesimama akionekana kuwaza kitu kama mtu aliyechanganyikiwa,,, Sonki hakujali kama ni Bosi wake lah!,alimpiga makofi mwawili ya nguvu yaliyompeleka Lina mpaka sakafuni,,,jamni Sonki unanipiga unanionea,imetokea tu bahati mbaya,,aliongea hivyo Lina huku akiwa chini akiugulia maumivu ya makofi hayo,,

Kwa hasira Lina aliondoka chumbani kwa Sonki ambapo ati ya chumba cha Queen,kwa muda huo Queen alijifanya amelala kwani alikuwa akifuatilia yanayoendelea muda si mrefu chumbani kwa Sonki,,,

Alipofika tu Lina alilivuta shuka alilojifunika Queen na kulitupa chini,Queen akabaki na gauni lake la kulalia pia kama alivyo Lina,,,umefanya nini mpuuzi wewe,,,!,au hutaki kazi,,,kwanza ngoja nikuonyeshe,,,aliongea hivyo Lina huku akimfuata Queen kitandani na kuanza kumwangushia kichapo,,,Lina hakuzoea maisha magumu hivyo hata makofi aliyokuwa anampiga Queen hayakuwa na uzito wa kuumiza sana,,,

Queen alishambuliwa na makofi ambapo kwa dharau alikuwa akimcheka Lina anavyompiga,, alichokifanya alimsukuma Lina kwa mkono mmoja na kujigeuza kisha akawa juu yake amemlalia,, mikono yote miwili ya Lina aliishikilia kwa juu na kujibana kiasi kwamba Lina wa watu na nwili wake alikukuruka lakini alishindwa kuitoa,,,sikiliza Bosi wangu,nina uwezo wa kukipiga mpaka nikakuua, lakini sitafanya hivyo, nilichotaka ni Sonki aachane na Celline kisha mimi niendelee kula raha na Sonki,lakini wewe umenitibua hivyo nilikuwa nakusubiri tu uje niondoke,,,aliongea hivyo Queen kwa kujiamini na kumfanya Lina kuwa mpole kabisa,,

Basi Queen baada ya kumchimba mkwara wa maana Lina aliyebaki juu ya kitanda akimwangalia tu Queen,alifungasha kila kilicho chake mule ndani,,kwaheri tutaonana mungu akipanda,nitakumisi,,alitoa maneno hayo ya mwisho na kuondoka,,,
Alipotoka nje,kumbe Celline alikuwa akimsubiri na gari lake,alipowasili aliingia ndani ya gari kisha gari ikawashwa na kuanza kuondoka,,
,,nashukuru umenisaidia sana Queen,,,
,,nashukuru na wewe pia,kwani hata sijui ningeenda wapi,,
,,usijali,kwangu utakaa salama kabisa,wala usiwe na wasiwasi,,

Kumbe kilichopo nyuma ya pazia,Celline alimtafuta Queen kwa hudi na uvumba kwa siri bila Sonki wala Lina kujua,siku hiyo aliwavizia wawili hao wapo mgahawani yeye akaenda nyumbani,lengo lake lilikuwa,endapo atamkuta mlinzi au mfanyakazi yeyote lazima atajenga urafiki naye hata hela atampa ili tu ajue kama Lina amwibii Sonki wake,,,

Basi kwa bahati nzuri siku hiyo Celline alimkuta Lina nyumbani hapo ambapo Queen alikubali kupokea kazi ya kumchunguza Sonki kama anatoka kimapenzi na Lina,masikini wa mungu Celline alifanya hivyo bila ya kujua huyo anayemkabidhi naye ni mmoja kati ya wanaomtamani Sonki,, kwahiyo Queen kichwani mwake alijua fika akafanikiwa kumwachanisha Sonki na Celline kwa upande wake anaweza kufurahi na Sonki,kilichomfanya Queen kupewa hifadhi na Celline ni kwasababu ya kumlinda Celine kutoka kwa Sonki na Lina,,,mawazo ya Queen juu ya Sonki yalikuwa tofauti na jinsi hali halisi ilivyotokea,hivyo naye alijikuta akijisemea moyoni ni bora hata amemwaribia Sonki kwa Celline

Tukirudi kwa upande wa Sonki alikuwa na mawazo sana juu ya tukio hilo lililotokea ambapo kwa upande mwingine lilikuwa na faida kwa Lina kwani alijisikia furaha sana kufumwa,alijua wazi ndoto zake za uishi na Sonki zitakuwa zimetimia,alichokifanya Lina wakati huo akiwa chumbani kwake alinyanyuka na kwenda kitandani kwa chumbani kwa Sonki ambapo alimkuta Sonki amejilaza chali kitandani huku mikono yake akiwa ameiweka kichwani,mawazo mengi yalimtawala,,,

Lina akiwa ndani ya vazi la khanga moja ambapo alishaoga tayari,lengo la kuja chumbani kwa Sonki lilikuwa ni kuomba msamaha kwa tukio alilolifanya,lakini akilini mwake alikuwa n alengo la kumtega Sonki ili waendeleze mchezo huo wa kikubwa,

Basi Lina aliingia ndani hapo na kumkuta Sonki akiwa amelala chali kanakwamba mtu aliyechoka sana,lakini harufu ya humo ndani kidogo ilimpa mashaka,akiwa hata hajamfikia Sonki,alipotupa jicho pembeni ya kitanda kwa chini aliona chupa kubwa ya pombe kali,kumbe ni muda mrefu Sonki alishakunywa Pombe ambapo muda zilianza kumkolea kichwani,,,

Lina ilimbidi asitishe alichokipanga kufanya Sonki kwa mara ya pili ambapo alimsaidia Sonki kwa kumrudisha katika hali ya kawaida,,alimwinua na kumlaza vizuri kisha akachukua maji ya baridi na kummwagia kidogo kichwani,,

Tukirudi kwa upande wa Celline ambaye alimpa hifadhi Queen nyumbani kwao,kadri siku zilivyozidi kwenda walizidi kuzoeana,wakawa marafiki sana kwani walijikuta wakiendana kila kitu,ndani ya moyo wa Queen ile dhana ya kumtamani Sonki ikamuisha,akawa anaeleza mambo wazi kwa Celline ambaye bado alikuwa anapenda kusikia habari za Sonki

Kuanzia mwanzo mpaka mwisho kuhusu Sonki na wanawake wake walioishi naye n akumsababishia mpaka kipindi kile kurudi TAMUNI,Queen alimsimulia yote Celline ambapo naye Celline alieleza kila kitu kuanzia siku ya kwanza anakutana na Sonki kule TAMUNI na kupendana mpaka kufikia hatua waliyopo sasa,lakini Queen badi hakumgusia kwamba hata yeye pia ni mmoja kati ya waliochezea mtalimbo wa Sonki kitandani

Siku hiyo Celline alikwenda Hospitari na Queen ambapo Queen alimsubiri kwa nje,kwavile alikuwa na Daktari wake maalumu hivyo haikumchukua muda mwingi,alimalizana na Daktari wake kisha akatoka huku akiwa hana furaha kama mwanzo,walipopanda gari kabla hawajaondoka Queen ilimbidi aulize kilichomsibu Celline,,
,,,nini tatizo Celline,,?
,,,we acha tu Sonki,aah!,Queen,,aliongea Celline huku akichanganya majina,Queen akamwita Sonki
,,,mbona sikuelewi jamani,,,
,,,Daktari amesema nina ujauzito wa mwezi mmoja na wiki mbili,,,
,,,jamani,sasa ndio unachukia Celline,,,?
,,,sichukii ujauzito lakini nachukia kuzaa na yule mwanaume,,,
,,,usijali,mambo yatakuwa sawa tu,hilo lisikupe shida,,
,,,sawa,,,

Tukirudi kwa upande wa kijiji cha TAMUNI,leo walikuja vijana walioshiba sita wakiwa na mzee Fulani wa makamo,ambaye alionekana ndiye kiongozi wao,watu hawa walitokea kijiji cha jirani kilichoitwa DALOYO

Historia fupi ya kijiji wanachotoka hawa watu waliokuja TAMUNI,ni kwamba wao ndio walikuwa waanzilishi wa SUKUTO,kipindi hicho kweny ekijiji chao waliita zoezi hilo ni DAKUTO, vijiji vingi walianzisha zoezi hili ambapo lilionekana likifanywa vyema sana na watu wa TAMUNI kitu kilichosababisha kijiji cha TAMUNI kujulikana kama ndio waanzilishi

Tangu waanzishe wawape watu mawazo ya kuanzisha utamaduni huo ni kwambawalikuwa n uataratibu wa kuwapitia kila kijiji na kukipima kama kweli wako vizuri kwenye kulifanya vyema zoezi hilo,

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni