MUUZA CHIPS (100) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 26 Aprili 2024

MUUZA CHIPS (100)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA MIA
ILIPOISHIA...
Sasa chidi kumuangalia vizuri huyo shemeji yake,.. Alishikwa na butwaa, lakini sasa hilo ni dogo, kumbe huku miriam na Ibrahim nao pia wanafahamiana, hivyo walikuwa nao wanashangaana, kwahio kila mmoja alikuwa akimshangaa mwenzie… Salma na chidi, afu miriam na Ibrahim.. Ukimya wa ghafla ulitawala eneo hilo,…

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Kilikuwa ni kitendo cha kushangaza sana kwa wapenzi hao, mana kila mmoja alikuwa akifahamiana na mwenzie,.. Lakini kwa chidi hakukuwa na shida ila kwa huyu miriam ndio kuna shida, yeye kajuana vipi na Ibrahim, ambae ni shemeji yake

Salma na chidi, afu miriam na Ibrahim.. Ukimya wa ghafla ulitawala eneo hilo,…

"we rashidi huyu ndio mkeo mtarajiwa"

Aliuliza Ibrahim, lakini chidi nae kabla hajamjibu kaka yake, nae akabandika swali juu ya swali…

"na mimi kabla sijakujibu, hebu niambie huyu ndio huyo mkeo mtarajiwa"

Aliuliza kijana chidi huku akimsogelea salma, na salma kaganda pale alipo hata hamu ya kuondoka eneo hilo

"nimekuuliza nikiwa kama kaka yako, we nijibu kwanza"

Aliongea Ibrahim, Lakini Sasa chidi akahisi mbona kama anafatilia kitu ambacho anakifahamu, hebu ageuke nyuma ajue huyu miriam na Ibrahim wanajuana kivipi…

Chidi akamlazimu kuachana na Salma na kuja huku kwa mke wake mtarajiwa..

"kwani vipi apa.. Nyie mnajuana"

Aliuliza kijana chidi huku akimnyookea miriam,

"ndio.. Kama huyu ni kaka yako ni mkorofi huyu"

Miriam aliongea hivyo huku akionyesha kumchukia sana Ibrahim,

"we umemjuaje kaka yangu"

Chidi nae alikuja juu huku akimsogelea miriam kwa ukaribu, tena ikiwezekana hata kumnasa kibao amnase pale atakapojua kuwa kuna uhusiano baina yao..

"huyu alikuwa mteja wetu mzuri tu, na alikuwa anakuja kupata lanchi na wafanyakazi wake,.. Ila alikuwa akimuhitaji mwanamke, anafanya nguvu"

"haaaaaa kwahio, hata wewe alikupata kwa nguvu"

"hapana chidi.. Ila namshangaa kumuona hapa na wakati mara ya mwisho alikamatwa na polisi na mimi ndio niliwaita pale hotelini kwetu"

Chidi baada ya kuskia hivyo alimgeukia kaka yake na kumuuliza

"sasa broo kumbe ni hivyo tu, mbona sasa unashangaa sana au kuna jipya"

"yaani mdogo wangu, mimi nashangaa kwa furaha, mana katika mke uliopata, basi huyu ni mke, kwanza hapendi ukorofi, cha pili ni mpole… Kweli kuna siku tulitia hasara kubwa sana pale hotelini kwao lakini aliishia kuleta polisi wanitoe nje tu, mana nilikuwa nimelewa, hivyo toka aiku hio sijawahi kufika hapo, ndio leo tunaonana hivi"

"aahhhh kumbe ujinga tu mananiumiza akili yangu buuuure"

Sasa chidi kugeuka akamuona salma, sasa hapo mada ikahamia kwao akina Ibrahim na salma…

"sasa broo… Ivi unajua kuwa unaishi na mke wangu ambe sijampa hata talaka"

Aliongea chidi lakini Ibrahim akaona kama ni utani hivi,..

"we babuu ulioa lini wewe, unamdanganya kaka yako bure"

Aliingilia mdada miriam,

"sio kuwa namdanganya… We hukumbuki nilishawahi kukuambia kuwa nina mtoto kijijini"

"yes, nakumbuka hilo"

"sa mama yake ndio yule"

"heeeeeeee we babuu mbona muongo hivyo"

Aliongea miriam kuhisi labda ni utani wa chidi tu

"broo, ulipolenga sio pabaya… Ila yule ndio huyo mke wangu wa kijijini, na sijui mlikutana wapi na vipi but huyo ndie"

Ibrahim kumuangalia salma, alimwona kainamia chini huku aking'ata kucha taratibu…

"eti wife anachosema huyu bwege ni kweli"

Salma bila kusita wala kugwaya gwaya, aliitika na kusema ni kweli

"ndio"

"chidi, hebu haya mambo tukayaongee nyumbani, ila tutokeni hapa Airport"

Aliongea Ibrahim huku wakichukuwa mizigo yao,

Tukija huku kwa akina miriam tunaona mabasi kama kumi hivi yakiwa tayari kwa ajili ya kubeba watu, yaani mama miriam alidhamiria kabisa kumuozesha mtoto wake kwa chidi, tena aliahidi mwenyewe kuwa ataigharamikia kila kitu mpaka mwisho,.. Mama miriam alikuwa bize kwa kualika watu, yaani spati picha huko kijijini, yaani kijana chidi anakwenda kutia aibu ya mwaka,.. Mana familia nzima ya baba na mama woote pamoja na marafiki zao wote, na watu wengine, kule kijijini kwa akina chidi kuna hali mbaya sana ya kimaisha, yaani ni aibu inakwenda kutokea huko kijijini, kwasababu nyumba ya akina chidi ina matobotobo kila mahari yaani sijui itakuwaje,… Baba yake na miriam nae alikuwa katika shamra shamra za kualika marafiki zake,

Mama miriam alinyanyua simu na kumpigia mama sarah

"haloo mama sarah habari yako"

"nzuri mama miri, hali yako"

"safi tu,.. Sasa si unajua kesho tunakwenda ukweni"

"ukweni??… Ukweni wapi tena"

Mama sarah alinifanya hajui kitu lakini anajua kila kitu juu ya ishu hio

"si unajua mwanao tunakwenda kumuoza kwa yule kijana uliomleta pale kazini kwangu"

"aaahhhhhh kumbe kesho ndio mnaenda"

"ndio, na wewe nakutegemea sana shost"

"heeeeeeee we ulifikiri nitaachaje kwenda"

Aliongea mama Sarah huku akiwa na furaha ya kwenda huko, lakini anajua atafanya huko,..

"ahsante sana shost wangu, basi wacha tuendelee kuandaa hapa"

"sawa, tutajua kesho tutaondoka saa ngapi"

"sawa"

Simu ilikata huku mama sarah akiwaza ni jinsi gani anampenda chidi kwa moyo wake wote, afu leo ndio huyo anaekwenda kufungishwa ndoa,… Ghafla sarah anakuja ofisini kwa mama yake,

"mama vp mbona kama una mawazo"

Aliongea sarah huku mama yake akisita kusema

"utaenda harusini"

"harusi ya nani"

"si ya kipenzi chako miriam"

"akaaaaa sina kipenzi kama yule,.. Hawezi kunipokonya mpenzi wangu nikamuangalia tu"

Sarah alimshtua mama yake kwa kuongea maneno hayo

"heeeee we sarah wewe, sasa unataka kufanya nini, na si nilishakuonya uachane na chidi"

"hapana mama sio kirahisi rahisi namna hio"

"Sarah,… We sarah. Wewe"

"mama, yaani huko kwenye harusi lazima niende, hata kama sijaalikwa lakini kwenda ni lazima, yaani sio ombi, na nitahakikisha ndoa haikamiliki"

"we sarah pumbavu wewe,.. Unajua nitakuachia laana wewe,.. Nasema achana na chidi na usimzoee tena"

Mama sarah bado hatamani kumuacha chidi, anampenda sana na katika vidume waliomkuna kimapenzi namba moja ni kijana chidi,.. Yaani mama sarah kampenda chidi mpaka kaoza yani…

Tukija huku nyumbani kwa kijana chidi, wakiwa wameshafika nyumbani kutoka Airport

"salma mke wangu, ina maana ni kweli we ulikuwa ni mke wa mdogo wangu"

Aliongea Ibrahim huku chidi akiwa hana hata wasiwasi na salma,

"ni kweli, lakini ilikuwa ni tamaa ya maisha mume wangu… Lakini kwa sasa nimeshamsahau na sihitaji kumfikiria yeye, ispokuwa wewe tu"

Aliongea salma huku akilia kwa uchungu

Chidi aliona yote ni maisha, hivyo kikubwa ni kusameheana tu mana kwa sasa huezi kuwatenganisha Ibrahim na salma mana tayari wameshapendana tena wanapendana kuliko hata kipindi wakiwa na chidi…

"skia broo,… Kwa sasa hata mimi sina wazo na huyu mwanamke… Kwa sasa nina mke wangu mtarajiwa ni huyu hapa,.. Na mpaka sasa nitamueshimu mkeo kama shemeji yangu,.. Naomba unisamehe kaka mana hukulijua mapema hili… Ila kazi kubwa nadhani ipo kule nyumbani… Sijui ataombaje msamaha kwa wazazi wetu ili kurudi tena katika familia yetu, ila kwa mimi nimesamehe na pia nimesahau kabisa"

Aliongea kijana chidi huku akitia heshma kwa shemeji yake

"shemeji Rashidi, naomba unisamehe kwa kumuacha mwanao kijijini, nisamehe sana"

Sasa chidi hakuna kitu kilimuuma kama kuachwa kwa mtoto wake… Hasira zilimpanda upya, kawa mbichiii…

Lakini chidi alifikiria sana kutokana na swala la kugombana na salma,.. Binafsi aliweza kujizuia hasira zake, mana tayari ni mke wa kaka yake, hivyo wakigombona mbele ya kaka sio vizuri, kikubwa ni kusameheana tu,

"mimi nimeshakusamehe kitambo tu baada ya kujua upo na kaka yangu,.. Lakini ombi langu kwako, naomba umpenda kaka yangu, na usije ukamkimbia kama ilivyo kwangu"

"siwezi, kwani nimeshakula kiapo juu yake"

"ok.. Sasa naombeni twendeni dukani ili tukawanunulie nguo kwa ajili ya kuipamba harusi yangu, tena mumekuja wakati muafaka"

Miriam na salma walichukuwana kama wake wenza, na chidi na kaka yake walichukuwana nao kwenda kwenye gari…

Walipofika dukani chidi aliingia na kaka yake katika upande wa kiume na Miriam kaingia na mke mwenzie katika upande wa kike,.. Salma alikuwa ana ujauzito mkubwa tu,..

"natamanije na mimi niwe kama wewe"

Aliongea Miriam huku akilishika tumbo la salma,

"mmmhhh mbona mume wako atakupa tu"

"ni kweli lakini khaaaaa… We si unamjua shemeji yako alivyojaaliwa, yaani kanishinda"

"jitahidi jamani.. Mi mwenyewe siku ya kwanza nililia lakini nilivumilia tu"

Salma aliongea kwa kumpamba Miriam na kumtoa hofu juu ya chidi,.. Salma anasema siku ya kwanza alipokutana na chidi alilia sana lakini alivumilia tu

"afu sasa kuna kitu nataka nikuulize kuhusu chidi… "

Aliongea Miriam huku salma akiwa na shauku na swali hilo

"nataka nijue anachokipenda katika mapenzi.. Mana nashindwa nimhendo vipi"

"tatizo lenu nyie watoto wa mjini.. Mmezoea kuruka ruka tu"

Aliongea salma huku akitaka kumwambia ukweli

"sio kuruka ruka, sema mie mwenzio nimekulia maisha ya pesa pesa sana hivyo mambo mengi ya uswazi siyajui"

"skia sasa nikwambie ukweli… Cha kwanza mumeo anapenda kuona chupi kubwa kubwa afu zile lainiiiiiii… Yaani ukivaa hizo kila siku upo nae kitandani"

"Uuuuuuuwwwiiiiiiiii…. Kumbe ndio mana alishawahi kuniletea chupi kubwa kubwa"

"sasa je"

"basi mke mwenzangu umenipa njia nzuri sana, na nitaifanyia kazi hio… Nampenda sana mume wangu"

Aliongea Miriam baada ya kupewa siri jinsi ya kumhendo chidi..

"ukiwa na swali lingine juu ya mumeo niambie, ntakwambia tu mana staki kukuficha"

Yaani kwa muda mfupi tu Miriam na salma walijikuta wanapendana mno, yaani damu zao ziliendana sana…

"ila kuna swali natamani kukuliza"

Miriam alikuwa ana maswali mengi sana ya kumuuliza salma, mana salma kakulia kijijini afu pia kaishi Dar es Salaam mji wenye vijembe vitupu,…

"swali gani tena hilo mke mwenzangu"

"eti naomba uniambie maana ya kuku na mayai"

Kumbe Miriam lile jambo hakulimalizia pale, kumbe bado lilibaki moyoni mwake…

"hahahaha ina maana hujui maana ya kuku na mayai"

"hapana"

"mmmhhhhh mke mwenzangu pole sana kama ni wewe ndio umefanyiwa hivyo nakupa pole"

Miriam alizidi kuogopa zaidi huku akiwa makini kusikiliza jibu lake

"kwani ina maana gani, niambie basi wifi yangu"

"skia… Maana ya kuku na mayai… Ina maanisha hivi, ni mwanaume aliofanya mapenzi na mama pamoja na mtoto wake, hio ndio maana ya kula kuku na mayai yake"

"mungu wangu weeeeeeeee, siamini macho yangu mimi Uuuuuuuwwwiiiiiiiii"

Hali ya Miriam ilianza kubadilika ghafla na kukunja sura..

"pole wifi yangu"

Wakati huo kijana chidi wanamaliza kuchagua suti kali mana kwenye harusi kaka mtu anatakiwa kupendeza kwenye harusi ya mdogo wake,… Na huku kwa akina miriam nao walishamaliza japo walikuwa wanaulizana maswali mengi juu ya chidi….. Wanakutana kwenye gari lakini miriam alikuwa hana raha tena, chidi alijua tu miriam hakuwa na raha kwa wakati huo,… Basi waliwasha gari mpaka nyumbani kwa akina miriam na kumtambulisha Ibrahim kuwa huyo ni kaka yake mkubwa, familia ya akina miriam ilifurahi sana kuendelea kuijua familia ya upande wa pili… Kila kitu kilikwenda sawa mipango yote ilikaa sawa…

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni