MUUZA CHIPS (101) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 26 Aprili 2024

MUUZA CHIPS (101)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA MIA NA MOJA
ILIPOISHIA...
Wanakutana kwenye gari lakini miriam alikuwa hana raha tena, chidi alijua tu miriam hakuwa na raha kwa wakati huo,… Basi waliwasha gari mpaka nyumbani kwa akina miriam na kumtambulisha Ibrahim kuwa huyo ni kaka yake mkubwa, familia ya akina miriam ilifurahi sana kuendelea kuijua familia ya upande wa pili… Kila kitu kilikwenda sawa mipango yote ilikaa sawa…

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
BAADA YA SIKU HIO KUPITA

Na leo ni siku nyingine tena, wakiwa katika jengo la kitajiri la akina miriam, leo katika jengo hilo kulikuwa kama stendi vile mana kulikuwa na mabasi yasiopungua kumi, na gari ndogo za private zilikuwa nyingi sana.. Mabasi yenyewe yamejaa watu mpaka wengine wamekosa nafasi,… Kaka wa chidi na mke wake ambaye ni salma walikuwa wamevalia vizuri sana, tena mke wa Ibrahim ndio alikuwa mtu wa karibu wa miriam

( Best Woman ).. Wakati chidi bado hajulikani wake atakuwa nani, na hapo ni safari tu ila harusi bado… Na hio nafasi ya Best Woman ilikuwa inamuhusu Sarah peke yake, lakini sarah na miriam kwa sasa ni simba na chuo na hakuna anayemtamani mwenzie hata kama wametoka mbali,

"mama.. Naomba usiwape kadi za mualiko mama sarah na mtoto wake, sitaki wafike kwenye harusi yangu"

Aliongea miriam baada ya kujua kuwa kuku na mayai maana yake ni kwamba, Sarah na mama yake wamehusika kumharibu mpenzi wake

"miri, unaongea nini mwanangu, mama sarah si mama yako yule sasa kwanini asije kwenye harusi"

"sitaki tu, yaani sitaki"

"ivi una mashetani wewe"

"mama yaani sarah ndio sitaki kumuona kabisa yaani hata kuisikia sauti yake sitaki"

Miriam aliongea hivyo huku hasira zikimtawala,..

"miriam mwanangu, sarah hana makosa, na mimi ndio niliomtuma sarah avishwe pete ili nione wewe utafanyaje"

Heeeeeeee kumbe ile pete aliovalishwa sarah kumbe mama miriam ndio alimtuma sarah…. Sasa mama anakumbuka siku anaongea na sarah ilikuwa hivi

"Haloo sarah… Sasa skia ukishamtoa huyo kijana kule sero, hakikisha unatumia njia yeyote hata kama ni pesa yeyote mpe ili akubali akuvishe pete, alafu piga picha ukiwa unavishwa pete kisha mtumie miriam hizo picha"

"kwanini mama nifanye hivyo"

"nataka nijue kama miriam anampenda chidi au inakuwa vipi.. Kikubwa nataka nichuje wanapendana kweli au wanadanganyana"

"mmmhh sawa mama nitafanya hivyo"

"ok.. Ngoja nikutumie milioni moja ili ukanunue pete afu pesa nyingine umhonge mpaka akubali"

"sawa mama nitafanya hivyo"

Sasa simu ilipokana sarah alicheka sana, mana ni sawa na mbuzi kufia kwa muuza supu,.. Mama miriam hakujua kama sarah na chidi wana mahusiano, hivyo sarah kufanya vile ni kutimiza lengo la mama miriam, lakini binafsi yeye kama yeye, alifanya kweli tofauti na mama miriam alivyotaka kumchanganya mtoto wake… Sarah alifurahi sana kwa kukumbushwa ishu kama hio mana ilikuwa haipo kwenye akili yake,

"sasa kama yeye anataka iwe hivyo, sasa mimi nataka miriam aje aone live ninavyovishwa pete na mpenzi wake, na sifanyi utani kama mama yake anavyotaka"

Aliongea Sarah huku akiitafuta namba ya miriam na kumpigia, miriam alikubali kuja kwenye kuvishana huko, lakini kama unakumbuka chidi alikwenda kumtibua miriam kwa kumrudihsia kadi yake, hivyo miriam akakasirika sana na kushindwa kwenda kwenye pete ya rafiki yake….

Lakini sarah hakuishia hapo,.. Kama unakumbuka kuna siku miriam alizimia ofisini kwa mama yake kisa ni picha zilizotumwa na sarah ambazo chidi alikuwa akimvisha sarah pete… Lakini miriam akiwa kazimia pale chini mama sarah aliiwahi ile simu na kuona picha ya sarah akiwa na chidi, ndipo ile simu ikajiweka lock ikiwa mkononi kwa mama sarah.. Afu mama sarah akaanza kucheka na kutikisa kichwa kichwa kuashiria kweli miriam alikuwa akimpenda chidi.. Ila sasa mama miriam alifanya kama mchezo wa kumchezea mtoto wake, bila kujua kuwa sarah alikuwa ni mpenzi wake wa kweli, hivyo sarah hakufanya mchezo mchezo kama alivyotaka mama miriam….. Mama anamaliza kukumbuka, miriam analia

"mama ina maana kumbe ulitaka nigombane na rafiki yangu bure tu"

"sikuwa na maana hio mwanangu nilitaka nijue kama kweli mnapendana na kijana wako"

Miriam hata yeye hajui vizuri uhusiano wa chidi na sarah, bali alipoona zile picha ndio akajua sarah na chidi wana uhusiano….

Miriam alitoa simu yake na kumpigia sarah, sarah aliifutaga namba ya rafiki yake, lakini anaijua kwa kichwa

"haloo wewe nani"

Sarah aliuliza lakini anajua kabisa ni miriam

"sarah shost yangu, nisamehe best yangu,.. Sikujua kama mama ndio alikuwambia uvishwe pete na chidi wangu"

Sasa Sarah ni mschana wa akili mingi kama mama yake,.. Aliona bora akubaliane nae ili akaharibu huko huko kijijini.. Hivyo sarah alikubali,.. Kumsamehe miriam, lakini ana lake moyoni

"usijali shost, hata mimi nilishangaa sana kwanini iwe hivyo"

"sarah kipenzi changu, naomba uje twende please nakuomba sana"

"sawa nakuja twende"

Best Man wa chidi alikuwa ni Saidi..

"sasa broo, itabidi wewe uyatangulie haya mabasi mana hawajui nyumbani"

Chidi alimwambia kaka yake kuwa yeye ndio aongoze msafara wa hayo mabasi mana madereva wa hayo mabasi hawajui nyumbani kwa akina chidi,…

Safari ilianza kwa shangwe za hali ya juu sana huku vigelegele vikilindima kwenye magari,… Mama miriam akiwa sambamba na mama sarah katika msafara huo… Mabasi ndio yalikuwa magari ya kwanza yakiongozwa na gari alilokuwa akiendesha Ibrahim… Tena Ibrahim alibeba watu kadhaa ambao walivalia suti ila hatukuwajua ni akina nani.. Baada ya mabasi gari iliofuata ni gari ya bwana harusi na bibi harusi, dereva akiwa mbele na best man.. Na best woman nae alikuwepo katika gari hio,.. Hivyo kwa ujumla walikuwa watu kama watano hivi katika gari la mabwana harusi, gari liliofata lilikuwa ni gari ya mama sarah akiwa na rafiki zake, gari iliofata ni gari ya sarah, nae alikuwa na baadhi ya rafiki zake… Hivyo kulikuwa na gari ndogo kama tano hivi ukijumlisha na ile ya Ibrahim kule mbele……..

Vijiji, Miji, Mikoa ilipitwa na kilometa nyingi walitembea, na sasa walikuwa wamebakiza kama kilometa 1 hivi wafike nyumbani kwa akina chidi ambako ndoa ndipo inapofungiwa,.. Lakini chidi kuangalia mbele alishangaa kuona gari ya Ibrahim inarudi tena kwa spidi kali mno,.. Yaani ilikuwa inarudi kana kwamba yeye keshafika, mana si alikuwa wa kwanza kwa kuongoza mabasi.. Sasa alikuwa akirudi na haikujulikana mabasai kayaacha wapi, mana yaliwapita na kutangulia kabisa.. Ibrahim alishika breki mbele ya gari la bwana harusi na bibi harusi… Kisha akashuka na kuwafata akina chidi…

"nini tena broo"

Chidi alimuuliza kaka yake kuna nini mbona karudi

"chidi mdogo wangu… Ni aibu tupu, yaani hakufai kwenda huko"

"kuna nini sasa si useme"

"huezi amini familia yetu haipo, na pale tulipokuwa tunaishi na wazazi wetu pameuzwa na sasa ni mali ya tajiri mmoja aliokuja kuwekeza pale, hivyo hata ile nyumba yetu haipo tena, sijui baba na mama watakuwa wapi"

Ibrahim ana zaidi ya miaka 7 toka atike nyumbani, yaani hata wazazi hajui wanaishi vipi, pesa yenyewe alikuwa hatumi, sasa leo mdogo wake kamsomba kwenda kwenye harusi yake, hivyo Ibrahim kakutana na utofauti wa hali ya juu, yaani kakuta jumba la kifahari ambalo kwa hapo tanga nzima kuacha mjini,.. Basi hukuja jengo kama hilo,..

Sasa Ibrahim alikuwa akiyaongoza mabasi kwasababu madereva wa mabasi hayo hawajui nyumbani kwa akina chidi…

Sasa chidi kumbe anajua kila kitu kuhusu hio nyumba…

Chidi anakumba siku ile anaongea na baba yake,… Ilikuwa hivi

"haloo baba"

"eeeh vipi mwanangu.. Nimeshawapata wale watu"

"baba una uhakika wanaweza hao"

"ndio nimekwenda kuwachukuwa tanga mjini… Yaani ni mafundi wale professional"

"ok.. Sasa kuituma hii pesa itasumbua sana, wacha nikuletee, pamoja na ramani ya nyumba"

"sawa baba wahi wahi"

"sawa mzee"

Kumbe chidi ile pesa yote aliokuwa anapewa na mama sarah, aliopewa na miriam, aliopewa na saida, aliopewa na jasmini… Yaani ni pesa nyingi sana kama milioni 250, afu pesa yote akaipeleka kijijini na kutafuta mafundi professional,.. Kisha nyumba ikajengwa,.. Hivyo nyumba hio imegharimu kiasi cha shilingi milioni 200,… Kwa kule kijijini ni jumba la kifalme, lakini kwa huku mjini milioni 200 ni nyumba ya kifahari ya kawaida tu, na sio nyumba ya kushangaza sana, lakini kule kijijini ni jumba moja kubwa kuliko, mana kijijini vitu vingi sio ghali kama mjini, hivyo nyimba ni kubwa mno,… Na ukubwa wa jumba hilo kama ni mjini basi huenda ingegharimu bilioni moja na pointi, kama lingejengewa mjini.. Lakini kwakuwa ni kijijini basi imegharimu shilingi milioni 200,…

Chidi anamaliza kukumbuka huku anacheka

"sasa unacheka nini chidi,… Tugeuze msafara, tudanganye kitu chochote chidi, ni aibu"

Miriam pia hajui kitu kuhusu nyumba hio

"lakini babuu, kwanini usingejenga hata kijumba kidogo"

Chidi alikuwa anacheka tu huku akifuraha mana anajua kuwa jumba hilo ndio jumba lao… Na hata kule mjini alijifanya kwao nyumba mbovu lakini alikuwa anatuzuga tu…

"kaka Ibrahim, ingiza gari kwenye hio nyumba"

"sasa nitaingizaje kwenye mjumba wa watu, ivi we umeuona huo mjumba ulivyo.. Sio wa mchezo mchezo chidi"

"hio ni nyumba yetu, kaongoze msafara bwana"

Ibrahim haamini kwa kile anachokiongea chidi,.. Na hata Ibrahim kwa maisha alioishi kwa muda mfupi yale ya kitajiri, angeweza kujenga, lakini kwakuwa alikuwa ni mtu wa wanawake basi alishindwa kuitunza familia yake,.. Mpaka mdogo wake tena wa mwisho ndio kaja kufanya mambo makubwa kiasi hiki… Ibrahim mpaka alilia sasa sijui ni kwa furaha au ni kwa uchungu….

Basi msafara uliendelea kwenda huku akina mama sarah na mama miriam wakifuata nyuma na magari yao ya kifahari,…

Tukija huku arusha kwa akina sabra na dada yake walionekana kupaki vitu katika mgari ili waweze kurudi kwao ambako ni hapo hapo arusha lakini ni katika kamji kengine wanachokaita USA,… Kafara la mtoto wake lilifeli baada ya sabra kuharibu masharti ya kutembea na chidi na wakati dada yake alishatembea nae, hilo ni moja ya masharti waliopewa,

Lakini jasmini kila akimuangalia mdogo wake, yaani haamini kama ndio kafelisha huo mpango,.. Maskini kitoto cha watu cha chidi kimeuawa bila hatia kiasa ni mali za kishetani.. Na hapo wanahamia nyumbani kwao na kama endapo watapata mtoto wanaweza kurudi arusha mjini na kuweza kuurudisha utajiri wao, ila ni kitu kinachohitaji moyo…

Sasa tukija huku kwa akina saida wakati kawekwa chini na wazazi wake ili aseme hio mimba ni ya nani mana yapata miezi mitatu na wiki kadhaa,

"saida mwanangu, sisi hatuna nia mbaya na wewe, tunataka tujue huyo kijana ni nani"

Aliongea mama yake saida huku akimwomba mtoto wake aseme kijana mwenye hio mimba…

"na usiposema uhame nyumbani kwangu, pumbavu wewe"

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni