USALITI WA KIAPO (14)

0
Mwandishi: NNea Makala

SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
Tony hakuwa na wasiwasi juu ya hiyo hali alijua labda mpenzi wake amebanwa na masomo lakini kila akifikiria kuhusu siku za awali mambo hayakuwa kama yalivyokuwa sasa, Walizoea kujuliana hali walau mara mbili kwa siku lakini sasa Martha amebadilika mno.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
“Tony una nini mdogo wangu, mbona umenyongea kiasi iko”

“Dada mie hata sielewi yaani, unajua sasa ni muda mrefu sana sijawasiliana na Martha”

“Mhmh! Umejaribu kumpigia hapatikani?”

“Sio hapatikani dada yaani kila nikipiga simu haipokelewi na hata nikimtumia meseji hajibu, nashindwa kuelewa ana shida gani?”

“Hauna namba za mtu anayesoma nae umuulize”

Kauli iyo ya dada ikampa Tony tumaini jipya akakumbuka jinsi alivyokuwa akiongea na kuchati na marafiki zake Martha ambao wanasoma chuo kimoja, akatabasamu kisha akamwambia dada yake,

“Nina namba za rafiki zake nitawatafuta niwaulize”

“Sawa mdogo wangu fanya ivyo”

Baada ya mazumgumzo hayo, Tony akaingia chumbani akajilaza kitandani akachukua simu yake na kuingia mtandaoni, kwa bahati nzuri akakuta Martha yupo online bila kuchelewa Tony akatuma meseji lakini hakujibiwa ikabidi atume tena na tena lakini meseji zikawa zinasomwa tuu majibu asipate. Hali iyo ikamtesa sana Tony asielewe nini kimemkuta mpenzi wake, akaamua amtafute mmoja kati ya rafiki zake amuulize kulikoni, majibu aliyoyapata ama kwa hakika yaliuvunja moyo wake.

“Samahani Tony kwa haya nitakayokwambia, kiukweli hata sisi tunaumia ila hatuna jinsi ni maamuzi yake, Martha kwa sasa yupo kwenye uhusiano mpya na kila tunapoongea kuhusu wewe, mwenzetu hataki kutuelewa”.

Tony alijikuta akiangalia meseji aliyotumiwa na mmoja kati ya marafiki wa Martha, akutaka kuamini hilo akakumbuka ahadi na kiapo walichopeana, akajikuta chozi likimtoka.

“Aneth naomba unisaidie kitu”

“Sema tuu Tony”

“Naomba fanya kila uwezalo niongee na Martha”

“Sawa nitajitahidi kwa hilo”

Baada ya maongezi mafupi na Aneth ambaye wanasoma chuo kimoja na Martha, Tony akashusha pumzi ndefu huku nafsi yake ikikaangika, hakutaka kuamini hata chembe kile ambacho Aneth amekisema. Akaamua aingie Facebook ili achunguze walau picha za Martha cha ajabu akakuta ameblokiwa hivyo hawezi kuona chochote, wazo la kuingia instagram likamjia alipoingia napo akakuta vile vile ameblokiwa, roho ilimuuma mno taratibu akaanza kusadiki yale maneno aliyoambiwa na Aneth.

“Kwanini uliuteka moyo wangu hili hali ulijua utakuja kuumiza, kwa nini ulinitega nikategeka ilihali ukupanga kudumu nami….”

Tony akajikuta anachukua kipande cha karatasi na kuandika maneno hayo.

Martha ni mmoja kati ya wasichana wa kiafrika, waliokuwa na mvuto usiokuwa na kifani katika chuo kikuu cha Selou nchini Korea kusini.Uzuri wake uliwavutia wengi si wanaume pekee ata wasichana wenzake walipenda kuwa karibu nae.Wavulana wengi toka mataifa mbali mbali walijaribu kurusha ndoano zao hili waone endapo kama wataweza kuuteka moyo wa binti huyo lakini yeye alijua vyema kilichompeleka katika nchi hiyo ya kigeni ni masomo na si mambo mengine, hata hivyo tayari moyoni mwake kuna mtu amevuta kiti na kukaa hivyo haikuwa rahisi kwake kumkubali mwanaume yeyote tofauti na Tony.

Uwezo wake darasani ulimfanya azidi kuwa maarufu chuoni hapo, kila mmoja alikubali kuwa yeye ni msichana mwenye kipawa cha pekee, hakupewa uzuri tuu hata akili zilikuwemo, pamoja na hayo yote hakuweza kumsahau barafu wa moyo wake ambaye kwa wakati huo alijua kua amemuacha katika wakati mgumu, akawa anajitahidi kuwasiliana nae karibu mara mbili au tatu kwa siku.

Ucheshi na ukarimu wake ulimfanya awe na marafiki wa kila haina, hakubagua aliongea na kucheka na kila mmoja. Kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo thamani ya mrembo huyo ilivyozidi kupanda katika kipindi iko cha masomo, akajikuta akipewa mkataba mnono na wa malipo mengi katika kampuni moja inayojihusisha na maswala ya mitindo na matangazo (Tae Xhian Sung Group).

Ndani ya kipindi kifupi akawa ni mwafrika wa kwanza kutikisa korea pamoja na ukanda wote wa Asia. Siku moja Tae Xhian Sung Group ikaandaa sherehe ambayo ikapangwa kufanyika katika visiwa vya Jeju.Hivyo wahusika wote wakaambiwa wawe tayari, wakati safari ya kutoka Selou hadi Jeju inaanza Martha yeye alikuwa kwenye mitihani, hakuweza kuungana na wenzie kwa wakati, lakini kampuni haikutaka kumkosa katika sherehe iyo hivyo ikamuacha nyuma kijana mmoja mtanashati hasa na mwenye muonekano maridhawa aliyetambulika kwa jina la Kim Chang Lee. Kijana huyu yeye anaasili ya Kikorea na anafanya kazi katika kampuni hiyo kama mwanamitindo pia. Kim Chang Lee alipewa jukumu la kuhakikisha Martha anafika Jeju bila shida yeyote.

“Daah! They did well to left me behind, (wamefanya vizuri kuniacha mimi)”.

Kim Chang Lee akajikuta akitamka punde tuu alipomuona Martha, kwa hakika hakujutia kuachwa nyuma na mrembo yule. Martha akamtazama Kim na akatabasamu,

“I like the way you smile, (napenda jinsi unavyotabasamu)”

“I think it’s my first to see you, my name is Martha, (nadhani ni mara ya kwanza kukuona, mimi naitwa Martha)”

“No need for introduction, I know almost each and everything about you! My name is Kim Chang Lee, am working at Tae Xhiang Sung Group as the Fashionist, so am your work mate, let’s keep intouch, (haina haja ya kujitambulisha najua kila kitu kuhusu wewe, mimi naitwa Kim Chang Lee ni mwanamitindo, tutakuwa pamoja katika kazi, ivyoo tuanze kuzoeana”.

Martha akacheka na tayari safari ya kwenda visiwa vya Jeju ikaanza, Kim akawa muongeaji sana karibu njia nzima yeye tuu akawa anaongea huku akijaribu kuiteka akili ya mrembo yule, kwa kiasi flani alifanikiwa maana wakajikuta wakiwa marafiki ndani ya kipindi kifupi.

Safari ilitia nanga hatimae wakajikuta wametua katika uwanja wa kimataifa wa ndege katika visiwa maarufu kwa utalii nchini korea (Jeju). Moja kwa moja walienda kwenye hotel ambako huko ndiko sherehe nzima iliandaliwa.

“Ladies and gentlemen, I would like to take this opportunity to welcome our honorable Model from Selou University, Miss Martha, applause for her please, (Mabibi na Mabwana, napenda kuchukua nafasi hii kumkaribisha mwanamitindo wetu toka Chuo Kikuu cha Selou, Martha makofi kwake tafadhali”

Yalikuwa maneno ya mshehereshaji wa siku iyo akimkaribisha Martha kwa ajili ya kusema chochote.

“Good evening everyone! (habari ya jioni!)”

Salamu ile ya Martha iliwapa nafasi watu wengi kumtazama mrembo yule kwa umakini, mwanga hafifu uliokuwapo sehemu ile ulifanya ngozi ya mwanadada huyo kung’aa mithili ya mshumaa. Kim akabaki kuduwazwa na uzuri wa msichana yule, hakuwa anasikiliza nini kinachoongelewa hadi pale aliposhituka kuona watu wakipiga makofi nae akaungana nao. Kim akajiapiza kuwa ni lazima ampate mrembo yule kwa gharama yeyote. Akamgeukia rafiki yake aliye kaa karibu na kumuuliza,

“Did you know anything about that girl? (Unajua lolote kuhusu msichana yule?)”

“I don’t get you! (Sijaelewa swali lako)”

“I want to know the man whom in love with, (naitaji kumfahamu mwanaume anayempenda)”

Swali lile lilimfanya jamaa acheke sana nusu ya kuanguka, Kim akamtazama jamaa kwa mshangao kisha akaendelea kusema;

“Why are you laughing? That girl capture my heart within this short period of time, (mboni unacheka msichana huyu ameuteka moyo wangu kwa kipindi hiki kifupi)”.

“That girl is not cheap as you think, She reject all my friends, (Msichana sio mrahisi kama ufikiliavyo, rafiki zangu wote wamekataliwa)”.

“So none succesed to have her? (Kwa hiyo hamna aliyefanikiwa kumpata?)”.

“Exactly! But they said she has a man of of her destiny, (Ndiyo! Ila inasemekana ana mwanaume wa maisha yake)”.

“Where is he? (Yuko wapi?)”

“He is from her mother Country Tanzania, (yupo nchini kwao Tanzania)”

“It’s too far from here! And I assure you, that woman will be mine within two weeks, (ni mbali sana toka hapa na nakuhakikishia ndani ya wiki mbili atakuwa wangu)”.

“All the best broo! (Kila la kheri kaka)”

“Thanks! The game started now, (Akhsante! Mchezo ndio unaanza sasa)” alisema Kim Chang Lee.

Sherehe iliendelea kila mmoja aliburudika na kufurahi sana, wakati wa kucheza muziki Kim akaona Martha akiwa sehemu ya peke yake, akajisogeza. Martha bila kinyongo akamkalibisha na wakaanza kuzungumza. Wakati wakiendelea kuzungumza wakawa wanapata burudani toka kwa mwanamuziki maarufu nchini Korea ambaye alialikwa kutumbuiza siku hiyo. Mwanamuziki huyo aliimba nyimbo za taratibu zilizowafanya watu wacheze bila kutoa jasho. Kim akaamua kutumia huo kumchombeza Martha,

“Mwanaume yeyote atakayekukalibia wewe atajihesabia kuwa ni mwenye bahati katika siku zote za maisha yake,” alisema Kim Chang Lee.

“Oooh! I thought you do not know how to speak Swahili, (Ooh! Nilidhani kuwa hujui kuzungumza Kiswahili),” alisema Martha.

“am fluently on it, (nakijua vizuri tu)”.

“Congrats! (Hongera)”.

“Thanks! (Akhsante)”

“Your welcome”.

“Ukweli wewe ni msichana mrembo sana, katika maisha yangu yote ya korea sijapata kuona wa kufanana nawe”

“Mhmh! Asante kwa hilo”

“Martha, can we be friends? (Martha, Je twaweza kuwa marafiki?)”.

“Ofcourse Kim, why not? (Bila shaka Kim)”.

Huo ndio ukawa mwanzo wa ukaribu kati ya Kim na Martha, Kim alijitahidi kufanya vitu vingi kwa mrembo yule kuhakikisha anateka akili yake. Kwa kiasi kikubwa alifanikiwa, Martha akapunguza mawasiliano na Tony. Kim alichipusha hisia za penzi jipya kwa Martha, wengi waliwapongeza wawili hao kuwa pamoja. Umaarufu wao uliongezeka maradufu, kiasi cha kuweka maisha yao ya kila siku mitandaoni, hii ikawaongezea watu wengi waliofata. Martha alijua wazi kuwa Tony asingeweza kuvumilia hali ile, hakutamani aone kinachoendelea ikabidi azuie kuonekana kwenye akaunti za Tony.

Mambo yakazidi kwenda kombo kwa Tony, ambaye alijikuta akishindwa kumakinika katika shughuli zake, alimpenda sana Martha lakini hayo yanayotokea sasa alishindwa kuelewa nini hatima yake. Hakutaka kusadiki yale aliyoyasikia kwa rafiki wa Martha kuwa yupo kwenye penzi jipya, aliamini kuwa hayo ni maneno yanayolenga kuvunja Imani yake kwa Martha. Jioni moja Yassir na Darmy wakamzuru Tony kwa minajili ya kumjulia hali, walimuhurumia sana swahiba wao huyo ambaye muda mwingi tabasamu lilikuwa likichanua usoni mwake,

“Kuwa mvumilivu kaka, sisi tunaamini Martha anakupenda labda anabanwa sana na masomo,” alisema Yassir.

“Kubanwa huko na masomo ndio hadi kuzuia nisimuone katika mitandao ya kijamii,” alisema Tony.

Hapo wazo jipya likaja vichwani mwao, Darmy na Yassir wakatoa simu zao na kuingia facebook, kisha wakatafuta jina la Martha cha ajabu Zaidi nao wakakuta wamezuiwa wasiweze kuona chochote katika akaunti ya Martha.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)