USALITI WA KIAPO (15)

0
Mwandishi: Nea Makala

SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA...
Hapo wazo jipya likaja vichwani mwao, Darmy na Yassir wakatoa simu zao na kuingia facebook, kisha wakatafuta jina la Martha cha ajabu Zaidi nao wakakuta wamezuiwa wasiweze kuona chochote katika akaunti ya Martha.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Daah! Ebhana eenh! Hadi sisi ametuzuia,” alisema Darmy.

“Ngoja tujiridhishe, nafungua akaunti mpya ya muda hili tuweze kuona,” alisema Yassir.

Akatumia kama dakika 10 kufungua akaunti mpya ya facebook na bila kupoteza muda wakatafuta jina la Martha, kwa bahati nzuri wakaliona. Wakaanza kuangalia picha moja baada ya nyingine. Tony akajikuta akishindwa kuvumilia yale aliyokuwa akiyashuhudia, mapigo ya moyo yakaenda kwa kasi mno, machozi yakatengeneza mifereji kwenye mashavu yake.

“Daah! Kweli hapa kuna ulazima wa kumtafuta Martha na kumuuliza kulikoni,” alisema Darmy.

“Yeah ni kweli bora tufanye hivyo mapema!” Yassir akaitika.

Muda wote huo Tony hakujiweza kwa lolote, Machozi ndiyo yakawa rafiki yake, Maumivu aliyoyasikia alishindwa kuyafananisha na maumivu yeyote katika dunia hii. Akaanza kujenga urafiki mpya na pombe, rafiki zake walifanya juhudi kubwa kumzuia lakini haikufaa kitu.

Jumapili moja baada ya Tony kutoka kanisani rafiki zake wakaamua wampeleke katika moja kati ya fukwe maarufu jijini Dar es Salaam, walau akatulize akili yake. Mambo hayakuwa hivyo kama wao walivyodhani kwani ni katika siku hiyo Martha aliamua kumuandikia ujumbe mzito Tony,

“Naomba unisamehe kwa haya nitakayokwambia, ukweli nimeshindwa kuitunza ahadi tuliyopeana, kwa sasa nina mpenzi mpya na nafikiri kuwa naye katika siku zote za maisha yangu. Sina hisia zozote zilizobaki juu yako, naomba unisahau ikiwezekana utafute mwanamke atayekufaa kwenye maisha yako. Najua nimekosa ila ndiyo hivyo imeshatokea”

Tony alihisi kuzirai alipousoma ujumbe ule, haikuwa rahisi kwake yeye kusadiki maneno yale, akarudia tena na tena lakini maneno yakabaki vile vile. Tony akajikuta akicheka mno, alicheka mpaka akagalagala huku machozi yakimtoka. Hali iyo ikawaogofya sana maswahiba zake wakahisi labda Tony anaweza kuwa amepata tatizo la akili, Tony akaanza kukimbia kwa kasi huku akicheka. Darmy na Yassir wakapata kazi mpya ya kumfukuzia hili wamkamate, Tony akawa na nguvu ya ajabu siku hiyo, rafiki zake wakajitahidi kumshika na kumtuliza,

“Mwanamke ninayempenda anampenda mwanaume mwingine, niambieni je kuna umuhimu wowote wa mimi kubaki katika dunia hii?” aliuliza Tony huku akilia.

“Tony wewe ni mtoto wa kiume tulia kwanza!” alisema Darmy.

“Niliposoma riwaya ya UKO WAPI, nilicheka sana kuona Nelly anamlilia Patricia, sikuwa najua maumivu yake lakini leo nimejua na sidhani naweza kuwa kama yeye,” alisema Tony.

“Kwa sasa kila utakalolifanya ni sawa na bure, turudi kwanza nyumbani utulize akili,” alisema Yassir.

Tony akawa kama nusu chizi, kuna wakati Alilia na kucheka kwa pamoja, hali ile ilimuumiza sana dada yake, ambaye hata yeye hakuamini kama Martha angebadirika kiasi kile. Dada aliamua kujiridhisha kwa kutaka kuongea naye yeye mwenyewe, akatafuta mawasiliano ya Martha na kupiga simu. Simu iliita kwa muda na baada ya muda ikapokelewa,

“Hallo! Are you Martha? (Hallo! Je wewe ni Martha?)”

“Yes! Who are you? (Ndio nani mwenzangu?)”

“Mimi ni dada yake na Tony”.

Martha aliposikia hivyo akakata simu, hakutaka kuongea lolote na dada huyo. Rozina akafikiri juu ya hatua ile aliyoichukua Martha, akapata majibu kuwa uhenda ni kweli mapenzi kwa mdogo wake yameisha. Wakati akiendelea kufikiri hayo ujumbe mfupi ukaingia katika simu yake,

“Samahani sana sina ujasiri wa kuongea nawe na hata hivyo siwezi kubadili msimamo wangu, kila kitu nimeshamuambia Tony, hivyo tafadhali naomba mniache”.

Dada alizidi kuchanganyikiwa aliposoma ujumbe ule hakuwa na haja ya kumficha mdogo wake, akamuonesha ingawa alijua ni wazi utamzidishia maumivu. Tony hakuongea lolote Zaidi ya kuendelea kufakamia pombe iliyopo kwenye bilauri.

“Mdogo haukuzaliwa kuwa dhaifu, inuka sasa haya ni majaribu na hutokea katika maisha ivyo pambana mdogo wangu,”

“Kwanini aliuteka moyo ilihali alijua kuwa atakuja kuumiza, kwanini alinitega nikategeka wakati hakupanga kudumu name, aliufunza moyo wangu kudunda nami nikajifunza kuvumilia kila gumu, dada najihisi siwezi tena bila ya yeye,” alisema Tony.

Maisha ya Tony yakabadirika sana toka kipindi hiko, akawa ni mtu wa kunywa pombe tuu kila kukicha, akaachana na maswala ya muziki kwani aliamini kufanya vile kungemsaidia kutoka kwenye kizungumkuti cha huba alichonacho kwa Martha.

Miaka miwili baadae, Tony akafungua kampuni ndogo iliyojihusisha na maswala ya video production, kampuni hiyo ilizidi kukua siku baada ya siku na kupata umaarufu mkubwa nchini. Kidogo alichokipata kutokana na kazi yake hiyo alikiongezea katika ununuzi wa vifaa vya kisasa. Falsafa yake mpya ikamfanya awe na staha kwenye matumizi ya mapesa. Toka aliposalitiwa na Martha hakuweka Imani yeyote juu ya mwanamke, hapo ndipo alipoanza uchakaramu, Tony hakuweza kuwa na penzi la dhati. Aliwatumia wasichana kukidhi haja zake na katu katika maisha yake hakuwahi kutamka neno nakupenda kwa kumaanisha. Kwa waliofahamu shida na dhahama alizopitia Tony hakuna aliyethubutu kunyanyua kinywa chake kusema kwa anakosea kuwa na uhusiano Zaidi ya msichana mmoja, japo ni kweli haikuwa sawa.

Mshauri wa kampuni alimaliza simulizi yake kwa kusema,

“Hayo ndiyo Tony aliyoyapitia na Martha anajua wazi alichofanya kuwa si sahihi na ndiyo maana anajaribu kutetea walau kulipa uovu alioufanya. Ninyi leo hii mnamuita Tony Malaya sijui hajatulia ila hamkujua nini amepitia, haya semeni sasa wangapi manta kuacha kazi eti kisa mkataba wa Tony”.

Wote wakakaa kimya na kujikuta wakimuangalia Martha kwa jicho baya, hawakuamini kama mrembo huyo angeweza kuwa mkatili. Wengi wakaelewa kwanini Martha alimtetea Tony mara zote alizojaribu kuzembea katika kazi. Jose akapata kufahamu kilichojificha nyuma ya pazia akakumbuka jinsi Martha alivyojipa shida ya kufanya kazi Zaidi na hata kufanya kazi za Tony. Alimuhurumia Martha kwani alijua ni wazi msichana yule bado anaumia kwa kile alichokifanya.

Swali likabaki kwa Martha kuwa huyo Kim Chang Lee bado wako katika mahusiano au la! Kama wameachana nini kilitokea na kama hawakuachana kwanini Martha aliamua kurudi Tanzania kufanya kazi. Hiyo ikabaki siri ya Martha mwenyewe ingawa wote walitamani kujua.

Ni mwezi wa 4 sasa toka Tony apate tatizo lile, Hali yake iliwakatisha tamaa sana, Mjomba alihangaika kadri alivyoweza lakini hakuweza kufanikiwa, alitumia pesa nyingi katika matibabu ya Tony. Mara ya mwisho kwenda hospitali wakaambiwa kuwa mguu ulishaaribika wote na sumu ilisambaa hadi usawa wa kiuno, hivyo ata kama watamkata mguu bado hawataweza kuzuia sumu kuendelea kushambulia sehemu nyingine za mwili.

Daktari akawaambia kuwa Tony anaweza kuishi walau kwa miezi mitano Zaidi ya hapo sumu itakuwa ishafika kwenye moyo na ndio utakuwa mwisho wa maisha yake.

Taarifa hiyo ikawafikia wafanyakazi wote, wengi walihuzunika kwa hilo Martha, akajihisi ni mkosaji Zaidi. Hakuelewa nini atakifanya endapo Tony atafariki, akaitisha kikao cha dharula kwa wafanyakazi wote.

“Nina wakati mgumu kwa sasa, nashindwa kumakinika katika kazi, hivyo naomba niache kampuni mikononi mwenu. Jose utakaimu nafasi yangu hadi pale mambo yatakapokaa sawa, naomba sana mzingatie kazi,” alisema Martha huku machozi yakimbubujika.

Wafanyakazi wote wakaa na kumsikiliza mkurugenzi wao huyo, simanzi ilikuwa kubwa mioyoni mwao. Kabla Martha hajaongea Zaidi akahisi kizunguzungu, kiza kikatawala macho yake na taratibu akaanguka chini. Jitihada za haraka zikafanyika kumuwahisha hospitali, baada ya dakika kadhaa daktari akatoka na kuwatazama Jose na Darmy,

“Nani ni mume wa binti huyu?”

Jose na Darmy wakatazamana wasijue nini la kujibu,

“Mbona mnashangaa au hamkuelewa nini nilichowauliza?”

“Daktari tuambie hali ya mgonjwa wetu,” akasema Jose.

“Ooh! Kumbe ni wewe! Hongera mkeo anaujauzito wa mapacha ambao huu ni mwezi wa 4 sasa!” alisema daktari huku akimpa mkono wa pongezi Jose.

Jose na Darmy wakaendelea kuduwazwa na habari ile, wakaingia chumba cha mapumziko ambacho Martha amelazwa.

“Atleast now I have a reason to live, (walau sasa nina sababu ya kuishi),” alisema Martha.

“Hongera! Tumesikia kila kitu toka kwa Daktari, sasa baba wa watoto hao yuko wapi?” akauliza Darmy.

Swali lile likamfanya Martha ashindwe kuzuia machozi yake kwa mara nyingine akajikuta akilia kama mtoto mdogo, Jose na Darmy wakafanya kazi kubwa kumbembeleza.

“Ni sawa tuu kama inakuwia ugumu kutuambia! Unauhuru huo pia,” alisema Darmy.

“Tony is the father of this kids, (Tony ndiye baba wa watoto hawa),” akasema Martha.

Darmy akahisi kama anaangalia tamthilia ya kifilipino, hakutaka kusadiki wala hakutaka kukataa kauli ya Martha. Jose alionekana kukubaliana na kile alichokisikia kwani alijua kila kitu kilichotokea kipindi walichokuwepo Tanga, hakuwa na shaka kwani ni kweli miezi 4 imepita toka watoke huko na ujauzito una umri huo.

“So it’s true that Tony is a biological father of those kids you conceive? (Kwa iyo ni kweli kuwa Tony ndiye baba halali wa watoto hao uliowabeba kwenye tumbo lako),” Darmy akauliza.

“Yeah! Its true, (ni kweli)”

Mbali na yote yaliyotokea Darmy alijawa na furaha sana kuona walau rafiki yake atapata warithi, japo mwenyewe hakuwa analifahamu hilo. Maandalizi ya kuelekea Mbeya yakakamilika Martha akaongoza na Darmy na Yassir, njia nzima Martha alijawa na hofu juu ya kipi atakachozungumza pindi akifika huko. Akakumbuka jinsi alivyoongea na dada yake Tony akajikuta nguvu zikimuisha,

“Usijali! Habari hizi zinaweza zikamfanya Tony atamani kuendelea kuishi, sizani kama atakufa na kuwaacha watoto wake nyuma bila malezi ya baba,” alisema Darmy.

“japo tunajua ni kiasi gani umemkosea rafiki yetu, ila sisi kinyongo hatuna kwa sasa tunataza hatima ya hao watoto walio tumboni mwako,” Yassir naye aliongea.

Kwa kiasi kikubwa Martha alianza kupata Amani ya moyo kwa kuona walau kuna watu walioweza kusamehe uovu wake na kuamua kuanza upya.

“Nitafurahi sana kama Tony atanisamehe, na wala sitohuzunika kama hatonisamehe sababu nastahili yote hayo,” aliongea Martha.

Maongezi yaliendelea huku wakiwa kwenye ndege inayoelekea jijini mbeya na saa chache baadaye wakafika na kuchukua usafiri mwingine wa kuelekea Tukuyu.

“Dada niahidi kuwa kuanzia leo hutolia tena,” alisema Tony.

“Hapana mdogo wangu siwezi, naumia sana ujue,” alijibu Rozina.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)