Mwandishi: Nea Makala
SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Dada niahidi kuwa kuanzia leo hutolia tena,” alisema Tony.
“Hapana mdogo wangu siwezi, naumia sana ujue,” alijibu Rozina.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
“Sasa dada kilio hiki hadi lini, mimi nimeshakubali kila kitu hata hivyo bado kitambo kidogo utasahau kila kitu kuhusu mimi, usilie dada,” alisema Tony kwa huzuni.
Rozina alishindwa kabisa kujizuia kila alipomtazama mdogo wake ambaye miezi michache iliyopita alikuwa ni mwanaume mwenye muonekano mzuri na mvuto wa aina yake, leo amelala, ngozi iliyong’aa imekuwa nyeusi kama kama mkaa. Mwili uliojaa leo umeisha mithiri ya muathirika wa ukimwi, hakika ilikuwa huzuni na pigo mno.
“Mdogo wangu hata wale wasichana zako wote hawaonekani!”
Tony alijikuta akicheka sana, hadi dada akamshangaa kwanini iwe vile, Tony akamtazama dada yake na kumwambia,
“wanahaki ya kufanya hivyo na walau wamepata mtu wa kuniadhibu kwa niaba yao, kwa niliyowafanyia kwa kweli acha waendelee na maisha yao,” alisema Tony.
Wakati wakiwa chini ya muembe na kuendelea na mazungumzo jioni hiyo ya saa 10, Rozina akawa wa kwanza kuwaona Darmy na Yassir alifurahi mno, hakuweza kumgundua Martha kwa haraka hadi pale walipofika karibu kabisa. Rozina akasimama tena kwa hasira sana,
“Umefata nini Martha! Au ndiyo umekuja kummalizia mdogo wangu?”
Martha hakuwa na la kujibu Zaidi ya kutoa tu machozi, Darmy na Yassir wakajalibu kumtuliza dada atulie hili wazungumze lakini dada hakukubali aliendelea kufoka na kumtaka Martha aondoke eneo hilo. Rozina hakutaka kuelewa wala kumsikia yeyote alimshushia lawama zote Martha, akadai kuwa hayo yote yaliyotokea kwa mdogo wake sababu ni yeye na wala hakuwa na umuhimu wa yeye kuja pale. Muda wote huo Tony hakusema lolote kwani naye alijua wazi kisa cha yeye kuwa vile ni Martha kama msichana huyo angetunza kiapo chake basi hakukuwa na namna yeyote ya Tony kukengeuka.
Baada ya mzozo wa muda mrefu mjomba akafika naye alishangaa sana kumuona Martha pale, wahenga wansema Jungu kuu siku zote alikosi ukoko. Mjomba akatumia ukubwa wake kumtuliza Rozina na kuwakaribisha wageni. Martha akasogea hadi alipo Tony na kuomba radhi huku akisindikizwa na machozi.
“Niko radhi kwa adhabu yeyote utakayonipa, sitojali ila kikubwa nahitaji msamaha toka kwako,” alisema Martha.
Rozina akamuangalia Martha kwa jicho la chuki mno hakutamani kumuona eneo lile.
“Sasa Martha kwanini ulimtenda mwenzako kiasi kile!, hadi kufika hatua ya kuharibu maisha yake kabisa,” Mjomba akauliza.
“Uncle! Nitawaambia kila kitu ila naomba nipumzike kidogo,” alisema Martha.
Mjomba akaridhia ombi lile, Rozina ikabidi aingie jikoni kuandaa chakula kwa ajili ya wageni. Darmy, Yassir na Martha wakabaki pale alipo Tony,
“Tumekumisi sana wa obey, inuka jamaa tukapige misele,” alisema Darmy.
“Ndiyo kama hivi nipo! Vipi Yassir mkeo hajambo,” alisema Tony.
“Yeah yuko poa sana! Salamu na pole nyingi toka kwake,” alijibu Yassir.
“Vipi Darmy na wewe jambo zako hazielewekagi au ndio mzee wa ngumu hiphop moja!” alisema Tony.
Kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu kupita wakajikuta wakicheka kwa pamoja. Muda wote huo Martha alikuwa ni mtu mwenye mawazo na huzuni nyingi,
“Martha binafsi nilishakusamehe siku nyingi, huna haja ya kuishi kwa majuto, kuwa huru na ufurahi na mwanume umpendaye, mimi mwisho wangu umekaribia. Bado miezi 5 tuu,” alisema Tony.
Martha akamsogelea Zaidi na kumkumbatia Tony huku akilia,
“Ni makosa yangu Tony samahani sana, ila sikuwa na jinsi kwa wakati ule.
“Basi usiseme kitu Martha usije pata homa bure,” alisema Yassir.
Hadi kufika hapo hakuna mtu aliyekuwa tayari kufichua siri ya ujauzito wa Martha, kwa kuwa hawakujua taarifa ile itapokelewa vipi kutokana na tofauti kubwa iliyotokea katika maisha ya wawili hao.
Muda ukasogea hatimaye giza likaingia, hakuna aliyeweza kukaa nje kutokana na baridi kuwa kali mno, wote wakaa sebuleni na kuendelea na mazungumzo.
“Nadhani ni wakati sahihi wa mimi kusema kile kilichonifanya hadi kuja hapa,” alisema Martha.
“Huna haja ya kusema, tushaelewa na tushakusamehe hivyo fanya tu uondoke,” alisema Rozina kwa hasira kidogo.
“Najua ni kiasi gani nimesababisha matatizo katika familia hii, nimemkosea Tony mwanaume aliyenipenda name ninampenda kuliko maelezo..”
“Wee! Koma! Ungekuwa unampenda ungemuacha,” Rozina akasema kabla ya Martha kumalizia sentensi yake.
“Rozina tulia basi tumsikilize,” alisema Mjomba.
Martha akakohoa kidogo kuweka koo lake sawa, kisha akamtazama kila mmoja usoni kwa zamu, alafu akaanza kusimulia..
Chuo kikuu cha Selou kinashikilia rekodi ya kuwa na mrembo wa vyuo vikuu nchini Korea aidha chuo kile ni moja kati ya vyuo vichache vinavyojali vipaji vya wanafunzi wake. Mimi nilienda kwa lengo la masomo tuu sikupanga kufanya lolote nje ya kusoma, lakini nilijikuta kuvutiwa kuwa mwanamitindo hasa baada ya marafiki zangu kufanya mambo hayo. Mashindano yaliandaliwa na nikaibuka mshindi mbele ya wenyeji, ushindi ule ukanipa mkataba mnono wa kufanya mambo ya mitindo katika kampuni moja maarufu nchini humo inayotambulika kwa jina la Tae Xhiang Sung Group.
Mambo yakabadirika baada ya mimi kuwa mshindi na pia kuanza kufanya kazi katika kampuni hiyo, mkataba ukanizuia mimi kuonekana na watu hovyo. Nikalazimika kufanya kila kitu change kwa usiri mkubwa mno. Ikatokea nikafahamiana na kijana mmoja aitwaye Kim Chang Lee, yeye huyu ni mwanamitindo wa kimataifa kwani kazi zake zilivuka mipaka ya asia na kusogea kabisa katika bara la ulaya na amerika. Akaniomba urafiki nami sikuona sababu ya kumkatalia sababu wote tulikuwa tunafanya kazi sehemu moja. Kijana yule alizidisha ukaribu sana upande wangu ikafika hatua ikabidi aeleze hisia zake waziwazi,
“Martha! I love you and I want you to be mine, (Martha nakupenda na nahitaji uwe wangu)” alisema Kim Chang Lee.
Kauli ile ilizua mshtuko sana kwangu, ukweli hata mimi nilimpenda lakini kama rafiki wa kawaida sikuwa na hisia zozote za kimapenzi juu yake. Mara zote alizoniambia hivyo nilimkataa na kumwambia kuwa nina mwanaume ambaye sifikirii kumpoteza.
Kim ikabidi aanze kufanya uchunguzi kupitia mtandao wake, na akamgundua Tony. Ukweli alinidhiaki sana na mwisho akaniambia,
“Usijali najua kuna mtu unampenda, hivyo sioni sababu ya mimi kuingilia kati mapenzi yenu, tuendelee kuwa marafiki wa kawaida”
Baada ya kuniambia hayo tukawa tunatembea sehemu nyingi na watu wengi wakajua kuwa wawili sisi ni wapenzi, tulipiga picha nyingi katika sehemu tofauti tofauti. Kuna siku ambayo siwezi nikaisahau katika maisha yangu, Kim alinialika sehemu Fulani akiwa na rafiki zake, nikaitikia wito na ndiyo siku hiyo iliyobadili kabisa muelekeo wa maisha yangu. Kim akishirikiana na rafiki zake waliniwekea madawa kwenye kinywaji nikawa sielewi wala kutambua lolote lilioendelea.
Nikaamka siku iliyofata na kujikuta nikiwa nyumbani kwangu, sababu sikuwa nahisi hosteli kampuni ilinipa nyumba ya kukaa. Sikuwaza chochote wala sikuona badiliko lolote katika mwili wangu Zaidi ya kichwa kuniuma mno. Niliendelea kulala kwa kuwa sikua na vipindi siku hiyo, nilishtushwa na ujumbe mfupi ulioingia kwenye simu yangu,
“Vipi mpenzi! Bila shaka uko poa, nataka nije niwe nawe siku ya leo”
Ulikuwa ujumbe kutoka kwa Kim, nilipousoma nikafikiri labda amekosea namba lakini nilivyomuuliza alisistiza kuwa aliukusudia kwangu. Nikashangaa sana, nikamkumbusha mipaka tuliyojiwekea kuwa sisi ni marafiki tuu na hamna cha ziada. Kim alicheka mno kisha akanambia,
“sizani kama utaweza kunikataa baada ya dakika 3 zijazo”
“hata Kama itakuwa mwezi ukweli siwezi kuwa nawe,” nilimjibu.
Baada ya dakika 2 nikapokea picha kwenye simu yangu, picha hizo zilionesha nikiwa kitandani na wanaume watatu, nguvu ziliniisha sana sikuelewa nini cha kufanya. Kim akatuma ujumbe mwingine,
“Muda mfupi dunia itatikisika kama utaendelea kunikataa, na huyo mpenzi wako unayelinga naye sizani kama atakuwa na mapenzi nawe tena,” alisema Kim.
Niliogopa sana, sikuwa na ujanja Zaidi ya kufata masharti yake, akanilazimisha niweke picha kwenye mitandao ya kijamii zilizoashiria kuwa mimi naye tupo kwenye mahusiano, kwa kuwa sikutaka kumuumiza Tony ikanilazimu nimzuie asione kinachoendelea. Haikuishia hapo nikalazimika kufanya mahojiano na vituo mbalimbali vya habari nchini Korea na kuelezea uhusiano wetu, ndani ya muda mfupi tukaongeza watu ambao wanatufata na kuziangalia kazi zetu. Nilijiona mkosaji sana sikuwa na ujasili wa kuwasiliana na Tony nikiwa katika hali ile, hapo nikalazimika nimtumie ujumbe wa kumtaka anisahau na awe katika mahusiano mapya.
Kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo nilivyozidi kuwa mtumwa kwa Kim, nililazimika kufanya vitu ambavyo sikuvipenda ila kutokana na yeye kushikiria mpini nami makali sikuwa na budi. Nikatafuta mtu ambaye alinishauri vizuri na kunitafutia mwanasheria, ambaye kwa pamoja tukatafuta ushahidi wa kumuweka Kim hatiani. Tulibahatika kupata vipande vya video vilivyorekodiwa na CCTV kamera zilizokuwa eneo la hotel na ilionesha kila kitu toka wakiniraghai na kuniwekea madawa, jinsi walivyonibeba na kunipeleka chumbani japo hatukuweza kupata picha juu ya kilichofanyika ndani ila walionekana wakitoka huku wakiwa na kamera. Hii ikaturahisishia kufungua mashtaka na Kim akapewa adhabu ya kulipa faini na kuhukumiwa miaka 10 jela kwa kosa la udhalilishaji. Hapo ndipo uhuru wangu ukarudi na kwa kipindi hiko nikawa nimeshahitimu masomo yangu. Nikashawishi kampuni kufungua tawi nchini Tanzania sababu sikupenda kabisa kubaki Korea, kampuni ikakubali ombi langu na kunipa mimi jukumu la kusimamia kila kitu. Hapo ndipo tukatoa nafasi kwa makampuni zawa kutuma maombi ya kuingia na kampuni yetu. Nilifurahi sana nilipoona Tony akiwa mmoja kati ya kampuni 50 zilizoomba, sikuwa na haja ya kuziangalia kampuni hizo nikaipitisha kampuni ya Tony huku nikiamini ni sehemu tuu ya kulipa uovu mabao naweza kusema niliufanya juu yake.
Hadi kufikia hapo kila mmoja alijikuta akilia na kumuhurumia Martha kwa yale aliyoyapitia, Rozina hakujizuia akamsogelea Martha na kumkumbatia,
“Nisamehe sana Martha, sikujua kama ulipitia magumu hayo,” alisema Rozina.
“Nisamehe pia,” Martha akasema.
USIKOSE SEHEMU IYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi