Mwandishi: Nea Makala
SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Nisamehe sana Martha, sikujua kama ulipitia magumu hayo,” alisema Rozina.
“Nisamehe pia,” Martha akasema.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
Tony akamuangalia Martha na kuangusha tena machozi, Martha akamsogelea na kumkumbatia kisha wote wakaungana kulia.
“Haya yote ni majaribu ambayo wawili ninyi mmepitia, hivyo yazikeni yaliyopita na kufikilia mapya,” alisema Mjomb.
“Tony, nilikupenda, nakupenda na nitaendelea kukupenda siku zote za maisha yangu,” alisema Martha.
“Martha nataka uishi maisha yako kwa furaha na Amani tele, mimi siwezi tena hapa unionavyo nimebakiza miezi 5 tuu,” alisema Tony.
“Hata kama ungebakiza siku 5 bado Tony siwezi kukuacha, nataka nifurahi nawe”
“Hapana siwezi kuruhusu hilo, Martha wewe ni msichana mrembo na unahitaji mwanaume mwenye nguvu na uwezo, katika hali yangu hii hapana sitoweza”
“Tony nami sitoweza kuwa na mwanaume mwingine tofauti nawewe”.
“Kwanini?”
Martha akafikiri kidogo kabla hajasema kile ambacho moyo wake umekusudia, kisha akawatazama Darmy na Yassir ambao walikaa kimya kwa muda mrefu kuacha wawili hao wazungumze. Darmy na Yassir wakatikisa kichwa kuashiria kuridhia lile ambalo Martha anahitaji kulisema.
“Tony! Tumboni kwangu kuna watoto wawili mmoja wakike na mwingine wakiume nawewe ndiye baba yao”
Taarifa hiyo ilimfanya Tony ainuke na kukaa kitako kama vile hakuwa anaugua na kwa muda mrefu hakuweza kunyanyuka mwenyewe Zaidi ya kubebwa kutokana na upande wake mmoja kupooza. Jambo ambalo lilimshangaza hata mjomba,
“Martha unasema kweli?”
“Ndiyo Tony! Usiku ule mmoja tuu ulitosha kufanya haya yote”
Tony akamkumbatia Martha, furaha ikalejea upya katika familia ile, Rozina alifurahi mno, mjomba, shangazi, Darmy na Yassir pia wote wakaungana kufurahia lile jambo.
“Eeh! Mungu naomba uniongezee muda kidogo niweze kuwaona watoto wangu,” alisema Tony.
“Hakuna lishindikanalo kwa Mungu naamini atatupa hitaji la nyoyo zetu”
Baada ya Siku kadhaa Darmy na Yassir wakarudi jijini Dar es salaam kuendelea na shughuli za kampuni. Martha hakutaka kwenda popote akatamani kuendelea kubaki na Tony wake,
“Tony nimeongea na mama amekubali mimi niendelee kukaa huku nawe, sababu nilishamueleza kila kitu,” alisema Martha.
Ilikuwa habari njema kwa Tony, wawili hao wakarudisha upendo upya, ingawa Tony alikuwa mgonjwa lakini alijitahidi kufanya kila aliloliweza kwa mpenzi wake. Siku moja Martha aliamua kwenda shambani na akiongozana na Rozina dada yake Tony,
“Wifi ungepumzika tuu,” alisema Rozina.
“Mhmh! Ni sehemu tu ya mazoezi wifi yangu, natamani sana watoto wazaliwe wakiwa na afya ndio maana najitahidi kufanya kila niliwezalo kuhakikisha naepuka magonjwa yasababishwao na uzembe au uvivu wa kutofanya mazoezi”.
Wakaendelea kutembea taratibu huku wakiongea hili na lile, wakafika sehemu yam to ambayo Martha aliikumbuka vizuri kuwa ndiyo sehemu ambayo kimbunga kikali kilitokea ile siku aliyokuja na Tony kwa mara ya kwanza. Martha akasogea karibu kabisa na mto ule, hapo hapo hali ya hewa ikabadirika ghafla, wingu zito likatanda na upepo mkali ukawa unapiga. Rozina akaogopa sana ile hali ikabidi arudi nyuma kwa haraka hadi alipo Martha,
“Hatuwezi kwenda shamba kwa hali kama hii, turudi usije nyeshewa na mvua,” alisema Rozina.
Martha hakupinga akainuka lakini wakajikuta wanashindwa kurudi walipotoka kutokana na upepo mkali kupiga na kusababisha baadhi ya matawi ya miti kuanguka,
“Sehemu iliyosalama kwa sasa ni hapa mtoni, tusubili kwa muda hadi upepo utakapo kata,” alisema Martha.
Rozina akakubali na wakaa eneo hilo, wingu likazidi kuwa jeusi na kuruhusu giza kutawala, tofauti na mafikirio yao mvua nyepesi ilinyesha badala ya mvua kubwa walioyotarajia. Wakati wakiendelea kufikiri pa kujifa akatokea yule mzee ambaye Tony na Martha walimsaidia miaka kadhaa iliyopita, akawapa ishara ya kuwataka wamfate nao wakatii,
“Wewe wifi! Unamjua yule mzee au ndio tunaenda tuu?” aliuliza Rozina.
“Anaonekana ni mtu mwema hawezi kutudhuru twende tukamsikilize,” Martha akajibu.
Wakatembea kwa hatua za haraka na kumfikia mzee yule ambaye alikaa chini ya mti mmoja,
“Simameni hapa, mtakuwa salama na mvua haitowalowesha,” akasema mzee yule.
“Akhsante babu”
Mzee yule akamtazama Martha kuanzia chini hadi juu kisha akamtazama Rozina na kutabasamu, akanyanyua kinywa chake na kusema,
“Nafikiri unaikumbuka vizuri kauli yangu kwamba wawili ninyi mtakuwa na furaha kama mtakuwa pamoja, na niliamini mtakiishi kiapo chenu. Hayo yaliyotokea ni malipo ya usaliti uliofanyika hata hivyo Mungu amewapa nafasi ya kufurahia matunda ya mbegu iliyopo tumboni mwako”
Martha akainua uso wake uliolowana kwa machozi na kumtazama mzee yule,
“Je! Vipi kuhusu Tony amebakiza miezi 3 sasa ya kuishi, kuna namna yeyote ya kufanya hili yeye awe mzima na kuwaona watoto zake?” aliuliza Martha.
“hilo siwezi kulizungumzia,” akajibu mzee.
Martha akainama chini na kuendelea kuangusha chozi, mzee akawaambia kuwa wanaweza kwenda maana upepo ulishatulia na mvua imekata. Safari ya shamba ikafa na wakaamua kurudi moja kwa moja nyumbani.
Katika mwezi wa 9 wa ujauzito wa Martha na mwezi wa tano toka Tony alivyoanza kuhesabu siku za kuishi. Ulikuwaa ni usiku mtulivu sana, baridi halikuwa kali kama ilivyozoeleka kwa siku zote, Martha alianza kusikia uchungu usiku huo. Juhudi za kumuwahisha hospitali zikafanyika kadri Martha alivyozidi kulalamika kwa uchungu ndivyo na hali ya Tony ilivyozidi kuwa mbaya. Mjomba akawaambia Rozina na Shangazi watangulie hospitali yeye amuangalie Tony.
Manesi wakampokea Martha na moja kwa moja wampeleka chumba maalumu kwa ajili ya wamama wajawazito walio tayari kwa kujifungua. Huku nyuma mjomba naye akashindwa kuvumilia kumuona Tony akiwa katika hali ngumu vile, ikabidi akodi gari na kumpeleka hospitali ambayo Martha alipelekwa. Tony hakujali hali yake alichokifikiri ni watoto wake na Martha,
“Hatuna namna ya kufanya kwake, sumu imeshafika eneo la Moyo hapa tusubili kudra za mwenyezi Mungu,” alisema daktari.
Kauli hile ilimsikitisha sana mjomba na Tony hakutaka kukubaliana na hilo,
“Uncle nizuieni nisife kwanza hadi niwaone watoto zangu,” aliongea Tony kwa shida mno.
“Hutokufa utawaona tuu”
“Daktari mbona naishiwa nguvu hivi, nisaidie daktari niwaone watoto zangu,” aliendelea kusema Tony.
“Tunaweza kumpeleka chumba alichopo mkewe lakini ni hatari mno, kama ikitokea amefariki mbele ya mkewe ni wazi tutawapoteza wote,” alisema daktari.
“Tumsogeze basi hata chumba cha karibu,” alisema mjomba.
“Hospital yetu ni ndogo mno hivyo, tuombe ajifungue salama na awaone watoto zake,” daktari aliongea.
Mjomba akamsogelea Tony na kumwambia,
“kwa wakati huu unapaswa kumuombea Martha awe na nguvu hili aweze kuwaleta watoto wako salama, omba Mungu atakusaidia,” alisema Mjomba.
Tony alifumba macho yake na kuomba Mungu ampe nguvu Martha katika jambo lile.
Martha akafanikiwa kujifungua mtoto wa kwanza ambaye alikuwa wa kiume, na muda mfupi baadaye akajifungua mtoto aliyesalia ambaye ni wakike. Rozina, shangazi na Martha mwenyewe walifurahi mno. Daktari akawahakikishia kuwa watoto wapo katika hali ya usalama. Wazo la Tony likamjia Martha na kumuomba daktari kuwa watoto hao lazima waonane na baba yao, mjomba wakiongozana na wauguzi waliowabeba watoto wakaingia chumba alichopo Tony na kukuta amefumba macho na mikono kama mtu anayefanya maombi. Shangazi na Rozina wakawachukuwa watoto na kusogea karibu na kitanda,
“Tony fumbua macho uwatazame watoto zako, hakika ni wazuri mno, wakike kafanana na mama yake na kidogo shangazi yake na huyu wakiume ni sura yako kabisaa!” alisema mjomba.
USIKOSE SEHEMU IYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi