Notifications
  • MY DIARY (15)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA TANOTULIPOISHIA...Hapo mzungu wa watu hakuweza kuvumilia tena aliichomeka yote.Mmmmmh mmmmmh ishiiiiiiiiiiii yeaaaaaahhhhhhhh yeaaaaaaah ni miguno niliyoitoa mara baada ya kusikia joto tamu la kiungo hicho.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Ikabid nijivute kwa nyuma ili lengo likiwa ni kukaa vizuri ili kichwa cha nyoka kiwe juu juu ya pango langu ili niweze kukisugua sawa sawa na pia…
  • MY DIARY (14)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA NNETULIPOISHIA...Nikamuuuuliza hivi wewe haugopi maradhi? Akanijibu kuwa angekuwa haogopi basi angeshakufa. Sikiliza Leah hapa nipo na vile vipimo vya ukimwi hivyo usiwe na wasiwasi tutapima wote wanne kama wapo fresh tutaingia kazini wewe si unatafuta hela ya kujiunga na chuo au?IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kabla sijajibu akanambia nitakupa na dawa ya kumeza ya kuzuia mimba na pia…
  • MY DIARY (13)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA TATUTULIPOISHIA...Joyce akaanza kujimiminia mwenyewe, kweli dunia ina mambo wakati wenzake wakichanganya nay ale maji makubwa yeye alikuwa akinywa kavu kavu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi mimi sikuwa na jinsi zaidi ya kuaagiza ile bia yangu ambayo alinifundisha yaani savanna. Safari hii hakusubiri ili ifike mwisho ili anitambulishe bali tulivyoanza tu kunywa akawaambia wale…
  • MY DIARY (12)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA MBILITULIPOISHIA...Niliamua kufanya ziara ili nijue pakoje na mwisho wa siku niliamini kuwa kutokana na umaarufu wa marehemu baba yangu isingekuwa kazi sana kulipata shamba lake..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilitembea kijiji hadi kijiji huku nikijaribu kuuliza kwa wenye viti wa mtaa kama walikuwa wakimjua marehemu Bura. Kwa kweli kazi ilikuwa ngumu sikuweza kuvimaliza vijiji…
  • MY DIARY (11)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA MOJATULIPOISHIA...Wakati akiongea maneno hayo mara mtarimbo ukaanza kusimama nikajisemeha nimeshakosea nilitakiwa niondoke nilivyoona kimelele tu, nikajua hapo lazima atanitafuuna bila huruma. Basi akaingia bafuni akachukua sabuni akajipaka ili kujisisimua ngoma isimame vizuri.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Yaaani nilichanganyikiwa na huko bafuni nilisikia maneno ambayo yalinichekesha…
  • MY DIARY (10)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMITULIPOISHIA...Nikamwambia Joyce ndo maana mimi nakupendaga. Nikamwambia “nitakuapa feedback ngoja nimpigie asije akaja na makufuli yake leo hii. Nikampigia baba mwenye nyumba eti kwa kujiamini kabisa akapokea nakusema “ Halow mrembo” Nikamwambia Yes mpenzi kitu ambacho kilimfurahisha sana..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kuokoa hela ya vocha nikamwambia nimekubali ombi lako alafu nikakata…
  • MY DIARY (9)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA TISATULIPOISHIA...Basi Dj wangu aliendelea na mautundu yake akaniwekea mambo ya pwani na hapo ndipo uvumilivu ulipomshinda akaja kunibambia na mimi sikuona haja ya kumbania kwa kuwa ni mali zake mwenyewe. Nilizungusha nyonga na kiuno mpaka nikachoka nikajitupa kitandani ili nipumzike. Nafsi yake ilikuwa imeridhika kwani hakutka tena penzi bali alichukua lap top yake na kuanza kunionesha picha na vitu vingine ambavyo vilinipa raha.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (8)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA NANETULIPOISHIA...Sijui hata haya maneno yalitoka wapi, fahamu zilinitoka na Ticha aliamua kuninyanyasa maana nilishajikojolea zaidi ya mara tano. Basi na yeye kwa kutafuta mbwembwe alianza yale mambo yao ya katerero, siunajua tena mwalimu John alitokea pande za Bukoba.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alinichezea sana na baadaye nilishangaa kukuta jamaa ameshaingiza kunako. Sikujielewa kwa…
  • MY DIARY (7)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA SABATULIPOISHIA...Kwaito zilivyonoga uzalendo ulinishinda nikajikuta na mimi nashuka ngazi kuelekea chini sehemu ya kuchezea.Nilizijua kwani shuleni tulikuwa tunazicheza sana hasa kwenye yale madisco yetu ya mwisho wa mwezi.John wangu alibaki juuu akiniangalia jinsi nilivyokuwa nikicheza vizuri.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Yeye alishindwa kushuka akiofika kile kitu kukaliwa na watu…
  • MY DIARY (6)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA SITATULIPOISHIA...Akanambia kuwa wamemwambia wapo East Africa Pub na tayari wamaeshaagiza mkuu wa mbuzi. Mmmmhhhh kusikia mguu wa mbuzi mate yalinijaa mdomoni. Basi kwa harakaharaka nikamwambia naomba niende niende nyumbani nikachukue viwalo vya club kisha nitawakuta hapo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alinambia mbona hizo nguo ulizofaa zipo poa tu wewe twende hivyo bhana si upo na…

DHAMANA (1)

Jina: DHAMANA

SEHEMU YA KWANZA
Hali ya simanzi ilikuwa imetawala katika eneo zima la kasri la kupendeza la kifalme katika himaya ya Majichungu inayopatikana katika bahari ya hindi, himaya hii ya kijini iliingia katika huzuni baada ya mfalme wao kuwa katika harakati za mwisho za maisha yake. Mfalm huyu aitwaye Zulain mwenye miaka yapata elfu tatu alikuwa katika ugonjwa kwa muda wa miaka kumi sasa leo ndiyo dalili za kufikia mwisho wa uhai wake zilionekana dhahiri kwa majini wote wa hapo kwenye kasri hilo.

Akiwa kalala kwenye kitanda chake cha thamani kwa muda wa miaka kumi kutokana na ugonjwa uliokuwa unamsumbua ambao haujulikani, kwa mara ya kwanza aliinuka kitandani ghafla akakaa kitako kisha akasimama akaelekea kwenye kiti chake cha enzi akiwaacha watumishi wake wakiwa na simanzi sana. Kuugua mfalme kwa muda mrefu kisha kuinuka ghafla ni dalili tosha ya kuwa siku za mwisho za miaka yake zimekaribia, hivyo hata watumishi wa ndani ya kasri hili walitambua kuwa siku za mwisho za uhai wa mfalme wao zimekaribia.

Hata mfalme mwenyewe alitambua kuwa ana masaa ya kuishi duniani au siku ya kuishi duniani hivyo alitaka kuongea maneno ya mwisho kabla roho yake haijaachana na mwili wake, alipokaa kwenye kiti chake jambo la kwanza kulitamka ilikuwa ni kuitiwa mawaziri wake wote pamoja na viongozi wengine waliopo chini ya utawala wake ili awaambie jambo la muhimu pamoja na kuacha kauli ya mwisho katika himaya yake. Amri ya kuitwa mawaziri na viongozi wa juu katika himaya yake ilitekelezwa mara moja na baragumu maalum likapulizwa kwa haraka sana na mpulizaji wake anayetoka katika himaya hiyo, ndani ya sekunde kadhaa chumba cha mkutano kilijaa mawaziri na viongozi wenye nyadhifa kubwa katika himaya hii ya kijini ambao walikuwa ni majini wa aina mbalimbali.

"Himaya ya Majichungu inaelekea kukumbwa na simanzi kubwa kwani kiongozi wake niliyetawala kwa muda wa miaka 2500 nakaribia kufa na dalili kuu ya kufa kwangu nadhani imeonekana kabisa dhahiri kwenu na kwa watumishi wangu, sasa basi suala la kutafutwa mrithi wa taji langu na kiti changu cha enzi nawapa nyinyi. Nahitaji mjukuu wangu Zalabain ambaye ndiye mrithi wa kiti changu cha enzi na taji langu apatikane haraka iwezekanavyo kwa namna yoyote na afutwe popote alipo aletwe huku akabidhiwe jukumu lake la ufalme kwani mwanangu Zaif ambaye ndiye baba mzazi wa Zalabain hatunaye na wote mnatambua ni jinsi alivyougua hadi akata roho katika himaya hii.

Sasa basi Zaif kabla hajafa alisema duniani yupo mjukuu wangu aitwae Zalabain, sasa inabidi huyo mjukuu wangu atafutwe. kwa hali yoyote hadi apatikane ili aje kuchukua wadhifa wangu kama mrithi pekee aliyebakia. Pia nahitaji mila na desturi za himaya hii zibaki kama nilivyozikuta na zisibadilishwe kwa namna yoyote na wala asitokee kiumbe akabadilisha au akamshawishi kiumbe yoyote abadilishe.

Mwisho kabisa nahitaji Sadik bin Zultash baba wa mapacha Saliim na Salmin aachiwe huru kuanzia sasa kwani uzao wake kwa faida moja umetusaidia kwa kutuletea jini mwenye nguvu kuliko wote na anayeifanya himaya yetu isidhuriwe na kiumbe wa aina yoyote, sina la ziada ni hayo tu" Mfalme Zulain alihitimisha na kikao kikamalizika mara moja karibia viongozi wote wakatawanyika wakiwa na simanzi juu ya mfalme wao. Siku iliyofuata ilikuwa ya simanzi zaidi kwa himaya nzima ya Majichungu kutokana na kifo kilichomkumba mfalme wao, himaya nzima iliomboleza kifo hicho kwa muda wa wiki saba na baada ya hapo jeshi la majini watatu ambao ni makomandoo likaundwa kwenda kumtafuta Zalabain popote alipo ili aje kurithishwa ufalme wa babu yake.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

WIKI MOJA BAADAYE
USIKU WA MANANE

AMBONI
TANGA
Eneo la miamba yenye mapango ya kihistoria jijini Tanga jirani kabisa na mto mkubwa Tanga nzima uitwao mto Sigi kulikuwa kuna kundi la vijana kumi waliokuwa wameuzunguka mti mmoja wa mkoko ambao unasadikika kuwa mti wa ajabu kutokana na kuota eneo ambalo lipo mbali na ufukwe wa bahari. Vijana hao walikuwa wameuzunguka mkoko huo ambao ulikuwa umening'inizwa chupa ya ukubwa wa lita moja ambayo ilikuwa ikijibadili rangi kila kukicha, walikuwa wamejifunga kaniki nyeusi kiunoni na vitambaa vyekundu kichwani na kwenye mikono yao. Muda wote walikuwa wapo makini kuitazama chupa hiyo pamoja na mazingira ysnayozunguka mto Sigi pamoja na upande wa mapango ya Amboni, walikuwa wapo kimya sana na umakini wao katika kuangalia mazingira ya hapo ndiyo ulizidi kwani walikuwa wanapambana na wachawi wa kila namna ili kuilinda chupa iliyopo hapo mtini ambayo huonekana usiku kwa wenye uwezo kuiona na mchana haikuonekana kabisa.

Siku hiyo majira ya saa nane usiku vijana hao walimshuhudia Mamba mmoja mkubwa akitoka ndani ya mto Sigi na akakaka pembezoni mwa mto huo mita chache kutoka pale walipo, wote walimpuuzia mamba huyo kutokana na dawa zao wanazotumia hawezi kuwaona. Walibaki wakimtazama yule Mamba kwa jinsi alivyo mkubwa huku kuliko hata Mamba wote waliowahi kuwashudia katika mto Sigi tangu wakiwa watoto, mmoja kati ya wale vijana alishikwa na shauku ya kwenda kumtazama yule Mamba na akasogea karibu zaidi kwani dawa zao zilikuwa zinawazuia wasionwe na wanyama wakali.

Alisogea akamtazama zaidi na akabaini ni mamba wa ajabu mwenye rangi tofauti na Mamba wa pale mtoni, akiwa anashangaa uajabu wa yule mamba ghafla alijikuta akipigwa mkia akatumbukia mtoni na mamba huyo naye akazama mtoni akiwaacha wale vijana waliobakia wakikimbia hadi pembezoni mwa mto wakiacha kuilinda ile chupa. Hilo lilikuwa kosa jingine kwao na hawakupata hata nafasi ya kulirekebisha kwa balaa lililotokea, kimbunga kikali kilivuma kuuzunguka ule kwa muda wa dakika kadhaa na kilipoacha ile chupa wanayoilinda ilikuwa imepasuliwa tayari. Kabla hata hawajatafakari kitu cha kufanya maji ya mto Sigi nayo yalianza kuzunguka kisha yakanyanyuka juu urefu wa mlima huku yakizunguka na yakatengeneza umbo la jitu kubwa ambalo mkono mmoja lilikuwa limemshikilia kijana yule aliyepigwa mkia na Mamba akaingia mtoni.

Vijana walipoona hivyo wakajua wameingiliwa na kazi yao imeshaharibika hivyo walitaka kukimbia ili kujiepusha na hatari kwani viumbe waliowavamia sio wa kawaida, walikimbilia upande lilipo pango wakijua ni salama kwao ili wapate sehemu ya kutorokea. Walipokaribia kuingia pangoni walikutana uso kwa uso na nyoka mwenye vichwa kumi na ikawabidi wakimbilie mtoni kwa upande mwingine bila ya kutambua wanajipeleka kwenye eneo la kifo, vijana hao walijitupa mtoni kwenye maji wakiwa wanataka kuokoa maisha yao tu na wala hakukumbuka kuwa dawa waliyojipaka ya kuzuia wasidhuriwe na wanyama wakali inatoka mwilini ikiwa utaingia kwenye maji. Walipokuja kukumbuka tayari walikuwa wamezungukwa na mamba zaidi ya kumi wa mto huo, walikuwa wamejirusha sehemu yenye maskani ya Mamba bila ya kujijua na wakawa kitoweo cha Mamba.

****

Sherehe kubwa ilifanyika katika kasri la kifalme la Majichungu katika kusherekea kupatikana kwa mjukuu anayepaswa kurithi kiti na taji la ufalme wa babu yake, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mjukuu huyo mwenye mchanganyiko wa binadamu na jini kufika katika himaya tangu azaliwe. Sherehe ilipoisha ndipo taratibu zote za kimila na desturi za kumpatia ufalme Zalabain zikaandaliwa kama ilivyofanyika kwa wafalme waliopita. Siku iliyofuata sherehe nyingine ya kuvikwa taji la ufalme ilifanyika katika uwanja mkubwa uliopo nje ya kasri la kifalme ambayo ilihudhuriwa na wanahimaya hiyo karibia wote, kiti cha kifalme kilitolewa kikawekwa sehemu yenye jukwaa lililopambwa kwa busati lenye rangi nyeupe.

Muda wa kuvikwa taji Zalabain ulipowadia Mkuu wa baraza la sheria la himaya hiyo aliingia akiwa amebeba taji la kifalme liliwekwa kwenye kasha lililopambwa na fito zenye rangi nyekundu, Zalabain akiwa nyuma ya Mkuu huyo wa baraza la sheria pembeni yake akiwa na walinzi wenye miili mikubwa pamoja na sura za ajabu. Zalabain na mkuu huyo walipanda katika jukwaa lenye kiti cha kifalme huku mamia ya wanahimaya ya Majichungu wakishangilia kwa nguvu, aliamriwa aketi kwenye kiti cha ufalme naye akatii akaketi na Mkuu wa baraza la sheria akashika kasha lenye taji la kifalme akasogea kisha akawageukia Wanahimaya ambao wapo hapo kushuhudia tukio hilo.

"Leo ni siku maalum na ya kihistoria ya kumpata kiongozi wetu aitwae Zalabain bin Zaif atakayeiongoza himaya yetu akirithi utawala wa Babu yake Zulaif, akiwa na miaka 26 tu atakuwa kiongozi mdogo kuwahi kutokea katika Himaya yetu hii hivyo naomba mumpokee" Mkuu wa baraza la sheria aliongea kisha akamgeukia Zalabain ambaye tayari ameshavaa mavazi ya kifalme akawa anatazama nae.

"Kwa mamlaka niliyokabidhiwa ninakukabidhi na kukuvisha taji hili la Kifalme litakalokufanya uwe mfalme, miongoni mwa wafalme, wa ukoo wa kifalme, waliowahi kuwa wafalme, uwe kiongozi wa kasri la kifalme. Zalabain sasa wewe ni mfalme wa himaya ya Majichungu" Mkuu wa baraza la sheria alipomaliza kusema maneno hayo aliliweka taji kichwani mwa Zalabain huku halaiki ya wanahimaya wakishangilia, kushangalia huko kulizimika ghafla mithili ya umeme unavyozimika eneo lenye giza. Wote walibaki wameduwaa baada ya taji la kifalme lililowekwa kichwani mwa Zalabain kuruka kando likaanguka kwenye busati lililotandazwa hapo jukwaani.

Mkuu wa baraza la sheria aliona ni jambo la kawaida sana na aliinama akalishika ili alinyanyue lakini taji halikuinuka na lilikuwa zito sana na ikambidi alishike kwa mikono miwili na akashindwa kuliinua vilevile. Aliamua awaite wale walinzi walioingia na Zalabain walinyanyue nao wakashindwa pia kulinyanyua eneo hilo. Wanajeshi wanaoaminika wana nguvu sana nao walishindwa kulinyanyua taji hilo, Zalabain mwenyewe alibaki akiwa anashangaa kwa tukio hilo ambalo hakulielewa limetokana na nini.

Mnajimu mkuu wa Himaya hiyo aliitwa mara moja na akapewa kazi ya kulitatua tatizo hilo kwani yeye ndiye anayeaminika katika himaya hiyo, mnajimu huyo wa kijini alianza kulizunguka taji hilo la kifalme kisha akajaribu kuliinua lakini alishindwa kabisa na akaanza kubadilisha macho yake yakawa kama ya paka akamtazama Zalabain.

"Siyo uzawa wa ukoo wa mfalme huyu ndiyo maana taji limemkataa na wala siye mtoto halisi wa Zaif, taji hili linahitaji abadilishwe kiongozi kwani kizazi cha ukoo wa mfalme alibaki Mfalme Zulain tu ambaye amefariki tayari.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
57 Dhamana featured Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni