KIJIJINI KWA BIBI (12)

0
Mwandishi: Alex Kileo

SEHEMU YA KUMI NA MBILI
TULIPOISHIA...
Siku ya harobaini baada ya kile kifo, usiku wakati tumelala

na baba yako, tulishtushwa na

upepo mkali ulioezua paa la nyumba

tuliyokuwa tunakaa, wote tukakurupuka kitandani na kuanza kushangaa hiyo hali, wakati

tunautafakari ule upepo, 

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
kilitokea

kiumbe cha ajabu sana, wote tukabaki na mshangao ulioambatana na uoga.

Kile kiumbe hakikuonekana kujali hali tuliyonayo, kilimwambia

baba yako kuwa kinaitwa

NDIFU, ni mzimu wa ukoo, na kimekuja kutaka hifadhi, baba yako

akapata ujasiri na kumuuliza alikuwa

anataka hifadhi ya nini?, kile kiumbe

kikasema kinataka kuishi ndani ya mwili

wa mtu alie hai, baba yako

akamwambia sawa aende tu

akaishi, kile kiumbe kikakataa na

kusema anataka kuishi kwenye mwili

wa baba yako au kaka yako ambae

ndio huyo tu, tuliebaki nae, baba

yako akakataa.

Kile kiumbe kikasema,

kitu kitakachotokea asubuhi

tutakapoamka tusishangae, Kisha

upepo mkali ukakibeba na paa la

nyumba yetu likarudi kama

mwanzo, tukabaki tunashangaa huku kila mmoja akiwaza lake, ila mwisho tukajadiliana na kukubaliana tusubiri mpaka kesho ili tuone hicho kitakachotokea, tukalala.

Kesho tulipoamka ndipo

tukapata kitu kilichotupa mshtuko,

kiasi kwamba nikapoteza fahamu..

tulimkuta mtoto wetu wa pekee

amekufa kwa mtindo ule ule aliokufa

nao mtoto wetu wa kwanza.

Ndugu wa mume wangu walikuwa wanajua

chanzo cha vifo vyote vya

wanangu,baada ya mazishi kuisha na

watu kutawanyika, ndugu wa baba

yako wakamuita pembeni na

kumshawishi aurudie ule mzimu na

kuuomba radhi ili mambo yake

yarudi kama awali, ila baba yako

akakataa.

Baada msiba kuisha, ule

mzimu uliendelea kumuandama

baba yako, mi kuona umezidi ikabidi

nimwambie baba yako aukubali ili

aulee kama mwanzo.

Baada ya kauli ile, usiku mzimu ulitutokea tena tukiwa tumelala kitandani na kuongea maneno makali na ya kutisha juu ya msimamo wa baba yako, na kisha mzimu ukaongea maneno mazuri na kunisifia sana juu ya ushahuri niliompa baba yako, kwa ushauri ule niliompa baba yako, kuanzia hapo

ule mzimu ulinipenda mimi na

kuahidi kuwa kamwe hautanidhuru

mimi na mtu yeyote yule ambae ana

damu au nasaba moja na mimi, yaani mwanangu

na ndugu zangu wote tuliochangia wazazi wote, au baba tu, au pia mama tu.

"ndio maana Sajenti Minja haukumdhuru eee!?" Omary akauliza huku akimuangalia Kayoza,

"inawezekana

mwanangu, labda Minja hakudhurika kutokana na ahadi aliyonipa mzimu" Mama kayoza akajibu,

"Duh, hii habari inazidi kunisisimua, inawezekanaje mimi nikawa mzimu?" Kayoza aliuliza huku akijishangaa,

"Je unaamini kuwa nabii Musa aliweza kuipasua bahari ya shamu na akapita na wanaisraeli?" Mama Kayoza alimuuliza mwanae,

"Hiyo naamini" Kayoza alijibu huku akimuangalia mama yake,

"Sasa kwa nini huamini kuwa hata wewe unaweza kuwa mzimu?" Mama kayoza alimuuliza mwanae,

"Sasa utafananishaje mambo ya Mungu na uchawi?" Kayoza alimjibu Mama yake huku akionekana kutofurahia hilo swali,

"Huo uchawi uliumbwa na Mungu na manabii waliutumia ila waliuita muujiza na si uchawi" Mama Kayoza alimfafanulia mwanae,

"Endelea na simulizi yetu mama bwana" Kayoza akamuambia mama yake,

"Ngojeni kidogo" Mama kayoza aliongea kisha akainuka na kuelekea msalani.

Sajenti Minja alienda mpaka nyumbani kwake, akaingia mariwatoni na kuanza kusafi mwili.

Alipomaliza alienda mpaka katika meza na kuanza kuandika barua ya kuacha kazi. Aliindika kwa ufanisi mkubwa kwa kutumia ile nakala ya barua aliyopewa na yule Dada polisi.

Alipomaliza kuandika aliirudia tena na tena kuisoma na kuona haina makosa.

Akaiweka vizuri katika bahasha na hakuona haja ya kuchelewa kuiwasilisha ofisini kwa mkubwa wake ingawa muda ulikuwa umeenda sana.

Akatoka nje na kuchukua gari iliyomfikisha katika kituo cha kazi, na kwenda moja kwa moja mpaka kwa yule dada aliyempa maelekezo hawali, kwa bahati nzuri alimkuta,

"Umerudi tena? umemaliza nini kuandika?" Yule dada aliuliza huku akiwa anaamini Sajenti Minja kuna kitu kingine kafuata na wala sio kuwasilisha barua ya kuacha kazi,

"Ndio nimeileta barua hivyo" Sajenti Minja alijibu huku akimpatia ile bahasha yenye barua ndani,

"Kha! Wewe mtoto mbona umeandika haraka hivyo, hujajipa hata muda wa kufikiri?" Yule dada alimuuliza huku akimshangaa Sajenti Minja,

CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Mpaka nimefikia hatua hii, ujue nimefikiria sana" Sajenti Minja alijibu huku akionekana kutofurahishwa na maswali ya yule dada,

"Wenzako wanatafuta kazi, wewe unaacha" yule dada alimuuliza Sajenti Minja huku akipokea ile bahasha,

"Ni bora nikae bila kazi kuliko kupambana na kiumbe cha ajabu" Sajenti alijibu kijeuri,

"Na kwenye barua umeandika sababu ya kuacha kazi ni kiumbe cha ajabu?" Yule dada aliendelea kuuliza huku akijua anamkera Sajenti Minja,

"Ifungue uisome, ukimaliza utairudishia kwenye bahasha nyingine" Sajenti Minja alijibu,

"Unaona huo ndio utakuwa ustaharabu?" Yule dada nae alimuuliza,

"Nadhani ndio itakuwa nzuri zaidi kuliko kuniuliza maswali ilihali majibu nimekupa ndani ya hiyo bahasha" Sajenti Minja alijibu,

"Okey, unaweza kwenda" Yule dada aliongea huku akiwa amekasirishwa na majibu ya Sajenti Minja,

"Kuna hivi vitu pia" Sajenti Minja alimpa bahasha nyingine ila ilikuwa kubwa zaidi ya ile ya mwanzo na pia haikufungwa,

"Na humu kuna nini?" Yule dada aliuliza huku akiipokea ile bahasha,

"Ipo wazi hiyo bahasha, unaweza tu kuangalia vilivyomo ndani" Sajenti Minja alijibu kisha yule dada akaingiza mkono na Kutoa kitu kimoja moja, ilikuwepo bastola, namba ya uaskari na kitambulisho cha Sajenti Minja mwenyewe.

"Sasa hivi unaniletea vya nini?" Yule dada aliuliza huku akimshangaa Sajenti Minja,

"Unapoacha kazi si unatakiwa kurudisha hivi vyote?" Sajenti Minja aliuliza,

"Hivyo utamkabidhi mkubwa wako, tena atakapokubaliana na maombi yako" Yule dada alijibu huku akivirudisha vile vitu katika mfuko ambao vilikuwepo hawali,

"Sasa kama nimeshawasilisha barua, hivi nikae navyo vya nini" Sajenti Minja aliuliza,

"Zingatia nilichokwambia, tusibishane hapa. Tena ulete mkanda, kofia na buti" Yule dada alimalizia,

"Sikupewa magwanda mimi, narudisha nilichopewa" Sajenti Minja alijibu huku akivipokea vile vitu vikiwa ndani ya ile bahasha,

"Sawa, kesho mchana nenda kwa mkuu, nadhani atakuwa ameshaipitia barua yako" Yule dada alimpa maelekezo Sajenti Minja.

Baada ya hapo Sajenti Minja akaondoka.

Mamá kayoza alipotoka msalani, akanywa maji kisha akaendelea,

"kuanzia siku ambayo mzimu aliniahidi hatonidhuru mimi na kizazi changu, nikawa najihisi niko tofauti na

mwanzo, kila nilichofanya

nilifanikiwa, nadhani mzimu aliamua kunionesha namna anavyonijali.

Baada ya miezi mitatu toka kaka yako wa pili amefariki, kwa bahati nikashika

mimba.

Siku ambayo niligundua nina mimba, mzimu alitutokea tena usiku na kuniomba sana niendelee na msimamo wangu wa kumshahuri baba yako juu ya kuujali huo mzimu, nami nikaitikia kwa kukubaliana nao.

Mimba ilipofikisha miezi tisa ndipo nilikuzaa wewe,

tena hapo ni baada ya kukaa mwaka mmoja tangu nilipompoteza

mwanangu wa pili.

Baada ya wewe kuzaliwa, sasa hapo yule

mzimu alichachamaa, alitutokea usiku na kusema kuwa anataka

kuingia kwenye mwili wa baba yako, Baba yako hakukubali hilo jambo,

hata baba yako alipokataa yule

mzimu hakuwa na cha kufanya kwa

sababu nilimuomba ampe baba yako muda wa kufikiri kwanza, na kwa kuwa mzimu aliniahidi kutonidhuru mimi

na ndugu zangu na damu yangu kwa

hiyo kazi yake ilikuwa kunilinda mimi

na nasaba zangu, mzimu akaondoka.

Miaka ikasogea na

mzimu haukuchoka kumsumbua

baba yako, ulitutokea kila siku na kuongea maneno ya vitisho juu ya Maisha ya baba yako, ila Baba yako aliendelea kushikiria msimamo wake.

Ikafika kipindi baba yako

akaanza kuumwa, aliumwa wiki

nzima na tulipoenda hospitali ugonjwa ukawa hauonekani, ghafla hali yake ikawa mbaya

zaidi, mwili ukadhohofika na hakuweza hata kuamka

kitandani.

Ule mzimu kuona Baba yako yupo katika hali ile, ukabadilisha

maamuzi ya kumuingia baba yako,

ukawa unataka kuingia ndani ya

mwili wako, ila baba yako

akapinga tena jambo hilo, tena alilipinga kwa nguvu zote ingawa alikuwa mgonjwa.

Kwa mila za kijijini kwa

baba yako mtu anapokuwa anaumwa

sana anatenganishwa na mke au

mme wake. Huduma zote muhimu anakuwa anahudumiwa na

mama yake au ndugu zake, kwa hiyo

baba yako alikuwa anahudumiwa na

mama yake ambaye ni bibi yako.

Sasa siku moja wakati niko nje

nakunyonyesha huku natayarisha

chakula, ghafla upepo ulivuma kwa

nguvu sana, kisha ukaingia katika

chumba alichokuwepo baba yako ambaye pia ndani alikuwa bibi yako.

Baada ya dakika tano za ukimya katika chumba kile, nikasikia mabishano yamezuka kati

ya bibi yako na baba yako, mara ghafla bibi yako akaja kukuchukua

mapajani kwangu, kwa ahadi ya kwamba kuna kazi anaenda kuifanya na

anakurudisha mda si mrefu.

Akaingia na wewe kwenye chumba alichokuwepo

baba yako, kisha yale mabishano

yakaendelea, baada ya muda kidogo

nikaskia baba yako analia kwa sauti

ya juu sana, ndipo nikatoka mbio hadi

katika chumba alichokuwepo Baba yako na

mama yake ambaye ni bibi yako, nikakukuta wewe Kayoza

unamnyonya damu baba yako" Mama kayoza aliongea

maneno haya huku machozi yakianza kumtoka….

mama kayoza akaendelea,

"baba

yako aliponiona aliniangalia kisha

akawa kama anataka kusema kitu, ila

nguvu hakuwa nazo, akaishia

kukunyooshea kidole, kisha akakata

roho, Alafu wewe ukapoteza fahamu,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

nilijisikia uchungu sana, nilianza

kulia kwa kwikwi pale mlangoni, nililia sana kiasi kwamba nikapoteza fahamu, nilizinduka nikaendelea kulia ila

cha kushangaza bibi yako

akuonyesha wasiwasi kabisa na wala hakutoa chozi la uchungu kuonesha kuwa amempoteza mwanae, badala

yake aliniambia kuwa yule mzimu wa

ukoo ameingia mwilini kwako wewe Kayoza

kwa ruhusa yake, yaani ruhusa ya bibi yako.

akaniambia kuwa kuanzia

hapo hakutakuwa tena na shida, na

kama shida itatokea ni kwa ajili ya

kukulinda wewe (Kayoza), na sharti

kubwa ambalo mzimu alitaka

uzingatie ni kwamba, usifanye

mapenzi mpaka uoe na pia ukae mbali na harufu ya damu ya aina yoyote na uepuke kuwa mtu wa hasira hasira. Shangazi yako hajawahi kumwambia hivyo?" Mama Kayoza akamuuliza mwanae,

"Uwa ananisisitizia sana hayo mambo na kiukweli niliyamudu sana, hakuwahi kuniambia sababu ya mimi kutofanya hivyo"

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)