KIJIJINI KWA BIBI (15)

0
Mwandishi: Alex Kileo

SEHEMU YA KUMI NA TANO
TULIPOISHIA...
"Siku zote mwanajeshi mpumbavu utulivu anaostahili ni huo unaoambatana na maumivu" Yule bwana mkubwa aliongea huku akitabasamu na wakati huo huo alikuwa anatoka nje ya lile jengo lililokuwa tulivu kwa nje, ila kwa ndani si sehemu salama kwa wanajeshi wenye makosa.

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
Baada ya muda kidogo Mchungaji Wingo alirudi huku akiwa na jagi lililojaa maji,

"Muda wa maombi unakaribia, umejiandaaje?" Mchungaji Wingo alimwambia Kayoza,

"Kawaida tu, ila naimani tutafanikiwa" Kayoza alijibu,

"Ni bora umetanguliza Imani mbele, ni jambo jema" Mchungaji aliongea kwa imani,

"Nimekuletea maji hayo unywe, ingawa hujaniagiza ila itabidi unywe" Mchungaji Wingo alimwambia Kayoza,

"Haina shida, nitakunywa tu" Kayoza alijibu huku akiyamimina yale maji katika glass.

Muda wote ambao mchungaji alikuwa anaongea na Kayoza, watoto wake walikuwa wanatayarisha chumba cha kufanyia maombi.

Baada ya maandalizi,

mchungaji Wingo alimkaribisha Kayoza

katika chumba cha maombi, kisha

watoto na mke wa mchungaji Wingo

wakaingia katika chumba cha maombi,

huku kila mmoja akiwa amebeba biblia yake mkononi, hapo ilikuwa yapata saa tano za usiku

usiku.

Baada ya wote kujumuika ndani ya kile chumba, maombi yakaanza rasmi,

Mchungaji Wingo na familia yake

walikemea kwa juhudi zote, mpaka saa

saba usiku, Kayoza alikuwa kama

mwanzo, hakuwa na mabadiliko yoyote, Ila Mchungaji hakukata

tamaa, pia alikuwa anahisi

akishindwa kumtibu Kayoza, heshima

yake inaweza kushuka katika kanisa, kwa hiyo alizidisha maombi .

Ilipofika saa nane za usiku mabadiliko yakaanza kwa Kayoza, alihisi kizunguzungu, hakuna aliyeyaona hayo kabadiliko isipokuwa yeye mwenyewe.

Wakati maombi yanaendelea Mchungaji

akahisi, kuna nguvu nyingine iko kwa

nje, inashindana nae, kwa maana yeye alikuwa na uwezo wa kuona mpaka visivyoonekana. Ile nguvu iliyokuwa inatoka nje ilikuwa haimdhuru ila hakuwa akiitaka iendelee kumuingilia katika maombi yake. Akaamua atoke nje mara moja na akaiacha familia yake inamuombea Kayoza. Ile

kutoka nje, akakutana na watu zaidi ya kumi, wote wako uchi, wamejipaka

majivu usoni.

Mchungaji Wingo

hakupata tabu kuwatambua kuwa

wale ni wachawi. Katika kipindi cha

maisha yake ya uchungaji ameshakutana na hayo mambo mara nyingi tu.

Akaona dawa yao ni ndogo tu, akaanza kukemea, Baada ya kupambana nao kwa

muda wa saa moja, wale wachawi

wakawa wanaelekea kushindwa.

Ila ghafla mambo yakabadilika, Mchungaji Wingo akaanguka chini kisha akapoteza

fahamu. Sasa wale wachawi

wakasogea pale alipolala mchungaji huku wakiruka ruka kwa furaha na kuongea lugha isiyoeleweka. Walimsogelea kwa ajili ya kummaliza kabisa Mchungaji Wingo, ila kila

walipojaribu kurusha makombora

yao, hayakumdhuru

mchungaji.Wakajua sababu ya hayo

mambo ni kutokana na nguvu ya maombi ya familia ya mchungaji

waliyokuwa wanaendelea nayo chumbani.

Wachawi wote wakavamia

katika kile chumba kwa ajili ya kupambana na maombi ya familia ya Mchungaji, ni kitendo cha

dakika kumi tu, familia yote ya

mchungaji ilikuwa imepoteza fahamu ni kutokana na kwamba hawakuwa na imani ya kutosha.

Wachawi wakawabeba kisha wakawalaza nje ya geti pamoja na

mchungaji mwenyewe, kitu kilichowashangaza wachawi ni kuwa

kulikuwa na kijana ambae ni kayoza, toka wale wachawi waanze kuloga,

yeye hakudhurika, ndipo wachawi

wakafanya kosa la mwaka,

wakamweka kayoza katikati yao,

kisha, wakaanza kumloga, bila kutegemea, kayoza akabadilika na

kubeba taswira ya kutisha, wale wachawi mawazo yao yakaona zoezi

lao limefanikiwa, mmoja kati ya wale

wachawi, akamsogelea kayoza ili

ammalize kabisa, ni kitendo bila

kuchelewa, kayoza ndani ya sekunde

kumi alishanyonya damu wachawi

watatu, ndani ya dakika moja

alishamaliza wachawi wote, nao

akawatoa nje, kisha akawalaza

pamoja na familia ya mchungaji,

kisha akarudi katika chumba cha maombi na akapoteza fahamu.

Asubuhi kulipokucha, watu wengi sana walijaa nje ya nyumba ya

Mchungaji Wingo, na wote walikuja kuangalia watu ambao walilala nje ya nyumba ya Mchungaji huku wakiwa na alama za meno shingoni.

Kati ya watu waliolala getini alikuwepo pia Mchungaji mwenyewe na familia yake… ila wao walikuwa na mavazi yao………….

ENDELEA

…waumini wa mchungaji Wingo nao walikuwa

wengi sana, polisi walifika mapema sana katika

sehemu ya tukio, katika uchunguzi wao wa haraka haraka katika eneo lile,

waligundua watu kumi waliokuwa uchi wa

mnyama, wote walikufa na watu wengine sita

walikuwa wamepoteza fahamu.

Askari wakajadiliana wenyewe kwa wenyewe na mwisho wakaamua kuwabeba wale watu waliokufa huku wakiwa tayari wamepiga simu hospitali kwa ajili ya kuhitaji gari la wagonjwa, Ila baada ya muda kidogo, au tuseme kabla gari la wagonjwa halijafika mchungaji alizinduka na kujikuta yupo nje ya nyumba yake huku baadhi ya watu wakimuangalia na pia wakionekana wana maswali mengi vichwani mwao na mwenye majibu ni yeye mwenyewe Mchungaji Wingo

"Vipi, unajisikiaje?" Polisi mmoja alimuuliza Mchungaji Wingo baada ya kuzinduka,

"Namshukuru Mungu, maana ni mkubwa kuliko kila kitu hapa duniani" Mchungaji Wingo aliongea huku akiwatizama watoto wake na mkewe ambao nao walianza kuamka mmoja mmoja,

"Hapa ni kwako?" Polisi akamtupia swali jingine,

"Ndio, ni kwangu" Mchungaji Wingo alijibu,

" unaweza kutueleza ni nini kimetokea?" Polisi aliendelea kuhoji,

"Hapa tunajaza watu tu, ni bora tukafanyie mahojiano kituoni" Polisi mwingine alimshauri yule polisi aliyekuwa anamuhoji Mchungaji Wingo,

"Sasa si inabidi tuwabebe wote ambao ni wazima" Polisi aliyekuwa anahoji alimuuliza mwenzie,

"Hiyo ni familia yangu, mngewaacha tu, twendeni mkanihoji mimi mwenyewe, nadhani natosha" Mchungaji Wingo aliongea huku akilazimisha tabasamu,

"Hapana, ni lazima tuchukue Maelezo ya watu wrote" Polisi aliongea huku akimhimiza Mchungaji Wingo aelekee mahali gari la polisi lilipoegeshwa. Polisi wakambeba yeye na familia yake kwa ajili

ya mahojiano zaidi.

Hii habari za hili tukio lililotokea nyumbani kwa mchungaji ilitangazwa na vyombo vya habari vya nchi nzima, habari zikawafikia wakubwa zake Sajenti Minja, Wakubwa zake, ikabidi washauriane,

" sasa tunafanyaje, au tumchague kijana mwingine aifuatilie hiyo kesi, kwa maana wapo wengi tu na si lazima awe Minja tu" Mkuu was polisi alimwambie mkuu wa jeshi,

"Hilo ni jambo zuri, hila kufanya hivyo ni kuitia aibu hii taasisi ya jeshi na serikali kwa ujumla. Huyu Minja hapo alipo hana hata miezi sita toka atoke mafunzoni Korea ya kaskazini, sasa huoni kumuachia asiendelee na hii kesi hayo mafunzo yake yatakuwa hayana manufaa yoyote kwa taifa?" Mkuu wa Jeshi alimuuliza Mkuu wa Polisi,

"Sasa kama kesi imemshinda tutafanyaje?" Mkuu wa Polisi aliuliza,

"Watuhumiwa unapowahoji na wakaonekana hawataki kusema ukweli uwa unawafanyaje" Mkuu was jeshi aliuliza huku akiiwasha sigara yake,

"Uwa nawashurutisha kwa kuwapa adhabu" Mkuu wa Polisi alijibu,

"Unawasulubu, si ndio?" Mkuu wa Jeshi aliuliza huku anamuangalia Mkuu wa Polisi,

"Ndio maana yake" Mkuu wa Polisi alijibu,

"Hill ndio jibu" Mkuu was jeshi aliongea huku akinyanyuka katika kiti,

"Kwa hiyo Minja nae utamsulubu?" Mkuu wa Polisi aliuliza,

"Sio nitamsulubu, tayari kishaanza kusulubiwa muda mrefu tu" Mkuu wa Jeshi alijibu huku akivaa miwani yake,

"Unamsulubia wapi?" Mkuu wa Polisi akauliza kwa mshangao,

"Nifuate" Mkuu wa jeshi aliongea huku akianza kupiga hatua kuelekea nje ya ofisi yake, wakatembea mpaka katika like jengo ambalo ndani ndipo yupo Sajenti Minja anasulubika. Walipofika walibonyeza kitufe cha kengele na baada ya muda kidogo mlango ulifunguliwa na akatoka mwanajeshi mmoja aliyewapigia saluti na kuwaachia mlango wazi ili wapite. Walipoingia ndani walinyoosha moja kwa moja mpaka sehemu alipokuwepo Sajenti Minja na kumkuta akiwa amewekwa ndani ya bwawa la kuogelea huku mikono yake ikiwa imefungwa kamba kwa nyuma na pia alifungwa jiwe kubwa ili asielee juu ya maji,

" mmemzamisha kwa muda Gani?" Mkuu wa jeshi aliwauliza vijana wake,

"Hii dakika ya ishirini" Mwanajeshi mmoja alijibu huku akiitazama saa yake mkononi,

"Dakika ishirini?, si atakuwa ameshakufa?" Mkuu wa Polisi aliuliza huku akishangaa,

"Hawezi kufa kirahisi hivyo, huyo anaweza kuzama hata siku nzima?" Mkuu wa Jeshi alijibu,

"Duh, aisee ni hatari sana" Mkuu Wa Polisi aliongea huku akisikitika,

"Mtoeni nje" Mkuu wa Polisi aliwaamuru vijana wake ambao walitekeleza agizo bila shurti yoyote. Wakamtoa Sajenti Minja nje ya maji na kumuweka pembeni. Sajenti Minja alikuwa amechoka na mwenye majeraha mengi sana usoni kutokana na mateso aliyokumbana nayo,

"Mfungueni hilo jiwe na mleteeni kiti" Mkuu wa Jeshi aliwaagiza vijana ambao walitii na kuleta kiti haraka,

"Kaa hapo mheshimiwa" Mkuu wa Jeshi alimwambia Sajenti Minja aliyekuwa anaugulia maumivu. Sajenti Minja akajinyanyua na kujiweka juu ya kiti,

"Mmempiga kama mharifu" Mkuu wa Polisi aliendelea kushangaa,

"Pole sana, sasa kilichotuleta hapa ni kitu kimoja" Mkuu wa Jeshi aliongea huku akimtupia gazeti lenye habari zilizotokea huko shinyanga kwa mchungaji. Sajenti Minja akaisoma ile habari kwa umakini mkubwa na kisha akamrudishia mkubwa wake gazeti lake,

"Umeielewa hiyo habari?" Mkuu wa Jeshi alimuuliza Sajenti Minja,

"Hapana Mkuu" Sajenti Minja alijibu,

"Hivo vifo waliokufa hao watu, havina tofauti na vifo vilivyokuwa vinafanywa na wale vijana unaowatafuta, kwa maana hiyo basi, sina budi kusema kuwa muuaji yupo shinyanga" Mkuu wa Jeshi aliongea huku akimuangalia Sajenti Minja ambaye naye alikuwa anamuangalia mkubwa wake,

"Sasa nambie unaendelea na hii kesi au bado umeshikilia msimamo wako?" Mkuu wa Jeshi aliuliza huku akiiangalia saa yake.

Sajenti Minja aakabaki kimya asijue la kujibu,

"Umesikia nilichouliza?" Mkuu wa Jeshi aliuliza huku akirudisha macho yake kwa Sajenti Minja,

"Ndio nimesikia mkuu" Sajenti Minja aliitikia kwa unyonge,

"Nipe jibu, maana kuna mambo mengine ya kufanya muda huu" Mkuu wa Jeshi aliongea kwa mamlaka,

"Naweza nikapata muda kidogo wa kufikiria?" Sajenti Minja aliuliza,

"Unahitaji muda wa dakika ngapi?" Mkuu wa Jeshi aliuliza,

"Nikipata angalau hata wa masaa kumi na mbili utanitosha" Sajenti Minja aliongea,

"Saa hivi ni saa kumi na mbili jioni, kwa maana hiyo mpaka kesho saa kumi alfajiri utakuwa una jibu, so ndio?" Mkuu wa Jeshi aliuliza,

"Ndio mkuu" Sajenti Minja alijibu,

"Mpelekeni akapumzike, mpeni kila atachohitaji" Mkuu wa Jeshi aliwaambia wale wanajeshi waliokuwa wamesimamia mateso ya Sajenti Minja,

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)