Mwandishi: Alex Kileo
SEHEMU YA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Akaenda mpaka ilipopaki gari ya polisi,
akawa anaongea na mwenzake
kuhusu ishu iliyopelekea wale askari
wenzake kuwa vile, na kibaya zaidi ni kwamba alimwambia mwenzake kuwa wale Askari wote wameshakufa, tena aliongea kwa hasira mpaka machozi yakawa yanamtoka.
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Ndani ya ile taxi, Omary alimjua fika sajenti minja,
akawashtua wenzake, wote uoga
ukawaingia, wakatega masikio ili wasikie maongezi ya Sajenti Minja na
wenzake,
"ngoja nikapumzike, maana
nimechoka mno" Sajenti Minja alimwambia mwenzake,
"taxi hiyo imeingia sasa hivi, ongea na dereva
akupeleke" mwenzake alimjibu huku
akinyooshea kidole gari waliomo ndani
wakina kayoza,
"poa basi, tutakutana kesho ili tujue ofisi itasema nini kuhusu hili tukio" Sajenti Minja aliongea Kisha
akapeana mikono na mwenzake ikiwa ni ishara ya kuagana.
Alafu akawa anaelekea kwenye gari ambalo ndani wapo wakina Kayoza….
Sajenti Minja aliendelea kuisogelea ile taxi waliyokuwamo wakina kayoza,
"Au mkuu…" Dereva wa kwenye ile gari ya Polisi aliita na kumfanya Sajenti Minja asimame,
"Unasemaje tena Timo?" Sajenti Minja aliuliza huku akisimama,
"Njoo nikukimbize mara moja, maana nahisi waliopo ndani hawatatoka sasa hivi" Dereva wa gari la polisi aliongea,
"Ni jambo la kheri, ila wakitoka alafu wakakukosa?" Sajenti Minja aliuliza,
"Wewe twende tu, hata usijali" Dereva wa Gari ya polisi alijibu na kumfanya Sajenti Minja aache kuifuata gari waliyokuwepo wakina Kayoza na kurudi kuipanda gari ya Polisi, kisha ikaondoka.
Wakina Omary walikuwa katika taxi walishuhudia kila hatua iliyokuwa inafanywa na Sajenti Minja, na kila mmoja tumbo lilikuwa na joto,
"Umeshakuwa mkosi huu, hamna ya kushuka, bora tuondoke tu" Omary aliongea huku akitetemeka,
"Na hivyo vidonda vyako vitapona vipi bila kutibiwa?" Denis alimuuliza Omary,
"Tutajua mbele ya safari" Omary alijibu,
"Usije ukaoza mgongo" Denis alimtahadharisha Omary,
"Dereva ebu tupeleke Lodge yoyote iliyo karibu na Stendi ya mabasi ya mikoani" Kayoza aliongea baada ya ukimya wa muda mrefu na kuwafanya wenzie wamuangalie,
"Vipi, unajisikiaje bab?" Omary alimuuliza kayoza huku akimshangaa,
"Tutaenda kuulizana mbele ya safari" Kayoza alijibu huku akijishangaa alivyochafuka kama alilala kwenye vumbi.
Dereva wa taxi aliindoa gari eneo la hospitali na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye eneo ambalo aliamini zinapatikana nyumba za wageni na pia ni jirani na stand ya mkoa wa Dodoma, na kuwashusha hapo,
"Shilingi ngapi unatudai?" Omary alimuuliza Dereva baada ya kushusha mabegi yao,
"Kwa mizunguko tuliyofanya, uwa nafanya shilingi elfu kumi na tano, kwa kuwa nyinyi Mi washkaji, nitawafanyia elfu kumi" Dereva taxi aliongea huku akitabasamu,
"Punguza bwana, sisi tuna elfu saba" Omary aliongea kwa kulalamika,
"Suka shika pesa yako" Kayoza aliongea huku akimpa noti ya shilingi elfu Dereva taxi,
"Ungesubiri kwanza nimsaundishe" Omary aliongea huku akimlaumu Kayoza,
"Hakuna kusaundishana hapa, unapoteza muda tu" Denis aliongea huku akibeba begi lake na kuingia ndani, Kayoza akamfatia.
"Niachie namba yako, kesho asubuhi tunaweza kukupigia utufuate ili utupeleke stand" Omary alimwambia Dereva taxi,
"Stand si hapo nyuma tu, mnaweza kwenda hata kwa mguu" Dereva taxi alimjibu Omary,
"Wewe nipe tu hizo namba, unakuwa kama sio mfanyabiashara bwana" Omary aliongea na kumfanya Dereva taxi ampe namba zake za simu na kisha wakaagana.
Omary akachukua begi lake na kuingia nalo ndani, kwa bahati nzuri aliwakuta wenzake wakimsubiri mapokezi,
"Jamaa unatuyeyusha sana" Denis alimwambia Omary huku wakielekea sehemu vyumba vilipo,
"Nawayeyusha na nini sasa?" Omary alihoji huku akiwafuata wenzake,
"Sasa muda wote ulikuwa unaongea nini na Dereva?" Kayoza alimuuliza Omary,
"Nilikuwa nachukua namba ya simu ya Dereva" Omary alimjibu kayoza,
"Sasa namba ya simu ya nini wakati stand ipo karibu?" Denis aliuliza,
"Hamuwezi jua, kama sio kesho anaweza kuwa msaada siku nyingine" Omary alijibu wakati Denis akiufungua mlango wa chumba walichotakiwa kulala,
"Alafu huo ujinga wako uachage. Kwanza jana ilikuwaje mpaka ukakamatwa?" Denis aliuliza wakati akikaa kitandani,
"Dah, ilikuwa kama movie yaani" Omary aliongea huku akicheka utadhani anasimulia jambo zuri,
"Hivi utakua lini wewe?" Kayoza aliuliza kwa hasira,
"Kwani nimefanyaje boy?" Omary aliuliza huku akimshangaa Kayoza,
"Wewe si umeulizwa ilikuwaje ukakamatwa jana? Badala ya kujibu unaleta utoto" Kayoza aliongea huku akivua suruali,
"Sasa si ndio nilikuwa naanza kujibu?" Omary aliongea,
"Jibu sasa, acheni kulumbana" Denis aliongea huku akimuangalia Omary.
Omary akaelezea mwanzo mpaka mwisho wa kukamatwa kwake na mpaka Mipango ilivyosukwa na Sajenti Minja ili kuwaingiza mtegoni Kayoza na Denis.
"Sajenti Minja ndiyo nani?" Denis aliuliza,
"Yule polisi aliyetaka kuja kwenye taxi tuliyokuwepo" Omary alimjibu Denis wakati huo Kayoza alikuwa ameingia bafuni kuoga,
"Alafu tumuulize Kayoza ni kwa nini alikuwa katika umbo la kutisha namna ile kule lodge?" Omary alimshauri Denis,
"Kweli aisee, ila tutaanzaje sasa? maana anaogopesha" Denis aliuliza kwa mashaka,
"Hawezi kutufanya kitu bwana, kama angekuwa na lengo la kutudhuru, angetudhuru toka zamani" Omary aliongea kwa kujiamini,
"Kama ni hivyo ni sawa, ila utamuuliza wewe" Denis alimwambia Omary,
"Sawa, mimi nitamuuliza" Omary alijibu kisha nae akavua suruali kwa lengo la kwenda kuoga Kayoza akitoka bafuni.
Baada ya saa moja, wote watatu walikuwa tayari wameshaoga na kila mmoja alikuwa akiwaza jambo lake,
"Jamani eeh, wote tumebeba mabegi lakini hatujahambiana kila mmoja wapi anaelekea" Denis aliuliza baada ya ukimya wa muda mrefu,
"Sasa si tulikuwa na matatizo, unadhani huo muda wa kuambiana ungepatikana vipi?" Kayoza nae aliuliza,
"Mimi naenda Tanga, hadi hapo tayari nimeshawajibu" Omary alijibu huku macho yakiwa kwenye simu yake,
"Tanga kufanya nini? Wewe kwenu si ni kondoa wewe?" Denis alimuuliza Omary huku akicheka,
"Kule kuna babu yangu, sijamuona siku nyingi na inabidi nikamuone kwanza kama wiki mbili hivi" Omary aliwaelezea wenzake,
"Na wewe Kayoza unaenda wapi?" Denis alimuuliza kayoza,
"Mimi nitaenda Bukoba" Kayoza alijibu,
"Mimi kama kawaida, Dar hiyo" Denis aliongea kwa furaha,
"Nadhani tutaondoka pamoja ingawa tutapanda mabasi tofauti" Omary aliwaambia wenzake,
"Wazo zuri sana hilo" Denis aliongea kukubaliana na Omary,
"Ila ndugu yetu, ebu tueleze nini tatizo?" Omary alimuuliza Kayoza,
"Tatizo lipi?" Kayoza nae akamuuliza Omary na kufanya washangaane,
"Hujui au?" Omary aliuliza kwa upole,
"Sio sijui, ebu liweke swali lako vizuri ili nijue nianzie kujibu wapi" Kayoza nae alijibu kwa upole,
"Sawa. Ilikuwaje ukawaua wakina Stellah kule Guest?" Omary aliuliza huku akiwa na wasiwasi kidogo,
"Dah, sijui nianzaje kujibu, ila kifupi Stellah naweza kusema sijamuua ila Tausi nilimuua bila kutegemea" Kayoza alijibu huku machozi yakimtoka kuonesha kujutia kile alichokifanya,
"Sasa kama hukumuua Stellah ni nani alimuua wakati mlikuwa peke yenu chumbani?" Denis aliuliza,
"Mimi sijui ndugu zangu, niliamka asubuhi nikamkuta katika hali ile na sijui nini kilitokea" Kayoza alijitetea,
"Na Kwanini ulimuua Tausi?" Omary aliendelea kuuliza,
"Tausi nilimuua bahati mbaya baada ya kumziba mdomo asipige kelele alipouona mwili wa stelah, Kumbe wakati namziba mdomo nilimziba na pua akajikuta anashindwa kupumua" Kayoza aliwaeleza wenzake,
"Hiyo hali ya kubadilika na kuwa kiumbe cha kutisha inatokana na nini?" Denis alimuuliza Kayoza,
"Mimi?" Kayoza aliuliza huku akijioneshea kidole,
"Sasa kwani naongea na nani?" Denis nae aliuliza huku amemtolea macho Kayoza,
"Mnanishangaza mjue, mimi sijaiona hiyo hali initokee" Kayoza alitoa jibu lililofanya wenzake waangaliane,
"Tulivyoingia kwenye chumba alichoruelekeza Omary tumfuate, ulifanya nini?" Denis alimkumbusha Kayoza,
"Si tuliwakuta polisi watatu, alafu sikumbuki kitu zaidi ya kujikuta nimelala barabarani" Kayoza alitoa jibu jingine lililowashangaza wenzake,
"Makubwa basi, Ngoja nilale mie" Omary aliongea kisha akajifunika shuka na kuwaacha wenzake wakiendelea kuongea.
Saa kumi na moja alfajili waliamka na kuanza kujitayarisha kwa ajili ya safari.
Ilipotimia saa kumi na mbili kila mtu alikuwa tayari na wakatoka mpaka mapokezi, wakakabidhi chumba na kuondoka kuelekea stand ya mabasi, walitembea kwa miguu tu kwa maana haikuwa mbali na lodge waliyoichukua.
Walipofika karibu na Stand walishangaa kuona Askari wakiwa wengi, wamejitawanya eneo lile la Stand ya mabasi,
"Nadhani wako Pale kwa ajili yetu" Kayoza aliongea huku akisimama na wenzake pia wakasimama,
"Dah, kweli imeshakuwa tabu" Denis aliongea kwa kukata tamaa,
"Tunafanyaje sasa?" kayoza aliuliza,
"Turudi tukajipange" Denis alijibu,
"Hapa hakuna kurudi, ngojeni kwanza" Omary aliongea huku akiitoa simu yake na kumpigia Dereva taxi,
"Kwa hiyo akishakuja ndio tunafanyaje?" Kayoza aliuliza,
"Anatupeleka mpaka nje ya mji, alafu uko mbele tutashuka kuyasubiri mabasi" Omary aliwaambia wenzake,
"Hapo umefanya vizuri" Denis alimpingeza mwenzake kisha wakasubiri dakika kadhaa na taxi ikaja kuwachukua,
"Mpaka nzuguni utadai shilingi ngapi?" Omary alimuuliza dereva taxi,
"Elfu kumi na tano tu bosi wangu" Dereva taxi alijibu kwa unyenyekevu,
"Twendeni wanangu" Omary akawaambia wenzake ambao waliingia ndani ya gari.
Safari ikaanza, ubaya ilikuwa ni lazima upite karibu na Stand, wakati wanapita eneo hilo kulikuwa na gari ya polisi imeegeshwa pembeni huku likiwa na Askari wamekaa pembeni yake.
Gari waliyopanda wakina kayoza ikasimamishwa na wale Askari,
"Usisimame wewe" Omary alimsisitizia Dereva taxi ambaye alikuwa anataka kusimama,
"Kwanini nisisimame? Au nyie waarifu?" Dereva taxi alijibu huku akisimama,
"Acha upumbavu wewe" Denis aliyekaa kiti cha mbele aliongea huku akimsukumia Dereva nje na yeye akakaa kwenye kiti cha Dereva na kuiondoa gari kwa kasi.
Polisi kuona hivyo nao wakawasha gari yao na kuanza kuifukuza ile gari waliyokuwemo wakina Kayoza.
"Umefanya jambo la maana sana. Kumbe nawe ni jasiri hivyo?" Omary aliongea kumpongeza Denis kutokana na tukio alilolifanya,
"Ilikuwa haina namna" Denis aliongea huku macho yakiwa mbele,
"Lakini umeona wako nyuma wanatufuata?" Kayoza aliongea huku macho yake yakiwa nyuma,
"Nimeshawaona, hapa tuombe tu gari iwe na mafuta ya kutosha, vinginevyo hawatupati"
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi