Mwandishi: Alex Kileo
SEHEMU YA TANO
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
"mimi ni kaka yake" Denis alijibu,
"Sawa, mdogo wako anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuua wasichana wawili akishirikiana na wenzake ambao nao bado wanatafutwa"
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
"Sawa, nipe dakika kumi nitakuja hapo" Denis
akamalizia kisha akakata simu na kuanza kupumua kwa nguvu,
"kaka kumeshaharibika, beba mabegi tuondoke" Denis alimwambia kayoza,
"Sikuelewi, ebu nyoosha maelezo" Kayoza aliongea huku akimuangalia kwa makini Denis,
"Omary amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ya pale guest" Denis alimjibu Kayoza,
"Mimi si niliwaambia hapa sio pa kukaa tena?" Kayoza aliuliza huku hiyo habari ikionekana kumgusa,
"Hakuna muda wa kubishana hapa" Denis aliongea kwa ukali kisha wakabeba mabegi yao haraka, safari ya
kwenda mjini ikaanza.
Omari baada ya kuchukuliwa na
polisi, alifkishwa kituoni kwa ajili ya mahojiano hawali.
"unaitwa Omary Said
Mkwiju, si ndio hivyo?" Sajenti Minja alikuwa anamuuliza Omary huku
kashuka kitambulisho cha Omary,
"ndio" Omary akajibu.
"sisi hatuna ubaya na wewe, ila ukweli wako ndiyo
utaokusaidia" Sajenti Minja alianza kwa mtindo huo, kisha akaendelea,
"mlikua watatu,
wenzako wako wapi mlioshirikiana
nao katika mauaji?"
"jaman mimi sijaua,
huyu dada kanifananisha" Omary alijitetea huku macho yakiwa makavu,
"mchukueni mmuweke
ndani, naona hayuko tayari kutoa ushirikiano" Sajenti Minja alitoa amri.
Omary akabebwa juu juu akapelekwa
Selo ingawa aliendelea kulalamika anaonewa kwani yeye hajui chochote kuhusu vifo vya hao wasichana.
"Kwanini asipelekwe magereza kabisa" Askari mmoja aliuliza,
"Muacheni huku kwanza, nitamrudia usiku" Sajenti Minja alijibu huku akichukua koti lake la suti alilokuwa amelitundika ukutani, na kisha aliondoka.
Usiku Sajenti Minja alirudi
tena, akaongea na askari wa zamu, kisha Omary akatolewa nje, akavuliwa
nguo zote, kisha akaanza kuhojiwa tena, ila bado alikua mbishi,
wakaitwa watu wanne waliokuwa wameshiba
haswa, ni mijibaba ya miraba minne,
wakaamrishwa wamchape.
walimchapa haswa. Hadi akalainika, akawataja wenzake. Mda huo huo wa usiku Sajenti Minja akamfundisha
Omari jinsi ya kuongea na simu, kisha akawapgia wakina wakina
kayoza.
"oya mko wapi wana?" Omary alianza kuongea
hivyo,
"vipi, wewe si uko polisi?" Kayoza
aliuliza huku akishangaa mwenyewe,
"ni habari ndefu ila
wameniachia, wamedai
wamenifananisha, wamenipa hela
kwa ajili usumbufu" Omary alijibu huku akishusha pumzi ndefu,
"ehe siku hizi polisi wanatoa hela!?, aya
upo wapi?" Kayoza aliuliza,
"Mi niko guest moja hivi karibu na Railway,
nimeona giza limeshaingia nikaona bora nipumzike tu kwa maana polisi wamenisumbua sana. Nyie mko
wapi?" Omari aliuliza,
"tupe ramani tukufuate hapo ulipo kwa maana hata mabegi yako ya nguo tumekubebea" Kayoza alimwambia Omary,
"Chukuenu bajaji, mwambieni awapeleke kilimani lodge, mtanikuta hapo" Omary aliongea huku Sajenti Minja akiwa pembeni akimfundisha maneno ya kuongea na kisha akakata simu.
Baada ya mtego wa Sajenti Minja kukamilika na kufanikiwa kwa
asilimia nyingi, akachukua taxi, kwa maana aliogopa kwenda na gari ya polisi kwa kuwa endapo wakina kayoza wataiona kipindi wamawasili, basi wanaweza kukimbia.
Sajenti Minja alichukua taxi na askari watatu wenye bunduki, wakafunga safari hadi eneo walilopanga kukutana na wakina Kayoza, akachukua chumba,
kisha wakamuingza omari na askari wote watatu wakaingia chumbani kwa ajili ya kuwakamata wakina Kayoza pindi watakapofika, kisha Sajenti Minja yeye alirudi
nje kakaa ndani ya ile taxi na Dereva, huku akifuatilia kila kinachoendelea nje.
Wakina kayoza walipofika Kilimani lodge, wakampigia simu Omary,
"Tumefika, tupo nje hapa" Denis aliongea baada ya Omary kupokea simu,
"njoon chumba namba
7" Omary akawaambia wenzake ambao walimlipa dereva wa bajaji pesa waliyokubaliana nae, kisha wakabeba mabegi yao na kuelekea ndani.
Sajenti Minja hakuwa na wasiwasi na vijana wake,
aliona jinsi wakina Kayoza wanavyopiga simu na aliwasikia pia wanachoongea na Omary,
ila hakua na pupa, aliamini wakina Kayoza wanaenda kukamatwa na vijana wake aliowaweka chumbani pamoja na Omary, kwa hiyo akaacha vijana wake wafanye kazi.
Denis na Kayoza
walipofika mlango namba 7, wakagonga mlango, na Omary akafungua,
"Karibuni ndani, ingieni" Omary aliongea huku akiwa amechangamka na wakina Kayoza wakaingia ndani bila kujua katika hicho chumba walichoingia,wapo Askari watatu wenye bunduki wakiwasubiri wao…..
wakakaribishwa na mdomo wa
bunduki,
"mko chini ya ulinzi" Polisi
mwenye bunduki aliwaambia. Ghafla
bin vuu, kayoza alimrukia yule askari
mwenye bunduki, akatua shingoni
mwake, ila hakumnyonya damu, badala yake yule Askari alipokea kofi zito na kuanguka chini huku bunduki yake ikidondokea chini ya kitanda.
Yaani hapo Kayoza alikuwa tayari kishabadilika,
macho yamekua meupe, meno yamechomoza.
Askari wa pili kuona
vile, nae akaokota bunduki,
akamfyatulia Kayoza risasi, Kayoza
akamuacha Askari wa kwanza, akamrukia wa
pili nae akamtandika kofi lilimfanya apoteze fahamu, yule
askari wa tatu kuona vile akakimbilia
mlangoni, Omari akachukua bunduki,
akampiga risasi ya mgongoni na akadondoka
pale pale.
Kayoza akiwa katika hali ile ile, akaenda dirishani akavunja nondo za madirisha, alikuwa na nguvu kama mnyama na alikuwa akiunguruma kama Simba.
Alipomaliza kuvunja zile nondo za madirisha, akawarudia wale Askari ambao wawili walikuwa hawana fahamu na mmoja alikuwa anaugulia maumivu baada ya kupigwa risasi ya mgongoni.
Akasukumia wale majeruhi chini ya
kitanda kisha akawaangalia wenzake ambao walikuwa wamekaa kwenye kona moja Pale chumbani huku wakiwa na hofu kutokana na muonekano wa Kayoza, kwa maana hawajawahi kumuona hivyo kabla.
Kayoza akarudisha macho dirishani na kisha akatokea dirishani, wenzake wakabaki wanaangalia,
"Bab umeiona hiyo?" Omary alimuuliza Denis,
"Ebu tutoke kwanza hapa, hayo tutayajadili baadae" Denis alijibu kwa upole,
"Poa twende basi" Omary aliongea huku akianza kuondoka kuelekea mlangoni,
"Usipitie uko wewe" Denis alimwambia mwenzie,
"Sasa na sisi tupitie dirishani?" Omary aliuliza,
"Hiyo ndio njia sahihi kwetu, maana nahisi Polisi wengine watakuwa nje" Denis aliongea,
"Sio unahisi, ni kweli kuna Polisi nje" Omary aliongea baada ya kukumbuka kuwa Sajenti Minja alibaki nje. Wakatoka nje wote kwa kupitia dirishani huku wakibeba mabegi yao na begi la Kayoza.
Nje, Sajenti Minja baada ya kusubiri muda mrefu
bila majibu, akapata wasiwasi, mara
akasikia mlio wa bunduki,
akakurupuka kwa kasi hadi mlango mkuu wa kuingilia ile guest, alipata
shida kuingia, kutokana na wingi wa
wapangaji ambao walikua wanatoka
huku wanakimbia baada ya wao kusikia pia mlio wa bunduki. Mara mlio
mwingne wa bunduki ukasikika.
Sajenti Minja akafanya juhudi binafsi, mpaka
akafanikiwa kuingia, alipofika mlangoni, akausukuma mlango lakini
haukufunguka, kipindi iko
wahudumu walikuwa wanamuangalia
tu,
"nipeni ufunguo wa hapa" Sajenti Minja akawaambia wale wahudumu waliokuwa wanamtolea macho,
"mwenye funguo
kakimbilia nje" wahudumu wakamjibu,
"Sawa, mimi navunja sasa" Sajenti Minja aliongea huku akionekana ana hasira,
"huwez kuvunja bila meneja wetu
kuwepo" Wahudumu wakamjibu.
Mara kwenye mlango mkubwa wa kuingilia ile Guest wakaingia askari wanne, wote
wamebeba bunduki, nyuma yao
anaonekana askari mwingine mrefu,
mweupe ana mwili wa mazoezi, huyu
anaitwa Afande Juma Ally Mbago.
"Sajenti Minja, umefika saa ngapi huku" Afande Mbago alimuuliza
Minja aliyemkuta eneo hilo na kisha Sajenti Minja akampa mkasa
mzima hadi yeye kuwepo pale.
"kama wamesema ufunguo hawana vunjeni
mlango" Afande Mbago aliwaamuru vijana wake.
Vijana wakavunja
mlango, walipoingia tu, wakakuta
dirishani hakuna nondo,
"bwana Minja si umesema, vijana wako
walikuwepo humu pia?" Afande Mbago aliuliza,
"ndio," Sajenti Minja
akajibu,
"sasa mbona hamna mtu
humu?" Afande Mbago akauliza tena,
"hata mimi nashangaa" Minja akajibu huku akishangaa.
Askari mmoja akapanda kitandani ili aende
karibu ya dirisha, alipofika mwisho
wa kitanda, akaangalia chini
akashtuka, tena alishtuka haswa,
"kuna mtu chini ya
kitanda" Askari akalopoka huku macho yakiangalia chini ilipokuwepo miili ya wale Askari waliopoteza fahamu. Wakavuta
kitanda, wakakuta miili ya askari
watatu ambao alikuja nao Sajenti
Minja,
"Wazima kweli hawa?" Sajenti Minja aliuliza huku hali ya hofu ikimuingia kuhusu watu anawafuatilia,
"Wote wazima" Afande Mbago alijibu baada ya kuwakagua kisha wakawachukua na wakawapakia kwenye gari la
Polisi, safari ya kuwapeleka hospitali
ikaanza.
kayoza akiwa katika hali yake ya kutisha,
aliendelea kukimbia,
mbele kidogo akadondoka chini, akawa
anajigeuza geuza kama mtu anayekata roho, mara akatulia kama mtu aliyekufa.
Wenzake ambao ni Denis na Omary walikuwa pia wanakimbia huku wakiwa hawana uhakika wa kumpata mwenzao, ila wakiwa katika marathon hizo, ndipo walipomkuta Kayoza akiwa amelala chini.
"Kafa au?" Omary alimuuliza mwenzake huku kila mmoja akiwa na uoga wa kumsogelea Kayoza kutokana na hali waliyoiona Pale lodge,
"Sijui" Denis alijibu. Baada ya muda wa mrefu wa sintofahamu kati yao, mwisho walijitoa mhanga na kuusogelea mwili wa Kayoza na kugundua kuwa amepoteza fahamu, ila baada ya muda kidogo fahamu zilimrudia na akarudi kwenye
hali yake ya kawaida, ila mwili wake haukuwa na nguvu.
Wenzake wakambeba, ila bahati nzuri wakaona taxi inakuja, wakaisimamisha, kisha wote wakaingia ndani ya ile taxi.
"tupeleke hospitali yoyote
Iliyo karibu na hapa" Omary akamwambia dereva
taxi,
"hospital kufanya nini?, we mjinga nini" Denis akaongea kwa ukali,
"polisi wamenitandika sana mgongoni, kwa hiyo nina vidonda vikubwa sana mgongoni" Omari
alimwambia Denis huku
akimuonesha hivyo vidonda,
"poa, suka twende hospital" Denis
akakubali baada ya kuviona hivyo vidonda.
Walipofika hospitali, gari
ikawa inaelekea sehemu ya maegesho, ilipofika ikasimama pembeni ya gari la polisi, wakati wanataka kushuka, Mara ghafla Sajenti Minja
akawa anatoka ndani ya hospitali na
kuelekea sehemu ya maegesho ya magari.
Akaenda mpaka ilipopaki gari ya polisi,
akawa anaongea na mwenzake
kuhusu ishu iliyopelekea wale askari
wenzake kuwa vile, na kibaya zaidi ni kwamba alimwambia mwenzake kuwa wale Askari wote wameshakufa, tena aliongea kwa hasira mpaka machozi yakawa yanamtoka.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi