SHETANI ALINIITA KUZIMU (10)

0

SEHEMU YA KUMI
TULIPOISHIA...
Aidha, wengine walikuwa na miguu yenye kwato kama za ng’ombe na vichwa vyao vilifanana na vya paka, vifua vyao vilikuwa sawa na vya binadamu na kulikuwa na wanawake wazuri sana. Nikiwa naendelea kutembea bila kumuona Lusifa niliyekuwa nikiongea naye, nilimuuliza kwa nini aliwadanganya Adam na Eva wakala lile tunda la mti wa katikati?.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
“Niliwadanga kwa sababu siku zote napenda binadamu wawe chini yangu kama nami ninavyotakiwa kuwa chini ya aliyeumba dunia hii ambaye tayari amenihukumu,” Lusifa aliniambia. Baada ya

kuniambia hivyo, nilimwambia anipatie magonjwa niliyomuomba pamoja na dawa za kuyatibu ili nirudi duniani, akaniambia atanipatia kwa sababu aliniahidi.

Lusifa aliniambia nigeuke nyuma nimuone nyoka aliyewadanganya Adam na Eva, nilipogeuka niliona joka kubwa sana, nikashtuka! Joka hilo lilikuwa na miiba mwili

mzima na kichwani lilikuwa na pembe mbili fupi ambazo zilivalishwa pete zilizokuwa zinang’aa. Lusifa ambaye hakutaka kujitokeza aliniuliza niliona nini

kichwani kwa joka hilo, nikamwambia pembe zilizovishwa pete, akacheka. “Haya lifuate joka hilo kisha kwa kutumia mkono wako wa kuume chukua pete moja kisha

uivae katika kidole chako cha mkono wa kulia.” Kwa kuwa nilikuwa naliogopa joka hilo, nilimwambia nisingeweza akaniambia nisiogope halitanidhuru ndipo

nililifuata na kuvua pete moja ya dhahabu na kuivaa kidoleni, mwili ukanisisimka. Pete hiyo ilikuwa inang’aa kama kioo na nilipojitazama niliweza kuiona sura

yangu, nikamwambia Lusifa tayari nilikuwa nimevaa. Lusifa alinieleza kwamba ile pete ilikuwa na kila kitu, kwa kuwa sikuelewa alimaanisha nini nikamuuliza

ndipo alisema; “Hiyo pete ina mambo mengi sana na itakusaidia kwa kila unachotaka kufanya, unachotakiwa kufanya ni kuiomba kitu chochote utapata.”

Nilipoingia mle chumbani kichawi nilimrushia pepo mchafu ili amvuruge akili ndipo mchungaji huyo aliyekuwa ametoka Kongo na alikuja jijini Dar es Salaam kufanya mikutano ya Injili, akashtuka na kuamka.

Alipoamka akaanza kunikemea kwa lugha ya Kikongo ambayo sikuielewa, wakati akifanya hivyo alikuwa akilia na machozi kumtiririka mashavuni.

Jambo lingine lililonishangaza, alikuwa akitokwa na jasho jingi mwilini licha ya kwamba kile chumba kilikuwa na kiyoyozi.

Wakati akinikemea, yule mwenyeji wake naye aliamka akaungana naye kunikemea ambapo alitamka maneno yafuatayo:

“Katika jina la Yesu Shetani toka rudi kuzimu, hauna mamlaka yoyote juu ya watoto wa Mungu, rudi katika makazi yako nyiye pepo wachafu toka!

“Nawaamuru nyiye pepo wachafu toka rudini mlikotoka…hamna mamlaka katika hii dunia kwa jina la Yesu toka!”

Wakati wakinishambulia kwa maombi sikukubali kuondoka nikawa nawasogelea ili niliwarushie moto lakini nilishindwa.

Kutokana na maombi yao mazito, walifanikiwa kunimaliza nguvu zangu lakini nami nilifanikiwa kumdhibiti yule mchungaji mwenyeji ambaye alianguka chini na kupoteza fahamu.

Yule mchungaji wa Kongo alipomuona mwenzake amelala chini, alichukua begi dogo lililokuwa pembeni ya kitanda, akalifungua na kutoa kichupa.

Wakati akifanya hivyo nilikuwa ninamwangalia kwa makini ndipo alichukua Biblia na kuishika pamoja na ile chupa, ghafla nikiwa kama pepo niliondoka na kuuacha mwili wangu wa asili.

Kukufafanulia hapo ni kwamba, mchawi anapokutana na nguvu za Mungu, nguvu za giza au mapepo yaliyomo mwilini mwake huondoka na kurudi yalikotoka na kuuacha mwili ukiwa huru.

Nikiwa katika nafsi hiyo ya kichawi, nilipofika kuzimu nikaanza kumuita Lusifa kwa kusema: “Baba, baba, baba!”

Lusifa aliitika na kunipa pole na kuniambia kwamba alikuwa akiniona jinsi nilivyokuwa katika vita kubwa na binadamu wenzangu.

Lusifa alirudia kunipa pole ndipo aliniuliza kama nilikuwa napenda kuendelea kumtumikia, nikamwambia nitaendelea.

Baada ya kumwambia hivyo, alinishukuru na kuniambia kitu alichokuwa akikihitaji ilikuwa sadaka ya damu ya wazazi na ndugu zangu wote.

Tofauti na siku nyingine zote alizokuwa akizungumza nami, alikuwa akitoa kauli hiyo kwa ukali sana mpaka nikaogopa!

“Kijana sasa unatakiwa kutoa sadaka ya damu ya wazazi na ndugu zako wote ndipo utakuwa tajiri mkubwa, nasisitiza kwamba muda wako wa kutoa damu umefika, umenielewa?” David anasema Lusifa alimwambia kwa ukali.

Baada ya kuniambia hivyo, nilisita kumjibu akaniuliza kwa nini nilikaa kimya, nikamwambia sitaweza kufanya hivyo, akacheka sana.

Alipomaliza kucheka akasema au anibadilishie masharti, nikamwambia sawa ndipo alisema nitafanyanaye mkataba mwingine wa kuwa tajiri kwa miaka 36.

Lusifa aliponiambia hivyo bila kujua ningepewa masharti gani nilifurahi sana na kumwambia nilikuwa tayari kutimiza masharti hayo lakini siyo kuwaua wazazi na ndugu zangu.

Baada ya kumweleza hivyo, aliniambia kuwa atanipa utajiri wa miaka 36, muda huo ukiisha nitatakiwa kuondoka kwenye sura ya dunia na kwenda kuishi kuzimu.

Alisema huo utakuwa mkataba wetu mimi na yeye lakini kama siku zangu za kuishi duniani zitafika mwisho kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu aliyeniumba, nitakufa muda wowote.

Kwa kuwa nilichokuwa nikihitaji ni utajiri, sikufikiria suala la kifo, nikamwambia tuwekeane mkataba huo ili nianze kufurahia maisha.

Baada ya kumwambia hivyo, Lusifa ambaye sikubahatika kumuona, alicheka sana na kuniambia nigeuke nyuma.

Nilipogeuka nililiona lile joka la kutisha ndipo aliniambia nikaichukue ile pete iliyokuwa imebaki juu ya pembe yake kisha niivae na kurudi nilipokuwa nimesimama.

Kwa kuwa sikuwa muoga, nilijongea mpaka lilipokuwa lile joka, nikatoa ile pete ya dhahabu iliyokuwa iking’aa sana na kuivaa katika kidole changu.

Niliporejea sehemu niliyokuwepo, Lusifa aliniambia kitendo cha kuivaa pete hiyo, tayari tuliwekeana mkataba na kwamba niiombe kitu chochote nitapata.

Alipomaliza kuniambia hivyo aliniaga na kunitakia safari njema ya kurudi duniani, nilimshukuru kwa kunipatia utajiri niliokuwa nautaka.

Lusifa alipoondoka nilirudi duniani nikiwa katika hali ya pepo na kutokea katika daraja la Salenda.

Kwa kuwa sikuwa na mwili wa kawaida baada mwili wangu halisi kuuacha pale hotelini, nilipokutana na wale wachungaji walionikemea na kuharibu nguvu zangu, niliamua kuufuata.

Mpenzi msomaji, kukufafanulia hapo ni kwamba mtu anapokuwa na mapepo anaweza kuuacha mwili wake halisi sehemu yoyote bila mtu ambaye hana nguvu za kichawi au Mungu kutambua.

Mwili halisi wa mtu anayeishi na mapepo, huweza kutenganishwa na mapepo kwa njia ya maombi au mchawi husika kuuacha sehemu anayoitaka mwenyewe.

Kwa upande wangu mwili wangu ulibaki pale hoteilini kufuatia kukemewa kwa jina la Yesu na wale wachungaji ndipo kabla ya kuanza kufanya kitu chochote niliamua kuufuata.

Nilipofika pale hotelini sikuukuta, kwa kuwa nilikuwa nina mapepo waliokuwa wakiniongoza nilibaini mwili wangu ulikuwa ukiombewa kanisani.

Hapo tena ngoja nifafanue, mtu mwenye mapepo anapoombewa yale mapepo huweza kuondoka na kuuacha mwili ambao watu wa kawaida wanaweza kufikiri ni binadamu halisi.

Hivyo ndivyo ilivyotokea kwangu, wale wachungaji waliponizidi nguvu nilibaki pale hotelini ambapo walinichukua na kunipeleka kunifanyia maombi kanisani kwao.

Sasa nilipogundua nilikuwa nimepelekwa kanisani, niliondoka nikiwa na nafsi ya kimapepo kuufuata mwili wangu.

Nilipofika kanisani, mapepo yangu yalifanikiwa kuingia kwenye mwili wangu lakini kabla sijafanikiwa kutoka nilisikia nimepigwa na kitu kizito kichwani.

Baada ya kupigwa na kitu hicho, kichwa kikawa kizito, nikaanza kuona maghorofa yote yaliyopo Posta yanazunguka kisha mwili wote ukaanza kuwaka moto.

Baada ya kupigwa na kitu hicho, kichwa kikawa kizito, nikaanza kuona maghorofa yote yaliyopo Posta yanazunguka na mwili wote ukaanza kuwaka moto. Kufuatia

maumivu ya moto niliyoyapata nikaanza kupiga kelele huku nikiomba msaada lakini sikupewa. Wakati nikilia nikasikia mapepo waliokuwa ndani ya zile pete

nilizopewa na Lusifa nao wakilia huku zile pete zikinichoma ndipo nilizivua na kuzitupa chini. Baada ya kuzitupa nikasikia yale mapepo ya kwenye pete

yakisema: “Tunarudi kwa baba yetu…hapa hapatufai…umetuleta wapi hapa hawa watu wanatuchoma moto.” Yale mapepo yalilalamika sana ndipo sauti zao zikaanza

kusikika kwa mbali kisha zikatoweka kabisa, kwa hali niliyokuwanayo nikalala na kupitiwa na usingizi mzito. Nikiwa nimelala fofofo nikaota ndoto nipo sehemu

yenye giza nene, kwa kuwa nilijua mahali pale hapakuwa salama nilianza kutembea bila kujua nilikokuwa nikienda. Baada ya kutembea kama mita ishirini hivi,

ghafla nilimulikwa na mwanga mkali ulionifanya nishindwe kuangalia, nikainamisha kichwa. Hata baada ya kufanya hivyo, nilihisi joto kali usoni kwangu ndipo

nikasikia mtu akiniamuru niuangalia mwanga huo kwani haukuwa na madhara kwangu. Mtu huyo aliendelea kuniambia kwamba alielewa mambo mazito niliyokumbana nayo

hivyo alinifuata ili anirudishe nilikotoka. “Mimi ni Lusifa nisiyeshindwa vita yoyote, hao watu waliotaka kukuangamiza hawana nguvu zozote, nitawaangamiza…

sasa nimekufuata kijana wangu,” David alimkariri mtu huyo. Mtu huyo aliendelea kuniambia kwamba hatua niliyofikia ilikuwa kubwa sana ndiyo maana aliamua

kuingilia kati vita iliyokuwa mbele yangu. Baada ya kunieleza hivyo, ulitokea muungurumo mkubwa ghafla likatokea lile joka kubwa lililowahi kunitokea huko

nyuma. Jambo la kushangaza licha ya kuchukua pete mbili zilizokuwa kwenye pembe ya joka hilo kama nilivyoagizwa na Lusifa, siku hiyo lilikuwa na pete zingine

zilizong’aa sana. Lusifa ambaye sikuwahi kumuona moja kwa moja, aliniambia alichohitaji ni kuniona nakuwa tajiri na ile kazi ya kueneza magonjwa inafanyika

kama alivyopanga. “Eti wanajifanya wachungaji wanaolitumia jina la Yesu kuharibu kazi zetu wakati nao ni washirika wetu, sasa wameshindwa na wakiendelea

kutufuata nitawapa adhabu ya kuja kunitumikia milele,” David alimkariri Lusifa. Kukufafanulia hapo ni kwamba, kuna watu ambao wanajifanya watumishi wa Mungu

lakini wakati huohuo wanamtumikia shetani. Watu hao wanapoyakemea mapepo huweza kutii kwa muda kisha yanawazidi nguvu na kuwarudia watu waliowaombea. Hicho

ndicho kilichotokea kwangu, kwani baada ya kuombewa nililemewa lakini Lusifa mwenyewe alipoingilia kati aliwazidi nguvu wale wachungaji. Lile joka likiwa mbele yangu, nilisikia sauti ikiniambia kwamba, nikachukue pete ya kulia na kuivaa katika kidole cha shahada nikisubiri kupewa maagizo mengine. Kwa kuwa haikuwa mara ya kwanza kukutana na joka hilo, nililisogelea ambapo liliinamisha kichwa chake, nikavua ile pete iliyokuwa kwenye pembe yake na kuivaa kidoleni.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)