Mwandishi: Shiwawa Binasalaan Al Jabry
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Lile joka likiwa mbele yangu, nilisikia sauti ikiniambia kwamba, nikachukue pete ya kulia na kuivaa katika kidole cha shahada nikisubiri kupewa maagizo mengine. Kwa kuwa haikuwa mara ya kwanza kukutana na joka hilo, nililisogelea ambapo liliinamisha kichwa chake, nikavua ile pete iliyokuwa kwenye pembe yake na kuivaa kidoleni.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Tofauti na awali, baada ya kuivaa, mwili ulinisisimka sana ndipo ile sauti iliniambia nilirejewa na nguvu zote zilizoondolewa na wale wachungaji.
Mtu huyo aliniambia kwamba nilitakiwa kurudi tena kuzimu kwa kupitia njia niliyoelekezwa na yule mzee tajiri yaani kupitia lango la kuzimu ambalo lipo Daraja
la Salenda. Alisisitiza nifanye hivyo haraka, alipomaliza kutoa kauli hiyo nilisikia muungurumo mkubwa ndipo nikashtuka kutoka usingizini. Jambo la
kushangaza nilipoangalia vidoleni mwangu, niliziona pete mbili zilizokuwa zinang’aa sana, nikafurahi kwani nilijua muda si mrefu nitakuwa tajiri mkubwa.
Nikiwa mwenye furaha, nilianza kuitafakari kwa kina ndoto niliyoota, nigandua yale yalikuwa maagizo ya Lusifa aliyoamua kuniambia kupitia katika ndoto.
“Kijana unatakiwa kurudi tena kuzimu kwa kupitia njia uliyoelekezwa na yule mzee tajiri yaani kupitia lango la kuzimu ambalo lipo Daraja la Salenda, tena
ufanye hivyo haraka sana!” Niliyakumbuka maneno ya yule mtu aliyezungumza nami ndotoni. Baada ya kuyakumbuka maneno hayo, nilikumbuka pia tukio lililonipata
nilipokwenda kwenye ile hoteli iliyopo maeneo ya Posta Mpya kwa lengo la kuwapatia maradhi matajiri ili watakapoanza kuugua, nijitokeze kwamba naweza
kuwatibu na kujipatia umaarufu na fedha nyingi. Nilikubuka nilivyopoteza fahamu na kuishiwa nguvu kufuatia maombi ya wale wachungaji waliokuwa kwenye moja ya
chumba cha hoteli hiyo niliotaka kuwaua kwa kuhofia wangeharibu mambo yangu. “Hapa sitakiwi kukawia, usiku wa leo lazima niende kuzimu kwa Lusifa kama
nilivyoagizwa,” niliwaza. Kwa kuwa nilikuwa nipo katika hali yangu ya kawaida, niliondoka eneo nililokuwepo nikaenda Mnazi Mmoja lakini njaa ilikuwa inaniuma
sana. Kwa vile sikuwa na fedha, nilikwenda kwenye hoteli moja nikawaeleza hali halisi kwamba sikuwa na fedha hivyo wanisaidie chai, chapati tatu na maharage.
Jambo la kushangaza ni kwamba wale wahudumu waliniambia pale haikuwa sehemu ya kuomba msaada na kwamba niliwezaje kununua pete za dhahabu halafu nishindwe
fedha za kununua chai. Licha ya kuwabembeleza kwamba sikuwa na fedha kwa wakati huo, mmoja wa wahudumu aliniambia niwaondolee kiwingu, walitaka kuwahudumia
wateja wenye hela zao. Mwingine alinibeza kwa kusema, kama pete zilikuwa zinaliwa nile kwa sababu nilikuwa mtu wa ajabu kujali kuvaa vito vya thamani kuliko
kula. Kwa kweli kauli za wale wahudumu ziliniumiza sana kwani ukweli wa zile pete niliujua mwenyewe, nikajisemea moyoni kwamba watanitambua. Wakati wale
wahudumu wananiambia hivyo, kuna bwana mmoja alikuwa anasikia akaniambia niagize kitu chochote atanilipia kwani alikuwa anajua maisha yana kukosa na kupata.
Nilimshukuru sana yule kaka, nikamwita mmoja wa wale wahudumu na kumwambia aniletee vitu nilivyoagiza ndipo yule kaka akasema badala ya maharage waniletee
supu! Kufuatia kuelezwa hivyo, yule mhudumu alileta vitu nilivyoagiza ambapo yule kaka ambaye aliniambia ni mwenyeji wa Mkoa wa Mbeya alilipa kisha akaniaga
kwa ahadi ya kukutana siku yoyote. Nikiwa nakunywa supu na kula zile chapati, nilikuwa nawaza niwafanye nini wale wahudumu, sauti moja iliniambia kwa kuwa
nilikuwa nina nguvu za kichawi niwaue. Sauti nyingine ya upole iliniambia wale akina dada walikuwa na watoto, nikiwaua watoto wao watapata tabu sana kwani
ndiyo waliokuwa wakiwategemea. Kwa kuwa nilikuwa na roho ya kikatili, nilisema lazima niwakomeshe ndipo katika hali ya kichawi nilimnyoshea kidole yule
aliyeniambia nilithamini kununua pete za dhahabu badala ya chakula. Baada ya kurudisha kidole changu, alianza kulalamika kwamba tumbo linamuuma na kuangua
kilio hadi wateja wakapigwa na butwaa. Wafanyakazi wenzake walimshika na kuanza kumuuliza lilikuwa linamuumaje na wengine kumuuliza alikula nini, akashindwa
kuwajibu na kuendelea kulia, nikasema moyoni kwamba akome. Kufumba na kufumbua, akiwa amezungukwa na wafanyakazi wa kike, kiume na baadhi ya wateja, akaanza
kutiririkwa na damu nyepesi kama maji. Wanawake waliokuwa pale kuona mwenzao anaumbuka wakambeba na kumwingiza chumba cha stoo, moyoni nikasema: “Utatokwa na damu hiyo mwezi mzima shetani wewe!”
Wanawake waliokuwa pale kuona mwenzao anaumbuka walimbeba na kumwingiza chumba cha stoo, moyoni nikasema; “Utatokwa na damu hiyo mwezi mzima shetani wewe!”
Kutowashtua watu na kuhisi mimi nitakuwa mtu mbaya, yule mhudumu aliyebakia nilimpa ugonjwa wa kupiga kelele na kuweweseka lakini ‘niliuseti’ ukamuanzie
nyumbani kwao usiku. Kwa hasira nilizokuwanazo nilipanga kuwafuatilia hadi makwao mpaka roho yangu itakaporidhika ndiyo niwarudishie uzima wao. Wakati dada
huyo akiendelea kulia, jamaa mmoja aliyekuwa amemaliza kunywa supu na muda huo alikuwa akisoma gazeti alisikika akisema yule dada alilaaniwa kufuatia kitendo
alichonifanyia. Kufuatia kauli hiyo, dada mmoja ambaye alipoingia alinikuta nakunywa supu na hakuelewa kilichotokea awali alimuuliza yule kaka alilaaniwa na
nani? Yule kaka akamsimulia kila kitu kuhusu mimi ndipo yule dada akasema kuna watu huadhibiwa hapahapa duniani kwa roho zao mbaya. Wakati wale wateja
wanazungumza hivyo, wale wanawake walioingia na yule mhudumu stoo kwa lengo la kumsitiri walitoka naye huku akiendelea kulalamika kwamba tumbo lilimkata
sana, wakakodi gari na kumpeleka hospitali. Nilipomaliza kula, niliondoka bila kujua nilikokuwa nikielekea kwani jijini Dar nilikuwa bado mgeni lakini lengo
langu lilikuwa ni kwenda kwenye duka la dawa asili. Huko nilitaka kwenda kununua mayai viza mawili ya bundi na paka jike mweusi ambaye hakuwahi kupandwa na
dume kwa ajili ya safari yangu ya pili ya kwenda kuzimu kwa Lusifa. Baada ya kushindwa kukumbuka sehemu tuliyonunua vitu hivyo na yule mzee tajiri
aliyenileta jijini Dar na kuniwezesha kwenda kwa Lusifa kwa mara ya kwanza, nikaamua kuuliza. Nilipoamua kufanya hivyo nilimfuata mzee mmoja wa makamo na
kumuomba anielekeze sehemu yalipokuwa maduka ya dawa za asili. Kabla yule mzee hajanielekeza aliniangalia usoni kisha aliniuliza kama nilikuwa mgeni
nikamwambia ndiyo, akaniuliza nani alikuwa mgonjwa! Kutokana na maswali yake nikagundua watu wa Dar es Salaam walikuwa wanapenda sana kudadisi mambo ya watu,
nikamwambia hakuwepo mgonjwa isipokuwa kuna kitu nilitaka kwenda kununua. Jambo la kushangaza badala ya yule mzee kunielekeza aliniuliza nilikuwa natokea
Mwanza sehemu gani, nikaduwaa dakika kadhaa na kujiuliza alijuaje nilikuwa natokea Mwanza. Nami nikamuuliza alijuaje kama nilitokea Mwanza, akacheka na
kuniambia alijua tu, nikamuuliza kama alikuwa mganga akacheka tena. Hata hivyo, alinielekeza niende Sokoni Kariakoo na hapo nimuombe mtu yeyote anielekeze
yalipo maduka ya dawa asili, nikamshukuru. Kabla sijaachana na yule mzee wa mjini, alinitahadharisha niwe makini kama nilikuwa na fedha mfukoni kwa sababu
Jiji la Dar lilikuwa na wezi wengi. Aliponieleza hivyo nilimshukuru ndipo tuliagana nikaanza kuelekea Sokoni Kariakoo alikonielekeza, cha kushangaza mfukoni
sikuwa na hela yoyote. “Jambo la muhimu ni mimi kufika kwenye maduka hayo, najua nitapa hizo dawa kwani uwezo wa kufanya kila kitu ninao,” niliwaza. Wakati
nikielekea huko nikawa nashangaa karibu kila kitu nilichokiona na jinsi wakazi wa jiji hilo walivyokuwa shapu, nikajisemea moyoni kwamba ‘kweli hili ni
jijini la Dar es Salam’. Baada ya kutembea kama dakika ishirini na kwa kuwauliza watu, nilifika sokoni Kariakoo ambapo nilimuuliza kijana mmoja aliyekuwa anauza mifuko ya rambo yalipo maduka ya dawa asili akanionyesha
Nilipofika kwenye moja ya maduka hayo nilimuuliza kijana mmoja aliyevaa kikoi kama ningeweza kupata mayai viza ya bundi. Kabla kijana huyo hajanijibu
aliniangalia usoni na kuniambia hakuwa na mayai hayo, nikamuuliza ni wapi ningeweza kumpata paka mweusi ambaye hakuwahi kupandwa na dume. Kama alivyofanya
nilipomuulizia kuhusu mayai viza ya bundi, aliniangalia tena usoni na kuniambia hakuelewa sehemu aliyopatikana paka niliyemhitaji. Hata hivyo, alinishauri
niende nikamuulize mzee wa duka la tatu aliyenieleza angeweza kunisaidia kwa sababu alifanya biashara ya dawa za asili kwa muda mrefu. Wakati huo nilikuwa
sikumbuki kama katika yale maduka nilifika na yule mzee tajiri wa Mwanza aliyeniambia atanisaidia ili nami niwe tajiri kama yeye. Nilipofika kwenye lile duka
nililoelekezwa, yule mzee alinikumbuka na kuniambia; “Kijana habari za tangu siku ile na vipi baba yako hajambo?” Alifikiri yule mzee tajiri alikuwa baba
yangu. Nilimwambia sijambo na baba yangu nilimuacha mzima, akasema alifurahi sana kuniona tena. Yule mzee aliyekuwa mcheshi sana aliniuliza kama siku ile
tulifanikiwa kupata mayai viza ya bundi na paka tuliyemhitaji, nikamwambia tulifanikiwa. Baada ya kumwambia hivyo, aliniuliza nilihitaji anisaidie kitu gani,
nikamwambia anielekeze tena kule tulikopata mayai viza na paka mweusi. Kufuatia kumwambia hivyo aliniambia kwamba kwa kuwa nilikuwa mgeni angenipeleka kwa
mganga huyo wa jadi aliyefanikisha kupata mayai viza ya bundi na paka jike mweusi ambaye hakuwahi kupandwa na dume. Nilimshukuru sana yule mzee, nilimsubiri
mpaka jioni alipofunga duka lake tukaenda Manzese ‘ndanindani’ kwa yule mganga. Tulipofika yule mzee alimweleza shida yangu ambapo alinifahamisha kwamba kwa
wakati ule hakuwa na mayai viza ya bundi. Hata hivyo, alinifahamisha kwamba mayai hayo na paka niliyemhitaji angeenda kunichukulia Kisarawe mkoani Pwani kwa
mganga mwenzake. “Kule ndiko tutapata mayai na huyo paka kwani yule rafiki yangu amekuwa akiwafuga wanyama hao kwa sababu wana kazi nyingi zinazohusiana na uganga,” David anasema yule mganga wa Manzese aliwaambia. Kwa kuwa nilikuwa mteja wake na sikuwa na ndugu jijini Dar, alimwambia yule mzee niliyetoka naye
Kariakoo kwamba nitalala pale kwake hadi atakaponiletea paka na mayai viza ndipo niondoke. Yule mzee niliyetokanaye Kariakoo alimshukuru kisha alituaga
akarudi nyumbani kwake. Nikiwa kwa mganga huyo tuliongea mengi ambapo aliniuliza kuhusu kazi niliyotaka kuifanya kwa kutumia paka na mayai viza. Kufuatia kuniuliza hivyo, nilimdanganya kwamba ndugu yangu alikuwa mgonjwa na vitu hivyo niliagizwa na mtaalamu aliyekuwa akimtibia.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi