SHETANI ALINIITA KUZIMU (9)

0

SEHEMU YA TISA
TULIPOISHIA...
Baada ya kusema nimsubiri, aliingia bafuni akaoga kisha alitoka akachukua nguo na kuingia tena bafuni ambapo alibadilisha na kutoka.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
“Kijana wangu ukikutana na jini utamuomba kitu gani?” aliniuliza. Kufuatia swali hilo nilimwambia nitamuomba anipe umaarufu ili nifahamike duniani kote,

akaniuliza kwa nini nisiombe fedha, magari, nyumba na vitu vingine! Aliponiuliza hivyo nilisisitiza kwamba nahitaji kuwa maarufu kama walivyo marais ambao

wanaheshimika kila wanakokwenda, akacheka. Katika kichwa changu nilijua kama nitakuwa mtu maarufu, fedha, magari na vitu vingine ningevipata kirahisi ndipo yule mzee aliniambia tuondoke.

Tulipotoka mle chumbani tulikwenda sehemu aliyoegesha gari lake tukapanda, kabla hajaliondoa aliniambia tunakwenda msituni ambako kazi hiyo ingefanyika,

nikasema sawa. Tukiwa tumeanza safari, mzee huyo aliniambia tulikokuwa tukienda ni mbali sana na tungefika kati ya saa nne, saa tano au saa tano na nusu na kwamba lazima zoezi hilo lifanyike saa sita.

Mzee huyo aliendesha gari kwa kasi ambapo tulipita kwenye pori na hatimaye tulifika kwenye msitu huo, akasimama na kuegesha gari. Baada ya kushuka

aliniongoza hadi sehemu iliyokuwa na njia panda akasema nimsubiri kisha alirudi kwenye gari lake akachukua kisu na fimbo nyeusi. Akiwa na vitu hivyo alirejea

alipokuwa ameniacha na kuniambia muda ule ulikuwa muafaka kuanza kazi yetu. Hata hivyo, alinifahamisha kwamba atanielekeza namna ya kufanya kisha ataondoka na kuniacha peke yangu kwani wakati wa zoezi hilo hakutakiwa kuwepo.

Mzee huyo alinifahamisha kwamba, kama jini angefika na kumkuta pale angemuua na kunywa damu yake kwa sababu angekuwa amekiuka masharti. Aliongeza kuwa,

wakati namuita jini huyo natakiwa kuwa peke yangu kwa sababu mimi ndiyo nakuwa mlengwa hivyo eneo lile hatakiwi kuwepo mtu mwingine. Baada ya kunieleza

hivyo, alinikabidhi kile kisu na fimbo na kuniambia nimfuate, nikafanya hivyo. Tukiwa tumesimama njia panda aliniambia kwa kutumia ile fimbo nichore duara, nilipofanya hivyo akaniambia nimpe zile udi na ubani maka.

Nilipompatia alivichukua na kuviweka katikati ya lile duara kisha akaniambia nimpe yale majani ya mtende. Baada ya kumkabidhi alijongea nayo hadi kwenye lile

duara akayatandaza kisha alinipatia kiberiti, kisu, ile fimbo nyeusi pamoja na saa. Aliniambia kwamba ile fimbo niishike mkononi wakati wote au niiweke

mfukoni na ile saa alinipatia kwa ajili ya kuangalia muda. Mzee huyo aliongeza kuwa, ikifika saa sita kamili niviwashe moto vile vitu yaani udi, ubani maka pamoja na majani ya mtende.

Aidha, aliniambia nikishavichoma moto nimchukue yule kuku mweusi niingie naye kwenye duara nimchinje na kumgawanya sehemu mbili zinazolingana.

Tukiwa safarini maongezi yetu yalihusiana na mambo ya kupata utajiri, kwani nilitamani sana kuwa kama yule mzee. “Siku nitakayokuwa tajiri kama wewe

nitafurahi sana kwani najua nitaheshimiwa na kila mtu,” nilimwambia yule mzee aliyeishia kucheka. Kwa kuwa Mwanza hadi Dar ni mbali, tuliwasili saa mbili

usiku ambapo yule mzee alikodi teksi iliyotupeleka katika hoteli moja iliyopo Kariakoo. Kulipokucha yule mzee aliniambia kwamba siku hiyo ndiyo ilikuwa ya mwisho kunipatia msaada, kauli yake ilinishtua nikamuuliza kwa sababu gani.

Mzee huyo alicheka na kuniambia hatua iliyokuwa imebaki ilinihusu mwenyewe na kwamba baada ya kukamilisha kila kitu tutaachana. Mzee huyo aliniambia huenda

tutaonana nitakapofanikiwa mambo yangu, yaani nitakapokuwa tajiri kama yeye. Baada ya kuniambia hivyo, alisema kazi iliyokuwa mbele yetu ni kwenda katika maduka ya dawa asili kununua vitu vitakavyoniwezesha kwenda kwa lusifa, nikamwambia sawa.

Tulipomaliza kunywa chai aliniambia kwamba vitu tunavyokwenda kuvinunua haikuwa rahisi kuvipata, nikamuuliza ni vitu gani akaniambia mayai viza mawili ya

bundi na paka mweusi ambaye hajawahi kupandwa. Aliponiambia hivyo, sikutaka kumuuliza vitu hivyo vilikuwa vya nini badala yake nilimpa moyo kwamba

tungevipata, akafurahi sana. Kama alivyokuwa amenieleza, tulitembea karibu maduka yote ya Kariakoo hatukupata ndipo tulikwenda Manzese tukabahatika kupata mayai viza ya bundi.

Alimpomuuliza jamaa aliyemuuzia mayai hayo ni wapi tungempata paka mweusi asiyepandwa akatuelekeza Buguruni kwa mzee mmoja, tukaenda huko. Saa kumi na moja

jioni baada ya kupata vitu hivyo, tulielekea ufukweni ambapo yule mzee alimchinja yule paka na kutoa jicho lake moja. Zoezi hilo lilipokamilika aliniambia;

“Sasa kila kitu kipo tayari turudi hotelini tukasubiri muda ufike ili twende Daraja la Salenda kwenye lango la kuendea kuzimu.”

Ilipotimu saa sita usiku tulitoka pale hotelini na begi dogo lililokuwa na mayai viza ya bundi na jicho la paka mweusi ambaye hakuwahi kupandwa ambapo yule

mzee alimwita dereva teksi mmoja. Dereva huyo alipokuja kutusikiliza alimwambia atupeleke katika Daraja la Salenda, baada ya kukubaliana kiasi cha fedha

alichohitaji tuliingia kwenye teksi yake tukaanza safari. Kwa kuwa kutoka Kariakoo kwenda Daraja la Salenda hapakuwa mbali, tulitumia muda mfupi kufika ndipo

yule mzee alimwambia dereva aegeshe gari mbali kidogo na daraja kisha amsubiri.

Baada ya dereva kufanya kama alivyoagizwa, tuliteremka na kwenda darajani ndipo yule mzee akaniambia kwamba siku hiyo ilikuwa ya mwisho kunipa msaada na

kwamba sijui kama tutaonana tena. Aliongeza kuwa, ikitokea bahati nzuri tutaonana nikiwa nimefanikiwa kama yeye kisha akasema nimpatie lile begi lililokuwa

na mayai viza ya bundi na jicho la paka. Baada ya kumpatia alilifungua akatoa jicho la paka akanikabidhi na kuniambia niliweke mfukoni, nikafanya hivyo.

Yule mzee hakuishia hapo, alitoa yale mayai mawili akanikabidhi na kusema moja ya yai hilo litanipeleka kuzimu kwa lusifa na lingine litanirudisha duniani.

Nikiwa namsikiliza kwa makini, aliniambia ikifika saa saba usiku nisimame kisha niangalie baharini na kusema maneno haya;

“Enyi mizimu ya baba na mama yangu, naombeni mnifungulie mlango wa kuingia kuzimu.”

Aliongeza kuniambia kuwa baada ya kutoa kauli hiyo nilitupe lile yai baharini nitaona lango kubwa la dhahabu likifunguka. Baadaye aliniambia kwamba panapo

majaliwa tungeonana, akaondoka kuelekea tulikomuacha yule dereva teksi na kuniacha peke yangu. Ingawa sehemu hiyo inatisha sana usiku, sikuogopa kitu nikawa naangalia saa yangu ili itakapofika saa saba kamili usiku nifanye kama alivyoniagiza.

Muda huo ulipofika niliinuka kwenye jiwe nililokuwa nimekaa nikatazama baharini na kusema yale maneno kisha nikalitupia lile yai baharini, kufumba na

kufumbua niliona lango kubwa la dhahabu likifunguka mbele yangu, nikastaajabu. Baada ya kufunguka nililifuata nikaingia kisha lilijifunga ndipo nilisikia

sauti ya mtu ambaye sikumuona ikinikaribisha kwa kusema: “Kijana wangu, karibu sana katika ufalme wangu na kitu nilichokuahidi kukupatia utakipata huku kuzimu, karibu sana!”

Baada ya mtu huyo asiyeonekana kunikaribisha, aliniambia nisonge mbele kisha nikate kushoto ili anionyeshe mambo yaliyokuwa yakijiri katika makazi yake ya

kifalme. Nilipofanya hivyo nilishangaa kuwaona watu waliokuwa wapo kwenye mateso makali wakilia kwa maumivu waliyokuwa wakiyapata. Mtu huyo ambaye

hakuonekana aliniuliza kama nimeweza kumtambua japo mtu mmoja kati ya wale waliokuwa wakiteswa na kulia, nikamwambia sikumtambua yeyote.

Nilipomwambia sikumtambua yeyote aliniambi niwasogelee karibu kisha niwaangalie kwa makini, nilipofanya hivyo nilipigwa butwaa kumuona kijana mmoja aliyekuwa

msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva hapa nchini. Mtu huyo aliniuliza kama nilikuwa namfahamu kwa jina nikamwambia nilikuwa namfahamu sana ndipo

aliniambia walifanya naye mkataba ili awe mtu maarufu na tajiri lakini alikiuka masharti akaamua kumuua kwa ajali.

Msanii huyo alikuwa akilia kwa mateso aliyokuwa akiyapata na baada ya Lusifa kumwambia nilikuwa nimetoka duniani na nilikuwa namfahamu, akaniomba nimuombe

ampunguzie adhabu. Baada ya msanii huyo (nalihifadhi jina lake) ambaye kufikia leo angekuwa mbali sana kimafanikio kuniambia hivyo, nilipata huzuni ikabidi nimuombee msamaha kwa Lusifa.

“Mtukufu Lusifa, naomba umpunguzie adhabu huyu ndugu yangu kwani anajutia sana makosa aliyoyafanya nitashukuru kama ombi langu utalipokea,” nilimwambia

Lusifa ambaye hakuonekana. Nilipomaliza Lusifa aliniambia kwamba hatamsamehe yule msanii kwani alifanya makosa makubwa na kwamba adhabu aliyopewa alistahili kuitumikia.

Licha ya kumbembeleza sana ampunguzie adhabu alikataa na kusisitiza kwamba asingemsamehe ndipo aliniambia hata mimi nikishindwa kufuata masharti

atakayonipatia yatanipata kama yaliyompata yule msanii na watu wengine niliowakuta kule kuzimu. Baada ya kuniambia hivyo, Lusifa alinifahamisha kwamba pale

kwenye himaya yake na duniani kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakimuabudu na kufuata masharti yake. Alipotoa kauli hiyo aliniambia kwamba lengo lake anataka

kuitawala dunia kupitia dini yake aliyoianzisha muda mrefu ambayo ina wafuasi wenye uwezo mkubwa sana kifedha na madaraka.

Lusifa aliniambia kwamba katika dini hiyo ana wafuasi ambao ni watumishi wa Mungu, wafanyakazi, wasanii na wafanyabiashara. Kwa kuwa nilitamani sana kumuona,

nilimuuliza kwa nini aliongea na mimi akiwa haonekani na kumuomba ajitokeze, akacheka na kusema: “Kijana wangu hapo ulipo hauna damu ya kuweza kunipatia ili

unione.” Alipotoa kauli hiyo nilimuuliza kwa nini alikuwa akipenda damu, akaniambia ndiyo kilikuwa chakula chao kikuu yeye na wafuasi wake. Baada ya

kuniambia hivyo alisema nitoke pale nilipokuwa nimesimama nianze kutembea huku na huko ili niweze kuwaona watu waliokuwa wakimtumikia. Wakati nikifanya

hivyo, niliwaona viumbe wa ajabu na wa kuogopesha, baadhi walikuwa binadamu kama mimi, waliponiona walinikimbia. Watu hao walikuwa na maumbo tofauti, baadhi

walikuwa na macho matatu makubwa kwenye paji la uso wao, wengine walikuwa na miguu mitano na mikia mirefu. Aidha, wengine walikuwa na miguu yenye kwato kama za ng’ombe na vichwa vyao vilifanana na vya paka, vifua vyao vilikuwa sawa na vya binadamu na kulikuwa na wanawake wazuri sana. Nikiwa naendelea kutembea bila kumuona Lusifa niliyekuwa nikiongea naye, nilimuuliza kwa nini aliwadanganya Adam na Eva wakala lile tunda la mti wa katikati?.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)