Mwandishi: Juma Hiza
SEHEMU YA KWANZA
Ilikuwa ni siku ya jumamosi majira ya saa kumi kamili za jioni, hali ya hewa ilikuwa ni ya mvua ya wastani sanjari na baridi kali. Nilikuwa ndani ya chumba changu nimejilaza kitandani huku nikiwa nimejifunika mashuka mawili kwa mpigo nikiamini hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kupambana na baridi iliyokuwa ikiendelea kunitafuna mifupa lakini haikuwa kama nilivyokuwa nikidhani, baridi ile iliendelea kunishambulia vilivyo.
“Aaagghh, hii baridi nayo,” niling’aka kisha nikajisemea maneno niliyoyasindikiza na tusi mubashara. Hiyo ilikuwa ni kawaida yangu hasa pale lilipotokea jambo la kunikwaza nilikuwa mwepesi sana wa kutukana.
Licha ya tabia yangu hiyo ambayo naweza kuiita ilikuwa ni tabia ya kipumbavu lakini nilijaaliwa kuwa miongoni mwa vijana ambao walisifika sana kuwa wapole na heshima.
Sijui ni nini kilitokea ila nilijikuta nikipokea sifa kedekede kutoka kwa ndugu, jamaa pamoja na majirani niliyokuwa nikiishi nao, walikuwa wakinisifu juu ya upole wangu ati! Mwenyezi Mungu alinibariki muonekano wa upole na kila mtu alivutiwa na upole wangu.
Kwa kweli sifa ambazo walikuwa wakinisifia hazikuendana kabisa na mimi, kuna kipindi nilikuwa nikihisi labda walikuwa wakinikejeli hii ni kutokana na tabia chafu zilizokuwa zimejificha ndani yangu, hakukuwa na mtu aliyekuwa akinifahamu undani wangu, sifa za upole zilizokuwa zimetawala pale mtaani nilipokuwa nikiishi zilinisaidia kuficha maovu niliyokuwa nikiyafanya nyuma ya pazia na hiyo ndiyo ilikuwa sababu kubwa iliyochangia mpaka watu wasifahamu kile kilichokuwa kikiendelea katika maisha yangu.
Labda nikuambie kitu ndugu msomaji mbali na sifa zangu za upole zilizokuwa zimetawala kila kona lakini nyuma ya pazia kulikuwa kuna mambo yalikuwa yakiendelea yasirisiri ambayo hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akiyafahamu.
Nilikuwa nikifanya kazi ya udereva wa bodaboda kazi ambayo ilinifanya nikutane na wasichana wengi sana ambao mwisho wa siku nilikuwa nao kimapenzi, miongoni mwa hao wasichana niliyokuwa nao kimapenzi mwisho wa siku wamefanya niwe kilema, niishi maisha ya kukisubiri kifo changu kwa maana siwezi tena kutembea wala kufanya lolote.
Kila nikikumbuka yale niliyoyafanya nyuma katika maisha yangu kwa kweli kuna muda nakiri kuwa hata kwa ukilema huu niliyokuwa nao ni haki yangu kabisa wala sitakiwi kumlaumu mtu yoyote yule.
Japo nimeamua kukusimulia kwa mfumo wa chombezo lakini naomba unifuatilie kwa umakini kuna vitu naamini utajifunza na kama kuna sehemu itatokea nitakuwa nimekukwaza basi utanisamehe bure.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA CnZ Media APP INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
Tuendelee na chombezo letu…..
Wakati mvua ikiendelea kunyesha huku baridi nayo ikiendelea kunishambulia nikaamua kuamka kwa ghadhabu pale kitandani, uso wangu nilikuwa nimeukunja vilivyo kwa hasira zilizokuwa zimenijaa kichwani.
Tatizo kubwa lililokuwa likiniweka katika hali hiyo ilikuwa ni mvua iliyokuwa ikinyesha, ilikuwa ikinizuia kwenda kumchukua mteja wangu aliyekuwa akijulikana kwa jina la Samira. Nilikuwa na kazi ya kumpeleka kila siku kazini kwake maeneo ya Posta na kumrudisha nyumbani kwake Tandika Azimio, alikuwa akinilipa kwa siku.
Niliamini kwa mvua ile iliyokuwa ikiendelea kunyesha bila kuwepo dalili zozote za kukata basi niliamini nilikuwa nikienda kuikosa hela ya Samira msichana ambaye nilikuwa nikiishi naye mtaa mmoja.
Niliichukua simu yangu aina ya Tecno R6 nikaiwasha, nikaitoa pattern kisha nikaingia katika uwanja wa kuandika ujumbe mfupi, nilikuwa nikimuandikia ujumbe Samira.
“Mambo my.”
“Poa Metusela niambie.”
“Kama kawa vipi bado uko kazini?”
“Ndiyo nakusubiri sikuoni.”
“Na mvua hii nakujaje sasa?”
“We njoo hivyo hivyo bhanaa.”
“Au uchukue bajaji?”
“Bajaji sitaki.”
“Au daladala.”
“Sitaki pia.”
“Unataka nini?”
“Nataka uje unichukue na pikipiki yako.”
“Jamani sasa nitakujaje huko?”
“Wewe tafuta njia yoyote ya kuja mimi siondoki mpaka uje unichukue,” alinitumia ujumbe huu Samira kisha huo ndiyo ulikuwa mwisho wa chatting zetu.
Mpaka kufikia wakati huo nilikuwa nimeshapagawa, sikujua nilitakiwa niende vipi mpaka posta kwenda kumchukua, nilipoitazama saa yangu ilikuwa ni saa kumi na nusu. Nilizidi kuwa katika hali ile ya ghadhabu huku kila wakati nikichungulia nje kutazama kama mvua ilikuwa imepungua.
Kama utani vile ilipofika saa kumi na moja kasoro dakika tano hatimaye mvua iliweza kukata, sikutaka kupoteza muda tena nilichukua koti langu nikalivaa kisha nikatoka nje nikaielekea pikipiki yangu na sasa safari ya kwenda posta nikaianza.
Barabarani nilikuwa nikiendesha pikipiki lakini nilikuwa nikiufikiria ule uzuri aliyokuwa nao Samira, moyoni sikutaka kuamini kama kweli alikuwa bado hajaolewa maana alikuwa ni msichana mrembo haswaaa.
Alikuwa na sura ya kuvutia, macho legevu ya kurembua, kifua chake kilibarikiwa chuchu za kusimama mithili ya ncha ya mkuki, umbo lake lilikuwa limejengeka vyema na kuunda namba nane. Alivutia mno kutazama si kwa nywele zake ndefu alizokuwa amezifunga kwa nyuma, mwendo wake wa maringo wala kwa sauti yake laini ya kubembeleza.
Kwa mwendo wa dakika kumi nilikuwa tayari nimeshafika Posta nje Kampuni ambayo alikuwa akifanya kazi Samira, nikampigia simu kumjulisha kuwa nilikuwa nje kwa wakati ule nikimsubiri, haikuchukua sekunde akaweza kutoka nje.
Alikuwa amevalia mavazi yake ya kiofisi, sketi nyeusi fupi iliyoyaacha vyema mapaja yake wazi kwa juu alivalia T-shirt nyeupe iliyokuwa imeandikwa jina la kampuni yake kwa maandishi ya rangi nyeusi.
“Umenisubiri sana?” nilimuuliza alipokuwa amesimama mbele ya pikipiki yangu aina ya Boxer huku akiwa amekishikilia kiuno chake kilichokuwa kimebonyea kwa ndani mithili ya kiuno cha mdudu nyigu.
“Ndiyo nimekusubiri sana muda mrefu yani mpaka nikakata tamaa,” aliniambia Samira kwa suti ya kudeka.
“Tatizo ni mvua yani isingekata sijui ingekuwaje?”
“Na mimi nisingeondoka kabisa ofisini.”
“Kisa nini?”
“Hujaja kunichukua,” aliniambia kisha nikacheka.
Niliendelea kuutazama uzuri wa Samira na kila nilipokuwa nikiyapeleka macho yangu kwake nilizidi kukiri alikuwa ni mrembo kupitiliza.
“Kumbe mpaka jumamosi unaingia ofisini?” nilimuuliza.
“Hapana kuna kazi zilibaki jana leo ndiyo nimezimalizia,” alinijibu.
“Hapo sasa nimekuelewa vipi twende zetu sasa maana hili wingu jinsi lilivyofunga muda wowote mvua itashuka tena,” nilimwambia.
“Usijali Metusela ila nahisi baridi sana unaweza kuniazima koti lako?” aliniuliza.
“Hakuna shaka,” nilimwambia halafu nikavua koti langu nikampatia kisha akalivaa baada ya hapo akapanda kwenye pikipiki kisha tukaondoka zetu.
****
Nilimfikisha nyumbani kwake salama salimini jambo ambalo lilimfurahisha sana, alipenda sana kunisifia kutokana na uhodari wangu katika kuendesha pikipiki kisha akaichukua pochi yake akatoa hela halafu akanilipa kama ilivyokuwa kawaida yake.
Nilimshukuru sana lakini ajabu hakupendezewa na kitendo kile, aliniambia kuwa sikutakiwa kufanya vile mbele yake kwani kile alichokuwa akinipa kilikuwa ni haki yangu yani jasho langu hivyo sikutakiwa kumshukuru sana.
“Oooh, halafu nilitaka kusahau,” aliniambia huku akionekana kusahau kitu.
“Ulitaka kusahau nini?” nilimuuliza.
“Koti lako halafu nimejisahau kabisa nimelifanya kama langu.”
“Usijali hilo naweza kulichukua siku yoyote,” nilimwambia kisha sikutaka kupoteza muda nikamuaga halafu nikaondoka eneo lile.
Nilipofika nyumbani kwangu bado niliendelea kuteseka na hisia za mapenzi ambazo zilianza kuniingia ghafla! moyoni, nilijikuta nikiutumia muda mrefu sana katika kumfikiria Samira msichana ambaye nilitokea kumpenda sana.
Sikujua nilitakiwa kuanzia wapi kumueleza ukweli wa siri iliyokuwa ikinitesa moyoni, nilimpenda sana na nilitamani alifahamu hilo.
Wakati nilipokuwa nikiendelea kumuwaza nikaichukua simu yangu nikaingia whatsApp na kitu nilichoamua kukifanya ni kulitafuta jina lake na kuanza kumuangalia profile picha ambayo alikuwa ameiweka. Alikuwa ameweka picha aliyopiga kipindi yupo kazini.
Nikazidi kudata na muonekano wake uliyonivutia kupitiliza. Picha yake ilionekana nusu tena akiwa amekaa, ilianzia kumuonyesha sura yake mpaka usawa wa mapaja yake. Nikamtazama kwa umakini kila kiungo chake nilichokuwa nikikiona katika picha hiyo, alikuwa amekaa hakika alinivutia mno.
Hali ya hewa bado ilikuwa ni ya ubarini iliyohamasisha sana kufanya mapenzi, nilizidi kumtazama Samira pichani na hakukuwa na kitu kingine nilichokuwa nikikifikiria zaidi ya mapenzi. Hisia za mapenzi zilizonijia zilikuwa ni juu yake na hata katika upande wa kifikra nilimuwaza yeye.
Wakati nilipokuwa nikiendelea kumuwaza Samira ghafla! Simu yangu iliingia ujumbe mfupi, nilipoufungua na kuusoma ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Sesilia msiichana ambaye nilikuwa katika mahusiano naye ya kimapenzi, alikuwa amenitumia ujumbe wa kunijulia hali lakini kutokana na chuki nilizokuwa nazo juu yake sikutaka kumjibu lolote.
“Metu mpenzi wangu vipi uko salama?” alinitumia ujumbe mwingine ambao sikutaka kuujibu hata aliponipigia simu pia sikutaka kupokea.
Nilimchukia sana Sesilia, nilimfanyia kila aina vituko, kila siku tulikuwa tukiingia katika mgogoro ambao chanzo kilikuwa ni mimi. Hakukuwa na usalama wa penzi kila siku nilikuwa ni mtu wa kuwaza kumkwaza, nilikuwa tayari nimemchoka na hii ndiyo sababu iliyonifanya mpaka hisia zangu za mapenzi nikazihamisha kwa msichana mwingine.
Alikuwa ni Samira msichana mrembo ambaye niliamini siku moja nitampata na angeweza kuufurahisha moyo wangu ambao ulikuwa tayari umeshamtamani. Niliamini kushinda katika hilo hivyo sikuwa na shaka hata kidogo.
Huyu Sesilia ambaye ni mpenzi wangu mwanzoni kabla ya uhusiano wetu alikuwa ni abiria wangu kama walivyokuwa wengine. Nakumbuka niliwahi kumpeleka sehemu nyingi sana ambazo alikuwa akihitaji nimpeleke na alikuwa akinilipa.
Hakukuwa na mazungumzo mengine kati yetu zaidi ya udera na uabiria. Alikuwa ni msichana ambaye alionekana kuwa na msimamo sana pia alikuwa akijiheshimu hata katika upande wake wa mavazi alikuwa akivaa nguo za heshima ambazo zilimuweka katika muonekano wa kuheshimika kila wakati.
Macho yangu ya matamanio kwa wasichana hayakuacha kumtamani Sesilia ambaye nilimuingilia na gia ya kumuoa kabisa endapo angeweza kunikubali na kunikabidhi moyo wake wa mapenzi.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi