Mtunzi: Yozz Piano Maya
SEHEMU YA KWANZA
Hahahahahaha mimi sidanganyi nakwambia ukweli kabisa...unajua usiku wa jana sijalala kabisa..niliota ndoto..ikawa inajirudia rudi kama mara tatu hivi..
Sauti hiyo ilisikika ikitokea ndani ya chumba katika nyumba ya Kijana aitwae MAKALA..alikuwa akimsimulia mkewe kuhusu ndoto ya kutisha aliyoiota usiku wa jana.....mke wa Makala alifahamika kwa jina la NOREGA...
Makala akasema,,"kama umemaliza kufunga nywele zako zima taa tulale,sasahivi ni saa sita kasorobo...Norega akafanya kama alivyoagizwa na mumewe..akazipiga hatua kadhaa kuifuata swichi iliyokuwa ukutani karibu na mlango wa kuingilia chumbani humo...akazima taa akapanda kitandani wakaanza kuutafuta usingizi....
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
Upande mwingine ilionekana Nyumba moja ikiwa imejitenga peke yake....jirani wa karibu na nyumba hiyo alikuwa umbali mrefu kama kilomita sita hivi kutoka kwenye nyumba hiyo iliyojitenga peke yake alionekana mwanaume mmoja wa makamo akichimba shimo usiku huhuo wa saa sita. nje ya nyumba hiyo....mwanaume huyo alifahamika kwa jina la JOSHI....aliendelea kuchimba shimo takribani kama masaa mawili mfululizo....aliopohakikisha kachimba shimo lenye urefu aliokuwa amekusudia,,akatoka ndani ya shimo hilo na kuzipiga hatua kuingia ndani kwake......na baada ya dakika tatu hivi...akatoka huku amebeba maiti ya binadamu...akazipiga hatua kulifuata lile shimo alilolichimba akadumbukiza maiti hiyo ndani ya shimo,,akaanza kufukia kwa kutumia koleo....
ilipofika saa kumi za usiku,,alimaliza kufukia shimo hilo...kisha akamwaga mbegu za za mchicha..ili paonekane kama ni bustani ya mbogamboga.....
kisha akaingia ndani ya nyumba yake..akafunga mlango...ndani ya nyumba hiyo palionekana kutisha kutokana na makorokoro kuwa mengi yamewekwa bila mpangilio...nyumba hiyo ni kubwa sana ilikuwa na vyumba Tisa...akazipiga hatua akaingia kwenye chumba kimojawapo..akawasha taa...kikaonekana kiti cha mbao kikiwa na kamba...pia chumba hicho kilijaa zana kutisha..... alizitumia katika shughuri zake ambazo hazifahamiki mpaka muda huu...Joshi hakuwahi kuwa na rafiki tangu utotowake mpaka umri huo alionao sasa....ni baada ya wazazi wake kuuwawa na mtu asiyejulikana...wazazi wa Joshi waliuwawa akiwa na umri wa miaka saba..alishuhudia mauwaji hayo..akiwa amejificha chini ya meza iliyokuwa sebuleni...
yule mtu katiri aliyefanya mauwaji hayo...alipokuwa anatoka nje ya nyumba ya kina Joshi...akatereza kwenye vigae kutokana alikuwa amekanyaga Damu zilizokuwa zimetapakaa chini akadondoka na kuangukia kisogo akupoteza fahamu....Joshi alipo ona muuwaji huyo kadondoka,,akajua amekufa...akaatoka pale alipokuwa amejificha chini ya meza akaanza kulia huku akitazama maiti ya Baba yake pamoja na Mama yake...waliuwawa kwa kuchinjwa shingo na kukatwakatwa mapanga mwili mzima...
Joshi akazipiga hatua kwa hofu kubwa..akamsogelea yule muuwaji....akamtazama usoni akaina kovu kubwa la mda mrefu lililokuwa kwenye shavu la kushoto mwa muuwaji huyo...akahisi kuwa amekufa....akazipiga hatua akarudi ndani.....baada ya sekunde kadhaa..muuwaji alizinduka akapata fahamu..Joshi alipomuona ananyanyuka akajificha haraka,,chini ua meza....yule muuwaji akajishika kisogo huku akiugulia maumivu...akazipiga hatua na kuondoka zake,akatokomea kusikojulikana....
****************
Joshi alijificha hapo masaa mengi kiasi...alipo ona kuna hali ya itulivu akatoka chini ya meza,,akakumbuka baba yake alimfundisha kuwa endapo akiona kunahatari..au siku nyumba ikiwaka moto alafu wazazi wake hawapo nyumbani basi apigege simu ya mezani kwenda namba 112..kisha ataje namba ya nyumba yao ambayo ni S/0043......joshi alikariri maneno hayo ya baba yake sikunyingi....
akachukua simu ya mama yake haraka,,akapiga namba hizo za Dharura 112..simu ikapokelewa kwenye kituo cha polisi..Joshi akaelezea tukio zima,,pia akatoa anuani ya nyumba..baada ya dakika kadhaa maaskari walikuja mpaka kwenye nyumba hiyo....wakachukua maiti zile mbili na kuzipeleka mochwari...kutokana zilikuwa zinamajeraha makubwa ya kukatwa na mapanga..ililazimika wazikwe siku hiyo hiyo ili maiti hizo zisiharibike na kutoa harufu....
taratibu za mazishi zikafanyika...wakazika...
Shangazi wa Joshi ambaue ni mdogo wa mwisho wa baba yake Joshi..alichukua jukumu la kuishi na kumlea Joshi katika nyumba hiyo....Jishi aliendelea kukua kadri miaka ilivyozidi kwenda..
alipotimiza umri wa miaka ishirini na tatu....shangazi yake ambaye alikuwa mlezi wake alifariki dunia.....
kutokana alikuwa tayari kafikisha umri wa kujitegemea Joshi aliamua kuishi mwenyewe ndani ya nyumba hiyo.....akiwa peke yake..
********BAADA YA MIAKA TISA KUPITA********
Joshi alitimiza umri wa miaka therathini na mbili(32)alikuwa anafanya kazi ya kupasua kuni anazikusanya..zikiwa nyingi anaziuza kwa pamoja....siku moja akiwa mjini kwenye matembezi alimuona mtu..akamfananisha..mtu huyo alionekana kuwa mzee kiasi..
Joshi akamsogelea mzee huyo akamtazama kwa makini..akaona lile kovu shavuni mwa mzee huyo.
akakumbuka kuwa huyu ndiye muuwaji aliyewauwa wazazi wake..akaamua kumfatilia mzee huyo mpaka anapokwenda..akagundua nyumba anayoisgi mzee huyo....akamteka na kumpeleka nyumbani kwake..kwenye ile nyumba waliyokuwa wakiishi wazaziwake..yule mzee alistuka kuona anapelekwa kwenye nyumba hiyo..akakumbuka kuwa miaka 25 iliyopita,,alifanya mauwaji kwenye nyumba hiyo...aliamua kumuuwa baba Joshi pamoja na mkewe....kwa sabavu walikuwa wanamdai pesa nyingi baada ya kuuziwa nyumba na baba yake Joshi...aliwauwa ili asilipe deni hilo...
Joshi akamtesa mzee huyo kwa mateso makali sana mpaka akafa...
kumbe ile maiti aliyoizika Joshi ilikuwa ni maiti ya mzee huyo aliyewauwa wazazi wa Joshi..
********BAADA YA MWAKA MMOJA KUPITA*****
Mzimu wa mzee huyo ukafufuka na kuanza kufanya mauwaji ya kikatiri na yenye kutisha..
Siku moja majira ya usiku wa saa saba..ule mzimu ulionekana ukifufuka kutoka kwenye ile bustani ya mbogamboga alizozipanda Joshi....
mzimu huo ukanyanyuka na kuzipiga hatua..mpaka kwenye mlango wa nyumba ya Joshi...ukaingia ndani...wakati huo Joshi alikuwa amelala...ghafla akaota ndoto kuwa yule mzee muuwaji..aliyewauwa wazazi wake,,amefufuka na kumfuata huku ameshikilia upanga mrefu uliokuwa na mpini mrefu kama wa jembe la kulimia......Joshi akastuka kutoka usingizini..akakurupuka kitandani..akawasha taa..akachungulia dirishani kutazana kule nje alipomzika yule mzee na kupanda bustani ya mbogamboga....ili aone kama pamefukuliwa...lakini hakuweza kuona vizuri kutokana na giza totoro kutanda upande wa nje...akazipiga hatua akafungua mlango na kutoka nje...akaelekea kwenye ile bustani ya mbogamboga...alipofika..hakuona kitu chochote zaidi ya mbogamboga..zikiwa vilevile kama anavyoziona kila siku.....akaamua kurudi ndani..akafunga mlango na kuufuata mlango wa chumbani kwake..alipoufungua alistuka sana kumuona yule mzee aliyemzika..yumo ndani ya chumba chake!!!macho yakamtoka Joshi,,akajisemea moyoni,,"inamaana ile ndoto niliyotoka kuiota dakika chache zilizopita ilikuwa ni ya kweli!!!?.....Joshi alibaki amesimama kama sanamu akistahajabu....wakati huo akili zilikuwa zimemruka....
alipotahamaki...akataka kutimua mbio....mzimu wa yule babu ukamvaa ukaingia ndani ya kiwiliwili cha Joshi....
ni kitendo cha sekunde,,akili ya Joshi ikaanza kubadilika,,akaingiwa na Roho ya ukatiri wa hali ya juu!!!..akili ya Joshi ikawa inaongozwa na ule mzimu.....akazipiga hatua za kikakamavu..huku uso wake ukionekana kuwa na msisitizo wa kufanya jambo fulani....akafungua mlango wa chumba kingine,,alichokitumia kama stoo ya kuhifadhi zana zake za kupasulia kuni,,,akachukua nyundo kubwa..akaitazama kwa umakini..akairudisha,,akachukua,,shoka akazipiga hatua kadhaa..akasita.akarudi akaiweka chini shoka hiyo...akachukua upanga mrefu uliokuwa na mpini mrefu..akaunyanyua upanga huo huku akiutazama kwa hisia kali,,akauramba kwa ulimi wake.......kwa mara ya kwanza Joshi akatabasamu..kwa sekunde mbili kisha akarudi katika uso wa msisitizo wa kutenda jambo fulani,,
akazipiga hatua na kutoka nje ua nyumba yake huku akiuwacha mlango wazi!!!!
akazipiga hatua za kikakamavu akatokomea kusikojulikana..........
***********************
Asubuhi palipokucha alionekana Makala akiwa nyumbani kwake akijiandaa kwenda kazini...mke wake Norega alimuandalia chai,,Makala alipomaliza kuvaa nguo..akatoka chumbani na kuelekea sebuleni,,akanywa cha haraka haraka huku akiongea na mkewe.....akasema,,"Leo nimechelewa kuamka alafu ile ndoto niliyoiota juzi imejirudia tena....nimeota wafanyakazi wenzangu smwatano wameuwawa kikatiri na mtu aisiyefahamika.....
Norega akasema,,"hiyo ni ndoto tu mume wangu..
baada ya dakika kumi Makala alimaliza kunywa chai,,akamuaga mkewe kwa kumbusu shavuni..akatoka nje na kuingia ndani ya gari lake..akaliwasha..na kuianza safari ya kuelekea kazini......
Makala alikuwa anafanya kazi katika shirika la kiserikari la HIFADHI YA MISITU NA UWOTO WA ASILI...
Alipofika kazini..akaingia moja kwa moja mpaka ndani ya ofisi yake...baada ya dakika tatu kupita..alikuja sekretari wake akamletea barua ikitokea MAKAO MAKUU...alipoifungua barua hiyo,,ilikuwa ikisema kuwa,,siku ya leo anatakiwa aende kwenye msitu UNGEBO uliopo ndani ya Mbuga ya wanyama ya SAADANI iliyopo hapahapa jijini dar es salaam....
safari hiyo ilikuwa ni ya kwenda kuchunguza mmea unaosadikika kuota ndani ya msitu huo..matawi ya mmea huo yalikuwa ni sumu...ilibainika baada ya kukutwa baadhi ya wanyama wamekufa na walipofanyiwa uchunguzi ikajulikana kuwa wamekula matawi ya mmea huo usiojulikana.....
Makala akaamuru wafanyakazi watano aongozane nao kuelekea kwenye msitu UNGEBO..
********************
upande mwingine alionekana joshi,,akiwa barabarani akizipiga hatua za kikakamavu huku lile panga lake refu likiwa limetapakaa Damu iliyoganda.....kwa mbali akaona nyumba,,akaamua kuifuata nyumba hiyo,,akaingia ndani bila kupiga hodi...akamkuta bibi kizee hajiwezi..akiwa amelala ndani ya nyumba hiyo...Joshi akamchinja na kuondoka zake....akasonga mbele zaidi,akatokezea kwenye pori,akasita kutembea akaangaza angaza macho yake huku na kule,,akatabasamu kwa mara ya pili,, akazipiga hatua kuingia ndani ya pori hilo...akasonga mbele zaidi,,akatokezea kwenye msitu UNGEBO akaonekana kufurahia mazingira ya msitu huo..akatabasamu mara ya tatu....
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi