Mtunzi: Yozz Piano Maya
SEHEMU YA PILI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Joshi akamchinja na kuondoka zake....akasonga mbele zaidi,akatokezea kwenye pori,akasita kutembea akaangaza angaza macho yake huku na kule,,akatabasamu kwa mara ya pili,, akazipiga hatua kuingia ndani ya pori hilo...akasonga mbele zaidi,,akatokezea kwenye msitu UNGEBO akaonekana kufurahia mazingira ya msitu huo..akatabasamu mara ya tatu....
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Upande mwingine kule kazini kwa Makala alionekana akiingia ndani ua gari..yeye pamoja na wafanyakazi watano..jumla wakawa sita...akaliwasha gari na safari ya kuelekea Msitu UNGEBO ikaanza.....
baada ya lisaa limoja walifika kwenye mbuga ya wamyama ya SAADANI..wakasonga mbele zaidi na kuingia ndani kabisa ya mbuga hiyo.....Makala alizidi kuzipanga gia hatimae wakatokezea kwenye msitu UNGEBO,,wakaingia ndani ya kabisa katikati ya msitu huo....Makala akalisimamisha gari..kisha wakashuka kutoka ndani ya gari...wakachukua vifaa vya kufanyia utafiti wa mimea...wakajigawa katika makundi mawili...Makala na wafanyakazi wawili wakaelekea upande mwingine..
na wale wafanyakazi watatu wakaelekea upande mwingine..ili kazi iwe rahisi kuliko kuwa eneo moja wote sita.......
kazi ikaanza wakazipiga hatua kuingia ndani zaidi ya msitu huo......wakati Makala na wenzake wawili wakiendelea kuutafuta mmea huo...Makala akastuka,,akasita kutembea...akasema,,"tazama kule!! wale wenzake wawili walipotazama wakaona mtu kalala chini akiwa amekatwa shingo.....wakaisogelea maiti ile..Makala akasema,,"mtu huyu kauwawa muda mchache uliopita si unaona damu bado mbichi!!!!?
wakaanza kuingiwa na hofu wakaamua kutimua mbio kurudi kule lilipokuwepo gari walilokujanalo.....
walipofika eneo hilo..wakastahajabu kutokulikuta gari lao....hofu ikaongezeka..wakaanza kutimua mbio bila kujua ni wapi wanaelekea.......mara ghafla Makala akawazuia wenzake wasiendelee kukimbia akawavuta mpaka kwenye kichaka akawafanyia ishara kwamba wakae kimya,,kisha akasema kwa sauti ya chini chini,,""TAZAMA KULE...walipotazama wakastuka..wakataka kutimua mbio..Makala akawazuia......
Akasema,,"msijaribu kupiga kelele,mkifanya hivyo tumekwisha,,huyu mtu anaonekana hana nia nzuri....
Joshi akazipiga hatua kuelekea upande mwingine.huku kashikilia upanga mrefu....Makala alipo ona Joshi kaondoka eneo hilo...akasema,,"tukimbieni...kabla hajamaliza kuongea hivyo...wale wenzake watatu,wakaanza kutimua mbio,,,walikimbia bila kujua ni wapi wanaelekea....
******************
upande mwingine walionekana wale wafanyakazi watatu..wakiendelea kufanya utafiti...wenyewe hawakuweza kufahamu chochote kwa sababu hawakuona ile maiti..wala hawakumuona Joshi...
waliendelea kufanya utafiti upande huo,,,lakini kila mmoja alipita njia yake...
akaonekana Joshi akizipiga hatua, akakutana uso kwa uso na mmoja kati ya wafanyakazi hao.....yule mfanyakazi hakujali akaendelea kufanya utafiti,,kwa kuweka kile kipimo maalu cha kuchunguza mimea.....hakujua kuwa kwa sasa Joshi hakuwa katika akili uake ya kawaida,, akamsalimia Joshi,,"habari yako
Joshi hakujibu kitu,akabaki amesimama kikakamavu..yule mfanyakazi alipo ona Joshi hajibu salamu yake akaamua kuendelea na utafiti...akastuka kumuona Joshi akizipiga hatua kumfuata,,,alipotahamaki Joshi alikuwa amemkaribia jirani kabisa...akamfyeka shingo kwa kutumia ule upanga mrefu...kichwa kikaruka kando..damu zikaruka...mfanyakazi huyo akatapatapa na kudondoka chini akafa papohapo.
Joshi akazipiga hatua kadhaa akamuona mfanyakazi mwingine....akamfuata na kumfyeka shingo....yule mfanyakazi aliyebaki kati ya wale watatu..aliona kitendo hicho cha mauwaji ya kikatiri alichofanyiwa mwenzake.....akaamua kutupa kile kifaa cha kufanyia utafiti akatimua mbio....
************************
upande mwingine alionekana Makala pamoja na wenzake wawili wakitimua mbio itadhani wanashindana mbio kwenye mashindano ya mbio za mita mia.....walikimbia wakajikuta wametokeze..ule upande ambao wale wenzao watatu walikuwepo huko...wakastuka kukuta maiti ya mfanyakazi mwenzao ikiwa haina kichwa..wakaingiwa na hofu..wakatimua mbio,,ghafla Makala akajikwa akadondoka chini,,kumbe hapo alipoangukia..ilikuwepo maiti ya yule mfanyakazi wa pili....Makala akaogopa sana.akanyanyuka na kuendelea kutimua mbio...
sasa hivi hakuwaona wenzake walikuwa wameshatokomea mstuni humo,,,walimuacha hatua nyingi kiasi wakati yeye alijikwa na kudondoka...wenyewe waliendelea kusonga mbele.....
*********************
upande mwingine, alionekana yule mfanyakazi mmoja aliyeshuhudia mwenzake akichinjwa kikatiri...akikimbia bila uelekeo...huku akiangaza angaza macho yake huku na kule.....akasikia matawi yakitoa mlio kama kunamtu anakimbia kumfatilia akageuka nyuma huku akikimbia kwa kasi ya ajabu,,,huenda Joshi anamkimbiza kwa nyuma....lakini hakuona kitu chochote zaidi ya miti....alipogeuka kutazama mbele anakoelekea ghafla akajikuta kajichomeka kwenye mti uliokuwa umechongoka,,ukatoboa tumbo na kutokezea mgongoni..akafa papohapo....wakabaki watu watatu.Makala pamoja na wenzake wawili
**********************
upande mwingine walionekana wale wawili wakitimua mbio,,,walitamani watoke ndani ya msitu huo lakini ni kilomita nyingi kutoka mstuni mpaka kuifikia barabara kuu....wakati wanakimbia wakaamua kuingia kwenye kichaka kwa lengo la kujificha,,
mmoja wao akagusa mzinga wa nyuki..akautingisha nyuki wakatoka na kuanza kuwashambulia,,wakakurupuka kichakani humo na kukimbia huku wakipiga mayowe ya kelele za maumivu....
kelele hizo zilimfanya Joshi,agundue ni wapi walipo akazipiga hatua kuzifuata kelele hizo....wakakutana uso kwa uso...wakabaki wamesimama huku nyuso zao zimevimba manundu manundu..kwa sababu wameumwa na nyuki...wakati wanatahamaki..Joshi akawafuata..wakaanza kutimua mbio kurudi walipotoka....Joshi akarusha upanga..kama mtu anayerusha mkuki...upanga huo ulikwenda moja kwa moja mpaka mgongoni mwa mfanyakazi mmoja..akadondoka chini...yule mfanyakazi mwingine alipo ona mwenzake kanaswa akaongeza kasi ya kukimbia...
Joshi akazipiga hatua za haraka haraka,,mpaka pale alipokuwa amedondoka yule mfanyakazi..akauchomoa upanga wake...kutoka mgongoni mwa mfanyakazi huyo..kisha akamchinja.....na kuondoka zake..
***********************
upande mwingine alionekana Makala akiendelea kutimua mbio huku macho yamemtoka..akaamua kupanda juu ya mti,,ili kujificha kwa usalama zaidi.
alipofika juu ya mti...akatazama upande wa chini,,akastuka kumuona Joshi akizipiga hatua kuja upande huo!!! akakumbatia mti huku akitetemeka kwa hofu...Joshi alipoukaribia mti huo..akasita kutembea akaangaza angazaacho yake huku na kule,,hakuona mtu.....akakasirika sana,,,akajiuliza,,mtu huyu kakimbilia wapi???
wakati huo mapigo ya moyo ya Makala yalikuwa yakipiga kwa kasi,,huku akipumua kwa kubana pumzi ili Joshi asisikie sauti ya Muhemo...
Makala akahisi kadondokewa na tone la maji..akainua shingo yakeili atazama ni nini hicho kimemdondokea begani..akastuka kumuona CHUI akiwa kwenye mti huo hou....alipotazama upande wa chini ili ajirushe..akaina bado Joshi kasimama
wala hana dalili ya kuondoka hapo alipo...
akafumba macho akajikaza kiume huku akimuomba Mungu....amnusuru na majanga hayo.
yule mnyama Chui akaona Damu kwenye ule upanga wa Joshi...na kwa jinsi Joshi alivyokuwa ametapakaa Damu kwenye nguo zake...Chui huyo akajitosa kwa kuruka kutoka juu ya mti akatua kichwani mwa Joshi...kutokana na uzito wa chui huyo...Joshi alidondoka chini....
Makala,,akaweza kupata upenyo wa kujirusha kutoka juu ya mti mpaka chini akaanza kutimua mbio na kutokomea mstuni,,bila kujua ni wapi anakoelekea........
Joshi akaanza kupambana na Chui..akafanikiwa kuchoma na upanda tumboni,, utumbi ukamwagika..chui akatapatapa mpaka akafa....Joshi akanyanyuka,,lakini uso wake ulikuwa umejeruhiwa vibaya kwa makucha ya chui yule.....ngozi ya usoni ikabanduka yote..na kubaki nyama ya ndani ya ngozi..huku akitokwa na damu..
Joshi alihisi maumivu makali sana...akapiga kelele huku amenyanyua upanga wake juu....kwa hasira...
*******************
upande mwingine alionekana yele mfanyakazi mmoja kati ya wale wawili waliokuwa na Makala,
alitimua mbio bila kugeuka nyuma....akatokezea kwenye sehemu yenye majani marefu kiasi,..akaona simba watatu wakiwa wamejilaza,,,Simba hao walionekana kuwa na njaa kali....
Yule mfanyakazi akasita kukimbia,,,hofu ikazidi kuongezeka,,akaamua kirudi alipotoka kule ndani ya msitu...alikimbia kwa kasi zaidi kabla Simba hawajamuona........akatokezea ile sehemu alipouwawa yule chui.....akastuka akasimama ghafl,,,kutokana alikuwa anakimbia kwa kasi na kile kitendo cha kisimama ghafla..akadondoka chini na kuserereka mpaka pale alipokuwepo chui yule aliye uwawa.....akanyanyuka haraka huku akimtazama yule chui kwa mshangao....
wakati huohuo wakaonekana maaskari wa kulinda wanyama pori..wakija upande huohuo....wakamuona yule mfanyakazi akiwa kasimama anamtazama chui huyo....maaskari walipo ona chui ameuwawa,,wakahisi kuwa mfanyakazi huyo ndiye aliyuuwa chui huyo kwa lengo la kumchuna ngizi,,,
mmoja kati ya maaskari hao,akapaza sauti,,"TULIA HIVYO HIVYO HAPO ULIPO..
yule mfanyakazi akaamua kutimua mbio bila kutazama ni nani anayesema maneno hayo....wale maaskari..wakaamua kufatua risasi wakijua kuwa mtu huyo ni jangiri...risasi moja ilimpata kichwani yule mfanyakazi akapoteza maisha papohapo..
**********************
Upande mwingine alionekana,,Makala akiendelea kutimua mbio,,kwa mbali akaona kuna HEMA limetengenezwa kama nyumba...akaamua kulifuata ili kuomba msaada...alipofika akaita kwa kusema,,"Hodi jamani...hakuona dalili yoyote ya mtu kutoka nje....akazipiga hatua kuusogelea mlango wa kuingilia ulikuwa wazi...mlango huo ulikuwa wa kufunga kwa zipu....akaingia ndani ya hema hilo.....hakukuta mtu,,akaangaza angaza macho akaona kuna kofia ya askari wa kulinda wanyama pori.....akagundua kuwa hema hilo ni kwa ni maalumu kwa ajili ya maaskari wa porini..
akaamua kujihifadhi humo,,kwa usalama wa maisha yake....
************************
upande mwingine,,walionekana wale maaskari pori,wakachukua kamba wakamfunga miguu ya mbele na ya nyuma....wakapitisha mti mrefu kiasi kati ya miguu ya mbe pamoja na miguu ya nyuma...wakimbeba yule chui wakaanza safari yakuelekea kule kwenye hema.....
wakiwa njiani kuelekea huko.....wakakutana uso kwa uso na Joshi,,wakastuka kumuona mtu akiwa hana ngozi usoni,,huku ameshikilia upanga mrefu ukiwa umetapakaa damu...
wakasita kutembea,,mmoja kati ya maaskari hao akauliza,,"umepatwa na nini?? mbona umeumia kiasi hicho?
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi