Mtunzi: Yozz Piano Maya
SEHEMU YA TATU
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
wakiwa njiani kuelekea huko.....wakakutana uso kwa uso na Joshi,,wakastuka kumuona mtu akiwa hana ngozi usoni,,huku ameshikilia upanga mrefu ukiwa umetapakaa damu...
wakasita kutembea,,mmoja kati ya maaskari hao akauliza,,"umepatwa na nini?? mbona umeumia kiasi hicho?
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Joshi hakujibu kitu akabaki kimya,huku akiwatazama maaskari wale...sura yake ilionekana kutisha sana.....akazipiga hatua kuwafuata,,akanyanyua upanga wake juu...
wale maaskari wakadhani Joshi anafanya mzaha..
na walipo ona haongei kitu...wakaamua kuendelea na safari yao...ghafla wakaona damu inaruka na kuwamwagikia,,,wakageuka nyuma haraka.....wakaona mwenzao anadondoka chini huku chingo yake ikiwa haina kichwa....wakamtupa chui waliokuwa wamembeba...wakaweka sawa.. bunduki zao,,, tayari kwa kumshambulia Joshi..kabla hawajaanza kifyatua risasi..Joshi akanyanyua upanga na kufyeka shingo ya askari mwingine.....kichwa kikaruka kando akafa papohapo......wakaanza kufyatua risasi mfululizo kuelekea kwenye mwili wa Joshi risasi ziliingia mwilini kwa joshi,..lakiniJoshi akawa anazitema risasi hizo kwa kupitia mdomoni mwake zikawa zinadondoka chini..wale maaskari wawili waliokuwa wanafyatua risasihizo..wakaona huyo sio binadamu wa kawaida wakaamua kutupa bunduki zao wakatimua mbio,,kila mmoja akapita njia yake.....
Joshi hakuwakimbiza akazipiga hatua kusonga mbele hukohuko walipoelekea maaskari hao...baada ya kutembea hatua kadhaa akasita kuendelea kutembea katazama huku na kule...akaamua kupita upande mwingine ili awanase kwa urahisi.....
baada ya muda wa dakika kumi kupita...akakutana uso kwa uso na mmoja kati ya wale maaskari wawili waliokuwa wakikimbia.....akamkamata akamchoma na upanga kwenye jicho..upanga huo ukatokezea kisogoni,,,kisha akauchomoa upanga huo kwa kuuvuta...askari huyo akadondoka chini na kupoteza maisha....
Joshi akazipiga hatua kadhaa akaangaza angaza macho huku na kule..akamuona yule askari mwingine akiwa anajinasua kwenye kichaka kilichokuwa na miba..aliingia kwenye kichaka hicho bila kujua kuwa kilikuwa na miba mirefu...
wakati akiendelea kujinasua...Joshi akamkaribia na kumfyeka kichwa kikaruka kando...akabaki kasimama kama sanamu..huku akiwa bado kanasa kwenye kichaka hicho chenye miba...
Joshi akatoka eneo hilo akasonga mbele zaidi....kwa mbali akaona kuna hema lililotengenezwa kama nyumba..akaamua kulifuata hema hilo.....
kule ndani ya Hema alionekana Makala,,akitafuta sehemu iliyojificha ajihifadhi ,,endapo kama mtu akiingia humo ndani asionekane kwa urahisi....aliamua kujificha kwa sababu ndani ya msitu huo,,Tayari kuna hali ya hatari.....na wenzake watano tayari wameuwawa na Joshi jitu katiri...
mapigo yake ya moyo yalipiga kwa kasi kutokana na hofu kubwa iliyokuwa imetanda juu yake....ghafla akasikia vishindo vizito vya miguu!!! akaogopa sana akahisi labda ni mnyama Tembo anatembea upande wa nje!! macho yakamtoka hofu ikazidi kuongezeka...akachungulia lakini hakuweza kuona upande wa nje,,
vishindo havikusikika tena,,,,ukimya ukatawala...
Pasipo kutarajia,, Joshi akaingia ndani ya hema hilo...akaangazaangaza macho..hakuona mtu yeyote......akazipiga hatua kadhaa kuingia ndani zaidi....kutokana na urefu aliokuwanao ilimlazimu kuina ili atoshe kuenea ndani ya hema hilo......katika kuangaza angaza...akajikuta amekitazama kioo kikubwa kiasi kilichokuwemo ndani ua hema hilo...akakisogelea kioo hicho...akaonekana kukitazama kioo kwa dakika kama mbili hivi,mfululizo....Joshi alichukia, akakasirika sana baada ya kuona uso wake ulivyojeruhiwa na chui...kumbe alitobolewa jicho na kucha za chui yule...........
Joshi akachukua upanga wake akauingiza ndani ya jicho hilo lililotobolewa akalinyofoa jicho na kulitupa chini,,,,akapiga kelele kwa hasira,,na maumivu ya hali ya juu...
kelele hizo zilitoa mngurumo wa kutisha.....na kwa sababu ukimya ulitawala ndani ya msitu huo....kelele za Joshi,,,zilisikika maili nyingi....
zikasababisha ndege warukao,,,kuruka kutoka kwenye matawi ya miti na kutokomea angani,,,pia wanyama wakatimua mbio na kutokomea ndani zaidi ya msitu huo....
**************************
Joshi akaanza kuvuruga vuruga vitu vilivyokuwemo ndani ua hema hilo...kwa kuvitupa chini...akanyanyua kiti kilichotengenezwa kwa mbao akakirusha upande mwingine...
kumbe ndio ule ule upande alipokuwa amejificha Makala...kiti kile kilikwenda moja kwa moja mpaka kwenye mgongo wa Makala....
Makala akahisi maumivu makali sana nusu anyanyuke hapi alipo..akajikaza kiume.....
Upande mwingine liliinekana gari likipita ndani ya msitu huo,,,,gari hilo lilikuwa limebeba maaskari wa kulinda wanyama pori....kumbe maaskari hao,,waliletwa ili wale maaskari waliokuwa wakilinda siku ya jana......leo watolewe wakapumzike.....wakiwa njiani kuelekea kule lilipokuwepo Hema....wakastka kukuta kuna gari limetobolewa magurudumu!!!! wakaamua kulisogelea garo hilo,,wakastahajabu kukuta teki ta kuhifadhia mafuta limeng'olewa na kutupwa pembeni,,kumbe gari hilo ndio lile gari alilokujanalo Makala pamoja na wafanyakazi wenzake humo mstuni kwa ajili ya utafiti.....
mmoja kati ya maaskari hao akasema,,"kutakuwa na tatizo!! kwa nini hili gari limetobolewa magurudumu na limetelekezwa hapa???
wakaweka siraha zao tayari kwa mapambano...wakaingia ndani ya gari lao na kusonga mbele kuelekea kwenye hema.......kabla hawajafika mbali wakaona maiti ya askari mmoja amekatwa shingo....huku kichwa chake kikiwa kando kabisa!!! wakastuka....dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo akaliendesha kwa kasi ili wawahi kuangalia kama maaskari wengine wapo salama kule kwenye hema!!! ghafla wakakutana na maiti nyingine ya mtu kakatwa shingo...
kumbe maiti hiyo ni ya mmoja kati ya wale wafanyakazi waliikuja na Makala....
maaskari wakaanza kuingiwa na hofu.....askari mmoja akasema,,"aisee geuza gari turudi tukatoe taarifa,, yule dereva akasema,," tutarudi vipi!!! je? wale maaskari wenzetu itakuaje?? unamaanisha tuwaache huku mstuni????
wacha tukawachukue....dereva huyo alitasema maneni hayo huku akizidi kuzipanga gia,wakaanza
kulikaribia hema.....walipotazama kwa mbali..wakaona kuna mtu akitikea ndani ya hema huku kavalia joho refu jeusi...likiwa limefunika upande wa kichwani mpaka usoni....huku kashikilia upanga mrefu wenye ncha kali.....yule dereva akasimamisha gari haraka,,ili watazame mtu huyo anataka kufanya nini....
Joshi akanyanyua usi wake ukutazama ule upande ambao lilikuwepo gari la maaskari wa kulinda wanyama pori.....akaanza kuzipiga hatua kulifuata gari hilo.....akaingeza kasi ya kutembea hatimae akaamua kukimbia huku akiwafuata wale maaskari....
yule dereva akaingiwa na hofu..akaamua kuliwasha gari ili wakimbie...alipojaribu kuzunfusha ufunguo gari halikuwaka...akajaribu tena na tena,, lakini bado gari hilo halikuwaka...akasema,,"gari imeflot mafuta yanarudi kwenye kabreta...wale maaskari wakachanganyikiwa baada ya kusikia hivyo!!!wakaamua kupiga simu makao makuu waletewe msaada...kabla hawajamaliza kutoa taarifamtandao ukawa unakatakata...hivyo hawakusikilizana vizuri..
walipoangaza macho yao kumtazama mtu huyo kafika wapi..wakastuka!!! hawakumuona tena....wakiwa bado wanatahamaki...ghafla alionekana Joshi akitokea kwenye kichaka kilichokuwa karibu kabisa na gari hilo...........walipojaribu kufyatua risasi kumlenga Joshi..tayari walikuwa wameshachelewa..Joshi aliwafyeka shingo zao kwa kutumia upanga wake... .wakafa papohapo,,,kumbe wakati wanapiga simu mtandao ukakata.... hawakukuta simu ile ilibaki hewani ikisikika kule makao makuu..
Kule ndani ya Hema,,alionekana Makala....akinyanyuka kutokea ile sehemu aliyokuwa amejificha,,akazipiga hatua za tahadhari...kuufuata mlango ili achungulie upande wa nje,,wakati huo mapigo yake ya moyo yalikiwa yakipiga kwa kasi,,huku jasho linamtiririka kama kamwagiwa maji....alipochungulia upande wa nje,,kwa mbali akaona kuna gari limesimama...akafurahi,,akajua atapata msaada wa kutoka kwenye msitu huo.....akaangaza macho yake kwa kutazama huku na kule,,hakuona dalili yoyote ya mtu kuonekana eneo hilo...akatoka ndani ya hema akazipiga hatua za haraka haraka huku akitazama kushoto kulia......alipolikaribia lile gari,,akastuka kuona watu wamo ndani ya gari hilo,,,akatazama kwa umakini akagudua watu hao..walikuwa hawana vichwa...vilionekana viwiliwili tu.....hofu ikatanda juu yake....akatimua mbio kulifuata gari hilo akafungua mlango wa upande wa dereva akamvuta yule askari aliyekuwa dereva wa gari hilo na kumtoa nje...akaingia ndani ya gari hilo akafunga mlango...akazungusha ufunguo ili gari liwake....lakini gari halikuwaka....macho yakamtoka....akaamua kufungua mlango kutoka nje....akaingia uvunguni, mwa gari hilo kwa ajili ya kujificha...
***********************
Upande mwingine kule makao makuu,,alionekana askari anayehusika na mawasiliano ya moja kwa moja na maaskari wakiwa huko porini kwa ajili ya kulinda wanyama, akajaribu kufanya mawasiliano kwenye ile simu iliyopigwa kutokea kule msituni
Makala alisikia mlio wa simu ikiita ndani ya gari hilo, kutokana na hofu kubwa aliyokua nayo hakuthubutu kutoka chini ya uvungu kuipokea ile simu..... simu iliita mpka ikakata na baaada ya sekunde kadhaa simu ikaita tena!!lakini Makala aliiacha hivyo hivyo ikiita, wazo likamjia akajiona yeye ni mjinga akajisemea moyoni,,"wacha nipokee simu hii huenda nikaweza kupata msaada..akanyanyuka haraka kutoka uvunguni mwa gari akafungua mlango wa gari akaangaza macho yake ndani ya gari hilo,, akafanikiwa kuiona simu,,alipotaka kuipokea simu ikakata
kumbe tayari alikua amekwisha chelewa!!! akajarbu kuipigia hiyo namba...lakini simu ikamwambia kuwa hakuna salio la kutosha kuweza kupiga simu hiyo....akaamua kuichukua simu hiyo akaiweka mfukoni mwake..akarudi chini ya uvungu wa gari.......akajificha.
baada ya dakika tano simu ikaita tena...akaitoa mfukoni haraka,,alipobofya kitufe cha kupokelea..simu ilikuwa imeishiwa umeme(charg) ikazimika,,Makala akajutia kwa kusema,,"USIPO ZIBA NYUFA UTAJENGA UKUTA..sasa wacha nijenge ukuta.....mimi ni mjinga kiasi gani,,,kwa nini mwanzo sikupokea simu ilipokuwa ikiita!!!
ghafla akasikia vishindo vizito vya mtu akitembia..
akastuka..hofu ikazidi kuongezeka....akasikia gari linatikiswa....akafumba macho....ili asishuhudie akiuwawa.... alipofumbua macho ghafla akaona gari linavurutwa....akaamua kulishikilia kwa nguvuzake zote...
kumbe Josgi alirudi na kulivuruta gari hilo aende akalifiche kwenye vichaka vilivyokuwa mstuni humo,,kama kunamtu anayetaka kutoroka,,basi atoke mstuni humo kwa kutumia akili zake mwenyewe,,..Makala aliendelea kushikilia kwanguvu...vyuma vilivyokuwa chini ya gari hilo...
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi