JICHO LA TATU (4)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mtunzi: Yozz Piano Maya
SEHEMU YA NNE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
kumbe Josgi alirudi na kulivuruta gari hilo aende akalifiche kwenye vichaka vilivyokuwa mstuni humo,,kama kunamtu anayetaka kutoroka,,basi atoke mstuni humo kwa kutumia akili zake mwenyewe,,..Makala aliendelea kushikilia kwanguvu...vyuma vilivyokuwa chini ya gari hilo...
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Joshi alilivuruta gari hilo umbali mrefu sana....kwa mbali akaona kuna korongo kubwa,,akatabasamu....akazipiga hatua za haraka haraka huku akilivuruta gari hilo akalitupe kule chini ya korongo.....Makala alipotazama ni wapi Joshi anaelekea,,akaona Joshi anaelekea kwenye korongo lililokuwa na mteremko mkali...akastuka macho yakamtoka.....akajilaumu kwanini asingebaki palepale lilipokuwa limesimama gari....
*************************
upande mwingine kule makao makuu...alionekana mkuu anayehusika na kitengi cha wanyama pori...akiamuru....askari waende kwenye msitu UNGEBO kuwaokoa maaskari waliokuwemo ndani ya msitu huo........
akamteuwa MICHAEL awe kamanda mkuu aongoze kikosi kitakachokwenda msitu UNGEBO..
zikaruka ndege mbili..zilizokuwa na maaskari watatu kila ndege moja...kuelekea msitu Ungebo
Michael na maaskari saba wakaingia ndani ya gari na kuianza safari ya kuelekea msitu Ungebo..
***********************
kule mstuni,,Joshi alionekana akiendelea kuliviruta gari akakaribia kabisa kwenye korongo...Ghafla akasikia mngurumo wa ndege....akanyanyua shingo yake kutazama angani.....
wakati huo huo..kule angani..alionekana askari mmoja..akiwa ameshikilia Darubini(BINOCOLUS)
Akitazama upande wa chini kwa kupitia darubini hiyo..akastuka kumuona mtu mrefu anavuruta gari..alipotazama kwa umakini..akaona viwiliwili vya maaskari vikiwa havina vichwa..ndani ya gari hilo....akazungusha (ZOOM)darubini ili kumuona yule mtu ni wa aina gani..ananguvu gani za kulivuta gari zito aina ya JEEP!!!akastuka kuona mtu huyo...hana sura...usowake ulionekana kama nyama mbichi......akasema,,"WEKA SHABAHA,, SHAMBULIA....bila kupoteza muda Rubani wa mdege hiyo ya kijeshi..aliweka shabaha akaanza kumshambulia Joshi kwa kubonyeza kitufe cha kufyatulia risasi mfululizo....
risasi hizo zilitoka nyingi nyingi kama mvua....
Risasi hizo ziliingia kila mahali kwenye mwili wa Joshi....akaamua kuliachia gari na kutimua mbio akatokomea mstuni...hapo ndipo walipoamsha hasira za Joshi!!! alikasirika sana......akaanza kung'oa miti kwa hasira huku akipiga kelele zilizotoa mngurumo mkubwa wa kutisha....akachukua mti mkubwa alioung'oa akauvunja katikati..akaurusha angani kuilenga ile ndege iliyokuwa ikimshambulia.....mti huo uligonga pembeni ya ndege...na kung'oa injini moja ya ndige hiyo..ikapoleza uelekeo na kudondoka kuelekea chini kwenye korongo ikaripuka.....wakati huo Makala alikuwa bado yupo kule chini ya gari....akitetemeka kwa uwoga...haja kubwa na ndogo zilimtoka mfululizo......
*****************
Upande mwingine alionekana Michael akiwa pamoja na maaskari saba(7) wakianza kuingia ndani ya msitu huo.... wakasikia sauti ya mripuko mkubwa!!!!....wakati bado wanataamaki..ghafla kuna mti mkubwa uliong'olewa ukarushwa na kutua mbele ya gari lao njia ikaziba na mti huo....
Michael pamoja na wale maaskari saba..wakastuka...wakashuka kutoka ndani ya gari haraka....wakaweka sawa bunduki zao..tayari kupambana na chochote kitakachotokea mbele yao...Michael akasema,,"Hakuna kurudi nyuma tusonge mbele kuhakikisha tunawaokoa maaskari waliokuwemo kwenye msitu huu..SAWA??
wale maaskari saba hawakuwa na budi kutii amri ya kamanda mkuu wa kikosi hicho.....wakaanza kuzipiga hatua kusonga ndani zaidi ya msitu huo...
walizipiga hatua kwa tahadhari...huku wakiwa katika mstari mmoja..
walitembea mwendo wa lisaa lizima,,lakini hawakufanikiwa kumpata askari hata mmoja...wakazidi kusonga mbele zaidi.....wakatokezea kwenye lile Hema....wakalifuata na kuimgia ndani ya Hema hilo kwa tahadhari huku maaskari watatu wamebaki nje..kwa ajili ya kulinda usalama...
miongoni mwa wale maaskari wanne(4) alikuwemo kamanda mkuu Michael...wakaona vitu vimevurugika huku matone ya damu yakiwa yamedondoka chini...wakastuka!!! Michael akasema kunatatizo ndani ya msitu huu..akafanya ishara ya kuondoka,,kisha wakatoka nje huku bunduki zao wameziwaeka tayari kwa kupambana. wakasonga mbele....
***********************
Upande mwingine alionekana Makala akiwa bado yupo kule chini ya gari...akatazama pande zote..akaona ukimya umetawala..akaamua kutoka chini ya uvungu wa gari hilo..na kuanza kutimua mbio..wakati anakimbia akatereza na kuanza kuserereka kuelekea chini ya korongo....alijigonga kwenye mawe mpaka akafika chini kabisa ya korongo hilo akajingonga kwenye jiwe upande wa kichwani akapoteza fahamu......
*********************
Upande mwingine walionekana watu wanaoishi mstuni...watu hao walikuwa wametoboa masikio yao na kuweka vipande vikubwa vya miti...yakaonekana kuvutika na kuwa marefu...walikuwa wameshikiria mikuki ikiambatana na upinde mishale....watu hao walijulikana kwa jina la jamii ya WAKOLOLO...walikuwa wamevalia ngozi za nyani!!! kufunika sehemu zao za siri...kwenye jamii hiyo..hakuwahi kukanyaga binadamu wa kawaida na akatoka akiwa hai katika ardi hiyo...watu hao waliishi kwa kula matunda na wanyama pori....
siku ya leo wawionekana vijana shupavu wa jamii hiyo ya WAKOLOLO wenye umri wa kuanzia miaka kumi na minane na kuendelea...wakizipiga hatua kwenda kutafuta kitoweo.....kutokana na ukame mkali..wanyama walilazimika kwenda mbali kutafuta majani mabichi pamoja na maji...hivyo jamii ile walipata vitoweo kwa tabu..walikuwa wakitembea maili nyingi kwenda kutafuta vitoweo..
************************
Upande mwingine alionekana Joshi akizidi kusonga mbele zaidi kuingia ndani kabisa ya msitu huo huku kashikilia upanga wake mrefu...akiwa anatembea akakutana uso kwa uso na mnyama chui..Joshi akapandwa na hasira akakumbuka kapoteza jicho lake kwa kuraruriwa na chui...akarusha upanga wake..ukaenda moja kwa moja mpaka ubavuni mwa chi huyo...chui akalia kwa sauti kali....kutokana na maumivu makali aliyoyapata..akatimua mbio huku upanga huo ukining'inia huku sehemu ya upanga huo ikiwa ndani ya ubavu wa chui huyo...alikimbia lakini hakufika mbali akadondoka chini...Joshi akamfuata,,alipomkaribia akauchomoa upanga huo..akazamisha vidole vyake kwenye jicho moja la chui huyo akalinyofoa jicho...na kulipachika katika lile sehemu iliyokuwa wazi ya jicho lake moja...kisha akachana kipande cha nguo yake akajifunga kichwani kuizungu sehemu ya paji la uso mpaka jichoni...akazipiga hatua na kusonga mbele zaidi.....
**************************
upande mwingine alioneka Michael akiwa na wale maaskari saba(7) wakizidi kusonga mbele huku macho yao yakitazama kwa tahadhari kubwa...wakakutana na Fisi wengi kiasi wakiwa wamezunguka wakionekana wanakula....wakawastua wale fisi kwa kuponda jiwe,,,lile eneo ambalo fisi hao walikuwa wamelizunguka,,
wale fisi wakatimua mbio na kutokomea mstuni...
Wakastuka kuona maiti ya askari ikiwa haina kichwa ndiyo ilikuwa chakula cha fisi hao....wakasikitika sana pia hofu ikaanza kuwaingia wakaanza kuwa makini zaidi...wakati bado wakiwa wanaitazama maiti hiyo.......kunaupanga ukarushwa kutokea kwenye kichaka..upanga huo ulikwenda moja kwa moja mpaka kifuani mwa askari mmoja.....akapoteza maisha papohapo hata bila kuvuta pumzi.....
wale maaskari wengine sita wakatimua mbio wakamuacha Michael akiwa kasimama..
*****************
Upande mwingine,,alionekana Makala...akiwa bado yupo pale chini alipodondoka na kupoteza fahamu......yale matukio ya mauwaji ya wafanyakazi wezake yalizunguka katika ubongo wake!! ghafla akizinduka akapata fahamu,,hakutazama kushoto wala kulia...alinyanyuka na kutimua mbio....akapanda korongo kuelekea upande wa juu..na baada ya nusu saa alifanikiwa kutoka ndani ya korongo hilo....akaanza kutimua mbio....kabla hajafika mbali akakutana uso kwa uso na wale watu jamii ya WAKOLOLO. wakiwa wameshikilia mikuki,,wengine wakiwa na upinde na mishale......
watu wale wakamtazama Makala kisha wakaanza kuwasiliana kwa lugha yao......wakati huo Makala alibaki kasimama akitafakari nini cha kufanya...mara ghafla watu wale wakaanza kumfuata huku wakipiga lele na kuongea lugha yao.......Makala akaingiwa na hofu kubwa akaanza kutimua mbio ghafla akajikwaa na kudondoka chini...........
akanyanyuka haraka akaendelea kutimua mbio....
akaonekana mtu mmoja wa jamii ya WAKOLOLO..akiweka mshale kwenye upinde..akauvuta...ghafla ikasikika sauti ya mkuu wa vijana hao akiongea kwa lugha yao,,akimaanisha,,"Muache hawezi kukimbia na kufika mbali...wengine piteni upande huu,,na wengine piteni upande mwingine...mumzunguke...
lile kundi la vijana wa jamii ya wakololo wakatii amri ya mkuu wao,,wakatimua mbio huku kila mmoja akipita njia yake....kwenda kumnasa Makala..
*******************
upande mwingine,,kule alipokuwa amesimama kamanda Michael...alistshajabu kumuona Joshi akija upande wake huku akizipiga hatua za kikakamavu...Michael akaanza kumshamburia kwa kufyatua risasi kuelekea upende ambao joshi alikuwepo!! akashangaa risasi zilingia kwenye mwili wa Joshi lakini bado akaendelea kumfuata..
Michael akaona mambo yamekuwa magumu akaamua kutimua mbio na kutokomea mstuni..
Joshi akaendelea kuzipiga hatua mpaka pale alipokuwepo yule askari aliyechomwa na upanga..
alipomkaribia akachumua ule upanga...kwenye mwili wa askari huyo...
akazipiga hatua kwenda kumnasa Michael pamoja na wale maaskari waliokuwa wamekimbia na kutokomea mstuni humo.....
***********************
wakati huo huo walionekana wale maaskari wakiendelea kutimua mbio ili kunusuru uhai wao..
wakaona kichaka kikubwa kilichozungukwa na miti mingi iliyo ota kwa karibukaribu...wakaamua kuingia ndani ya kichaka hicho na kujificha...
Upande mwingine alionekana Kamanda Michael akititua mbio....akaamua kupanda juu ya mti akatazama huku na kule huenda akaona njia ya kutoka ndani ya msitu huo.....alipotazama kwa mbali aliliona lile gari walilokuja nalo mstuni humo..akakumbuka kuwa,,ndani ya gari hilo walibeba silaha nzito za kivita....akashuka haraka kutoka juu ya mti akatimua mbio kulifuata gari hilo....baada ya dakika kadhaa alifanikiwa kulifikia gari hilo akafungua mlango akachukua silaha maalumu kwa kutungulia ndenge angani...ROCKET RANGER(RPG) akaweka kombora moja ndani yake pia akabeba kombora jingine akaliweka ndani ya begi..
wakati huo alionekana Joshi akija upande huo huo...safari hii Joshi aliongeza kasi ya kutembea....
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni