JICHO LA TATU (5)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mtunzi: Yozz Piano Maya
SEHEMU YA TANO
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
baada ya dakika kadhaa alifanikiwa kulifikia gari hilo akafungua mlango akachukua silaha maalumu kwa kutungulia ndenge angani...ROCKET RANGER(RPG) akaweka kombora moja ndani yake pia akabeba kombora jingine akaliweka ndani ya begi..
wakati huo alionekana Joshi akija upande huo huo...safari hii Joshi aliongeza kasi ya kutembea....
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Upande mwingine alionekana Makala akiendelea kutimua mbio.....ghafla wale wakololo wakajitokeza mbele yake wakamuweka katikati yao......Makala akapagawa.....akajiuliza nini cha kufanya...
akaonekana yule mkuu wa vijana hao..akizioiga hatua kumfuata makala,,,lipomkaribia akaongea lugha ya Kikololo,,,Makala aliweza kuelewa baadhi ya maneno yaliyotamkwa..kwa sababu Makala alikuwa akisoma vitabu kudadisi na kutaka kujua makabila pamoja na jadi zao....akajibu kwa kuongea Lugha yao!!! yule mkuu wa vijana hao wa wakololo akastuka akamtazama Makala kwa macho ya msisitizo....akanyoosha mkono wake juu akiwafanyia ishara wenzake,,wasimdhuru Makala...wale wakololo wengine wakastahajabu....lakini hawakuwa na budi kutii amri ya mkuu wao....wakamchukua Makala kumpeleka kwenye kijiji cha Wakololo.....Makala akaanza kuingiwa na imani kiasi...akajipa moyo kuwa yupo katika mikono salamaa.....wakololo
walipofika kwenye kijiji chao wakampeleka Makala moja kwa moja mpaka kwa MTEMI wa jamii hiyo..
yule mkuu wa vijana akaanza kuongea na Mtemi kwa lugha yao....mtemi akanyanyuka nakumtazama Makala kwa umakini huku akimzunguka..........akaamuru Makala apelekwe kwenye nyumba iliyotengenezwa kwa miti awekwe humo.....
************************
upande mwingine alionekana Michael akizipiga hatua za tahadhari...kumuwinda Joshi huku akiwa amebeba begani ile silaha maalumu ya kutungulia ndege(RPG) alimuwinda Joshi lakini hakufanikiwa kumpata....hatimae usiku ukaingia....
upande mwingine walionekana wale maaskari sita waliobaki hai miongoni mwa wale maaskari saba aliokujanoa Michael....maaskari hao waliendelea kujificha ndani ya kichaka hicho tangu mchana....
**************************
Upande mwingine,,kule kwenye kijiji cha Wakololo alionekana Makala ameketi kwenye ngozi ya simba,,iliyokaushwa ndani ya ile nyumba iliyotengenezwa kwa miti...
kwa mbali alionekana mwanamke mmoja akizipiga hatua,,huku akiangaza angaza macho yake huku na kule...
mwanamke huyo aitwae,,,VIDA kumbe ni bimti wa pekee wa MTEMI wa Wakololo,,,,mwanamke huyo aliinekana kuvutiwa kimapenzi na Makala Tangu alipomuona mchana akiletwa na vijana wa jamii hiyo ya wakololo....
mwanamke huyo alizipiga hatua akafungua mlango wa nyumba aliyokuwemo Makala...
Makala akastuka kumuona mwanamke ameingia ndani ya nyumba hiyo iliyokuwa na vyumba viwili..vilivyotenganishw.....Vida alikuwa kavalia ngozi ya nyani iliyokuwa imefunika sehemu zake za siri huku makalio yakiwa wazi pamoja na matiti..akamsogelea Makala...
wakati huohuo alionekana Mtemi akiwaamuru walinzi wake wa karibu wakamuite Vida anamaingezi nae.
wale walinzi walipoingia chumbani kwa Vida hawakumkuta,,wakamtafuta kila kona..hawakufanikiwa kumuona vida.. wakarudi kwa Mtemi kutoa taarifa kuwa Vida hayupo..Mtemi akastuka akahisi huenda binti yake hayupo katika sehemu salama!!! akaamuru vijana wote wamtafute Vida usiku huohuo..na popote watakapomkuta...wahakikishe wanamrudisha haraka iwezekanavyo.....akasema,,"mtu yeyote atakayekutwa na binti yake...akamatwe...na kunyongwa hadharani.....
msako ukaanza..........
Upande mwingine alionekana Michael,akiwa bado yumo ndani ya kichaka kajificha.....upepo ulikuwa ukivuma kwa kasi kutokana msitu huo ulikuwa na miti mikubwa....
upepo huo ulisababisha baridi kali..na mbu pamoja na wadudu watambaao/siafu walimng'ata Michael lakini hakuwa na namna alivumilia.akakumbuka mafunzo na mateso kipindi amejiunga na jeshi...ghafla zikaanza kusikika ngurumo za radi.....wingu likaanza kutanda na kuzifunika mbaramwezi na nyota...giza likatanda ghafla Mvua ikaanza kunyesha....
ilinyesha mvua kubwa kupita kiasi...
*******************
Upande mwingine walionekana wale maaskari sita waliobaki...wakiwa bado wamo ndani ya kile kicha walichokuwa wamejificha tangu mchana..mvua iliwanyeshea...ikiambatana na baridi kali sana..wakaanza kutetemeka......mmoja kati yao..kumbe alikuwa anasumbuliwa na kifua.....huwa kinambana na kushindwa kumpumua,,,,akipigwa na baridi kali.......ghafla akaanza kushindwa kupata pumzi...akahangaika sana..wenzake walijitagidi kumsaidia kwa kumkumbatia kwa pamoja wakamuweka katikati,,,lakibi haikusaidia...na baada ya dakika kadhaa..askari huyo alikata Roho....wale maaskari wenzake waliskitika sana wakajikuta wanadondokwa na machozi bila kutarajia,,wakabaki maaskari watano.
mvua iliendelea kunyesha kwa kasi kubwa...walitamani ardhi ipasuke watumbukie ndani yake.....
*************************
Upande mwingine alionekana Vida akiwa ameketi kando ya Makala huku akimtazama kwa macho ya kimitego mitego(kimahaba) vida alishindwa kuongea na makala kutokana kila alichomwambia Makala,,,Makala alibaki kimya bila kujibu...kutokana na lugha aliyokuwa akiitumia Vida kuongea nae,,,Makala aliweza kuyaelewa maneno machache...lakini akaagundua kuwa Vida anamtamani kimapenzi....uzalendo ulimshinda Vida akaanza kumtomasa Makala....
Makala alijizuia,,kwa sababu alikuwa anampenda sana Norega...hakuwahi kufikilia kumsaliti mkewe.
Kumbe wakati Vida anatoka chumbani kwake kuelekea kwenye nyumba aliyokemo Makala...
SUBI alisikia mlango wa chumba cha Vida ukifunguliwa....Subi ni mama mzazi wa Vida....akaamua kufatilia ili abaini binti yake anaenda wapi usiku huo!!! akamuona binti yake anaingia kwenye ile nyumba alipomokuwemo makala.....Subi akazipiga hatua za kunyatia...akazunguka nyuma ya nyumba hiyo...
kutokana nyumba hiyo ilitengenezwa kwa miti.....Mama Vida aliweza kuchungulia na kuona kila kitu kilichokuwa kinaendelea mule ndani......macho yakamtoka...kumuona binti yake anamlazimisha Makala kufanya nae ngono....akaamua kuondoka aende akamshtaki Vida kwa Baba yake...lakini alipoingia upande wa ndani ya nyumba...akamkuta Myemi ambaye ni mumewe anafanya matambiko yake......na alishasema tangu mwanzo..kuwa kama akiwa anafanya matambiko....asiongeleshwe na mtu yeyote hata mkewe......
Mama vida akaingia chumbani akaketi kumsubiri Mumewe amalize kufanya matambiko,,ili amueleze kile alichokiona vida anakifanya..
********************
wakati huo huo kila kijana wa jamii ya wakololo alikuwa kashikilia kitani cha moto..kilichotengenezwa kwa mti,,huku upande wa juu kumefungwa kwa kuzungushiwa kamba zilizochunwa kwenye magome ya miti..na kupakwa mafuta ya wanyama...
vijana hao wakaingia mstuni zaidi kumtafuta vida,,binti Pekee wa Mtemi...walitafuta kwa muda mrefu sana mpaka majira ya saa nane za usiku,,lakini hawakuweza kufanikiwa kumpata vida,,wala hawakuona dalili yoyote ya vida kuwepo maeneo hayo..wakaamua kurudi kule kijijini kwao,,ili wakatoe taarifa kwa Mtemi kuwa,,hawajafanikiwa kumpata vida.....wakiwa njiani wanarudi alionekana mkuu wa vijana hao wa kikololo,,,akiwa nwenye mawazo mazito,,alikuwa akitafakari neno la kumwambia MTEMI....kwa sababu Mtemi wao huwa hataki kusikia kauli ya kushindwa....endapo akitoa agizo....ni lazima litekelezwe na endapo wakishindwa kufanya walichoagizwa,,huwa anawachinja bila huruma vijana kadhaa wa kikololo......waliendelea kuzipiga hatua kurudi kule kijijini.....hatimae wakafika,,,lakini yule mkuu wa vijana hao..akasema,,"kabla sijaenda kutoa taarifa kwa Mtemi,,,itabidi tukague nyumba moja hadi nyingine..huenda Vida yupo hapa hapa kijijini....wakaanza kufanya msako kwenye nyumba moja baada ya nyingine.....walimtafuta vida bila mafanikio....mkuu wa vijana hao akapagawa....lakini hakuwa na namna ya kufanya....akazipiga hatua kuufuata mlango wa Mtemi ili akatoe taarifa....ghafla wazo likamjia akasita kutembea akageza shingo yake na kuitazama nyumba iliyo kuwa mbali kidogo na hapo alipo......akajisemea moyoni,,"hiyo nyumba hatujaikagua..yawezekana vida akawemo ndani ya nyumba hiyo....
pia akawaza kuwa,,huenda Makala katoroka na vida....
akapaza sauti,,"akaongea kwa lugha yao akimaanisha waende kufanya msako kwenye ile nyumba iliyotengenezwa kwa miti,,
nyumba hiyo ndio ile nyumba aliyokuwemo MAKALA pamoja na VIDA......
wale vijana wa Kikololo wakatii amri ya mkuu wao,,wakazipiga hatua kuifuata nyumba hiyo.
wakati huo huo alionekana Vida akiendelea kumpapasa Makala.,
Makala akaongea kwa sauti ya ukali nakusihi acha hilo jambo unalotaka kulifanya Vida akastuka ingawa hakuelewa lugha aliyoitumia Makala lakini akagundua kuwa makala hataki yeye afanye jambo hilo.
kitendo hicho kilimfanya Vida akose furaha kwa sababu mwili na hisia zake zilikua tayari kufanya ngono na Makala ,Vida akachukia akanyanyuka kwa hasira .
Upande wa nje wa nyumba hiyo walionekana vijana wa Kikololo wakiizunguka nyumba hiyo huku wakipiga kelele za mayowe kwa lugha yao, Vida akastuka akaingiwa na hofu baada ya kujua mayowe hayo yakiashiria hali ya hatari akamtazama makala kwa macho ya mshangao!! Vida akatimua mbio huku akinyata akaingia kwenye kile chumba kingine akajificha chumba hicho kilikua na makololo mengi yakiambatana na ngozi pamoja na pembe za wanyama mbali mbali
******************
Upande wa nje ya nyumba hiyo....alionekana yule mkuu wa vijana hao wa kikololo akiwaamuru vijana watatu kuingia ndani ya nyumba hiyo wafanye msako...ni kitendo cha sekunde wakafungua mlango na kuingia upande wa ndani..wakamkuta Makala.....ameketi wakaanza kuangaza angaza macho huku na kule....hawakumuona Vida!!! Makala akaanza kuingiwa na hofu...wale vijana watatu wakaingia kwenye kile chumba alichokuwemo Vida..wakaangaza angaza macho lakini hawakumuona vida...
kijana mmoja kati ya vijana hao watatu,,akazipiga hatua kuelekea kwenye zile ngozi zilizokuwa zimepangwa.....akaangaza angaza macho lakini hakumuona Vida,,,kumbe Vida alikuwa amejificha kwenye kona ya chumba hicho na kujifunika ngozi ya chui iliyokuwa imekaushwa......
wakati anazipiga hatua kutoka hapo...akasita akahisi kitu,,,akawaita wenzake kwa lughatq yao....akimaanisha waje wasaidiane kuzitoa ngozi hizo ili watazame huenda Vida kajificha chini ya ngozi hizo......
wale vijana wawili wakaja haraka...wakaanza kutoa ngozi moja moja.....lakini kijana mmoja akasema kwa lugha yao akimwambia yule yule kijana aliyewaita,,akimaanisha,,"utakuwa umeona vibaya hakuna mtu hapa.....wakarudisha haraka ngozi hizo.....kwa kuzipanga.
walipomaliza wakazipiga hatua kutoka nje ya chumba hicho.......
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni