JICHO LA TATU (7)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mtunzi: Yozz Piano Maya
SEHEMU YA SABA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
wakati huo huo walionekana wale maaskari watano wakizipiga hatua za tahadhari huku macho yao yakitaza kwa umakini mkubwa......ghafla wakasikia vishindo vizito vya miguu ikikimbia.....wakaanza kushambulia kwa kufyatua Risasi mfululizo kwenye ule upande ambao vishindo hivyo vilisikika....
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Waliendendelea kushambulia kwa muda wa dakika tano mfululizo....
kisha wakaacha na kutulia kimya,,,,, hawakusikia vishindo hivyo tena...wakajipa imani kuwa tayari wamemuuwa Joshi....wakaamua kuzipiga hatua za kunyatia kulekea ule upande waliokuwa wakifyatua risasi...wakastahajabu kumuona Kifaru mkubwa sana akiwa amedondoka chini huku akitokwa na damu nyingi kwenye matundu baada ya kupigwa risasi nyingi......
wale maaskari wakajiona wamefanya jambo la kijinga kwa kupoteza Risasi nyingi kwa lengo ambalo silo....wakaamua kusonga mbele wakaendelea kuitafuta njia ya kutoka mstuni humo......wakatokezea lile eneo ambalo kamanda mkuu wa kikosi (Michael) alikuwa hapo muda mchache uliopita.......ghafla maaskari wili wakakanyaga ule mtego alioutega Michael kwa ajili ya kumnasa mnyama ili ajipatie kitoweo....
Mtego huo ulifyatuka na kuwatoboa tumboni maaskari hao wawili...wakapoteza maisha papohapo....
wale maaskari watatu waliobaki,,wakaanza kutimua mbio,,,walikimbia bila kujua ni wapi wanaelekea......kwa mbali wakaona mto,,wakaamua kuufuata ili wavuke na kutokuzea upande wa pili....
***************
upande mwingine alionekana Joshi akizipiga hatua za kikakamavu huku akiwa na hasira za hali ya juu.....kwa mbali akaona mto...akaamua kuufuata mto huo anywe maji...kwa sababu alihisi kiu kikali.
wakati huohuo alionekana Makala akiendelea kutimua mbio akiwa uchi wa mnyama..huku akidondoka mara kwa mara.....akatokezea kando ya mto akaufuata mto huo ili apoze njaa angalau kwa kunywa maji...ghafla akakutana uso kwa uso na Joshi....Makala akastuka! hofu kubwa ikatanda juu yake....akatimua mbio.....
kutokana na mwili wake kuwa mnene pamoja na kitambi akajikuta hawezi kukimbia kwa kasi..ghafla akakanyaga sehemu iliyokuwa na udongo tifutifu akatereza na kudondoka akatumbukia ndani ya mto...
Joshi akamfuata Makala ndani ya Mto huo...
wale maaskari watatu wakomuona Joshi...wakaanza kumfyatulia Risasi mfululizo.. Joshi akaacha kumfuata makala akawafuata wale maaskari....
kumbe kamanda Michael hakuwa mbali na eneo hilo akasikia milio ya Risasi akaamua kuja upande huo..akakawaona wenzake wakiendelea kumfyatulia risasi Joshi lakinj Joshi aliendelea kuzipiga hatua kuwafuata....!!
Kamanda Michael akajumuika na wenzake akaanza kufyatua Risasi mfululizo
Risasi ziliingia kwenye mwili wa Joshi lakini akazitema kupitia mdomo wake....
Michael akachukua ile silaha maalumu kwa kutungulia ndege angani...iliyokuwa mgongini mwake...akaweka shabaha kumlenga Joshi.....akabofya kitufe cha kufyatulia...likatoka kombora likaenda moja kwa moja mpaka kifuani mwa Joshi....likatoa mripuko mkubwa ukiambatana na moto pamoja na moshi mkubwa,,,punde si punde ukaonekana ule mzimu ulioingia kwenye kiwiliwili cha Joshi ukitoka na kupotelea hewani,,,kitendo hicho wale maaskari hawakukiona kwa sababu walikuwa wakipongezana kwa ushindi ....baada ya dakika mbili moshi pamoja na moto ukatoweka... lakini wakamuina Joshi akiwa anaelea juu ya maji huku kafumba macho...wakafurahi sana...wakaamini kuwa wamemuangamiza Joshi....
******************
upande mwingine alionekana Makala akitimua mbio..akakutana uso kwa uso na kundi la watu wengi wa jamii ya Wakololo wakitimua mbio kuja upande wake....akastuka..akageuza na kukimbia kurudi alipotoka..akajikwaa na kudondoka chini...alipotaka kunyanyuka akaona tayari amechelewa!! kwani wakololo walikuwa wamemkaribia hatua tano kutoka hapo alipo..akakata tamaa akajua ndio mwisho wa uhai wake..akafumba macho na kufunika uso kwa kutumia viganja vyake....lakini akastahajabu kusikia tu vishindo vya miguu.... akafumbua macho yake..akashangaa kuona wakololo wanatimua mbio wakimpitiliza bila kumgusa....akajiuliza,,"watu hawa wanamaanisha nini? mbona hawanikamati!!?
kumbe ule mzimu ulitoka kwa Joshi na kwenda kuingia kwenye kiwiliwili cha Mtemi...akili ya Mtemi ikabadilika,,akaingiwa na Roho ya kikatiri..akaanza kuwafyeka shingo Wakololo wenzake.....kwa kuanza kuangamiza familia yake,,alimchinja Vida(binti yake) pamoja na Subi(mkewe)
wale wakololo waliobaki walishuhudia Mtemi akifanya mauwaji hayo...wakajisemea moyoni ,," kama Mtemi kaweza kumchinja binti yake kipenzi, pamoja na mkewe,,,sisi hatoweza kutuacha tukiwa hai wakaamua kutimua mbio ili kuokoa uhai wao.....
Makala aliendelea kuwashangaa wakololo wakizidi kumpitiliza na kutokomea mstuni.....wakati anastahajabu na kujiuliza maswali ghafla...akasikia kitu kimedondoka kando yake..alipogeuza shingo yake kutazama...akaogopa sana baada ya kuona kichwa cha mkololo mmoja aliyechinjwa.......
Makala akanyanyuka haraka,,akatimua mbio kusonga mbele zaidi angalau atafute sehemu ya kujificha.......
*******************
upande mwingine kule makao makuu,,
yule kuu wa kitengo cha utafiti,,akaanza kuipatwa na wasiwasi,,,lei ni siku ya tatu hajapata taarifa yoyote!!! pia hata kile kikosi cha maaskari saba(7) wakiongozwa na Kamanda Michael hawajawasili kazini,,,kutoka kwenye msitu UNGEBO.....akateuwa kikosi kingine cha watu kumi(10) waende kule mstuni kuchunguza nini kinaendelea... huenda kamanfa Michael na maaskari wenzake wamepatwa tatizo....
amri ikatekelezwa mara moja..na safari ya kwenda msitu UNGEBO ikaanza...
*****************
upande mwingine kule mstuni..alionekana Michael pamoja na maaskari wenzake watatu....wakiwa bado wamesimama kandi ya mto...Michael akauliza,,"wenzenu watatu mmewaacha wapi??
wale maaskari wakashindwa kujibu....huku nyuso zao zikionesha kuwa na huzuni ya ghafla baada ya kuulizwa swali hilo......
askari mmoja akasema,,"jana usiku mvua ilipokuwa inanyesha askari mmoja alipatwa na maradhi ya kifua....yaliyosababishwa na baridi kali..mpaka akapatwa na Mauti...
Michael alisikitika sana kusikia taarifa hiyo...akauliza tena,," na wenzenu wawili wapo wapi??
kabla hajamalizia sentensi,,yule askari akadakia na kusema,,"wameuwawa kwa mitego hatari iliyotegwa mstuni....
Michael akauliza kwa mshangao,," Mitego??? upande upi??
yule askari akasema huku aikisonta kwa kidole chake,,"upende ule kwenye ile miti mirefu....
Michael akastuka!! akasema,,"MUNGU WANG inamaana ile mitego imeuwa askari wangu mwenyewe??
wale maaskari wakatazamana wakauliza kwa pamoja,,"unamaanisha nini Kamanda??
Michael akajibu,,"Mimi ndiye niliyetega mitego hiyo kwa lengo la kuwinda mnyama kwa ajili ya kitoweo....
wakajikuta wapo katika hali ya majonzi....ghafla wakamuona Joshi anakurupuka baada ya kupata fahamu,,sasa hivi alikuwa katika hali ya kawaida alikuwa ni binadamu kabisa,,baada ya ule mzimu kutoka ndani ya kiwiliwili chake,,,lakini Uso wajoshi ulikuwa vilevile unatisha,,,kwa sababu uso wake haukuwa na gozi ya juu hivyo ilionekana nyama ya ndani kama kilivyo kidonda.....
Michael na maaskari wenzake wakaweka bunduki zao tayari kwa kumshambulia Joshi....wakabofya vitufe vya kufyatulia risasi...hazikutoka...walipotazama bunduki zai wakagundua Risasi zimekwisha....wakahisi kuchanganyikiwa....
Joshi aliona wale maaskari wameshikilia bunduki zao kuzielekezea upande wake..akanyoosha mikono yake juu,,kisha akapaza sauti,,"jamani msiniuwe!! mimi ni raia mwema..
Kitendo kile kilimshangaza Michael..naye akapaza sauti,,"hivyohivyo ulivyo njoo huku ukiwa umenyoosha mikona yako juu...
Joshi alifanya kama alivyoambiwa akazunguka na kupita kwenye mawe yaliyokuwa yamepangana kwa mstari akavuka na kutokezea upande wa pili....Kamanda Michael akasema,,"lala chini
Joshi akalala chini haraka...Michael akamfuata na kumfunga kamba kwenye mikono na miguu....
kisha akamnyanyua na kumkalisha kitako..
akaanza kumuhoji,,kwa nini alikuwa anafanya mauwaji!! Joshi alishangazwa na swali la Michael..akauliza kwa mshangao,,"MAUWAJI?? mbina mimi sijafanya mauwaji!! kwani hapa nimefikaje??
Michael akastuka akachomoa kisu akakiweka kwenye shingo ua Joshi akasema,,wewe umeuwa askari wangu mmoja kwa kurusha upanga ukamchoma....alafu unajifanya haujui kilichokuwa kinaendelea???? sasa nasema hivi! usiponiambia ukweli nakuchinja bila huruma...Joshi akaingiwa na hofu akasema kwa sauti ya unyenyekevu...Utaniuwa bure...lakini ukweli ni kwamba mimi sijui chochote...na sijui nimefikaje huku mstuni.......
maneno hayo yalimfanya michael akasirike...kwa kuona Joshi anadanganya hajafanya mauwaji..wakati yeye alimshuhudia kwa macho yake....akakandamiza kisu ili amchinje Joshi....ghafla wakaona askari mmoja anadondoka chini...Michael akastuka...pia wale maaskari wawili wakaingiwa na hofu kubwa...kumuona mwenzao kadondoka chini huku kisu kikiwa kimeingia upande wa ndani ya koo..kikining'inia...Michael akamtazama Joshi kwa macho ya chuki na hasira za hali ya Juu akamdunga kisu cha paja kisha akasema kwa sauti ya ukali,,"NIAMBIE NINI KINAENDELEA...akabla hajamaliza kuongea wakasikia vishindo vikubwa....mpaka aridhi ikawa inatetemeka...alipotazama uoande wa pili wa mto..akamuona Mtemi akiwa ametapakaa damu mwili mzima..Michael akamuacha Joshi...
huku akisema tukimbieni...wakaanza kutimua mbio huku wamemuacha Joshi pale chini.....
Joshi akaingiwa na hofu kubwa......huki akihisi maumivu makali sana kwenye lile jeraha alilochomwa kisu na kamanda Michael kwenye paja...alipotazama ule upande aliokuwepo Mtemi...hakumuona tena....Joshi akazidi kuchanganyikiwa alishindwa kunyanyuka kutoka pale chini kwa sababu alikuwa kafungwa mikono na miguu...mapigo yake ya moyo yakazidi kupiga kwa kasi.. akajikuta vinamtoka vijampo mfululizo.(bhu bhu) kutokana na uwoga wa hali ya ju..
********************
Upande mwingine...alionekana Michael na maaskari wenzake wakitimua mbio..lakini Michael akaingiwa na roho ya huruma!! akajisemea moyoni,,"sio vyema kumuacha pale yule mtu...wakati kunahatari...akaamua kurudi kumfuata Joshi amfungulie kamba....
wale maaskari wawili wakashangazwa na kitendo cha kanda Michael...kurudi kule kwenye hatari!! lakini Michael hakujali alitimua mbio mpaka kule alipomuacha Joshi..akamfungulia kamba kisha akasema,,"tuondoke haraka..
Joshi alimshukuru Michael..alimuona kama Mwokozi wake........
*********************
upande mwingine...walionekana wale maaskari kumi(10) waliotumwa kutoka makao makuu kuja msitu UNGEBO..maaskari hao walianza kukaribia kufika msitu Ungebo na baada ya dakika tano wakafika...wakashuka kutoka ndani ya gari na kuanza kusonga ndani zaidi ya msitu huo kwa kutembea kwa miguu....ghafla wakakutana uso kwa uso na wakololo wakitimua mbio kuja upande wao huku wameshikilia mikuki na mishale....
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni