Mtunzi: Yozz Piano Maya
SEHEMU YA NANE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
upande mwingine...walionekana wale maaskari kumi(10) waliotumwa kutoka makao makuu kuja msitu UNGEBO..maaskari hao walianza kukaribia kufika msitu Ungebo na baada ya dakika tano wakafika...wakashuka kutoka ndani ya gari na kuanza kusonga ndani zaidi ya msitu huo kwa kutembea kwa miguu....ghafla wakakutana uso kwa uso na wakololo wakitimua mbio kuja upande wao huku wameshikilia mikuki na mishale....
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Wale maaskari wakasema mpo chini ua ulinzi....
wakololo hawakusikia wala kutii amri ya maaskari hao...wakololo walizidi kutimua mbio kuja ule upande walipo maaskari hao....
maaskari wakaingiwa na hofu wakajihami kwa kufyatua risasi angani.....lakini wakololo hawakusimama waliendelea kukimbia wakapitiza kuelekea upande ambao maaskari walitokea bila kuwagusa maaskari hao...
mpaka wakatokomea na kutokuonekana kabisa..
maaskari wakashangazwa na kitendo hicho...lakini hawakujali wakazidi kusonga mbele kuingia ndani ya msitu huo...
wakati huohuo alionekana Mtemi akiendelea kuzipiga hatua kusonga mbele zaidi....ghafla akakutana uso kwa uso na wale maaskari kumi...
akasimama na kuwatazama..... askari mmoja akauliza,,"wewe ni nani? mbona umevaa ngozi ya mnyama(Simba)? ulipata wapi kibali cha kuuwa mnyama wa mstuni na kumchuna ngozi??
Mtemi alibaki kimya bila kujibu chochote.....Maaskari hao waliendelea kumshangaa,, yule askari mmoja akasema,,"upo chini ya ulinzi,nyoosha mikono yako juu...
Mtemi aliendelea kumtazama yule askari,,kisha akazipiga hatua kuosogelea....alipomkaribia akarushakofi kali sana,,likampiga yule askari usoni...kofi hilo lilimrusha mbali askari huyo....
wale maaskari tisa wakastuka wakaanza kumshambulia Mtemi kwa risasi......walifyatua risasi mfululizo lakini Mtemi hakudhurika na risasi hizo...zilindunda kwenye mwili wake na kudondoka chini... wale maaskari wakaingiwa na hofu..wakaanza kutimua mbio..kurudi nyuma walipotoka...
Yule askari aliyepigwa kofi,alionekana kalala chini akiwa amekufa....
Mtemi akazipiga hatua na kusonga mbele zaidi....
*****************
Upande mwingine alionekana kamanda Michael akiwa na Joshi,pamoja na wale maaskari wawili..
wakikimbia na kuingia ndani ya pango kubwa kiasi...wakajificha.....Kamanda Michael akaanza kumuhoji Joshi,,alimuuliza juu ya mauwaji aliyokuwa akiyafanya....Joshi akajibu,,"kiukweli mimi sifahamu chochote,,kama nilivyokueleza mwanzo,,hata sifahamu nimefikaje ndani ya msitu huu!!!! lakini kwa kumbukumbu zangu,,mara ya mwisho nilimzika muuwaji...
Kamanda Michaeli akauliza kwa mshangao,,"MUUWAJI?? ni yupi huyo??
Josgi akasita kuongea... akashusha pumzi,kisha akasema,,"ndio,,namaanisha Muuwaji aliyeuwa wazazi wangu..
Michael bado alibaki mdomo wazi,,hakuelewa maneno aliyokuwa anayaongea Joshi.....
akauliza,,"ulimzija wapi huyo muuwaji? inamaana kuwa huyu anayefanya mauwaji ndiye yule muuwaji uliyemzika??
Joshi akajibu,,"mimi sijui chochote!!
Michael alizidi kuchanganyikiwa,,,hakumuelewa joshi anachokiongea....
********************
Upande mwingine walionekana wakololo wakiendelea kutimua mbio....walikimbia umbali mrefu,,wakaliona lile hema lililokuwa kama kambi ndogo yakupumzika maaskari wanaokuwa kwenye zamu ya kulinda wanyama pori...
wakololo wakasimama na kulitazama hema hilo...wakaamua kuelekea kwenye hema hilo....walipolikaribia,,yule mkuu wa vijana wa kikololo akaingia upande wa dani,,akaangaza angaza macho yake kila kona ya hema hilo....kisha akatika nje na kuongea kwa lugha yao akimaanisha,,"Tutapumzika hapa panaonekana kunausalama..
***************
upande mwingine alionekana Mtemi akizidi kusonga mbele zaidi....alitembea umbali mrefu,,hatimae akatokezea jirani kabisa na lile hema..
wakati huo huo walionekana wale maaskari tisa wakimbia kuelekea ule upande lilipokuwepo hema...
********************
Upande mwingine kule ndani ya pango Joshi alionekana kama kuna jambo atataka kumueleza Kamanda Michael.....ghafla simu ya mawasiliano kutoka makao makuu ikaita.... Michael akaipokea..
akamsikia mkuu wa kitengo cha hifadhi ya wanyama pori akisema,,"mbina tunajaribu kuwatafuta lakini mtandao haukamati mawasiliano yenu? kunatatizo gani? Michael akajibu,,"kunaatatizo makubwa sana ndani ya msitu huu..na sidhani kama kuna mtu atafanikiwa kutoka akiwa hai..kabla hajamaliza kuingea....simu(Radio call) ikamponyoka na kudondoka kwenye jiwe ikapasuka na kusambaratika....
*******************
kule kwenye hema walionwkana wakololo wakitengeneza silaha za jadi kwa kutumia...miti kuchonga mishale mingi sana!! mkuu wa vijana hao wa kikololo akatengeneza mshale moja.na kuupaka dawa maalumu....dawa hiyo ni ile dawa ya kumuangamiza mzimu aliyeingia kwenye kiwiliwili cha binadamu.....mkuu wa vijana wa kikololo alipewa dawa hiyo na babu yake...alimkabidhi dawa hiyo,,usiku kabla ya kifo chake....mkuu wa vijana wa kikololo akaitunza dawa hiyo kwa kuihifadhi kwenye kipande cha ngozi ua nyani aliyokuwa akitembea nayo kila sehemu aendako....
akachukua ule mshale alioutengeneza,,maalumu kwa kazi hiyo akapaka dawa ile kwenye ncha ya mshale huo.......
wakati wakololo wakiendelea kutengeneza mishale ya kutosha...wakamuina mtemi anakuja upande wao kule hema lilipo...
TAHARUKI....
wakati huo huo walionekana wale maaskari tisa kati ya wale maaskari kumi..ambao mmojawapo aliuwawa na Mtemi. walitimua mbio kulifuata hema...walipolikaribia hema hilo wakastuka kuwakuta wale wakololo...pia wakamuona Mtemi...
walipojaribu kushambulia kwa Risasi..wakakumbuka bumduki zao hazina hata risasi moja..wakaamua kutimua mbio kurudi kule mstuni...
***********************
upande meingine alionekana Makala akiwa anakimbia akaingia ndani ya kichaka kwa lengo la kujificha....akastuka kukuta joka kubwa ndani ya kichaka hicho,, akaingiwa na hofu kubwa..akakurupuka na kutimua mbio....alikimbia mwendo mrefu kiasi...akakutana na maaskari wawili wameuwawa kwe mtego uliokuea umetegwa mstuni humo...
kumbe ndio wale maaskari walionaswa na ule mtego uliotegwa na Machael....
Macho yakamtoka Makala!! akaingiwa na wazo,kuwa achukue nguo zilizokuwa juu ya mwili wa askari...ili ajistili kwa sababu alikuwa uchi wa mnyama.....akazipiga hatua akainasua kutoka kwenye mtego maiti moja ya askari.ili achukue zile nguo avae.....alipomaliza akaanza kuzipiga hatua kwa tahadhali huku macho yake yakitazama
kwa umakini wa hali ya juu...alitembea umbali mrefu kiasi akiifuata ile njia iliyokuwa ikielekea kwenye hema pasipo yeye kujua.....Makala aliamua kuifuata njia hiyo akihisi huenda itamsaidia kutoka nje ya msitu huo
*****************
wakati huohuo alionekana kamanda Michael akiwa na Joshi pamoja na wale maaskali wawili...wakizipiga hatua kutafuta njia ya kuelekea kule kwenye Hema angalau wapumzike pia waangalie namna ya kufanya mawasiliano na makao makuu.. ili iletwe ndenge waweze kupata msaada.....walipokaribia wakaona wakololo wakimshambulia Mtemi kwa mishale mingi mfululizo...mishale hiyo iliingia kwenye mwili wa Mtemi lakini haikumdhuri...
wakololo waliendelea kumshambulia Mtemi wao kwa mishale....
akaonekana yule mkuu wa vijana wa kikololo akiuchukua ule mshale alioupaka dawa maalumu ya kuangamiza mzimu ulioingia kwenye kiwiliwili cha binadamu....akauweka mshale huo kwenye upinde na kupiga hatua mbili kulifuata dirisha la hema hilo......akaweka shabaha kumlenga Mtemi katikati ya kifua...
wakati huo huo akaonekana makala akitokeza kwenye eneo lilipokuwepo hema hilo...akastuka kuwaona wakololo wakimshambulia Mtemi kwa mishale...akajificha nyuma ya mti mkubwa kiasi huku akiendelea kushuhudia vita ya Wakololo na Mtemi wao....kumbe kamanda Michael,,,Joshi pamoja na wale maaskari wawili walikuwa eneo hilohilo..wakatokea nyuma ya makala,, Kamanda Michael akasema,,"nyoosha mikono yako juu..Makala aliposikia hivyo akakurupuka na kutimua mbio bila kugeuka nyuma..akakimbia na kutokeza sehemu iliyokuwa wazi hakuna miti...jirani kabisa na lile hema...
kule mdani ya hema alionekana yule mkuu wa vijana wa kikololo akiuvuta upinde kwa nguvu zake zote..mpaka misuli ya mikononi,,svhingoni pamoja na kichwani ikachomoza.....akauachia mshale..kuelekea kwenye kifua cha Mtemi,,punde si punde Mtemi akageuka kumtazama makala akikimbia bila muelekeo huku akidondoka chini mara kwa mara kutokana na ukubwa wa kitambi,
mshalee ule ukawa umempiga Mtemi kwenye bega lake la kushoto...ghafla ule mzimu ukatoka ndani ya kiwiliwili cha Mtemi na kuelekea angani...
kumbe mshale ule ungeingia katikati ya kifua cha Mtemi basi ndio ungekuwa mwisho wa mzimu huo......
ule mzimu ulionekana ukielea hewani kuelekea ule upande alipokuwepo kanda michael.....Joshi pamoja na wale maaskari wawili,,
Wakati huo Makala alikuwa kadondoka chini...wakati ananyanyuka ule mzimu ukaingia kwenye kiwiliwili cha Makala.......akili ya Makala ikabadilika..akaingiwa na Roho ya kikatiri kuliko Mtemi na Joshi..walipoingiliwa nazimu huo.
Makala akawa ni mtu katiri wa kutisha..akazipiga hatua kulifuata hema....
kitendo cha Makala kuingiwa na mzimu,,,, hakuna mtu yeyote aliyeweza kuona jambo hilo.....
Wakololo walionekana kufurahia kuutoa Mzimu uliokuwa umeingia kwenye kiwiliwili cha Mtemi wao....walimpongeza sana mkuu wa vijana wa Wakololo...huku wakipiga kelele za shangwe kifurahia ushindi.....Mtemi alizinduka akanyanyuka pale chini..baada ya kupata fahamu!! akainekana kustahajabu kujikuta yupo eneo hilo...wakololo wakamsogelea Mtemi wao....huku wakimpa pole kwa kuongea lugha yao.....ghafla wakamuona Yule mtu aliyetakiwa kuuwawa kwa kunyongwa(Makala)..baada ya kukutwa na Vida(binti wa mtemi)
wakastuka kumuona kavaa nguo za kiaskari zilizofanana na wale maaskari waliowapita kulestuni....wakabaki wakimtazama Makala...
Makala alizipiga hatua mpaka pale walipokuwa wamekusanyika wakololo kumzunguka Mtemi wao...alipofika akasimama na kutazama nyuso zao...ghafla akamvuta kijana mmoja wa kikololo na kumnyang'anya mkuki..akamdunga kwenye koo!!
wakololo wakastuka wakaingiwa na hofu..
wakati wanatahamaki..Makala akamchoma mkuki wa tumboni kijana mwingine wa kikololo..
Mtemi akapaza sauti kwa lugha yao..akimaanisha,,"shamvulia mtu huyu...
vijana wa kikololo wakaanza kumshambulia Makala kwa mishale...lakini mishale hiyo haikumdhuru Makala..
Makala aliendelea kufanya mauwaji ya kikatiri...
kwa mbali alionekana kijana wa kikololo akimfuata Makala kwa nyuma ili amchome mkuki...Makala akageuka na kumchoma mkuki wa Jicho ukatokezea kisogoni..kisha akauinua mkuki huo na kumrusha mkololo huyo mbali zaidi...
wakololo wakamchukua Mtemi na kutimua mbio kuelekea mstuni....baada ya dakika kadhaa hakuonekana hata mkololo mmoja...wote walitokomea mstuni...wakabaki baadhi ya wakololo waliouwawa wakiwa chini.....
kamanda Michael,,, Joshi pamoja na wale maaskari wawili wakatimua mbio kurudi stuni.. baada ya kuona mambo yamekuwa magumu.....
****************
Upande mwingine walionekana Wakololo wakiendelea kutimua mbio wakajikuta wametokezea kwenye kijiji chao...Mtemi alikasirika sana kukuta binti yake(Vida)kauwawa pamoja na mke wake(Subi) akawachukia sana wale maaskari kwa kuhisi,,maaskari ndio wameleta mzimu huo ndani ya Msitu....
kwa sababu..Mtemi alipozinduka na kulata fahamu baada ya mzimu kutoka kwenye kiwiliwili chake.....alimuona Makala akiuwa wakololo,,,na kwa sababu makala alikuwa kavaa nguo za kiaskari...basi Mtemi akajua maaskari watakuwa wanajua kuhusu mzimu huo....
Mtemi akatoa amri kwa vijana wa kikololo waende kuangamiza maaskari wote waliokuwemo ndani ya msitu huo.....vijana wa kikololo wakaandaa zana za kazi...ikiwemo mishale,,,mikuki,,pamoja na silaha nyinginezo za jadi...wakaingia mstuni kuwatafuta maaskari......
VITA KABAMBE...
Wakati huo huo alionekana Kamanda Michael,Joshi pamoja na wale maaskari wawili...
Michael akasema,,"itabidi tufanye jambo ili tuweze kutoka nje ya msitu huu tukiwa hai..
Joshi na wale maaskari wawili walimsikiliza Kamanda Michael kwa makini,,huku wakimtazama usoni....askari mmoja akauliza,,"kamanda sasa tufanye jambo gani? na bunduki zetu hazina risasi hata moja...
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi