JICHO LA TATU (9)

0

SEHEMU YA TISA
TULIPOISHIA...
Michael akasema,,"itabidi tufanye jambo ili tuweze kutoka nje ya msitu huu tukiwa hai..

Joshi na wale maaskari wawili walimsikiliza Kamanda Michael kwa makini,,huku wakimtazama usoni....askari mmoja akauliza,,"kamanda sasa tufanye jambo gani? na bunduki zetu hazina risasi hata moja...

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
Michael akasita kuongea,,akafungua bunduki yake akatazama upande wa risasi..akaona kabakiwa na risasi moja tu....akasema,,"tafuteni miti mirefu migumu..,,muichonge zitengeneze ncha kali,,angalau mpate silaha kwa ajili ya kujihami....wale maaskari wawili wakakubali kutekeleza wazo la kamanda Michael..wakazipiga hatua na kuingia ndani zaidi ya msitu huo kutafuta miti mirefu migumu.....

**************************

Upande mwingine walionekana wale maaskari tisa wakiwa bado wamejificha kwenye kichaka kikubwa kiasi...walikaa hapo kwa masaa mengi..walipo ona ukimya umetawala wakaamua kutika ndani ya kichaka hicho..wakasonga mbele kutafuta njia ya kutoka ndani ya msitu huo... walipotembea mwendo wa dakika arobaini mfululizo...wakakutana uso kwa uso na Wakololo! kijana mmoja wa jamii hiyo ya wakololo akaweka mshale kwenye upinde akauvuta,,,kabla hajaachia mshale huo vikasikika vishindo vizito!! punde si punde wakamuona Makala anakuja upande wao huku mikono yake ikiwa imetapakaa damu...

wale maaskari tisa wakatimua mbio....na kutokomea mstuni..walikimbia kila mmoja alipita njia yake.....

Wakabaki wakololo wakipambana na Makala walimpiga mishale mingi isiyokuwa na idadi....lakini mishale hiyo haikumdhuru makala..akamkamata kijana mmoja wa kikololo akamnyofoa kichwa na kukirusha mbali....wakololo wakaamua kutimua mbio,baada ya kuona mabo yamekuwa magumu....

*************************

Upande mwingine kule makao makuu alionekana mkuu wa kitengo cha wanyama pori akiamuru ndege tatu za kivita zielekee msitu Ungebo..kisha akatoa amri kuwa wahakikishe wanaangamiza kila kitu kitakachoonekana ndani ya msitu huo...

mkuu wa kitengo hicho..aliamini maaskari wote wamekufa ndani ya msitu huo...kwa sababu leo ni siku ya nne hajapata taarifa wala mawasiliano yoyote kutika kwa maaskari waliokwenda ndani ya msitu huo.........ndege gizo za kivita aina ya (chopper) zikaruka angani kuelekea msitu Ungebo..

********************

kule mstuni walionekana wale maaskari wawili wakiwa wanachonga fito ndefu ngumu....ghafla wakololo wakaonekana wakikimbia kuja upande huo...walipowaona maaskari wakawashambulia kwa kuwachoma mikuki mpaka wakafa....

upande mwingine alionekana kamanda Michael akimwambia Joshi..aende kuwatazama wale maaskari wawili waliokwenda kutafuta fito kwa ajili ya kutengeeza silaha mbadala.....Joshi akazipiga hatua kuelekea ule upande walioelekea wale maaskari wawili akastuka kukuta wakiwa chini wameuwawa huku damu nyingi zikiwatoka mwilini!! joshi akatimua mbio kurudi kwa kamanda Michael...akatoa taarifa...kuwa amekuta wale maaskari wameuwawa. Michael akastuka macho yakamtoka baada ya kupokea taaeifa hiyo kutoka kwa Joshi.....

**************************

upande mwingine walionekana maaska wanne waliokimbia njia moja kati ya wale maaskari tisa...walikimbia wakajikuta wamerudi kulekule kwa Makala.....walipomuo makala wakatimua mbio Makala akang'oa mti mkubwa..akaurusha kwa wale maaskari wanne waliokuwa wanaharibu kumkimbia...mti ule uliwaponda na kuwakandamiza,maaskari watatu wakafa papo hapo...na askari mmoja aliyekuwa amekandamizwa mguu na mti huo..alipiga kelele kwa maumivu makali aliyoyapata baada ya kuvunjika miguu yote miwili huku ikiwa bado imekandamizwa na mti huo.....Makala akazioiga hatua kumfuata askari huyo alipomkaribia akampiga teke kali la uso,,kichwa cha askari huyo kikang'oka na kuruka kando!! akafa papohapo...

Makala akazipiga hatua kusonga mbele zaidi...kuelekea ule upande aliokuwepo Kamanda Michael na Joshi......wakati huo huo alionekana Michael na Joshi wakitoka eneo hilo kuelekea ule upande aliokuwepo Makala....ghafla wakakutana uso kwa uso na Makala.....Michael na Joshi wakashtuka!!!

wakati wanatafakari wafanye nini! ikasikika milio ya ndege za kivita zikiwa tayari zimeingia kwenye anga la msitu huo........

Ndege hizo zikaanza kurusha makombora mfululizo...Ghafla rubani mmoja akahisi kama kaona watu ndani ya msitu huo..akamwambia mwenzake aliyekuwa ameketi kwenye kiti cha pembeni yake,,"nahisi kama nimeona maaskari wenzetu....ebu chukua darubini(Binocolus)tazama kwa makini upande wa chini,,tusije tukawaangamiza maaskari wenzetu,,yawezekana bado wapo hai! yule askari akachukua darubini..akatazama upande wa chini kwa kutumia Darubini hiyo...akastuka kumuona Kamanda Michael akipambana na Makala....wakaamua kufanya mawasiliano na makao makuu...ili watoe taarifa kuwa baadhi ya maaskari wapo hai ndani ya msitu huo!! hivyo zoezi la kufanya mashambulizi kwa kurusha makombora lisitishe..

*************************

Upande mwingine walionekana wakololo wakiendelea kuwawinda maaskari waliokuwemo ndani ya msitu huo.....wakakutana na maaskari watatu..kati ya wale maaskari tisa....wakawauwa kwa kuwalenga na mishale..wakafa papo hapo.

kisha wakololo wakazidi kusonga mbele kutafuta maaskari waliobakia wawaangamize...

**************************

upande mwingine alioneka Kamanda Michael akiendelea kupambana na Makala....

Makala akastahajabu sana kwa nini kamanda Michael anamsumbua mpaka Muda huu hajaweza kumkamata Mikononi mwake!!

wakati huo Joshi alikuwa kando kajificha kwenye kichaka akishuhudia vita kabambe,,baina ya Kamanda Michael na Makala.....Jishi akaingiwa na wazo akajisemea moyoni,,"yanipasa nikimbie. huyu ,,kamanda Michael hawezi kupambana na huyo Mtu!! na bila kutumia akili ya ziada hatuwezi kutoka tukiwa hai ndani ya msitu huu.

Joshi akakurupuka kutoka ndani ya kichaka hicho akatimua mbio...baada ya kukimbia mwendo wa dakika tatu akakutata uso kwa uso na wakololo...

akaingiwa na hofu kubwa..punde si punde ikasikika miripuko ya mabomu ndani ya msitu huo...mabomu hayo yalitoa mlio mkali sana kwa mfululizo..Wakololo wakaingiwa na hofu...tangu wamezaliwa ndani ya msitu huo,,hawajawahi kusikia mlio wa namna hiyo..

wakaamua kutimua mbio wakamuacha Joshi..kumbe ule upande ambao Wakololo wanaelekea,,ndio ule upande ambao yupo Makala anapambana na Kamanda Michael...

**********************

Ulande mwingine kule makao makuu alionekana Mkuu wa kitengo akipokea mawasiliano kutoka kwa rubani mmoja kati ya maruban watatu waliokwenda msitu Ungebo..na ndege tatu za kivita aina ya (chopper)

akaamuru wasitishe kurusha makombora kwenye msitu Ungebo....amri ikatekelezwa wale marubani..wakasitisha kuendelea na mashambulizi.....

******************

kule ndani ya msitu,,Kamanda michael alionekana kuzidiwa nguvu na Makala.....

Michael akaanza kuchoka..kwa sababu alikuwa akimkwepa Makala kwa kutumia akili na nguvu nyingi... ..ghafla Michael akadomdoka chini..huku akionekana kuregea kupita kiasi,,jasho lilikuwa linamtoka mfululizo,,,Makala akazipiga hatua kumfuata michael pale chini alipokuwa amedondoka.....alipomkaribia akanyanyua mguu wake ili ampige teke la uso ang'oe kichwa cha Michael...ghafla wakalolo wakatokezea sehemu hiyo..wakaanza kurusha mishale kumshambulia Makala..Makala akamuacha Michael na kuwafuata Wakololo...

Wakololo walirudi nyuma huku wakiendelea kumshambulia Makala kwa mishale...

*********************

Upande mwingine alionekana Joshi akiendelea kutimua mbio baada ya kunusurika kifo kutoka kwa Wakololo...wakati anakimbia..akaingiwa na roho ya huruma,,akajisemea moyoni,,"kamanda Michael aliokoa maisha yangu...sio vyema kumtelekeza ndani ya msitu huu,,Joshi akaamua kurudi kule alipomtelekeza kamanda Michael!!

alipofika akakuta wakololo wakimshambulia Makala kwa mishale mfulilizo..Wakololo wakaanza kupungukiwa mishale..hatimae wakajikuta kila kijana wa kikololo kashikilia upinde tu ba hata kuwa na mshale mmoja!! walipo ina mambo yamekuwa magumu wakaamua kutimua mbio..na kutokomea mstuni...

wakati huo kamanda Michael alikuwa hoi!! bado kalala pale chini alipodondoka......akanyanyuka kutoka pale chini..........

wakati huo huo Makala akamuona Joshi amejificha nyuma ya mti..

akamfuata,,alipomkaribia akanyanyua akanyanyua mguu ili amkanyage kifuani...Ghafla ikasikika sauti ikisema,,"Muache mtu huyo..kama unauwezo wa kupambana njoo upambane na mimi...

Makala akamtazama Michael kwa hasira kisha akamtazama Joshi...

Makala akainua mguu wake...kabla hajaushusha kifuani mwa Joshi...Michal akachomoa kisu chake kilichotengenezwa kwa madini ya shaba...alichozawadiwa na mkuu wa kitengo...kama pongezi ya askari mtiifu,,,akakirusha kisu hicho,kikaenda moja kwa moja mpaka kwenye mgongoni wa Makala..Punde si punde!!,, ukaonekana moshi ukitokea kwenye ile

sehemu alipodungwa kisu hicho cha shaba..

kumbe ule mzimu haupatani na madini ya shaba..ni mwiko kwa mzimu huo...Makala akaanza kupiga kelele..ghafla moshi ukazidi kuongezeka...kumbe moshi huo ndio mzimu ulikuwa unajitoa kwenye miwiliwili cha Makala..ghafla moshi huo ukatoweka kimiujiza na ikawa ndio mwisho wa mzimu huo...Makala akaonekana kujishangaa!!! huku akiutazama mwili wake....akaangaza angaza macho yake..akamuona Michael akauliza,,"kwani wewe ni nani??

Michael akashangaa kumsikia makala akimuuliza swali hilo!! Joshi akadakia na kusema,,"huyu aliingiliwa na mzimu ule ulioniingilia mimi...

hata mimi pia niliushangaa mwili wangu baafa ya mzimu huo kutoka ndani ya mwili wangu...lakini hawezi kukumbuka chochote....kwa sababu mawazo na akili haikuwa yake...alikuwa anaongozwa na mzimu huo......punde si punde wakaonekana wale maaskari watano waliobaki hai kati ya wale maaskari kumi...waliokuja mstuni humo kwa awamu ya pili..Walifurahi kumuona kamanda Michael...

Michael akasema tusipoteze muda..tuondokeni...wakaanza safari ya kutoka ndani ya msitu huo....walitembea mwendo wa masaa matatu mfululizo...

kwa mbali wakasikia mngurumo wa gari....wakatimua mbio kuufuata mngurumi huo..wakafanikiwa kuliona gari la jeshi lao...wakapiga mayowe ili wale maaskari waliokuwemo ndani ya gari hilo wasikie pia waweze kuwaona.....

kwa sababu walikuwa wameanza kutoka nje ya msitu huo...waliweza kuonekana kwa urahisi..kutokana miti ya eneo hilo haikuwa mingi sana...gari hilo likawafuata na kuwachukua...Wale maaskari watano,,kamanda Michael pamoja na Joshi.....wakaianza safari ya kutoka nje kavisa ya msitu huo na kuelekea makao makuu..

*************************

Baada ya mwendo wa masaa kadhaa...wakaanza kuingia mjini...Joshi na Makala wakaomba washushwe hapo mjini...wakawashusha....kisha kamanda Michael pamoja na wale maaskari wengine wakaendelea na safari ya kuelekea makao makuu..

Makala akaamua kukodi pikipiki impeleke nyumbani kwake....na baada ya nusu saa alifika nyumbani salama...NOREGA(mke wa Makala) alifurahi kumuona mumewe....kisha makala akaingia chumbani akafungua kabati akatoa noti ya shilingi elfu kumi..akasema,,"kaampe dereva bodabida pesa hii...Norega akatoja nje akamlipa dereva bodaboda..na kueudi ndani huku akitabasamu akauliza,,"nguo zako ziko wapi?? mbona umevaa nguo za kiaskari??

Makala akamsimulia yaliowapata huko mstuni..Norega akasikitika sana..lakini akamshukuru Mungu kwa kumrudisha mumewe nyumbani akiwa hai...tangu siku hiyo makala akaacha kazi ya utafiti akawa mfanya biashara....

*******************

Asubuhi palipokucha,,,alionekana Joshi akiwa kule nyumbani kwake aliamua kuhama mji...akachukua vitu vyake vya thamani na kuviweka ndani ya begi...alipomaliza akatoka nje ya nyumba yake akafunga mlango...akaondoka kuelekea ubungo...akapanda basi kuelekea Mbeya....akaishi huko pia akaamua kuwa mkulima wa mazao ya chakula..

******************

kule makao makuu kamanda Michael akapandishwa cheo....kutokana na kufanya kazi kubwa kwa umakini na ushupavu.....

MWISHO

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)