KIJIJINI KWA BIBI (16)

0
Mwandishi: Alex Kileo

SEHEMU YA KUMI NA SITA
TULIPOISHIA...
"Ndio mkuu" Sajenti Minja alijibu,

"Mpelekeni akapumzike, mpeni kila atachohitaji" Mkuu wa Jeshi aliwaambia wale wanajeshi waliokuwa wamesimamia mateso ya Sajenti Minja,

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
"Sawa mkuu" Wanajeshi walijibu na kumuinua Sajenti Minja na kumpeleka wanapojua wao, Mkuu wa Jeshi akatoa tabasamu moja la karaha sana,

"Kesho akija na jibu tofauti na ninalolitaka mimi, Kambi itapata habari mbaya za mwenzao" Mkuu wa Jeshi aliongea huku akianza kuondoka,

"Utamuua au?" Mkuu wa Polisi aliuliza huku akimfuata,

"Hata wewe pia utajua kesho hiyo hiyo" Mkuu wa Jeshi alijibu na kumfanya mkuu wa Polisi anyamaze kimya.

Katika kituo cha polisi mahojiano kati ya

mchungaji na polisi yaliendelea vema, ila

mchungaji hakutaka kuwaambia kuwa mhusika

wa mauaji alikuwa nae, ila alichowaambia polisi

ni kwamba, hata yeye haelewi na hakumbuki kitu

chochote kilichotokea, zaidi ya kujikuta yuko nje

ya nyumba yake wamelala na familia yake na watu hasiowajua,

"Hiyo inawezekanaje?" Askari mmoja alimtupia swali Mchungaji huku akiwa ahamini maelezo yake,

"Hata mimi sijui imewezekanaje, ni kama maajabu Fulani hivi ya kiimani" Mchungaji Wingo alijibu huku akionekana dhahiri kushangaa,

"Kwa hiyo unadhani wale watu kumi ambao wamekufa kwa kunyonywa damu ni nani tutamuhusisha na vifo vile?" Askari akamtupia swali jingine,

"Sasa unaponiuliza mimi unataka nikujibuje, au unadhani nitasema unihusishe mimi na hivyo vifo?" Mchungaji Wingo aliuliza kwa sauti ya upole,

"Kisheria ni kwamba wewe na familia yako mpo hatiani kwa vifo hivyo" Askari aliongea huku akiandika andika katika kikaratasi kidogo juu ya meza,

"Sawa, ila hakuna mtu katika familia yangu ambaye ana uthubutu wa kuua hata mbu, sembuse mtu" Mchungaji Wingo aliongea kwa kujiamini,

"He nikikuweka ndani nitakuwa nimekosea ingawa unajitetea hivyo" Askari aliuliza,

"Siwezi kukupangia, fanya vile kazi yako inavyotaka" Mchungaji Wingo alijibu na kumfanya yule askari anyanyuke huku pingu zikiwa mkononi,

"Afande kati ya wale watu waliokutwa wamekufa kwa mchungaji, mmoja kumbe mzima" Askari mwingine aliongea wakati anaingia ndani ya chumba cha mahojiano,

"Kwa hiyo waliokufa ni tisa tu?" Askari aliyekuwa anamuhoji mchungaji aliuliza huku akianza kumfunga pingu mchungaji Wingo,

"Sasa huyo Mzee usimfunge pingu kwa maana yule mtu ambaye amezinduka amesema kuwa wamepata ajali na wala mtu yoyote asiusishwe na vifo vya wenzake" Askari aliyeingia aliongea na kumfanya mwenzake amkodolee macho,

"Una maana gani kusema hivyo?" Askari alimuuliza mwenzake,

"Kwa Maelezo ya yule mtu kule hhospitali, basis huyu mzee hana hatia" Askari mwenzake alijibu,

"Cha kuwashauri ni kwamba, kwa kuwa Huyo mmoja ameamka, ni vyema mngenipeleka na familia yangu mbele yake na aseme kama sisi tumewaua wenzake" Mchungaji Wingo aliongea kwa upole,

polisi walionekana kuridhika na maneno ya

mchungaji na familia yake, tena walimuamini

zaidi kwa sababu alikuwa mtumishi wa Mungu.

Baada ya mahojiano, polisi walimuachia

mchungaji arudi nyumbani kwake, ila wakamwambia wakimuhitaji watamfuata.

Mchungaji alipofika nyumbani kwake, moja kwa

moja akaenda kwenye chumba chake cha ibada,

akamkuta kayoza amekaa kimya anasoma biblia,

akamsalimia, kisha akamsimulia kilichotokea,

alafu akamrudisha kwa mama yake.

BAADA YA SIKU TATU..

Jioni wakati wanaongea kuhusu mambo yaliyotokea siku tatu nyuma.

Sebuleni alikuwepo mama kayoza, Kayoza na Omari,

"Hili tatizo hata mimi linaanza kunitisha, ina maana hata mchungaji ameshindwa?" Kayoza aliuliza huku anamtazama mama yake,

"Hakuna kinachoshindikana kwa Mungu, sema tu hayo mambo yaliyotokea usiku yalimvuruga" Mama kayoza alimjibu mwanaye,

"Kwa hiyo lini tena naenda Kuombewa?" Kayoza aliuliza,

"Mchungaji amesema utakuwa unaombewa kila Siku kwa ajili ya kukujenga imani" Mama Kayoza alijibu,

"Kwani mimi sina imani?" Kayoza aliuliza,

"Yaani hauna kabisa, kwa ninavyofahamu mimi, hata ungekuwa na imani kidogo tu ungepona" Mama Kayoza alijibu,

"Alafu kitu Kingine, hii habari ya tukio lililotokea juzi kwa Mchungaji lilivyotangazwa nchi nzima, hivi huoni hatari iliyopo mbele yangu?" Kayoza aliuliza,

" mimi sioni tatizo, mbona hhakuna hata chombo cha habari kilichokuhusisha na hizo habari" Mama Kayoza alijibu,

"sawa, ila ukae ukijua kuwa Polisi wana akili sana kuliko sisi raia wa kawaida" Kayoza alimwambia mama yake,

"Wana akili kama sisi tu, mwenye akili kuliko sisi ni Mungu peke yake" Mama Kayoza aliongea kwa ukali kidogo,

"Sasa mimi sijamaanisha hivyo mama" Kayoza alijitetea,

"Mungu ni mkubwa kwa maana yoyote ile uliyoimaanisha" Mama kayoza alitilia mkazo maneno yake,

"Alafu nasikia kama mlango unagongwa vile"Omary aliongea baada ya ukimya wa muda,

"Hata mimi Nimesikia hivyo hivyo" Kayoza nae akamuunga mkono Omary

"Sasa si mkafungue, mbona mmelegea hivyo nyie?" Mama Kayoza aliongea kwa ukali.

Omary akasimama na kuelekea mlango ulipo, akaminya kitasa chini na kuvuta mlango, ile kufungua tu akakutana uso kwa uso na Sajenti Minja, Omary akarudishia mlango haraka na kukimbilia ndani…………

Omary alivyofungua na kufunga mlango, kisha akarudisha

kichwa ndani, Sajenti Minja aliiona sura ya Omary na kupata mshtuko mkubwa sana, maana sura aliyoiona ndiyo ile ile inayotafutwa na serikali.

Sajenti minja bado alikuwa na uoga kutokana na lile tukio la kutaka kunyonywa damu,

kwa hiyo akabaki nje kaduwaa, huku anajiuliza

pale ndio kwa dada yake, au kakosea nyumba

kabla hajaamua chochote, akasikia mlango

unafunguliwa tena, kwa haraka sana Sajenti

Minja akatoa bastola yake, na kuilekezea mlangoni.

"vipi tena kaka, unataka kuniua mwenzio" ilikua sauti ya Mama Kayoza baada ya kufungua

mlango.

"nimemuona kijana ndani ambae anatafutwa nchi

nzima" Sajenti Minja akaongea kwa pupa huku bado akiwa anashangaa hali anayokutana nayo,

"ndio, karibu basi kwanza ndani, alafu ndio ujue

kwanini yupo hapa" mama kayoza aliongea kwa

busara,

"Haiwezekani kuingia humo, ngoja niwasiliane na Polisi makao makuu Shinyanga wake wanipe msaada" Sajenti Minja aliongea huku akiitoa simu yake mfukoni,

"We Joel acha ujinga, unatapopiga simu na kuwaita polisi utakuwa umeniweka hatiani mimi na sio huyo kijana uliyemuona" Mama Kayoza aliongea na kumfanya Sajenti Minja asitishe zoezi lake,

"Mbona sikuelewi Dada, unamaanisha nini kusema hivyo?" Sajenti Minja alimuuliza dada yake huku akimshangaa,

"Twende ndani utanielewa tu" Mama Kayoza alimwambia Sajenti Minja,

"Lakini dada ujue una hatari sana kuishi na Huyo kijana" Sajenti Minja aliongea kwa unyonge,

"Twende ndani bwana" Mama Kayoza aliongea huku akiingia ndani na Sajenti Minja akaingia ndani huku akiongozwa na

mama Kayoza, ila bastola yake, hakutaka kuificha tena, alivyoonekana, alikuwa amejiandaa

kwa lolote litakalotokea

Alipoingia sebuleni hakukuta mtu,

"kaenda wapi?" Sajenti Minja akauliza kwa mshangao na wasiwasi,

"baba vipi?!, mbona una haraka hivyo" mama

kayoza aliongea huku akiwa anaelekea sehemu kulipokuwa na vyumba ambavyo wakina Kayoza walikimbilia kujificha. Alipofika katika mlango wa chumba cha wakina Kayoza, aligonga na mlango ukafunguliwa,

"Haya twendeni mkamsalimie mjomba wenu" Mama Kayoza aliwaambia,

"Mama mbona unataka kutupeleka matatizoni?" Kayoza aliongea huku akiwa ana hofu kuu,

"Ebu twendeni uko, yule hana tatizo" Mama Kayoza aliongea na kuanza kutoka nje, nyuma yake alikuwepo Kayoza na Omary.

Walipotokea sebuleni Sajenti Minja akawaelekezea bastola na kuwafanya wakina Kayoza kutaka kukimbia ila mama yao aliwahi kuwashika,

"Mnakimbia nini nyie? Na wewe jiheshimu basi, kwangu ni mahali pa amani, hayo mabastola yako use unayatolea huko huko na sio hapa" Mama Kayoza aliongea kwa ukali huku anamuangalia Sajenti Minja,

"ehe!, dada unaishi vipi na wauaji?" Sajenti Minja akamuuliza mama kayoza huku bado bastola yake ikiwa mkononi,

"Ebu lifiche hilo libunduki lako ndio uhoji hayo maswali yako" Mama Kayoza alimwambia Sajenti Minja na Sajenti Minja akatii kwa kuirudisha bastola sehemu yake,

"Dada mbona unawatetea sana, ni nani zako Hawa?" Sajenti Minja aliuliza huku akiwaangalia kwa chuki wakina Kayoza,

"hao ni wajomba zako, huyo hapo ndio kayoza, na

huyo mwingine ni rafiki yake" Kama kayoza

alimwambia sajenti Minja huku akiwaonyeshea

kidole wakina Kayoza.

"Kayoza? Kayoza mwanao au?" Sajenti Minja aliuliza huku akiwa ahamini kilichozungumzwa na dada yake,

"Haswaa, Kayoza mwanangu ndio huyo" Mama Kayoza alijibu kwa furaha,

"alah!, kayoza ndio kawa mkubwa hivi?" sajenti

Minja alijishtukia kauliza bila matarajio.

"kawa mbaba haswa" mama kayoza akajibu.

Sajenti Minja akairudisha bastola yake kiunoni,

kisha akamgeukia kayoza,

"hujambo mjomba?" Sajenti Minja akamsalimia kayoza.

"sijambo shikamoo" kayoza nae akamsalimia

mjomba yake huku nae akiwa ahamini kinachotokea ingawa ni kweli aliambiwa Sajenti Minja ni ndugu yake,

"marhaba, za siku?" Sajenti Minja akaendelea kumjulia hali Kayoza tena kwa uchangamfu kama hawakuwa maadui muda mfupi uliopita,

"nzuri tu" kayoza akajibu.

"unanikumbuka mimi?" Sajenti Minja akamuuliza kayoza,

"sikukumbuki" kayoza alimjibu huku akitingisha kichwa kwa kukipeleka kushoto na kulia,

"kalikuwa kadogo sana" Sajenti Minja alisema huku akimgeukia dada yake.

"tena sana, kalikuwa na miaka sita, kipindi tulipoenda kumuona mimi na wewe kule kigoma" Mama kayoza akamjibu.

"ehe, kakuelezea sababu ya kufanya mauaji ya kutisha namna ile" Sajenti Minja akamuuliza dada

yake,

"yeye mwenyewe alikuwa hajui, hadi mimi nimemwambia ndio akajua" Mama Kayoza ndivyo

alivyomjibu sajenti Minja. Sajenti akaonekana kushtuka kutokana na lile jibu kutoka kwa dada yake,

"kwa hiyo wewe unajua

sababu?" Sajenti Minja akamuuliza Mama Kayoza.

mama kayoza akamuelezea mwanzo mpaka

mwisho wa tatizo analokumbana nalo Kayoza.

"Sasa utachugua mwenyewe umpeleke kwenye vyombo vya sheria au umlinde" Mama Kayoza alimaliza kwa maneno hayo na kumfanya Sajenti Minja ainamishe kichwa chini akitafakari,

"Kwa hivyo unataka kuniambia kwamba huyu Kayoza hawezi kuwa mtu bila sababu mpaka huyo mtu mwenyewe stake kumdhuru?" Sajenti Minja aliuliza baada ya muda kidogo wa kutafakari,

"Ndio hivyo na pia kama huyo mtu atataka avunje masharti ya mzimu" Mama Kayoza alijibu,

"Kumbe nilikuwa nataka kumdhuru mtu asie na hatia, tens ndugu yangu" Sajenti Minja aliongea kwa masikitiko,

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)