KIJIJINI KWA BIBI (17)

0
Mwandishi: Alex Kileo

SEHEMU YA KUMI NA SABA
TULIPOISHIA...
"Ndio hivyo na pia kama huyo mtu atataka avunje masharti ya mzimu" Mama Kayoza alijibu,

"Kumbe nilikuwa nataka kumdhuru mtu asie na hatia, tens ndugu yangu" Sajenti Minja aliongea kwa masikitiko,

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
"Na hayo majeraha usoni kwako ni ya nini?" Mama Kayoza alimuuliza Sajenti Minja,

"Hii ni adhabu ndugu yangu" Sajenti Minja alijibu,

"Adhabu?, adhabu gani kama umepata ajali?" Mama Kayoza aliuliza,

"Ndio adhabu zetu za kijeshi" Sajenti Minja alijibu,

"Na ulifanya kosa gani mpaka upewe hivyo adhabu?" Mama Kayoza aliuliza kisha Sajenti Minja akaeleza mwanzo mpaka mwisho.

"Kwa hivyo hii kesi ndio imekutesa hivyo" Mama Kayoza aliuliza,

"Yaani nnilikubali kuirudia kwa sababu nilitaka nipate mwanya wa kukimbia nje ya nchi kabisa" Sajenti Minja aliongea,

"Haya sasa, wewe kama mjomba kama baba, una maoni juu ya hili tatizo" Mama Kayoza alimuuliza Sajenti minja,

"Hapa hakuna njia zaidi ya mganga, kwa maana hili tatizo limekaa kihasili hasili sana" Sajenti Minja akashauri kuwa ni lazima Kayoza

apelekwe kwa wataalamu wa tiba za jadi,

"Haiwezekani, atapelekwa kuombewa atapona tu" Mama

Kayoza alipinga,

"Ujue mama kwenda kwa mganga sio kupinga nguvu ya Mungu, inawezekana huko ndipo Mungu atatusaidia" Kayoza alimshauri mama yake,

"Na pia tukienda kwa mganga sio mwisho wa kwenda kanisani, ikifika siku ya kwenda kanisani aende na ikifika siku ya kwenda kwenye tiba asili aende" Sajenti Minja aliongezea,

"Sawa, maana cha muhimu ni mtoto kupona" Mama Kayoza alikubaliana na kaka

yake na maongezi mengine yakaendelea huku Mama Kayoza akiandaa mezani chakula cha jioni.

Baada ya chakula cha pamoja, Sajenti Minja alimwambia kayoza kuwa kesho atakuja

kumchukua asubuhi, ampeleke kwa mzee mmoja

ambae ni mganga anaefahamika pale Shinyanga.

"Wewe si umekuja Leo tu, huyo mganga umemjulia wapi?" Mama Kayoza aliuliza kwa mshangao,

"Shinyanga nimekaa sana na naijua vizuri sana kuliko unavyodhani" Sajenti Minja alijibu huku akicheka na kumfanya Mama Kayoza aishie kuguna tu,

"Kwa hivyo umefikia wapi, au lodge?" Mama Kayoza alimuuliza Sajenti Minja,

"Kuna nyumba nimepewa na viongozi ambayo nitaishi kwa muda" Sajenti Minja alijibu,

"Mi nikajua utaishi hapa bwana na ndio maana Jana ulivyonipigia simu na kuniambia unakuja sikutaka kuwaambia hata wanangu kuwa unakuja" Mama Kayoza aliongea,

"Mimi naona niwaache, ila Kayoza jiandae kesho mapema nakuja kukuchukua ili nikupeleke kwa babu" Sajenti Minja aliongea huku akisimama,

"Mbona unaondoka mapema, hata hukai tuongee ongee" Mama Kayoza alimwambia Sajenti Minja,

"Ngoja niwahi kupumzika maana nnimechoka sana" Sajenti Minja aliongea na kisha akasindikizwa na Dada yake mpaka nje na kuondoka zake.

Kesho yake, sajenti Minja aliwai kufika pale kwa

dada yake na kunywa chai kabisa, kisha Kayoza

na Omari wakajitayarisha, saa nne iliwakuta wapo

katika foleni ya kuingia kwa mganga,

foleni ilikuwa ndefu.

Baada ya kusubiri sana, muda wao ulifika na waliingia kuonana na

mganga saa sita kasoro, mganga akawaambia

kuwa tatizo lao ni kubwa, na wakitaka liishe, ni

lazima wapeleke maiti ambae katoka mochwari.

Ilikuwa ngumu, ila kwa ajili ya shida, wakasema wataipeleka usiku, mganga akasema itakuwa

vizuri sana hiyo maiti ikifika usiku, ili kazi ianze usiku huo huo.

Walipotoka kwa mganga wakaelekea moja kwa

moja hospitalini, walipofika, Sajenti Minja

akashuka ndani ya gari, kisha akaenda moja kwa

moja hadi mochwari, akaongea na mzee mmoja hivi ambae ndiye alikuwa mlinzi wa kile chumba cha kutunza maiti na alimueleza

kuhusu shida yake ni kutaka kupatiwa maiti moja, mara ya kwanza, babu

anaetunza maiti alikuwa mgumu kukubali, ila

alipoambiwa anapewa laki laki tatu, akakubali

haraka, na akampa mbinu ambayo sajenti Minja

atatumia kuchukulia maiti maiti usiku.

Wakampa babu pesa kiasi cha laki moja na wakakubaliana kuwa kiasi kilichobaki watammalizia usiku pindi watakapokabidhiwa maiti.

Kisha wakaenda zao nyumbani kusubiri muda ufike.

Usiku ulipofika, Sajenti Minja na wakina Kayoza

wakaenda nyuma ya chumba cha kuifadhia maiti,

ilikuwa saa tano usiku, hata watu waliokuwa

wanapita katika sehemu ya mochwari walikuwa

wanahesabika,

Yule babu mtunza maiti, akaingia ndani, akatoka

na maiti amembeba mabegani, kisha akafungua

geti la nyuma, akawakabidhi wakina Sajenti

Minja, kisha akapewa pesa yake iliyobakia na kuwaachia maiti yao.

Ile maiti waliiweka katika buti ya gari, kisha

wakaanza safari ya kwenda kwa mganga. Ulikuwa usiku tulivu na ukizingatia kulikuwa nje ya nje, basi kulikuwa na hali ya kutisha kidogo kutokana na mapori machache maeneo Yale.

Walipofika katika sehemu ambapo kulikuwa

kumetulia na kulikuwa na kapori kidogo, ni umbali

mdogo kutoka nyumbani kwav mganga aliyewaagiza maiti, walisimamishwa na gari

ya polisi wa doria waliokuwa wanaimarisha ulinzi kile kipindi cha usiku.

"mnaenda wapi?" askari mmoja akawauliza,

"nyumbani" Sajenti Minja akajibu huku wasiwasi mwingi ukiwa umemtawala,

"huku juzi tulipishana na watu nao tulipowauliza

wakasema hivyo hivyo, kesho yake tukasikia

majambazi yamepavamia na kuiba mali za watu, na nyie msije mkawa ni miongoni mwa hao waarifu" Askari yule akamwambia sajent Minja huku akiwa anawatilia mashaka,

"sisi hatuwezi kuwa majambazi, afande" Sajenti

Minja akajitetea,

"hatuwezi kuwaamini, hadi tuwakague" yule askari aliongea huku akimulika upande wa ndani wa gari kwa kutumia tochi,

"Sisi ni watu safi" Sajenti Minja aliongea huku ndani ya nafsi yake akiomba Askari wasikague buti ya gari,

"Na huku kuna mini?" Askari mwingine aliongea huku akifungua buti ya gari na kuwafanya wakina Sajenti Minja waishiwe nguvu….

…"ebu toa lock ya buti" Askari yule akamuamrisha Sajenti Minja baada ya kufungua buti bila mafanikio.

Sajenti Minja akaona akifanya uzembe kidogo,

anaweza kuvuliwa nguo bila kutegemea, kwa

maana kwa Sajenti kama yeye kukutwa na maiti

ndani ya gari ni aibu kubwa.

"unajua unaongea nani?" sajenti Minja akamuuliza yule askari wa doria kistaharabu,

"haijalishi, kukujua wewe nani nadhani hakutasitisha kukukagua. fungua buti bwana" yule askari akaongea kwa ukali.

"Ngoja nikuoneshe kitambulisho changu" Sajenti Minja akatoa kitambulisho chake, akamtupia yule

askari,

"alafu inaonekana una jeuri sana kijana?, unamtupia nani likitambulisho lako?" yule afande

akawa anaongea huku akiwa anamfuata Sajenti Minja akiwa na gadhabu, alipomfikia, yule askari

akamtandika sajenti Minja kibao cha nguvu.

"haya okota likitambulisho lako na unipe mikononi, sio unirushie, umeona mi limbwa

eeh!?", yule askari wa doria akahoji kwa ukali mpaka mate yakamtoka,

Sajenti Minja akaona asilete mabishano wakati wanachelewesha kazi kwa mganga, akakubali kuwa mjinga, akakiendea

kile kitambulisho, akakiokota kisha akampatia yule askari wa doria.

Yule askari akakipokea,

akashtuka baada ya kukiangalia kwa nje, maana kilikuwa cha kipolisi, alipokifungua kwa ndani, akakisoma ndani, kisha

akammulika Sajenti Minja na tochi usoni, ghafla

akampigia saluti, wale askari aliokuwa ameongozana

nao, kuona hivyo, nao wakampigia saluti Sajenti Minja.

"samahani sana mkuu, mi sikujua kabisa" yule

askari wa doria aliongea huku sura yake

ikionesha kama anataka kulia kutokana na hofu aliyokuwa nayo,

"usijali, ndio kazi inatakiwa kufanywa hivyo" Sajenti Minja ndivyo alivyomjibu, kisha

akamuuliza, "bado unataka nifungue buti?"

"ha…hapa…hapana mkuu" yule askari wa doria akajibu kwa sauti iliyojaa kitetemeshi.

"Kwa hivyo mnaweza kuturuhusu twende?" Sajenti Minja aliwauliza,

"Nenda tu mkuu, samahani sana kwa usumbufu" Askari alijibu huku akimrudishia Sajenti Minja kitambulisho chake.

Sajenti Minja akakipokea kitambulisho chake na wakaingia ndani ya gari, kisha wakaendelea na safari yao.

"wajomba pale bila kutumia akili tulikuwa tunaumbuka" Sajenti Minja alianzisha maongezi baada ya kuondoka eneo walilosimamishwa,

"Mimi ndio nilikuwa nimekata tamaa kabisa" Omari nae akachangia,

"Mimi akili niliyokuwa nayo ilikuwa ni kutoka nduki tu" Kayoza aliongea na kufanya wenzake wacheke,

"bila ya kitambulisho, sasa hivi sijui tungekuwa

wapi?" Sajenti Minja akasema huku akiwa anaipaki gari nje ya nyumba ya mganga.

Wakashuka, kisha wakaenda hadi mlangoni kwa

mganga, wakabisha hodi, wakafunguliwa na

msaidizi wa mganga,

"sisi tulijua hamuwezi kuja tena, maana giza limekuwa kubwa sana" Msaidizi wa Mganga

aliwaambia baada ya kuwagundua,

"tulipata matatizo kidogo njiani, ila yameisha" Sajenti Minja aliongea huku akiwa anaingia ndani na nyuma yake wakina Kayoza wakimfuata.

"Sasa itabidi ifanyike ingawa tumechelewa kidogo" Mganga aliongea baada ya kuwaona,

"Itakuwa vyema sana" Sajenti Minja aliongea,

"Sasa huyo kijana mwenye tatizo inabidi asogee hapa tumfanyie mambo kidogo" Mganga aliongea huku akitandika kitambaa cheusi chini. Kayoza akasogea na kuambiwa Amalie kile kitambaa cheusi na mganga akaanza kufanya matambiko.

Baada mganga kumaliza matambiko madogo pale

nyumbani, wale wasaidizi wa mganga, walikuwa

wanne, wawili wakambeba yule maiti na wawili

wengine wakabeba vifaa vya uganga, hapo

ilikuwa saa sita na dakika zake za kutosha,

mganga akawa anaongoza msafara.

"Hizi sehemu zinatisha ila mnabidi mzizoee" Mganga aliwaambia wakina Sajenti Minja wakati wakiwa njiani,

"Hizi sehemu za kutisha nimeshazizoea sana, labda vijana wangu hapa ndio wageni" Sajenti Minja alijibu,

"Kwa hivyo mambo haya ya kutembea kwa waganga ushayazoea sana?" Mganga alimuuliza Sajenti Minja,

"Hapana, kwa masuala ya kiganga mi ndio mara yangu ya kwanza" Sajenti Minja alijibu,

"Sasa hata mazingira ya kutisha umeyazoeaje?" Mganga aliuliza,

"Kutokana na kazi zetu mzee wangu" Sajenti Minja alijibu,

"Kwani nyie mnafanya kazi gani?" Mganga aliwauliza,

"Hao vijana wangu wanasoma chuo, mimi ni muangaikaji tu wa sehemu mbalimbali katika kutafuta ridhiki" Sajenti Minja alijibu,

"Sasa kama huyu kijana mwenye matatizo yupo Chuo huko chuo anaishi vipi na chuo mzimu" Mganga alihoji,

"Matatizo matatizo tu na ndio maana tumemleta hapa" Sajenti Minja alijibu na ukimya ukatawala tena njiani.

Walitembea mda wa saa nzima hadi sehemu za makaburini.

" inabidi tuchague kaburi moja ambalo limetengenezwa vizuri na liwe la mwanamke" Mganga alitoa maelekezo na wale wasaidizi wake wakatawanyika kila mmoja na upande wake wakitafuta hilo kaburi zuri alilozikwa mwanamke.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)