Mwandishi: Alex Kileo
SEHEMU YA KUMI NA NANE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
" inabidi tuchague kaburi moja ambalo limetengenezwa vizuri na liwe la mwanamke" Mganga alitoa maelekezo na wale wasaidizi wake wakatawanyika kila mmoja na upande wake wakitafuta hilo kaburi zuri alilozikwa mwanamke.
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
"Naona hili hapa linafaa" Msaidizi mmoja wa mganga alipaza sauti na watu wote wakaelekea eneo alilopo.
Walipofika katika kaburi moja lililosakafikiwa
vizuri, Mganga alilidhika nalo baada ya kuona kila anachokihitaji kipo.
Mganga akawaamuru wasimame, kisha
akachukua kikapu cha uganga akatoa vifaa vyake
akavipanga kulizunguka lile kaburi,
"Were kijana njoo ulale hapa juu ya hili kaburi" Mganga alimwambia kayoza,
"Mi naogopa mzee" Kayoza aliongea huku akiwa na wasiwasi,
"We mpumbavu mini, ebu lala hapo kabla sijakuchapa makofi, we unafikiri utaponaje kama ukikahidi maneno ya mganga" Sajenti Minja aliongea kwa ukali, Kayoza akakubali kulala hivyo hivyo huku aakitetemeka.
Baada ya Kayoza kulala juu ya kaburi, mganga akammwagia madawa yake Kayoza kichwani, haikuchukua
hata dakika moja, Kayoza akapoteza fahamu na kulala kama maiti,
"Haya mchukueni huyo maiti na mumlaze pembeni ya huyo kijana" Mganga akawaamuru wasaidizi wake
wamchukue yule maiti na kumlaza pamoja na
kayoza, wasaidizi wakatekeleza agizo.
"Kazi ndiyo inaanza, sharti kubwa na la kuzingatia ni kwamba kazi itakapoanza haitatakiwa ionekane damu ya kitu chochote kile" Mganga aliongea,
"Hata ya mbu?" Sajenti Minja aliuliza kutokana na eneo like kuwa na mbu wengi,
"ndio, kama mbu atakung'ata hata usimuue, maana ukimuua ile damu yake inaweza kuwa tatizo kwetu" Mganga aliongea kwa msisitizo,
"Na ikionekana ni kipi kitachotokea?" Sajenti Minja aliuliza,
"Huu mzimu tunaoutoa hapa, nguvu zake zipo kwenye damu ya kila kiumbe, kwa hiyo damu itakapoonekana, mzimu atapata nguvu na kati yetu hapa hakuna atakayepona" Mganga alitoa Maelezo,
"Hilo litawezekana" Sajenti Minja alijibu,
"Na pia kama mtu ana kidonda ajitahidi akizibe kisionekane" Mganga alitilia mkazo,
"Basi kazi ifanyike tu, naona Maelezo yako yamejitosheleza" Sajenti Minja aliongea,
"Kwa hiyo hapa kazi inayofanyika ni kuutoa huu mzimu kutoka kwa kijana wenu na kuuingiza katika maiti alafu kazi itayofuata ni kuizika hivyo maiti pamoja na mzimu" Mganga alimaliza.
Mganga akaanza kazi yake, alimwaga madawa
eneo lote, kisha akaanza kuongea lugha
anayoijua yeye, alifanya kwa nusu saa, kisha
likatokea dubwana la ajabu kwenye mwili wa
Kayoza, kila mtu alipata uoga isipokuwa mganga tu.
Sasa like dubwana likawa kama linavutwa kutoka kutoka kwenye mwili wa Kayoza, ila likawa
halitaki,
hiyo hali ilienda kama saa nzima, mganga
akaanza kuona mafanikio, lile dubwana lilishatoa
mwili mzima ikawa bado miguu, na mwisho hadi miguu ilitoka na likaanza kudumbukia katika ile maiti.
Mara ghafla panya akatokea
kichakani, alikuwa kama anakimbizwa na kitu,
akawa anaelekea kwenye miguu ya Omary, katika
jitihada za kumkwepa, Omary akajikuta anamkanyaga yule Panya,
damu ikaenea katika viatu vya Omari, mganga
aliliona lile tukio,
akajikuta anasema kwa sauti iliyokata tamaa
"tumekwisha…".
Na wakati huo huo mzimu ukachomoka kutoka katika mwili wa maiti na huku ukifoka kwa hasira kiasi kwamba ndege na wadudu walioloala maeneo Yale ya makaburini waliamka na kukimbia hovyo…………..
"Hapa sijui kama tutapona" Mganga alitamka maneno hayo, huku akiwa
kama anajitayarisha na pambano jingine.
Mzimu ulipiga kelele zilizowatisha watu wore pale, kisha ulirudi
kwa kasi ndani ya mwili wa Kayoza, kisha Kayoza
akanyanyuka taratibu, alikuwa tayari
keshabadilika, alikuwa anaogepesha ukimtazama msoni, macho yalikuwa
meupe yasiyo na mboni na meno ya mbele pembeni yalikuwa marefu kama
ya mnyama simba.
Kayoza akawatazama wote, alafu akawa
anamfuata Omari, Omari kuona hivyo, mkojo
ukaanza kumtoka na hata kukimbia akawa anashindwa ila alibaki
ametoa macho huku machozi yakimtoka ingalikuwa halii.
Kayoza alipomfikia Omary
akamuangalia kisha akaachane nae, sasa akawa
anafuata mganga ambaye muda wote alikuwa bado anafanya mambo yake
ya kiganga kwa ajili ya kujaribu kuutuliza mzimu wa Kayoza.
Mganga baada ya kuona mzimu unamfuata, maamuzi aliyoyachukua ni
kutoka tu
mbio, akasababisha na watu walikuwepo katika
hilo eneo nao watoke mbio
mganga hakufika hata mbali, Kayoza akamkamata,
"Wewe ni nani mpaka utake kunitoa katika nyumba yangu?" Mzimu
ulimuuliza mganga huku ukiwa umemkaba katika shingo na kusababisha
kucha zake ndefu zipenye kwenye shingo ya mganga,
"Mi…mii..nimeagi..zwa tu na ndugu za…ko" Mganga aliongea kwa
tabu huku damu zikimchuruzika shingoni.
Ila pamoja na utetezi wake ule mzimu ulimbeba juu na kung'ata
shingoni kisha aakaanza kumnyonya damu, alipomaliza akamtupa
pembeni.
Kisha mzimu ukatoka mbio na kuwakuta wasaidizi wa mganga wakiwa
wanakimbia na wale
wasaidizi wake pia wakanyonywa damu.
Kisha Kayoza akamfuata sajenti Minja, ambae yeye alikimbia ila
mwisho akaamua asimame tu maana aliona hata kama akikimbia ni
lazima tu akamatwe.
Mzimu akamkamata mkono Sajenti Minja alafu akawa anamvutia
kichakani sehemu ambayo kulikuwa na miti mingi, alipofika katika
eneo lenye miti,
"Usipate kichwa kwa kuwa niliahidi kutoidhuru damu yenu, wewe ndiyo
utasababisha nivunje ahadi yangu" Mzimu uliongea huku
Ukikata fimbo, na kisha ukaanza kumtandika Sajenti Minja,
alimtandika
kisawa sawa, mpaka sajenti Minja akawa analia kama mtoto.
Mzimu uliporidhika na bakora alizozipata Sajenti Minja ukamuachia
na Sajenti Minja akatoka mbio kama mwendawazimu na kuishika ile
njia waliyokuja nayo ambayo ilikuwa inaelekea nyumbani kwa Mganga.
Mzimu ulipomuachia Kayoza, Kayoza akadondoka chini kama kifurushi
na akapoteza fahamu.
Omary yeye baada ya kuachwa na mzimu wala hakukimbia, alikuwa
anaangalia tu unyama unaofanywa na mzimu na hata wakati Kayoza
anaanguka na kupoteza fahamu Omary aliona na akaamini tayari mzimu
umemuachia rafiki yake, Maamuzi aliyoyachukua Omary ni kwenda kumpa
msaada Kayoza, alipofika, akambeba Kayoza kisha akawa kwenda
walipoacha gari lao ambapo ni nyumbani kwa Mganga.
Walifanikiwa kufika salama nyumbani kwa mganga na wakamkuta Sajenti
Minja anaangaika kufungua mlango wa gari ili aingie,
"Vipi huyo tayari au bado?" Sajenti Minja alimuuliza Omary baada ya
kumuona anakuja na Kayoza,
"Tayari amerudi katika hali yake" Omary alijibu huku akifungua
mlango wa gari na kumuingiza Kayoza,
"Aisee hii siwezi kuisahau" Sajenti Minja aliongea huku akiwasha
gari na kuiondoa kwa kasi.
"Hii ilikuwa hatari, ila wewe hajakudhuru" Omary aliongea huku
akijua fika Sajenti Minja alipewa bakora zisizo kuwa na idadi,
"Usiseme hivyo wewe, dah yaani nimefanywa mtoto Leo, tena mtoto wa
shule" Sajenti Minja aliongea kwa huzuni,
"Umefanywaje kwani mjomba?," Omary aliuliza huku akimcheka
kimoyomoyo,
"Hata kuhadithia siwezi, ni kitendo cha aibu sana" Sajenti Minja
aliongea,
"Si uniambie tu mjomba" Omary alikazania huku akiendelea kumcheka
moyoni,
"Nitakuambia tukifika bwana" Sajenti Minja alijibu huku akiongeza
mwendo wa gari.
Katika hospitali ya mkoa kulikuwa na kasheshe
kubwa sana, kuna watu waliambiwa ndugu yao
amefariki, ila walipoenda monchwari hawakuikuta
maiti ya ndugu yao, walipowafata madaktari
wakawathibitishia kuhusu kifo cha ndugu yao, na
hata babu wa monchwari alithibisha kupokea maiti
ya huyo ndugu yao, sasa cha ajabu maiti ikawa
haionekani
Polisi walipofika pale hospitali, wakamchukua
babu wa mochwari huku wakiwa na uhakika kuwa
huyu mzee anahusika kwa namna moja au nyingine
katika upotevu wa ile maiti.
Babu akachukuliwa hadi kituoni, walipomfikisha
wakaanza kumuhoji,
"Mzee kuwa mkweli, tuambie huo mwili umeupeleka wapi?" Askari
alimuuliza Babu wa monchwari,
"Yaani hata mimi sielewi, ule mwili kweli niliupokea ila hata
ulivyopotea mimi sijui" Babu alijibu kwa kujiamini,
"Kwani walinzi mpo wangapi pale monchwari" Askari aliuliza,
"Tupo wawili" Babu alijibu,
"Umesema wewe ndiye uliupokea mwili, he wakati mwili unapotea
ilikuwa zamu ya nani kulinda?" Askari akaendelea kuuliza,
"Yaani huo mwili niliupokea Jana saa mbili usiku, na imeonekana
haupo Leo saa kumi na mbili alfajiri" Babu alijibu,
"Ilikuwa zamu ya nani?" Askari aliuliza,
"Zamu yangu" Babu alijibu,
"Babu acha kutuchanganya, inaonesha wewe unajua kila kitu kuhusu
kupotea kwa huo mwili" Askari aliongea huku akitabasamu ili
asimtishe Babu,
"Unadhani nakutania mjukuu wangu?, kweli mimi sijui kitu,
inawezekana mile chumba cha monchwari kina wachawi, si unajua
wachawi wanazipenda sana maiti" Babu alijitetea na kumfanya askari
acheke,
"Babu sema kweli usiogope, hata kama umeusika hatuwezi kukufunga,
maana utakuwa kama shahidi, na si unajua shaidi hafungwi?" Askari
alimlainisha Babu huku akiendelea kucheka,
"Kweli hamuwezi kunifunga?" Babu aliuliza huku akimuangalia Askari,
"Kama utamtaja muhusika hautofungwa mzee, ila ukishikiria msimamo
wako wa kuficha ndio utakaokuingiza matatizoni" Askari alimwambia
babu wa monchwari,
"Kusema ukweli aliyeuchukua ule mwili namjua kwa sura ila jina
simjui" Babu aliamua kusema ukweli,
"Anakaa Wapi?" Askari aliuliza,
"Sijui ila nikimuona tu sura yake namjua hata kama nikitoka kulala"
Babu aliendelea kukazania maneno yake,
"Kulikuwa na makubaliano yoyote kati yenu mpaka auchukue huo
mwili?" Askari aliuliza,
"Hapana aisee" Babu alikataa,
"Sasa alichukuaje na wakati wewe mlinzi ulikuwepo?" Askari
aliendelea kumbana kwa maswali,
"Alikuja na bunduki akanitishia, kisha akaingia ndani na kubeba
maiti" Babu wa monchwari aliamua kusema uongo,
"Sasa kwa nini tokea mwanzo hukusema hivyo?" Askari aliuliza huku
akimuangalia usoni,
"Nilikuwa siamini kama mtaniamini" Babu alijibu,
"Sawa babu, itabidi urudi ndani" Askari aliongea huku akisimama,
"Ndani tens kufanya mini?" Babu aliuliza kwa kuamaki,
"Utatoka tu babu, ila kwa sasa mtuhumiwa bado unahesabika ni wewe
mpaka apatikane huyo mwingine unaedai alikuvamia na bunduki" Askari
aliongea na kubonyeza kitufe kilichopo mlangoni na mlango
ukafunguka wakaingia Askari wengine wawili,
"Mpelekeni selo" Askari aliwaamrisha wenzake ambayo walimshika babu
huku na huku na kutoka nae nje.
wanamtoa katika chumba cha mahojiano, ili
wampeleke rumande.
Mida ya saa tano asubuhi, ndio sajenti Minja
alikurupuka, akaangalia simu yake, akukuta
missed call 12 za mkubwa wake wa polisi,
akawaamsha wakina Kayoza, kisha wakaenda
kujiswafi, wakatengeneza chai wakanywa.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi