KIJIJINI KWA BIBI (23)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mwandishi: Alex Kileo
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
"hii kesi ya huyu mzee mbona mnaiendesha pole pole sana". Mkuu wa
polisi aliwauliza wale askari.
"ushaidi ndio unatuchelesha mkuu" Askari mmoja alijibu
"niambieni katika uchunguzi wenu mmefikia wapi" Mkuu wa Polisi
akawatupia swali jingine,
"hakuna mwanga wowote tuliopata" yule askari akamjibu tena mkuu wa polisi.
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
"nyie wazembe kweli, ile maiti iliyoibiwa si iliokotwa pamoja na
zile maiti zilizonyonywa damu?" Mkuu wa polisi akauliza kwa jazba,
"ndio mkuu" wale askari wakajibu kwa pamoja,
"mlienda kumuhoji yule mtu aliekutwa hai?" Mkuu wa Polisi akawapa
swali jingine.
"hapana mkuu" akajibu yule Askari ambae siku zote uso wake
utawaliwa na hasira.
"kwanini" mkuu wa polisi akaendelea kuwabana na maswali.
"yule anahusika na kesi ya sajenti Minja" yule askari akajitetea
kipumbavu.,
"ok, sasa hii kesi ya huyu babu nampa sajenti Minja kwa sababu
mmesema zinaingiliana, basi atazishughulikia zote" Mkuu wa polisi
alimaliza kisha akawaamuru watoke ofisini kwake, wamuache babu wa
monchwari peke yake, wakamtii kisha wale askari wakaondoka.
Kisha mkuu wa polisi akachukua simu yake ya mkononi alafu akapiga,
"hallow Minja uko wapi?"mkuu wa polisi aliuliza. Baada ya kujibiwa
akaendelea,
"Nipo ofisini kwangu" Sajenti Minja alijibu huku akishangaa ile
simu ya ghafla kutoka kwa mkubwa wake,
"ok, njoo ofisini kwangu" Mkuu wa Polisi aliongea kisha akakata
simu.
"nakukabidhi kwa mtu anaejua kazi" Mkuu wa polis alimwambia babu wa
mochwari,
"Nashukuru sana kwa kunijali mwanangu" Babu wa monchwari aliongea
huku akiangalia chini.
"Sio nakujali, huo ndio utaratibu wa kazi" Mkuu wa Polisi aliongea.
Sajenti Minja baada ya simu aliyopigiwa na mkuu wake kukatwa,
akatoka ofisini kwake huku akiwa na maswali kibao juu ya kuitwa
kwake na Mkuu wa Kituo.
Akawa anaelekea ofisi ya mkuu wa polìsi, alipofika mlangoni
akagonga hodi,
"yes, come in" sauti ya mkuu wake kutoka ndani ilimjibu,
Sajent Minja akashika kitasa cha mlango akanyonga kwa nia ya
kufungua mlango…..
…sajenti Minja akanyonga kitasa, haikuonekana dalili ya mlango
kufunguka, mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani, mara akasikia mlango
unafunguliwa, akatoka mkuu wa polisi,
"minja nisubiri ndani mara moja, naenda msalani dakika moja", mkuu
wa polisi alipofungua mlango aliongea maneno hayo huku akiwa
anatembea kumuacha sajenti Minja, mlango ulikuwa bado uko wazi,
Sajenti Minja akanyanyua mguu wa kulia ili kuingia ndani,
"jesus christ" alijikuta anasema kwa sauti ya chini baada ya
kugundua kuwa aliekuwa ndani ni babu wa mochwari, ila bahati nzuri
ni kwamba yule babu alikuwa ameinamia chini, kwa hiyo hakuweza
kumgundua Sajenti Minja.
Sajenti Minja alirudi nje kwa kasi, kisha akaurudishia mlango huku
anahema kwa fujo kama katoka kukimbia mbio ndefu,
"vipi Minja, mbona unaonekana hauko kawaida", sauti ya mkuu wa
polisi ilimshtua Sajenti Minja,
"nimepigiwa simu, nyumbani kuna matatizo" Sajenti Minja alitumia
uongo,
"ila kulikuwa na kazi nataka kukupa, tuingie ndani kuna kesi nataka
kukupa, alafu utaendelea na ratiba zako", Mkuu wa Polisi alimwambia
Sajenti Minja,
"samahani mkuu, niko chini ya miguu yako, naomba hiyo kesi unipe
baadae, uko nyumbani sio kwema kabisa", Sajenti Minja aliongea uku
akiwa ameweka sura ya huzuni,
"mmmh, ok, sawa, ukimaliza ya nyumbani, unijulishe, maana nataka
nikupe kesi ya mzee mmoja hivi", Mkuu wa polisi alimkubalia,
"Nikimaliza nitakujulisha na asante mkuu kwa kunikubalia niende
nyumbani, nikirudi nitakufahamisha" , Sajenti Minja alijibu huku
akiwa anaanza kuondoka,
"Minja" Mkuu wa Polisi aliita tena wakati Sajenti Minja anaanza
kuondoka,
"naam mkuu" Sajenti Minja aliitikia baada ya kuitwa,
"unaondoka tu, ila hujaniambia nyumbani kuna tatizo gani", Mkuu wa
Polisi alihoji,
"kuna kajomba kangu, ambacho ni katoto ka dada yangu ambae
nilikuambia anaishi hapa, nimeambiwa amegongwa na gari na hali yake
sio nzuri", Sajenti Minja aliendelea kutunga uongo mbele ya bosi
wake,
"ooh, poleni sana, haya bwana wahi,"Mkuu wa Polisi alimruhusu
sajenti Minja kwa mtindo huo.
Sajenti Minja aliondoka kwa mwendo wa haraka haraka mpaka gari yake
ilipokuwepo,
"mhm, nimesevu so hadi raha, leo nilikua nahaibika mbele ya bosi",
Sajenti Minja aliongea wakati anajipakia kwenye gari yake.
"duh, mama ujue mi nashindwa kuelewa, naona kama ndio mmeniacha
niendelee kuwa katika hali hii", Kayoza alimwambia mama yake wakiwa
wanapata chakula cha mchana,
"ebu, acha uwendawazimu uko, mzazi gani anaependa mwanae awe katika
matatizo?, we msubiri mjomba ako arudi labda atakuwa na mpya", Mama
kayoza alimjibu mwanae huku akiwa anasafisha mikono yake kwa maji,
"lakini mama", Kayoza kabla hajamaliza kuongea, ilisikika sauti ya
mtu ikigonga mlango,
"sukuma, mlango uko wazi", Mama Kayoza aliongea kwa sauti ya juu
kidogo, ili mgongaji amsikie,
"hodi mpaka ndani, eeh, nina mguu mzuri kweli, yaani nimefika
wakati wa mahakuli", Sajenti Minja aliongea huku akiurudishia
mlango
,"karibu anko, ingawa ndo kinaisha", Omari alimwambia sajenti
Minja, kisha wote wakacheka,
"ebu tuachane na hayo, leo kidogo nipate aibu ya mwaka mbele ya
bosi wangu", Sajenti Minja alibadilisha stori,
"ehe, nini tena?", Mama Kayoza aliuliza kwa shauku.Sajenti Minja
aliwaeleza mwanzo mpaka mwisho,
"kwa hiyo inavyoonekana anataka na kesi ya yule babu wa mochwari
iwe chini yako?" Mama Kayoza aliuliza,
"ndio hivyo" Sajenti Minja alijibu kinyonge,
"sasa utafanyaje" Mama Kayoza aliuliza,
"nitamkimbia kimbia hivyo hivyo mpaka achoke", Sajenti Minja
alialiongea,
"Mimi naona bora uichukue na hiyo kesi hili uweze kuwadhibiti
vizuri wahusika" Omary alichangia
"Hapana, mimi nitajitahidi niikwepe tu" Sajenti Minja aliongea,
"Ichukue hiyo kesi kwa maana huwezi jua mipango ya Mungu" Mama
Kayoza aliongea,
"Tutajua uko mbele ya safari. jamani kuna kaugali kalichobaki?"
Sajenti Minja aliuliza,
"ugali upo, ila mboga ndo imeisha, ngoja wajomba zako wakakununulie
maziwa kwa mchungaji", Mama kayoza alimjibu Sajenti Minja huku
akimpa kayoza hela ya maziwa,
"Kwani hatuwezi kununua mboga nyingine zaidi ya maziwa" Sajenti
Minja aliuliza,
"Mbona tunaweza kununua hata maharage au nyama, tatizo tukiinjika
mpaka viive si utakuwa umeshakufa na njaa yako?" Mama Kayoza
aliongea,
"Kweli Dada, basi nyie wahini, maana njaa niliyonayo ni ya
hatari…
baada ya wakina kayoza kutoka, Sajenti Minja na dada yake
waliendelea na maongezi yao.
"afadhali umekuja mwenzangu, maana mjomba ako kanichachamalia
hapa", Mama Kayoza alimwambia Sajenti Minja
"kachachamaa na nini tena?"Sajenti Minja akauliza,
"eti anadai tuko kimya katika kufuatilia matatizo yake", Mama
Kayoza akajibu,
"kuna askari niliongea nae jana, akaniambia kuna mtaalam wa jadi
ana uwezo mkubwa wa kusaidia watu", Sajenti Minja alimwambia dada
yake
,"kwa hiyo ulimwambia una ndugu yako ananyonya damu?", mama Kayoza
aliuliza kwa mshtuko,
"kwani mi sina hakili mpaka nimwambie hivyo?, nilimdanganya
natokewa na mauzauza kila nikitaka kulala", Sajenti Minja akamjibu
dada yake,
"ataweza kweli kumtibia kayoza?", Mama kayoza akamtupia mdogo wake
swali jingine,
"dada nawe kwa maswali!, tutajua uko uko kama ataweza au lah",
Sajenti Minja alimjibu dada yake,
"lini mtaenda uko", mama Kayoza akauliza tena
"nafikiri kesho, kama nitapata nafasi", Sajenti Minja alijibu
"haya bwana, wacha nikakutayarishie chakula jikoni", mama kayoza
aliongea huku akinyanyuka kwenye kochi,
"hayo ndo mambo sasa, kama kuna pilipili niwekee", Sajenti Minja
alisema na kumfanya mama kayoza ahangue kicheko.
"Sasa hiyo pilipili utaiweka katika maziwa?" Mama Kayoza aliuliza
huku akicheka,
"Nitaitafunia tu na ugali" Sajenti Minja alijibu,
"Ngoja nikutafutie kama ntaipata" Mama Kayoza aliongea huku
akiingia jikoni.
"Sema siku hizi umekuwa mswahili kweli Dada yangu" Sajenti Minja
aliongea huku akitabasamu,
"Kwanini unasema hivyo?" Mama Kayoza aliuliza huku akisimama,
"Naona nawe unakubali tu tumpeleke mwanao kwa waganga sio kama
zamani ulivyoshikilia msimamo wako wa kanisani" Sajenti Minja
alimwambia Dada yake,
"Ujue Mungu hana njia moja ya kukupa mafanikio, unatakiwa upitie
njia nyingi lakini ukimuamini yeye tu na sio vitu vingine" Mama
Kayoza alimwambia Sajenti Minja,
"Sawa mama mchungaji, inabidi na wewe ujenge kanisa lako sasa"
Sajenti Minja alimwambia Mama Kayoza,
"Ebu kwenda zako uko, kwanza ulivyosema mchungaji umenikumbusha awa
wendawazimu waliofuata maziwa, mbona wamechelewa hivyo?" Mama
Kayoza aliuliza,
"Wana mambo mengi wale vijana, usikute wanamnyatia yule binti wa
mchungaji" Sajenti Minja aliongea kwa utani huku akicheka,
"Acha uwendawazimu wako, watoto wa mchungaji wana maadili wewe"
Mama Kayoza aliongea,
"Sio wote, kama yule binti mcharuko niliekutana nae juzi ni bure
kabisa, bora angeishi uswahilini tu" Sajenti Minja aliongea huku
akicheka,
"Kwani ana kosa gani? Si alikuwa anaenda polisi kusema habari za
ukweli" Mama Kayoza aliongea huku akitabasamu,
"We si ni mlokole? Nenda na wewe polisi kaseme hizo hizo habari
kuwa mwanao muuaji" Sajenti Minja alimwambia Mama Kayoza,
"Mtoto anauma bwana, mtoto mwenyewe ndio huyo huyo mmoja kama roho"
Mama Kayoza aliongea huku akicheka,
"Nenda jikoni bwana, maana story zimezidi mpaka unasahau kuwa mimi
njaa inaniuma" Sajenti Minja alimwambia Dada yake,
"Hata baba, usije ukanifia bure kwa njaa" Mama Kayoza aliongea huku
akielekea jikoni.
Baada ya mkuu wa polisi kurudi ndani, alimpgia simu askari mwingine
na kumwambia amrudishe rumande Babu wa mochwari,
"jamani nitakaa huku mpaka lini, nina mke na watoto mimi",Babu wa
mochwari aliongea huku machozi yakimtoka,
"usijali mzee wangu, upepelezi utakamilika hivi karibuni", Mkuu wa
polisi alimjibu Babu wa mochwari kwa huruma.
"Mwanzo askari wako waliniambia nikiri kosa ili niachiwe, nikakiri
kosa kuwa ni kweli mwili umeibwa, lakini hawajaniachia, naambulia
kipigo tu mpaka viungo vinateguka" Babu wa monchwari alilalamika,
"Mzee ujue upelelezi sio kitu cha kukurupuka tu, inahitajika muda
mrefu wa kuchunguza na kujiridhisha na jibu la kile
kilichopelelezwa, na hapo sasa ndipo sisi tutaachana na wewe na
kesi yako itakuwa mahakamani" Mkuu wa polisi alimuelewesha Babu wa
monchwari,
"Mahakamani tena?, si nitafungwa jamani mie?" Babu wa monchwari
aliuliza huku akilalamika,
"Sasa sisi hatutaki ufungwe, na ndio maana tunaendelea kukuhifadhi
ili utusaidie kumpata huyo aliyeichukua hiyo maiti" Polisi
alimwambia Babu wa monchwari,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Maoni 2
Chapisha Maoni
-
Bila jina3 Julai 2024, 16:40ProfileBila jinaSaid: Simulizi zako kali sana asante kwa kutuburudishaView profileSimulizi zako kali sana asante kwa kutuburudishaReplyReply