NIFANYE NAMIMI KAKA (6)

0
Mwandishi: Juma Hiza

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
Nilifahamu pindi atakapomwambia mume wake hakuna baya lolote ambalo lingeweza kutokea. Aliipokea simu na kuanza kuzungumza na mume wake ambaye mawazo yake pamoja na akili zake zilionekana kugoma kufikiria mbali na hiyo ndiyo sababu niliyokuwa naitumia katika kumpiga huku namchekea mithili ya panya anavyokula na kupuliza.
SASA ENDELEA...
Nilianza kumsikiliza Precious jinsi alivyokuwa anamjibu mume wake, alionekana kuwa muoga sana lakini aliweza kufanya kama vile nilivyomwambia na hatimaye mume wake aliweza kumuelewa. Alikata simu baada ya kumaliza kuzungumza na mume wake.
“Dick,” aliniita.
“Niambie.”
“Kwanini umeniambia nimjibu hivyo?”
“Nina maana yangu.”
“Maana gani?”
“Kwanza embu niambie amesemaje?”
“Hajasema kitu ila ana hamu ya kutaka kujua ni nini kinachoniliza.”
“Hahahaha.”
“Unacheka nini?”
“Sasa utaenda kumwambia nini?”
“Kumwambia nini?”
“Hicho kinachokuliza.”
“DiCk embu niambie basi.”
“Wakati mwingine inabidi utumie akili ya ziada katika kubadilisha uhalisia wa kitu. Mwanzo mumeo alikuwa na shahuku ya kutaka kujua ni wapi ulipo na kwanini hukurudi nyumbani lakini sasa yote ameyasahau na hivyo anataka kujua ni kwanini unalia,” nilisema kisha nikacheka kidogo halafu nikaendelea.
“Unajua sisi wanaume ni viumbe waajabu sana,” nilimwambia.
“Kwanini?”
“Tunaonekana kuwa na nguvu nyingi, akili na uwezo mkubwa lakini linapokuja suala la wanawake lazima vitu vyote hivyo viwe chini, vinakuwa havina nafasi tena.”
“Ni kweli hata mimi naamini.”
“Mumeo anakupenda sana?” nilimuuliza swali la kizushi huku nikimtazama usoni, alionekana kuwa na aibu, akacheka bila kutarajia.
“Kwanini umeniuliza hivyo?”
“Lakini hujajibu swali?”
“Ndiyo naweza kusema ananipenda.”
“Unaweza kuulezea upendo wake?”
“Kiukweli nilikuwa nikimpenda sana mume wangu hata yeye pia alikuwa ananipenda, niliamuakuingia kwenye ndoa nikiamini kuna vitu ambavyo naweza kuvipata, ni kweli nimevipata vyote lakini kuna jambo moja nahisi halitimizi ipasavyo.”
“Jambo gani hilo.”
“Haniridhishi, mume wangu amekuwa mvivu sana tunapokuwa kwenye tendo amekuwa mwepesi wa kuchoka muda mwingine ananiacha nabaki naumia tu usiku kucha.”
“Duh!”
“Huo ndiyo ukweli?”
“Sasa unasemaje?”
“Kiukweli Dick nimetokea kukupenda na sijui kwanini imekuwa mapema kiasi hiki kwani tayari unanifahamu kila kitu.”
“Na mumeo je?”
“Kuhusu mume wangu usijali mimi ninachotaka ni wewe unipe mapenzi ambayo kwa muda mrefu nimekuwa nikiyatafuta nayakosa.”
“Usijali mrembo,” nilimwambia kisha sikutaka kupoteza muda, nilichoamua kukifanya ni kufanya mapenzi na yeye tena.

Kilichokuwa kikiendelea mule ndani ni sauti za vilio pamoja na miguno ya kimapenzi aliyokuwa akiitoa Precious. Nilihakikisha namkuna ipasavyo kila kona na kila sehemu ambayo nilikuwa namgusa alizidi kulegea na kupiga kelele. Mapenzi yangu yalimnogea sana.

Tulipomaliza tulienda kuoga na baada ya kuoga tulijiandaa na sasa tukatoka kuliekea gari. Nilikuwa nimechoka sana kwa wakati huo, njaa ilikuwa imenitawala kila hatua niliyokuwa naipiga niliipiga huku nikilishikilia tumbo. Kimoyomoyo nilikuwa nikilalamika njaa.
“Una nini?” aliniuliza Precious.
“Tumbo.”
“Limefanyaje?”
“Linaniuma.”
“Limekuanza saa ngapi?”
“Muda huu huu.”
“Nikakununulie dawa?”
“Hilo tumbo si la kutumia dawa bhana nisikufiche nahisi njaa ya hatari.”
“Hahahaha! Haya twende tukanywe chai halafu mimi ndiyo niondoke zangu,” aliniambia mara baada ya kulifikia gari lake.
“Sawa kwahiyo tunaenda wapi.”
“Wewe panda utajulia huko huko.”
“Sawa,” nilimjibu kisha tukapanda kwenye gari na kuianza safari.

Safari yetu iliishia katika moja ya hoteli kubwa ya kifahari iliyokuwa maeneo ya Sinza kwa Remi, tuliingia kisha tukaweza kupata huduma ya chakula iliyotupeleka na baada ya hapo Precious aliweza kuondoka na kuniacha huku mkononi akiwa amenikabidhi kiasi kidogo cha pesa ambacho kingeweza kunisaidia kwa kuzogeza siku.

Nilipokuwa narejea magethoni akili yangu ilikuwa ikiwaza mambo mengi sana, nilikuwa nikijaribu kukumbuka vitu vingi sana na ni katika kumbukumbu hizo niliweza kumkumbuka Evadia msichana ambaye niliwahi kukutana naye Mlimani City. Nilikumbuka kuwa aliwahi kunipa ‘Business Card’ yake kwa lengo la kuwasiliana.

Sikutaka kuendelea kukumbuka tena kitu chochote, nilichokuwa nakitamani kwa wakati ule ni kuwahi kufika nyumbani na kuitafuta ‘Business Card’ yake kisha nianze kumchombeza kama ilivyokuwa kawaida yangu.

Nilitumia dakika chache kutoka Sinza mpaka Tandale kwa Tumbo nilipokuwa naishi, hata hivyo niliweza kuchukua usafiri wa bodaboda ambao uliweza kunifikisha kwa haraka zaidi.

Kichwani mwangu hakukuwa na kitu nilichokuwa nakifikiria zaidi ya Evadia msichana ambaye nilijikuta natokea kumkumbuka sana. Moyo wangu ulihisi kitu cha tofauti sana. 

Nilipoingia katika chumba changu kitu cha kwanza kabisa nilichokifanya ni kuanza kuitafuta suruali ambayo niliivaa siku ile ambayo niliweza kwenda nayo Mlimani City, niliamini kwa asilimia zote kuwa ‘business card’ ilikuwemo katika mfuko moja wapo. 

Nilianza kutafuta kwa utulivu na hatimaye niliweza kuipata, niliizamisha mikono yangu ndani ya mifuko yake, naam! Ilikuwa kama matarajio yangu, niliikuta ‘business card’. Niliichukua na kuanza kuisoma kwa umakini wa hali ya juu.

Evadia alikuwa akimiliki duka kubwa la nguo lililokuwa likijulikana kwa jina la ‘Eva Fashion Wear’ lilikuwa ni duka kubwa lililokuwepo Kinondoni. Sikutaka kujali jina la duka wala ule urembo uliyokuwepo katika ile ‘business card’ kitu nilichokuwa nakiangalia ni namba za simu. 

Sikutaka kupoteza muda haraka niliitoa simu yangu na kuanza kunakili namba za simu za Evadia, moyoni nilikuwa nashahuku ya kutaka kuwasiliana naye. Nilipohakikisha zimetimia namba kumi nilizisave kabisa, nakumbuka nilimsave kwa jina la ‘Eva’ ikiwa ni kifupi cha jina lake halisi.

Akili ilinituma nimpigie lakini nilisita, nilihisi kutojipanga kwa mazungumzo yetu. Nilichoamua kukifanya ni kuingia upande wa WhatsApp na kuanza kumuangalia kama alikuwa online, hakuwa online kwa wakati huo lakini nilipotazama muda aliyotoka hayakuwa yamepita masaa mawili tangu alipotoka.

Alikuwa ameweka picha ya kikatuni ambacho kilikuwa kikionekana kuwa na furaha lakini nilipoangalia upande wa ‘status’ yake alikuwa ameandika maneno ambayo kwa kweli yalinifanya nicheke mwenyewe kama mwendawazimu baada ya kuyasoma, alikuwa ameandika maneno yaliyosomeka “Utamu wa kaka Dick.” Kisha akayasindikiza kwa kuweka kimdoli kilichokuwa kina macho ya kopa.

Mpaka kufikia wakati huo nilijiona kuwa mshindi tayari yani kama ni mbuzi basi alikuwa amefia kwa muuza supu. Wakati nilipokuwa nikiendelea kumuangalia ghafla! Nilimuona akirudi online. Sikutaka kupoteza muda niliamua kumtumia ujumbe mfupi, nakumbuka sikuwa nimeweka picha yoyote kwenye ‘profile’ yangu hivyo ilikuwa ni ngumu sana kunifahamu.
“Mambo mrembo.”
“Nani mwenzangu.”
“Pokea kwanza salamu halafu ndiyo uniulize kuwa mimi nani?”
“Okey poa, nani wewe?”
“Vipi kwani kuna ubaya wowote hata usiponifahamu?”
“Unajua sikuelewi embu jitambulishe halafu sema shida yako.”
“Naitwa Majaliwa Majuni.”
“Majaliwa?”
“Ndiyo.”
“Wa wapi?”
“Nipo Dar.”
“Dar sehemu gani?”
“Mbagala ila kwa sasa niko hapa Mwenge.”
“Mbagala?”
“Ndiyo.”
“Nikusaidie nini?”
“Wewe ndiyo Evadia?”
“Yes ndiyo mimi nikusaidie nini?”
“Nimeona matangazo ya nguo zako mitandaoni sijui naweza kupata huduma na mimi?”
“Yeah! Unaweza kupata ni pesa zako tu.”
“Ok unapatikana sehemu gani?”
“Duka langu lipo Kinondoni wewe ukifika tu hapo nitafute nitakuja kukuchukua.”
“Nitashukuru dada yangu.”
“Poa.”

Huo ndiyo ulikuwa mwisho wa chatting zetu, nilikuwa nimechart naye lakini mpaka kufikia wakati ule hakuwa amenifahamu kabisa, alionekana kuwa na dharau kiasi fulani lakini sikutaka kujali sana, nilichokuwa nimepanga kwa wakati huo ni kwenda kukutana naye 

Hukohuko kwenye duka lake la nguo, niliamini pindi ambapo angeweza kuniona hakika asingeweza kuamini macho yake, nililifahamu hilo kutokana na umaarufu wangu wa kuandika machombezo mitandaoni, nilikuwa nikipendwa sana, kila mwanamke alikuwa akitamani kuniona hii ilisababishwa na kipaji changu. 

Machombezo yangu yalikuwa yakiwasisimua sana watu, nilikuwa nikipokea jumbe mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa hadithi waliyokuwa wakiyafatilia machombezo yangu, walikuwa wakinilalamikia kwa kuwaumiza kila siku na machombezo yangu.

Niliamua kwenda kuoga kisha nikajiandaa vyema tayari kwa safari ya kwenda kukutana na Evadia ambaye kwa wakati ule alikuwa akinifahamu kwa jina la Majaliwa Majuni, niliamua kumdanganya jina langu kwa makusudi kabisa kwani kama ningeweza kumtajia jina langu halisi nadhani hata leo hii ninapokusimulia chombezo hili kamwe lisingeweza kukuvutia kwani ungeshafahamu kila kitu ambacho kilikuwa kinakwenda kutokea. 

Nakumbuka yalikuwa ni majira ya saa tisa kasoro, nilitoka katika chumba changu na sasa ilikuwa ni safari ya kuelekea maeno ya Kinondoni lilipokuwa duka la Evadia msichana ambaye nilipanga kutoka naye kimapenzi. Nilikumbuka kumtumia ujumbe mfupi WhatsApp kumfahamisha kuwa nilikuwa naenda kwenye duka lake.
“Ndiyo nakuja Dada Eva.”
“Sawa haina shida ukifika utaniambia.”
“Haya,” nilimjibu kama mtu fulani ambaye nilikuwa mshamba, nilifahamu kuwa hata Evadia naye alinidharau kwani kila ujumbe ambao nilikuwa nikimtumia alionekana kuudharau na kunijibu kama mtu ambaye alikuwa akilazimishwa kujibu.

Kutoka Tandale mahali nilipokuwa nikiishi mpaka lilipokuwepo duka la Evadia maeneo ya Kinondoni hapakuwa na umbali mkubwa sana, niliweza kufika na kwa wakati huo nilikuwa nje ya duka moja kubwa lililoonekana kuwa na kila aina ya nguo za kisasa. Lilikuwa ni duka la nguo za kiume pamoja na za watoto.

Nilikuwa nikilitazama katika namna ya kutamani kila kitu, sikutaka kuingia ndani kwa wakati ule niliamua kumpigia simu, haikuchukua sekunde nyingi tangu simu yake ilipokuwa inaita kisha alipokea.
“Hallo,”alisema huku akionekana kuwa bize.
“Naam!.”
“Nani?”
“Umenisahau mara hii tena?”
“Ooh! Nani Majaliwa sijui?”
“Ndiyo.”
“Umefika?”
“Ndiyo.”
“Uko wapi?”
“Niko hapa nje.”
“Ingia basi ndani.”
“Hapana njoo tu kwa hapa nje.”
“Ok sawa nakuja basi.”
“Sawa,” nilijibu kisha nikakata simu, nilikuwa nikimsubiria Evadia ambaye aliniambia kuwa muda mfupi alikuwa akinifuata. 

Nilijitathmini ile suruali ya kadeti iliyokuwa imenikaa vyema huku juu nikiwa nimevalia T-Shert aina ya Manga pamoja na kikoti cha kizushi ambacho niliamua kukivaa kwa lengo la kumechisha na kofia aina ya pama niliyokuwa nimeivaa, ilikuwa na rangi ya kijivu. 

Nilionekana kuwa wa kisasa zaidi hasa ukizingatia mahali nilipokuwepo palikuwa ni pa kijanja pia, kila kona nilikuwa nimezungukwa na maduka ya nguo.

Wakati nilipokuwa nikiendelea kujitathmini mara simu yangu ikawa inaita, nilipoangalia nililiona jina la Eva likisomeka. Haraka niliyatupa macho yangu kwenye langu kuu la duka lake ili niweze kumuangalia. 

Nilimuona akiwa katika wakati wa kuweweseka hakujua ni wapi mtu huyo aliyekuwa akimpigia simu alipo. Nililifahamu hilo na hivyo sikutaka kuipokea, niliamua kuikata kwa makusudi kitendo ambacho kilimuudhu sana, nilimuona akitokwa na mfyonzo kisha akawa kama anayetaka kurudi ndani.

“Eva!” nilimuita lakini kutokana na ile kofia aina ya pama niliyokuwa nimeivaa hakuweza kuiona vizuri sura yangu kwa wakati ule. Alikuwa akinitazama tu bila kusema lolote kwa wakati ule.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)