Mwandishi: Alex Kileo
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
"we kijana unaitwa nani?",Mkuu wa polisi alimuuliza Omari, tena aliuliza kwa sauti ya ukali,
"remmy, naitwa Remmy", Omari akataja jina la uongo, alikuwa na wasiwasi ila alijitahidi kuficha hofu yake mbele ya Mkuu wa Polisi,
"Minja ni nani kwako?", Mkuu wa polisi akamuuliza tena Omari,
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
"ni mjomba wangu", Omari akajibu huku akikwepesha macho yake yasigongane na macho ya Mkuu wa polisi,
"Mjomba ako kivipi?" Mkuu wa polisi akamtupia swali lingine Omary,
"Mimi ni mtoto wa Dada ake" Omary akajibu,
"unamfahamu Omari Mkwiji?",Mkuu wa polisi akamtupia swali lingine tena, ila hili swali la kipindi hiki ndilo lililokuwa gumu kuzidi yote aliyoulizwa kabla, na hata jasho lilianza kumtoka,
"hapana", Omari akajibu, wakati huo wote, Kayoza moyo ulikuwa unamuenda mbio sana, mpaka jasho likawa linamtililika mgongoni kuelekea sehemu za makalio,
"mh!, kweli duniani wawili wawili", Mkuu wa polisi aliongea huku akimgeukia Daktari,
"vipi kamanda, umemfananisha na ndugu yako nini?",Daktari alimuhoji mkuu wa polisi,
"hapana, kafanana na mtu mmoja hatari sana"Mkuu wa polisi aliongea kitu ambacho kilimpelekea Omari atoe ushuzi kwa mbali kwa ajili ya uoga,
"kama ni mtu hatari, basi asingekuwepo eneo hili",Daktari aliongea kauli iliyompoteza kabisa mkuu wa polisi.
"Kweli kabisa, kama angekuwa mtu mbaya basi asingesogea eneo hili" Mkuu wa polisi aliamua kumuunga mkono Daktari.
"Na wewe ni nani yake Minja?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akimuangalia Kayoza,
"Na mimi ni mjomba wake pia, mtoto wa Dada yake" Kayoza alijibu huku akijitahidi kujiamini,
"Kwa hiyo nyinyi ni ndugu?" Mkuu wa polisi aliwauliza huku akiwaangalia kwa zamu,
"Ndio" Omary alijibu,
"Mnakaa na mama yenu?" Mkuu wa polisi aliwauliza,
"Ndio tunakaa nae" Kayoza alijibu,
"Basi baadae nitarudu hapa, naomba niwakute ili mnipeleke nyumbani kwenu nikapajue na pia nimjue mama yenu" Mkuu wa polisi aliongea,
"Sawa haina shida, tena itakuwa vizuri sana" Omary alijibu huku akijitahidi kutabasamu,
"Alafu inaonesha wewe ni muongeaji sana kuliko mwenzako" Mkuu wa polisi alimwambia Omary huku nae akitabasamu,
Baada ya maongezi ya hapa na pale pamoja na kutambulishana, Mkuu wa polisi aliagana na wakina Kayoza kwa ahadi ya kuwafuata baadae pale hospitali na wampeleke akapajue wanapoishi.
"pppfffuuuu", wakajikuta wanashusha pumzi nzito baada ya Mkuu wa polisi kuondoka,
"duh!, mwana mi makalio yameloana hapa", Kayoza ndiye alieanza kuongea,
"dah!,we acha tu, ebu twende tukatafute maji ya baridi nje, maana naisi moyo uko kasi sana",Omari aliongea huku akitanguliza mguu wa kulia mbele, hali iliohashiria waondoke.
Wakina Kayoza walirudi kwao muda huo huo, ila hawakutaka kumwambia mama yao kama wamekutana na mkuu wa polisi na kukubaliana nae kuwa jioni atakuja hapo nyumbani, walitaka kumfanyia kama kitu cha kushtukiza.
Kibaya ambacho hawakukijua ni kuwa kwa kufanya ujinga wao huo wa kutaka kumshtukiza mama yako, ni kitu ambacho kinaweza kuja kuwagharimu wao wenyewe.
"Haya nipeni habari za hospitali" Mama Kayoza aliongea huku akijibwaga katika kochi lilokuwepo hapo sebuleni,
"Hakuna mabadiliko yoyote mama, bado hali ya mjomba ipo vile vile" Kayoza alijibu kwa masikitiko,
"Jamani mfunge na kusali, mmuombee mjomba wenu, kwa ile hali aliyokuwa nayo ni hatari sana" Mama Kayoza aliongea kwa huzuni,
"Mke wake umempa taharifa?" Kayoza alimuuliza Mama yake,
"Hapana, ila nimeongea na baba na yeye amesema tusimwambie mke wa Minja kwanza, tuvute subira huku tukiangalia ni namna gani tumueleze" Mama Kayoza alijibu mwanae,
"Mimi naona hakuna haja ya kumficha, mwambieni tu ukweli ili kama likitokea la kutokea, asimlaumu mtu" Kayoza alimshauri mama yake,
"Hakuna anayemficha, ila tunatafuta wakati sahihi wa kumwambia hilo tatizo" Mama Kayoza alijibu,
"Na kama make wake anampigia simu na hampati hewani? Huoni na hiyo itampa wakati mgumu?" Kayoza aliendelea kuuliza,
"Kwanza unachotakiwa kujua ni kwamba Minja anapoondoka nyumbani kwake kikazi uwa habebi simu, hii simu anayotumia aliinunua kwa ajili ya hii kazi tu, alipanga akimaliza hii kazi na ile simu na laini yake anachoma moto" Mama Kayoza aliwaambia kitu wasichokijua,
"Sasa inawezekanaje muda wote huo asiwasiliane na mke wake?" Omary aliuliza huku akionekana kutokubaliana na Maelezo ya mama Kayoza,
"Kwani imewezekanaje wewe kutowasiliana na wazazi wako kipindi chote hiki?" Mama Kayoza alimtupia swali Omary,
"Sasa mama mimi si Nina matatizo, ni hatari sana nikiwasiliana na ndugu zangu, naweza kuwaingiza matatizoni pia" Omary alijibu, ila alijibu kinyonge,
"Ebu tuachane na hayo, pumzikeni ili jioni mrudi hospitali" Mama Kayoza aliongea huku akielekea chumbani kwake.
Jioni, Mkuu wa polisi aliwafuata wakina Kayoza pale hospitali, Kisha akawachukua, ili wampeleke wanapoishi.
Njia nzima walikuwa wanapiga stori za hapa na pale, walipofika katika eneo ambalo ajali ilitokea, Mkuu wa polisi akashtuka,
"mhm, wanakaa huku, yule Babu nae si alikuwa anakuja huku, mh, bado nina wasiwasi na huyu Remmy, ntaendelea kumchunguza taratibu", mkuu wa polisi aliongea kimoyo moyo.
Wakafika kwa wakina Kayoza.
"karibu nyumbani", Kayoza alimkaribisha mkuu wa polisi,
"asante mheshimiwa, kumbe mlikuwa karibu sana na eneo la ajali?", Mkuu wa polisi aliuliza kinafki,
"hata kile kishindo tulikisikia",Kayoza akamjibu.
Wakamkaribisha ndani, kisha wakamtambulisha kwa mama yao, mama Kayoza akafurahi sana kutembelewa na mtu mkubwa pale nyumbani kwake. Mama yao alipata faraja kutembelewa na mkuu wa polisi,
"Sasa mbona hamkunitaharifu kama ugeni?" Mama Kayoza aliwauliza wanae,
"Tulitaka kukufanyia shambulizi la kushtukiza" Kayoza alijibu huku aki tabasamu,
"Siku nyingine muwe mnasema bwana, ili tumuandalie mgeni chakula" Mama Kayoza alimwambia mwanae,
"Kweli lakini, mlitakiwa mseme bwana, sasa si mnaona mmenikosesha chakula?" Mkuu wa polisi aliongea kwa utani huku akicheka,
"Ila hakuna ubaya kaka yangu, ngoja nikuandalie" Mama Kayoza aliongea,
"Hapana usiangaike, nitakula siku nyingine" Mkuu wa polisi aliongea kwa ucheshi,
"Mama sisi yupo ndani" Kayoza aliongea huku akiinuka pamoja na Omary,
"Mlitakiwa mkae tuongee na mgeni" Mama Kayoza aliwaambia wanae,
"Nyie ongeeni tu, sisi tunarudi muda si mrefu" Kayoza alijibu huku wakielekea ndani na Omary na kuwaacha Mkuu wa Polisi na Mama yao wakiongea.
Wakaongea sana kuhusu Sajenti Minja, undugu wa Mama kayoza na Sajenti Minja.
Mwishowe, Mkuu wa Polisi aliamua kuaga, ila Omari na Kayoza walikuwepo wako ndani, ikabidi Mama Kayoza hawaite, ila alikuja Kayoza peke yake,
"Naam mama, nimeitikia wito" Kayoza aliongea alipotoka ndani,
"mgeni anataka kuwaaga", Mama Kayoza alimwambia mwanae,
"sawa, karibu tena", Kayoza alimwambia Mkuu wa polisi,
"Sio karibu tena, unatakiwa umsindikize" Mama Kayoza alimwambia mwanae,
"Amekuja na gari" Kayoza alijibu mama yake,
"Hata kama amekuja na gari, unatakiwa umtoe nje, ndio uungwana upo hivyo" Mama Kayoza alimwambia mwanae,
"Yule mwenzio yupo wapi, yeye hataki kuniaga?" Mkuu wa polisi alimuulizia Omary,
"Alafu kweli, ebu kamuite na Ommy, aje amuage", mama Kayoza aliongea huku akimuangalia Kayoza,
"OMMY?", Mkuu wa polisi aliuliza kwa mshangao….
.."we Remmy njoo mgeni akuage",Kayoza aliita kwa sauti ya juu ili kumvuruga mkuu wa polisi.
Mkuu wa polisi ikambidi anyamaze, maana hakuna aliejibu swali lake, na isitoshe hata mama Kayoza alihisi kuna kitu, haiwezekani Omary aitwe Remmy ghafla kiasi mile.
Baada ya sekunde chache, Omary alitoka ndani na kujongea sebuleni kujumuika na wengine waliokuwako eneo hilo.
"bwana mdogo mi naenda, nawakimbia bwana",Mkuu wa polisi alimwambia Omari huku akiwa amemkazia macho na pia alikuwa anatabasamu tabasamu moja la kinafki sana, ila hakuna aliegundua jambo hilo,
"haya, karibu tena",Omari akamuitikia huku nae akilazimisha tabasamu lake halisi,
"Mama ukiwa na shida ndogo ndogo kipindi hiki Minja mgonjwa, usisite kuniambia" Mkuu wa polisi alimwambia Mama Kayoza,
"Hata usiwe na shaka baba angu, tushakuwa kama ndugu sasa" Mama Kayoza alijibu Mkuu wa Polisi
Baada ya maongezi hayo machache, wakamtoa mpaka nje, kisha Mkuu wa polisi akajipakia kwenye gari, gari ikaondoka.
Mama Kayoza na wanae wakarudi ndani.
"ehe mwenzetu, hilo jina umeliokota wapi?",Mama Kayoza alimuuliza Omari kwa utani,
"jina gani hilo",Omari nae aliuliza kanakwamba hajui,
"si hilo la Remmy Ongala!",Mama kayoza akajibu.
"Kwanza mama bado kidogo tu uharibu" Kayoza aliongea huku akijitupia katika kochi,
"Niharibu nini tena,!!?" Mama Kayoza aliuliza kwa mshangao,
"Ujue huyu mkuu wa polisi alivyomuona omary Kyle hospitali alimtilia shaka, na alipomuuliza jina lake, omary ndipo alipodanganya anaitwa Remmy. Sasa wewe tena ukamuita ommy" Kayoza alimlalamikia mama yake,
"Sasa huo ni ujinga wa nani?, huo ni ujinga wenu, kama mlitambua huyu mkuu wa polisi atakuja hapa, kwanini hakunitaharifu?" Mama Kayoza aliuliza kwa ukali,
"Sasa sisi tungejuaje kama yangetokea haya?" Kayoza nae aliuliza,
"Sasa ndio yameshatokea, ujinga wenu utawaponza, sijui mkuu wa polisi ameyaacha hapa hapa au ameenda nayo?" Mama Kayoza aliongea kwa hasira,
"atakuwa ameyaacha" Kayoza alijibu,
"Atakuwa ameyaacha" Mama Kayoza alirudia maneno ya mwanae, ila yeye alirudia kwa kebehi huku akiwa amebana pua.
Baada ya hapo Mama Kayoza akaenda sake ndani kwa hasira huku akiwaacha wakina Kayoza wakiwa wamekaa wanatazamana kwa jicho la kulaumiana,
"Hakuna haja ya kumtafuta mchawi, sisi sote tumehusika" Omary aliongea huku macho yake yakielekea kwenye runinga,
"Kweli, tulikosea kumficha mama, ila hakuna kilichoharibika" Kayoza aliongea huku akijilaza katika kochi.
Mkuu wa polisi hakuridhika kabisa na hali aliyokutana nayo, tayari akili yake ilimwambia kuwa kuna kitu kinafichwa katika familia ya wakina kayoza.
"yule Babu alisema kuwa kuna mwenzetu anatuzunguka, alikua anamaanisha Sajenti Minja au?",Mkuu wa polisi alijiuliza mwenyewe, kisha akaendelea,"na huyu Remmy nae….simuelewi kabisa, nilisikia kwa masikio yangu mwenyewe yule mama kasema OMMY, mara yule kijana akabadilisha akaita Remmy, mh.., kuna kitu kinaendelea hapa, ngoja nichunguze mwenyewe", Mkuu wa Polisi alikata shauri na kuamua kuifatilia mwenyewe ile kesi.
"Ila kama yule babu alisema amemsahau jina huyo askari anaetuzunguka, inawezenaje amsahau Minja?, ila hapana, hii kesi ngoja niichukue Mimi mwenyewe kimya kimya, nitaujua tu ukweli.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi