KIJIJINI KWA BIBI (31)

0
Mwandishi: Alex Kileo

SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
TULIPOISHIA...
"unamjibu nani hivyo?",Mama Kayoza alipamba moto, tena wa gesi, Kayoza akanyanyuka alipokaa na kuelekea chumbani kwao,

"endelea tu na kiburi chako, ila kina mwisho wake, na nina uhakika Kayoza utakuja kuniua na ugonjwa wa moyo", Mama Kayoza alimwambia mwanae wakati anaondoka, kisha akamgeukia Omari,

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
"Omari mimi sikujui ila nakulea kama mwanangu, hata siku moja sikuwai kufikiria kama utafanya kitendo kama nilichokiona leo, tena hadharani, alafu unakuja hapa unaanza kujisifu kwa ujinga uliokuwa unaufanya!?, wewe unafikiri heshima ninayokupa itakuwa katika kiwango gani?, ee!, nijibu Omari" ,Mama Kayoza alikuwa kama mbogo aliyejeruhiwa na risasi,

"mama naomba sana msamaha, ila haya ni mapito ya ujana mama yangu",Omari aliongea kwa hekima,

"mbadilike, nyie ni wasomi bwana, nawashangaa mnavyofanya ujinga",Mama Kayoza alimwaga sera zake,

"nakuahidi mama, haitokaa itokee tena, naomba uniamini mama yangu",Omari aliongea katika sura ya majuto na upole sana,

"shauri yenu bwana, kamuite mwenzio, muende mkaninunulie maziwa mie",Mama Kayoza aliongea huku anaelekea jikoni.

Omary akatoka sebuleni na kuelekea chumbani ambapo ndipo Kayoza alikuwepo,

"Twende tukanunue maziwa, mama ametutuma" Omary alimwambia Kayoza,

"Bado anawaka au amepoa kidogo?" Kayoza alimuuliza mwenzake,

"Amepoa, ila dah..inawezekana ni kweli tumefanya kitendo cha kipuuzi" omary aliongea kwa majuto kuonesha kuwa amekosa,

"Uwa inatokeaga, ila kumbuka kuwa hata katika kipindi cha huzuni uwa kuna muda mchache wa furaha" Kayoza aliongea huku akivaa fulana yake,

"Kweli ila sio kwa kiwango kile tulichofikia, tulipitiliza" Omary aliongea huku akitoka nje kumfuata mwenzake.

"Kawaida tu bwana, haina haja ya kujuta wala kusikitika" Kayoza aliongea huku nae akitoka,

BAADA YA MIEZI MIWILI

wakina Kayoza na Mkuu wa polisi wakiwa katika eneo la hospitali, Mkuu wa polisi alitaka kuwatega tena, safari hii alitaka kujua kama awa vijana wameshawahi kuishi mkoani Dodoma.

"Nyie mmezaliwa mkoa huu huu?" Mkuu wa polisi aliwauliza,

"Mimi nimezaliwa bukoba" Kayoza alijibu kwa ufasaha huku akitabasama,

"Na remmy wewe ulizaliwa wapi rafiki yangu?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akimfunga Omary kifungo cha juu cha shati,

"Mimi kwetu Tanga na ndipo nilipozaliwa?" Omary alijibu huku nae akitabasamu,

"Elimu zenu zopoje, yaani mmesoma mpaka kidato cha ngapi?, maana nyie ni ndugu zangu sasa, nataka nijue elimu yenu ili niwaangalizie hajira" Mkuu wa polisi aliuliza swali kwa kutumia akili nyingi ili aweze kuwataka hisia wakina Kayoza na atimize upelelezi wake,

"Sisi tuna elimu ya chuo, chuo kikuu" Kayoza alijibu huku akidhani ni sifa kubwa kusema ana elimu ya chuo, hajui kuwa kama anapelelezwa,

"Chuo gani?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akitabasamu,

"Chuo kikuu cha Dodoma, UDOM" omary alitoa jibu lililoanza kumpa mwanga mkuu wa polisi,

"Mlisomea nini pale?" Mkuu wa polisi aliuliza,

"Public relation, yaan mahusiano ya kijamii" Kayoza alijibu kwa kujiamini,

"Mmemaliza mwaka gani" Mkuu wa polisi aliendelea kuuliza,

"Mwaka jana, mwezi wa sita" Omary alitoa jibu lililomfanya Mkuu wa polisi aridhike kuwa ni kweli uenda awa vijana ndio wahusika wa mauaji, maana hata taarifa aliyokuwa nayo ulikuwa inasema ni wahitimu wa chuo, ila hawajarudi tena kuchukua vyeti vyao kutokana na kutafutwa na polisi baada ya kugundulika kuwa waliwaua wanafunzi wenzao wawili wa kike,

"Mna vyeti vyenu ili mniletee copy kesho na barua ya kuomba kazi, maana kuna kampuni ya jamaa yangu ya uchimbaji madini hapo kahama" Mkuu wa Polisi aliuliza sasa kupata uhakika wa vyeti,

"Vyeti hatuna, hatukwenda kuvifuata" Kayoza alijibu huku akijiuliza itakuwaje kama mkuu wa polisi atauliza sababu ya wao kutokwenda kuvifuata vyeti vyao, na kipindi hicho mkuu wa polisi alishaamini tayari hisia sake kuhusu Hawa vijana kuwa ndio wauaji wenyewe,

"Kwanini hamjavichukua sasa?" Mkuu wa polisi aliuliza,

"Matatizo ya ada, hali ya kiuchumi nyumbani ilikuwa ngumu kweli" Omary alijibu baada ya kumuona Kayoza akibabaika,

"Hata mjomba wenu hakuwasaidia?" Mkuu wa polisi aliwatupia swali jingine, ila kabla hawajajibu walimuona Daktari akiwafuata mbio mbio huku akihema juu juu, naona kwa ajili ya kukimbia sana na hata uso wake ulikuwa na furaha sana Siku hiyo tofauti na furaha anayokuwaga nayo siku nyingine,

"vipi Dokta, mbona hivyo?",Mkuu wa polisi alimuhoji Daktari,

"Taratibu mkuu, usiwe na papara na maswali yako ya kipolisi" Daktari aliongea kwa pupa huku furaha yake ikiwa bado ipo nae,

"Na wewe nawe uwa huishiwagi vituko? Sasa unavyokuja unakimbia hivyo alafu unapigia breki kwetu, ntaacha vipi kukuuliza?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akionekana hajapendezwa na kile kitendo cha daktari,

"OK, nisamehe mkuu, ila sikukusudia kukukera, nipo hapa mbele yako kwa sababu maalum" Daktari aliongea huku ile hali ya mzaha aliyokuwa nayo mwanzo ikiwa haipo tena,

"Sasa si ndio utuambie hiyo habari, wewe bwana vipi bwana" Mkuu wa polisi aliongea kwa sauti ya ukali kidogo,

"mgonjwa wenu kafumbua macho",Daktari aliwaletea habari ile ambayo ilikua kama uokovu kwao maana hata hasira zao zilikuwa zimeyeyuka ghafla kutokana na hizo habari,

"vipi, anaongea?",Mkuu wa Polisi aliuliza swali huku akiwa amemtolea macho daktari,

"sijajua bado, maana nilipomkuta katika hali hiyo nilimuacha na Daktari wa zamu na kuamua kuwafuata nyie",yule Daktari alijibu,

"Si tunaweza kwenda kumuona?" Kayoza alimuuliza daktari baada ya muda mrefu wa ukimya,

"Twendeni" Daktari alijibu huku akiondoka na kufanya wote waanze safari ya kuitafuta wodi ambayo kalazwa Sajenti Joel Minja.

Walipoenda wodi ya wagonjwa mahututi ambayo alilazwa Sajenti Minja hapo hawali, walikuta kitanda alicholala Sajenti Minja kitupu, ikambidi Daktari aliefuatana na wakina Kayoza amtafute Daktari wa zamu ili kujua mgonjwa amehamishiwa wapi. Alichukua simu yake na kumpigia mwenzake ili amuulize ni Wapi Sajenti Minja amehamishiwa,

"twendeni grade C",Daktari aliwaambia baada ya kukata simu, walipofika huko grade C, walimkuta Daktari wa zamu anamalizia kumpima Sajenti Minja, wakasubiri kwa muda kidogo, kisha wakaruhusiwa kuingia, walipofika katika kitanda alicholala Sajenti Minja, wote watatu wakajenga tabasamu katika nyuso zao, lakini Sajenti Minja alikuwa tofauti kidogo, hakuonesha kuwakumbuka kabisa,

"bado kumbukumbu hazijamrudia vizuri",Daktari wa zamu alimuambia Mkuu wa Polisi,

"itachukua muda gani kurejea katika hali yake?",Mkuu wa Polisi aliuliza,

"itategemea na nyinyi wenyewe, maana anapomuona mtu mara kwa mara ndio anapata kumbukumbu",Daktari alimjibu Mkuu wa Polisi, kisha wote wakawa wanamuangalia Sajenti Minja ambae alikuwa amelala uku macho yake yakiwa wazi yakipepesa pepesa,

"Amekonda aisee" Mkuu wa Polisi aliongea huku akiwa bado anamuangalia Sajenti Minja,

"Kukonda lazima, maana alikuwa anakula kwa mipira na dripu pekee" Daktari wa zamu alijibu huku akiuweka vizuri mkono wa Sajenti Minja,

"Sasa mpaka atengemae kabisa itachukua muda gani?" Mkuu wa polisi alimuuliza Daktari wa zamu,

"Hatuwezi kujua, ila kama atakuwa anakula vizuri na kunywa maji ya kutosha, anaweza kurudi kama hawali" Daktari alijibu,

"Ila hata hii hatua aliyofikia, ni hatua ya kumshukuru sana Mungu" Kayoza aliongea huku machozi ya furaha yakimtoka, alishindwa kuzuia hisia zake, aliamini mpigania ubinadamu wake amepona kwa hiyo ana uhakika wa kupona kwa maana Sajenti Minja ndiye mtu pekee aliyekuwa anaangaika nae kwa vitendo na maneno.

Wakati wakiwa bado wanaongea pembeni ya kitanda ambacho amelala Sajenti Minja, ndipo Sajenti Minja akamtolea macho mkuu wake wa Polisi huku akiwa kama anajitahidi kuvuta kumbukumbu juu ya mtu huyo,

"vipi Minja mbona unaniangalia sana, unanikumbuka?",Mkuu wa polisi akamuuliza swali Sajenti Joel Minja,

"ndio nimekukumbuka vizuri sana, ni mkuu wangu wa kazi",Sajenti alijibu kwa ufasaha kwa sauti iliyochoka sana kutokana na kulala kwa wiki nyingi sana.

lakini jibu la Sajenti Minja likampa njia Mkuu wa Polisi, akaona huo ndio wa wakati halisi wa kumjua na kumuumbua mtu anayejiita Remmy, na muda huo ndio alitaka ahakikishe kuwa yule kijana ambae anamtilia mashaka ni yeye haswa,

"huyu nae unamkumbuka?",Mkuu wa Polisi aliongea huku akimshika bega Kayoza, alikuwa na maana yake kuanza na Kayoza,

"huyo ni mtoto wa dada, anaitwa Kayoza",Sajenti Minja alijibu tena kuashiria kumbukumbu zimemrejea.

Omari na Kayoza waligundua mchezo anaocheza Mkuu wa Polisi, na wote walinyong'onyea kwa kujua kwamba wameumbuka, kwa maana anaefuata kutambulishwa ni Omari.

"huyu nae anaitwa nani?, taja majina yake yote matatu, ili nijue kumbukumbu yako imerudi",Mkuu wa Polisi alimuuliza Sajenti Minja huku akimsogeza Omary mbele ya macho ya Sajenti Minja….

…"jamani waungwana muda wa kuangalia wagonjwa umekwisha",Daktari mmoja mwenye umri ulioenda kidogo aliingia ndani ya wodi na kutamka maneno hayo,

"ebu tufanyie subra kidogo, kama dakika tano za nyongeza",Mkuu wa polisi alimwambia Daktari zamu ambaye alikuwa nae muda mrefu ,

"haiwezekani kamanda, ni makosa makubwa sana kuongeza muda wa ziada wa kumuangalia mgonjwa",yule Daktari mwenye umri mkubwa kidogo aliongea huku akiwafungulia mlango ikiwa ni ishara ya kuwaruhusu watoke,

"Minja mimi nitakuja baadae",Mkuu wa polisi alimwambia Sajenti Minja, ambae muda wote alikuwa kimya huku akijaribu kuvuta kumbukumbu zake kuhusu Omary,

"sawa mkuu",Sajenti Minja alijibu kwa sauti ya uchovu,

"baadae tukuletee chakula gani anko?",Kayoza alimuuliza Sajenti Minja,

"mleteeni juisi au uji, msisahau maji, haya nendeni nje waheshimiwa",Daktari wa zamu alidakia, kisha akawaondoa wodini wakina kayoza.

Sajenti Minja akageukia ukutani na kutabasamu,

"Anaitwa Omary mkwiji, hilo ndilo jina lake mkuu" Sajenti Minja aliongea peke na kuendelea kutabasamu.

Kayoza, Omary na Mkuu wa Polisi Waliondoka wakiwa na furaha sana,

Kayoza alipata tumaini jipya la kupöna, kwa sababu mtu aliekuwa anamsaidia amepona.

Huku Mkuu wa polisi akipata zaidi imani ya kumchunguza Sajenti Minja, nae alijikuta anatabasamu,

"Naona leo umefurahi mjomba kupona" Kayoza alimwambia Mkuu wa polisi baada ya kumuona akitasamu, na kumfanya Mkuu wa polisi ashtuke maana alikuwa anatabasamu bila kujijua,

"Eeh, ndio…kwani nyie hamjafurahia?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akijifanya ni kweli anafurahia Sajenti Minja kupona,

"Kwanini tusifurahi, lazima tufurahi" Omary alijibu huku akicheka,

"Jambo la heri sana, bora ameamka maana akishatengemaa kabisa kila kitu kitakuwa sana" Mkuu wa polisi aliongea,

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)