Mwandishi: Alex Kileo
SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
"Eeh, ndio…kwani nyie hamjafurahia?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akijifanya ni kweli anafurahia Sajenti Minja kupona,
"Kwanini tusifurahi, lazima tufurahi" Omary alijibu huku akicheka,
"Jambo la heri sana, bora ameamka maana akishatengemaa kabisa kila kitu kitakuwa sana" Mkuu wa polisi aliongea,
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
"Kweli kabisa" Kayoza alijibu,
"Mnaelekea wapi sasa?" Mkuu wa polisi aliwauliza wakina Kayoza,
"Ni nyumbani tu, tukampe taharifa mama" Kayoza alijibu,
"Atafurahi sana akisikia mdogo wake amefungua macho" Mkuu wa Polisi aliongea huku akitabasamu,
"Tena sana, anaweza hata kuchanganyikiwa" Omary alimsapoti mkuu wa polisi,
"Sasa Mimi leo siwapeleki, kuna sehemu kuna kikao natakiwa ndani ya dakika kumi hizi, chukueni hii hela mkapande bajaji" Mkuu wa polisi aliongea huku akitoa noti shilingi elfu kumi na kuwakabidhi,
"Asante, ila baadae naimani baadae tutakutana hapa hapa" Kayoza aliongea huku akiiweka pesa mfukoni,
"Lazima nine baadae, kikao kikiisha tu nitakuja kushinda hapa hapa" Mkuu wa polisi aliongea,
"Haya, sasa sisi acha twende tukatafute hiyo bajaji ya kutupeleka nyumbani" Kayoza alimwambia Mkuu wa polisi,
"Sawa wajomba, baadae" Mkuu wa polisi aliongea huku akiingia katika gari yake na kuwaacha wakina Kayoza wakienda upande wa pili wa barabara ambapo ndipo bajaji zilikuwepo.
BAADA YA WIKI MOJA
Sajenti Minja aliruhusiwa kutoka hospitali, ila Mkuu wa polisi alimuomba akae nae nyumbani kwake, mpaka pale Sajenti Minja atakapotengemaa kabisa ndipo arudi kwake. Ilo halikupingwa, Sajenti Minja aliamua akae kwa muda kwa Mkuu wa polisi kwa maana ndani ya nyumba ya Mkuu wa polisi alikuwa anaweza kupata kila kitu alichokitaka kutokana maisha mazuri aliyokuwa nayo Mkuu wa polisi ambayo yalikuwa tofauti na maisha ya kwa dada yake.
Maisha katika nyumba ya Mkuu wa polisi yalikuwa ni mazuri sana, wakina Kayoza walikuwa wanaenda kila siku kumtembelea Sajenti Minja katika nyumba ya Mkuu wa polisi, na watu wote pale katika nyumba ya Mkuu wa polisi waliwazoea, kuanzia wafanyakazi, mke wa Mkuu wa polisi na mtoto wa kike na wa pekee wa Mkuu wa polisi.
Sasa tatizo lilikuwa kwa mtoto wa pekee wa mkuu wa polisi, ambae alikuwa anaitwa Martha, huyu Martha toka aanze kuzoeana na Kayoza amekuwa akimuonesha dalili zote za kumpenda, ila Kayoza hakuelekea kabisa, sio kwamba hakuwa na hisia na huyo binti, la asha, aliohofia mzimu ambayo ungeweza kumletea matatatizo anapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi. Kwa hiyo alimuwekea ngumu kabisa.
Mkuu wa polisi alifanikiwa kumpata kijana mmoja pale mtaani kwa wakina Kayoza, yule kijana aliitwa Ismail, ila wengi walizoea kumuita Suma, huyo kijana aliambiwa mkanda mzima jinsi ulivyo, kwa hiyo kazi yake ilikuwa kumchunguza Omari.
Suma alikua ni kijana mchangamfu sana, na kwa kuanzia tu, alianza kwenda katika kijiwe cha mchezo wa drafti ambacho Omari alipenda sana kwenda, hatua ya kwanza alifanikiwa kujua kuwa Remmy sio jina halisi la Omari, ila hata hivyo hakujua jina halisi la Omari, maana pale walikuwa wanamuita mzee wa supa, ni kutokana na mtindo wa magoli anayowafunga wenzake. Ila suma hakukata tamaa, akajipa moyo kuwa lazima aifanikishe kazi aliyopewa, maana hata posho aliyoahidiwa kupewa na Mkuu wa polisi, ilikuwa ni posho nzito, ilimtosha kununua kila kitu cha ndani.
Na sifa nyingine ya ziada, Suma aliweza kujenga mazoea ya haraka sana, tena na kila mtu.
Jioni moja tulivu, Kayoza na Omari wakiwa nyumbani kwao,
"Twenzetu basi, maana sioni kama una dalili za kutoka" Kayoza alimwambia Omary,
"Si nilishakwambia najisikia hovyo, sijui ni malaria?" Omary aliongea kinyonge huku akiwa kitandani,
"Sasa unaumwa alafu unakaa ndani?, si uende hospitali man" Kayoza alimwambia Omary,
"Hela hamna kaka" Omary alijibu kinyonge,
"Acha mambo yako bwana, si umuombe mama, usimuogope bwana, yule ni mama yako" Kayoza alimwambia Omary,
"Sijamzoea kama wewe, basi kaniombee" Omary alimwambia Kayoza,
"Ngoja nikamwambie, ila usirudie tena, utakuja kufa umelala" Kayoza alimwambia Omary,
"Kamwambie mama bwana, acha blah blah blah nyingi" Omary alimwambia Kayoza,
"Mi ndo natoka hivyo, sirudi tena huku chumbani, naenda kumcheki mjomba" Kayoza aliongea huku akitoka nje,
"Poa, mwambie naumwa na ndio maana sijafika" Omary aliongea,
"Poa" Kayoza aliongea huku akitoka.
Alipofika sebuleni alimwambia mama yake hali ya Omary, kisha akaaga kuwa anaenda kwa Mkuu wa polisi kumuangalia mjomba ake.
++++++++
Kayoza alifika nyumbani kwa mkuu wa polisi na kumkuta Martha yupo peke yake, na Martha alimwambia Kayoza kuwa Sajenti Minja na Baba yake ambae ni Mkuu wa Polisi wametoka, wameenda kunyoosha miguu kidogo.
Sasa Martha akaona kuwa huo ndio muda mzuri wa kufanya, anachotaka kwa kayoza, Martha akaaga anaenda ndani Mara moja kufanya usafi na kumuacha Kayoza akiwa sebuleni anaangalia runinga.
Baada ya dakika chache…….
"mama weee, jamani panya panya",Martha alipiga kelele ndani ya chumba chake, kisha akatoka nje huku anakimbia, akaenda alipokaa Kayoza,
"Yaani wewe mkubwa hivyo unaogopa panya?" Kayoza alimtania Martha huku akimcheka,
"Usiseme huvyo Kayoza, kwanza naomba ukanisaidie kuua panya",Martha alimwambia Kayoza,
"Sasa huyo panya atakuwa amekaa tu anakusubiri?" Kayoza alimuuliza Martha huku akiendelea kumcheka,
"Yupo kwenye kabati, alafu limefungwa, yupo kwa ndani. Twende bwana ukamuue, uwa ananisumbua sana" Martha alimwambia Kayoza, Kayoza bila kubisha akanyanyuka alipokaa na kwenda chumbani kwa Martha, huku Martha akimfuata kwa nyuma.
Kayoza alipoingia ndani, Martha akaubana mlango na funguo kisha funguo akaidumbukiza ndani ya kifua chake, kisha akamgeukia Kayoza,
"Kayoza hakuna panya, ila ninachotaka toka kwako unakijua, Kayoza unaumiza moyo wangu sana, nifanyaje ili ujue nakupenda, eee?",Martha aliongea huku machozi yakimtoka,
"Dah, Martha si nilishakuambia haiwezekani lakini?" Kayoza aliuliza baada ya kukaa muda mrefu akimuangalia Martha kwa hasira,
"Naomba tu iwezekane, mpaka Mimi kufikia hata hii ya kukutamkia maneno haya, ujue hisia zangu zimenishinda" Martha aliongea huku akipiga magoti,
"Sawa nimekuelewa, naomba unifungulie mlango nitoke nje" Kayoza aliamua kumkubalia ili amridhishe Martha,
"Hapana sitaki utoke" Martha aliongea kwa hisia huku akimtazama Kayoza…
mara sauti ya Mkuu wa Polisi ambaye ndiye Baba yake Martha ikasikika mlangoni,
"we Martha unaongea na nani uko chumbani? Ebu nifungulie mlango"
…"hakuna kitu daddy",Martha alimjibu Mkuu wa polisi,
"kwa hiyo unaongea peke yako uko"Mkuu wa polisi akamtupia mwanae swali jingine,
"si naongea na simu",Martha akajibu.
"Fungua basi mlango niingie" Mkuu wa polisi akamwambia mwanae,
"Daddy navaa bwana, kwani unataka nini huku?" Martha alimjibu baba yake huku akideka.
Hivyo ndivyo alivyolelewa na wazazi wake, amelelewa malezi ya kujibishana na wazazi wake kama rafiki zake,
"Si nilitaka nikuone mwanangu, au vibaya mama?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akiwa mlangoni,
"Nakuja sebulebi daddy, mammy umemuacha wapi?" Martha aliuliza,
"Nimerudi nae, ameenda kuoga" Mkuu wa polisi alijibu huku akiamua aondoke zake, na kurudi sebuleni kuongea na Sajenti Minja,
"naweza kupata juice",Sajent Minja alimuuliza Mkuu wa polisi alipokua anakaa,
"mhmm..sidhani kama ipo, ebu ngoja, we Martha, marthaa",Mkuu wa polisi alijibu kisha akamuita mwanae,
"nakuja daddy" Sauti ya Martha ilisikika kutoka chumbani kwake.
Baada ya sekunde chache Martha akawa mbele ya Sajenti Minja na baba yake,
"shikamoo anko",Martha alimsalimia Sajenti Minja,
"marhabaaa anko, kuna juisi?",Sajenti Minja aliitikia, kisha nae akauliza swali,
"ipo anko,",Martha alijibu,
"naomba unipe ya pera",Sajenti Minja aliwasilisha ombi lake, mmmh, ya pera hamna, ipo ya orange, strawberry,mango na passion",Martha alijibu,
"nipe ya chungwa na maji ya baridi",Sajenti Minja aliagiza na martha akamletea,
"Vijana wangu hawajaja leo?" Sajenti Minja alimuuliza Martha, alikuwa akiwaulizia wakina Kayoza,
"Hawajafika anko" Martha alijibu huku nafsi yake ikimsuta kwa maana aliongea uongo,
"Leo naona watakuwa wamechoka" Mkuu wa polisi alimwambia Sajenti Minja,
"Wamechoka wapi, itakuwa wameona nimeshapona kwa hiyo hawaoni umuhimu wa kuja kunijulia hali" Sajenti Minja aliongea,
"Acha wapumzike, maana wale watoto walikuwa wanashinda hospitali mpaka nikawa nawahurumia" Mkuu wa polisi aliwatetea wakina Kayoza,.
"Hakuna haja ya kuwahurumia, hilo ndilo lilikuwa jukumu lao, mama yao umri wake umeshakwenda, anatakiwa apumzike" Sajenti Minja aliongea,
"Wameshawahi kuishi Dodoma ee?" Mkuu wa polisi aliuliza swali lililomshtua Sajenti Minja,.
"Nani alikwambia?" Sajenti Minja aliuliza huku akijifanya anacheka ili kuuficha mshtuko wake, ila tayari Mkuu wa polisi alikuwa ameshamsoma,
"Waliniambia wenyewe, wakadai wamemaliza pale UDOM ila hawajachukua vyeti vyao" Mkuu wa polisi alizidi kutiririka na kuendelea kumshtua Sajenti Minja,.
"Yah ni kweli walimaliza pale" Sajenti Minja alijibu kifupi,
"Sasa ni kwanini hawajachukua vyeti?" Mkuu wa polisi aliuliza swali la kumtega Sajenti Minja ili zone kama jibu lake litafanana na la wakina Kayoza,
"Hawajachukua vyeti?, mbona Mimi hawajaniambia kama hawajachukua vyeti vyao?" Sajenti Minja alijifanya kushangaa huku akiuliza,
"Alah!!! Kumbe hujui?" Mkuu wa polisi aliuliza,
"Aisee hawakuniambia, labda wamefanya makosa wanaogopa kuniambia, au wamekula ada?" Sajenti Minja aliamua kumuigizia sasa Mkuu wa polisi, alivyokuwa anaongea utasema kweli yaani,
"Wameniambia wameshindwa kulipa ada ndio maana hawajachukua" Mkuu wa polisi aliamua kumwambia ukweli,
"Wanekudanganya, niliwapa pesa yote, itakuwa wamefeli au wamekula ada…yaani awa watoto awa, utakuta hata mama yako hajui kama hawana vyeti" Sajenti Minja alijifanya kusikitika,
"Kwani walikuwa wanasomea nini?" Mkuu wa polisi aliuliza swali jingine lilimuweka mtegoni Sajenti Minja,
"Hawajakwambia?" Sajenti Minja alimuuliza mkuu wa polisi huku akijitahidi kuvuta kumbukumbu ya masomo waliyokuwa wanasoma wakina Kayoza,
"Hawakuniambia" Mkuu wa polisi alijibu huku akibonyeza controller ya runinga,
"Mi hata nilikuwa sifuatilii wanachukua kozi gani, ili mradi nilikuwa nawalipia ada wamalize tu chuo" Sajenti Minja alilipangua swali la Mkuu wa polisi,
"Ulikuwa unatakiwa uwafuatilie bwana" Mkuu wa polisi alimwambia Sajenti Minja,
"Shauri yao bwana kama walichezea masomo, ngoja nikajimwagie maji" Sajenti Minja alijibu huku akinyanyuka na kuondoka ili kuyakwepa maswali ya Mkuu wa polisi, maana yalimpa mashaka na akahisi inawezekana babu wa monchwari alimchoma.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi