Nyumba ya Wachawi (1)

0
Mtunzi: Denis Benard

SEHEMU YA KWANZA
Ni asubuhi na mapema kijana Faluu amelala huku manyunyu yakiwa yanapiga kwa mbali,ilikua ni asubuhi iliyojaa mvuto saana maana ilitokea kupamba usingizi wa Faluu na kufanya iwe ngumu sana kwake kuachia shuka na kuingia katika mahangaiko ya maisha,wakati akiwa katikati ya ndoto Faluu    aliamshwa na mama yake ili awahi shambani,

“Faluu mwanangu kumekucha sasa amka uende shambani’’

(kwa sauti ya uchovu Faluu alijibu)

‘’Mmh!!,sawa mama ngoja niamke ila mwili wangu umechoka sana’’

‘’Jitahidi mwanangu maana kadiri unavyowahi kwenda shambani,ndivyo utakavyowahi kurudi’’ mama aliongea kwa upole sana na kumtia moyo mwanae

‘’Sawa mama..’’aliongea Faluu.

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

Baadae aliamka na kujiandaa na kisha alimuaga mama yake huku nafsi yake ikiwa na wasiwasi sana..

‘’Haya mama yangu mimi naenda shambani,ubaki salama..Ilaa! Basi tutaongea baadae’’aliongea Faluu.

Kitendo kile kilimfanya mama yake kutomuelewa Faluu juu ya nini anachokimaanisha,ilibidi amuulize…

‘’Usiondoke kwanza,embu niambie kulikoni mbona sikuelewi??’’ aliuliza kwa shahuku kubwa sana ya kutaka kujua nini mwanae anafikiria..

‘’Hamna mama kawaida,tutaongea baadae ,ngoja niende shambani’’Faluu alijibu

Maneno yale yalimfanya mama yake Faluu kua na wasiwasi juu ya nini mwanae anamaanisha,hivyo ikambidi aendelee kumdadisi mwanae..

‘’Embu nieleze mimi mama yako ilinijue nini unafikiria mwanangu,kwa sababu unanifanya niwe na wasiwasi sana mama yako’’

(kwa uchungu sana,Faluu alijibu)

‘’Sawa mama yangu najua,lakini naomba usiwaze sana,ni hivi najikuta akili yangu haiko sawa sana  kukuacha wewe peke yako mama yangu mpendwa’’

(Mama alicheka sana)

‘’Yaani mwanangu  unakua na wasiwasi kwa sababu ya kuniacha hapa nyumbani mimi peke yangu??kwani leo ndio mara ya kwanza,embu usiwe hivyo,nenda tu mimi nitakua salama sawa mwanangu’’

(Huku akiwa na tabasamu,Faluu alijibu)

‘’Sawa mama,mimi naenda,ubaki salama eeh mama yangu’’aliongea Faluu na baadae aliondoka.

Kutokana na maongezi yale,yalimfanya Faluu achelewe kufika shambani ,maana mpaka jua la saa moja na nusu asubuhi linatoka alikua bado hajafika shambani.Lakini pamoja na faraja zote za mama yake,alijishangaa sana pale ambapo alijikuta akiingiliwa na mawazo mabaya katika kichwa chake.

‘’ Hivi mbona nakua katika hali hii??,kitu gani kinaendelea?? Na mwili wangu unakua mchovu hivi??’’ alijikuta akiwa na awazo sana.Alifika shambani na bila kupoteza muda alianza kufanya kazi yake.

Ilipofika saa nane mchana,alijikuta kichwa chake kikiwa kizito sana na macho yake yaliacha kuona mbali, ghafla alipoteza fahamu .Wakati akiwa amepoteza fahamu katika shamba lile walitokea viumbe wa ajabu wakamchukua na kumpeleka  barabarani na katikati ya viumbe kulikua na kiongozi wao ambaye

(aliongea maneno haya kwa sauti ya kutisha sana )

‘’Baada ya mambo yote ya msiba kuisha hakikisha unaenda kwa mjomba wako,hayo ndiyo maneno ya mwiso nilioachiwa na mama yako” huyo kiumbe aliongea na baada ya hapo walipotea na kumuacha Faluu pale barabarani peke yake. Baada ya muda wa dakika kadhaa alipita jamaa mmoja katika eneo lile,alishangaa sana alipoona mtu kalala mbele yake na hivyo ikamfanya asogee ili ajue nini na ni nani kimemkuta mtu Yule…

‘’ Nani Yule na kwa nini kalala pale ?? ‘’alijiuliza na kuongeza mwendo ili afike haraka katika eneo lile alipokua amelala na alipokaribia alishtuka sana kumuona Yule…

‘’ Heeee! Kumbe ni Faluu rafiki yangu, sasa kafanyaje ?? ‘’ alijiuliza na kumkimbilia ili ajue nini kimemkuta.

‘’ Faluu ! Faluu! Faluu rafiki yangu nini tena kaka?? ‘’ aliongea Yule kaka kwa sauti ya uchungu sana. Baada ya muda kidogo Faluu alishtuka sana..

(Kwa mshtuko mkubwa sana ,Faluu aliongea)

‘’ Mama yangu , Mama yangu ! “ aliongea  Faluu na  baadae alikimbia kutoka eneo lile na  kumuacha Yule kaka pale………

Baada ya Faluu kukimbia,alimuacha Yule kaka pale huku akibaki kumshangaa asijue nini cha

 kumsaidia.

‘’ Huyu nae kawa kichaa nini ? Mbona anafanya mambo ya ajabu? ,aah! Shauri yake ! ‘’ alijiongelea Yule kaka na baadaye aliondoka kuelekea kwao.

Baada ya Faluu kukimbia akielekea kwao, alikua kama mtu aliyechanganyikiwa na kwa wakati huo wote ile sauti aliyoisikia wakati akiwa amepoteza fahamu ilikua ikimrudia katika mawazo yake..

‘’ Hapana !! Itawezekana vipi yale maneno niliyoyasikia ?? , Haiwezekani !! “ alijiongelea na kutokana na maneno yale,Hasira ilimpanda na kujikuta akiongeza mwendo ili akajue ukweli wa kinachoendelea. Wakati akiwa njiani,alikutana na watu wengi na wengi wao walikua wanamfahamu  Faluu,walijitahidi kumzuia ili waongee naye..

(Walitanda njiani ,huku sura zao zikiwa zimetawala uzuni )

‘’ Na nyie hapo shida yenu nini?? Mbona mmezuia njia mimi nisipite ??’’ Faluu aliwauliza…

( Mmoja wao alisogea mbele na kisha akapiga magoti )

‘’ samahani ndugu yetu, tunaomba utuisikilize japo kidogo ‘’ yule mtu aliongea

( Kwa pamoja wote waliobaki , walijibu)

‘’  Kweli kaka tunaomba utusikilize ‘’

Kutokana na maombi ya wale watu , Faluu ilibidi atulie na awasikilize wale watu shida yao..

‘’ Enhe nawasikiliza , mnaweza kuongea ….’’ Alijibu Faluu

Baada ya Faluu kuongea vile , alijikuta Jadhiba ikipungua na kutaka kuwasikiliza wale watu nini shida yao.

‘’ Tunaomba tusogee pembeni kidogo ili tuongee, si unajua hapa njiani ‘’ aliongea mtu mmoja. Lile swala la kusogea pembeni lilimpa wasiwasi kidogo Faluu , maana sehemu aliyokua akielekezwa wasogee waongee ilikua ni porini .

( Faluu Akiwa na wasiwasi aliwaeleza)

  ‘’ Kwanini tusiongelee hapa hapa ?? ‘’ Faluu aliwauliza

( Huku wakiwa wanatabasamu mmoja alijibu )

‘’ Hamna kaka hapa naona tunaongea tukiwa hatuna uhuru , mimi naona tusogee pembeni kidogo ‘’

Wakiwa wanajibizana katika ile njia , wale watu walianza kuhisi kama kuna mtu atapita muda si mrefu katika eneo lile , hivyo walipeana ishara na bila kupoteza muda Faluu alijikuta akiwa amebebwa juu juu na wale watu na wakaingia katika pori hilo..

( Faluu alianza kupiga kelele akihitaji msaada )

‘’ Jamani nisaidieni , nisaidieni sana jamani ! Nakufa mimi!! ‘’

( Wale watu walimjibu kwa jeuri )

‘’ Utajua tu ! ‘’ waliongea huku wakiwa wanazidi kuingia naye katika pori hilo..

Kumbe wakati Faluu akipiga kelele , kuna mtu msamalia mwema alimsikia , alikua ni yule mtu aliyemkuta amelala pale njiani..

‘’ Mmh ! ni nani huyu ?? nah ii sauti mbona kama inafanana na ya Faluu ?? ‘’ alisogea mpaka karibu na sehemu walipokua wamesimama, kabla hawajaingia naye katika pori..

‘’ Halafu inaonekana hii miguu walikua wamesimama hapa na kama sio kusimama , basi walipita eneo hili  ,  sasa mimi nitafanyaje ??kumsaidia‘’ yule kaka alikua akijiongelea na baadae mawazo yalimjia aingie ndani ya lile pori..

Wakati yule kaka mawazo yakimjia afatilie ili ajue nini kinaendelea , na wale watu hisia ziliwapelekea kama kuna mtu anakuja kuwafatilia , hivyo walijikuta wakiwa makini sana..

‘’ Oya sasa tunafanyaje ? maana hapa kuna mtu anakuja nyuma anatufatilia ‘’ aliongea mmoja.

‘’ Hatari sana ,maana inaonekana mtu mwenyewe yuko kasi sana ‘’mwingine alijibu.

‘’ Mimi naona tuongeze mwendo hadi katika lile shimo letu kule ‘’ kiongozi wao aliongea

(Kwa pamoja walijibu)

‘’ Sawa mkuu ,inabidi tuwahi ‘’

Wakati maongezi yao yakiendelea , Faluu alikua akiwafatilia sana na kumfanya kua na hofu sana na maisha yake na kitu kikubwa zaidi ilikua ni hali ya mama na taarifa alizozipata..

(Kwa unyonge alijibu )

‘’ Hivi jamani mimi nimefanya nini ?? , huku mnanipeleka wapi ?? na nini maana yenu ? ‘’

‘’Unajifanyab unaongea kinyonge , wewe subiri hata usiwe na haraka utajua tu sawa , punguza maneno ,kwanza sehemu yenyewe tumeshafika mshusheni hapo ‘’aliongea mtu mmoja. Baada ya huyo mtu kuongea hivyo hawakumchelewesha ,walimshusha na moja kwa moja walimtupa katika shimo moja kubwa sana na kiongozi wao aliongea neno moja…

‘’ Wachawi ! wachawi ! na huo ndio mwanzo tutajua tu ,twendeni ‘’ Wakati wanageuka na kuondoka ,walikutana uso kwa uso na yule kaka Msamalia mwema………..

Wakati watu wale wanageuka walikutana uso kwa uso na Yule kijana akiwa anafatilia ni sehemu gani yule mtu atakua anapelekwa.Kitu kile kiliwashtua sana na sio wao tu hata yule kijana naye alipata mashaka kutokana na mazingira yao na pande zote  mbili zilijikuta zikishindwa kufanya kitu chochote kwa wakati ule.

(Wale vijana walibaki wakijinong’oneza )

‘’Mkuu tunafanyaje sasa?, maana tunaona kama huyu mtu sio salama sana kwetu,embu sema kitu chochote’’

(Mkuu wao alitikisa kichwa na kuongea neno moja tu)

‘’Hana lolote huyu,nyie muacheni ‘’ aliongea na baadae waliendelea na safari yao, huku wakiwa na maongezi binafsi.

Katika kipindi chote hicho,Yule kijana alikua akiwaangalia huku nguvu zikiwa zimemuisha na zaidi wasiwasi ulikua ni juu ya mazingira waliyokutana  kule msituni,hivyo hakua na namna nyingine ya kufanya pale.

(Huku akitetemeka alijiongelea)

‘’Mmmh! Hawa ni akina na nani na mbona nimewakuta huku porini ,halafu ndiko sauti ile ilikoelekea?, bila shaka huku kutakua na namna tu! Mh!,ila bora wameondoka,maana ilikua hatari sana hapa”alijiongelea huku akiwa anapumua sana.

‘’Ila hapa cha msingi nianze kumtafuta huyu mtu na nina amini hawa hawa ndio watakua wanafanya,lakini pia watakua wametoka wapi?,maana sura zenyewe ngeni sana katika macho yangu na ninafikiri hata kwa kijijin ni wageni pia’’ alikua akijiongelea tu mwenyewe huku asijue jibu gani ni sahihi kutokana na maswali aliyokua akijiuliza mwenyewe na mwisho wa siku aliyapuuzia na kuendelea kusonga mbele huku akimtafuta Faluu huku na kule ili ajue hatima yake.

“Faluu !Faluu! Faluu!Faluu!....’’ na kwa mbali alihisi kama kuna mtu aliitikia sauti sauti yake na wakati huo Alikua anatembea huku akiita.Lakini kipindi hicho alikua amesonga mbele kwa muda mrefu sana huku akiita jina la Faluu yeye ,kutokana na mabadiriko ya hali yake,alianza kuhisi kama kuna mtu alikua anamfatilia kwa nyuma huku akimpulizia upepo kwa nyuma.Kitu kile kilimfanya ageuke nyuma,Alipogeuka nyuma hakuamini maana alikutana na lile kundi la wale watu,kumbe muda ule hakuondoka na badala yale walifika mbele na kurudi huku wakimfatilia ili wajue lengo lake nini katika msitu ule.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)