Notifications
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…
  • MY DIARY (29)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TISATULIPOISHIA...Hapo sasa nikazidi kuchanganyikiwa ikabidi nimuulize mama huyo alikuwa akifanyia shughuli zake za kujipatia kipato sehemu gani.? Yule dada akanambia kuwa anafanyia soko la ndizi huko Korongoni. Sikuwa na jinsi nilimuomba anipeleke lakini na yeye alisita sita kwa madai kuwa alikuwa na kazi nyingi za kufanya na bado anatakiwa ampeleke mtoto shule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (28)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NANETULIPOISHIA...Sisi tumesomea mambo haya bhana waliendela kuzungumza wale walinzi huku wakishuka ngazi kwa polepole. Hapo na mimi nikawa nimejifunza kitu kuwa kumbe unaweza kuingia na mtu guest akakuzuru kisha akaondoka zake.Sasa sijui kwenye zile guest zetu za uswahilini kama wanalijua hili.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilala japo usingizi ulikuwa hautaki kuja kwa…
  • MY DIARY (27)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SABATULIPOISHIA...Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijifanya simwelewi lakini ukweli ni kwamba nyota ya mwanaume huyu ilikuwa ni kali sana zaidi yangu na…
  • MY DIARY (26)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SITATULIPOISHIA...Joyce alinambia yeye haendi kujipanga foleni kama makahaba wengine hivyo yeye hufanya biashara hiyo kitaalamu zaidi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alisistiza pia kuwa eti huwa anatumia kinga kuwakinga wengine. Wakati mwingine alinambia acha awaambukize kwa sababu wanaume wangekuwa na akili basi wasingeenda kununua mwanamke. Anasema kuwa laiti biashara hiyo…
  • MY DIARY (25)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TANOTULIPOISHIA...Sikuisha hapo pia nilimpongeza kwa kunijali na kunipenda na kuhakisha kuwa siingii kwenye majanga kama yake mara baada ya kutoka jela. Siku hiyo nilimuelewa sana Joyce na nilikuwa tayari kumsapoti kwa lolote ili mradi tu atimize athma yake hiyo ya kuzaa. Tuliongea mengi sana na baadaye alinionesha picha ya mtu ambaye alitaka kuzaa naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (24)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NNETULIPOISHIA...Kwa kweli siku hiyo niliwaza sana na kutafakri vitu vingi. Wale wanachuo wenzangu wamenambia kuwa Msouth alikuwa kwa kimada mwingine na japo stori haikumalizikia ila ukweli ni kwamba alifumaniwa na kupigwa vibaya na huenda walimtupa mahali na ndio maana chanzo cha kifo chake hakieleweki.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijaribu kuijikontrol ili nisiwaze kitu…
  • MY DIARY (23)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TATUTULIPOISHIA...Alinisihi sana nisitoe niilee na yeye atatoa huduma zote lakini tuendelee kufanya siri ili tusije tukahatarisha ndoa yake na kusababisha familia yake kuyumba. Kwa kweli sikuweza maana ilikuwa ni kujipa tabu mimi na huyo mtoto atakayezaliwa. Bora ataa ingekuwa ni mimba ya ule mwalimu ambaye hajaoa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilitamani nimchomekee hiyo mimba…
  • MY DIARY (22)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILITULIPOISHIA...Alitumia vizuri umbo lake la kimiss kutembea kimiss na kuweka mapozi ya maana. Na baada hapo alilala kwenye kile kigodoro na akachojoa vyote isipokuwa kufuli jeupe ambalo nalo alipewa hapo hapo kwa ajili ya kazi hiyo. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi sikumpa nafasi Joyce niliingilia nafasi yake na kuchukua ule uume wa bandia nikamfuta yule dada.…
  • MY DIARY (21)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJATULIPOISHIA...Nilichomeka simu chaji na kuiweka hewani ili nione kama kutakuwa na sms yeyote iliyoingia.Hofu ilizidi kunitawala na wakati naendela kufikira simu yangu iliita niakzani labda ni Joyce na nilipoiangalia nilimkuta ni Msouth. Sikutaka kuipokea nikaiacha iite mpaka ikate yenyewe.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nikajiuliza kwani amepatwa na nini usiku huo mpaka…

Nyumba ya Wachawi (2)

Mtunzi: Denis Benard

SEHEMU YA PILI
TULIPOISHIA...
Kitu kile kilimfanya ageuke nyuma,Alipogeuka nyuma hakuamini maana alikutana na lile kundi la wale watu,kumbe muda ule hakuondoka na badala yale walifika mbele na kurudi huku wakimfatilia ili wajue lengo lake nini katika msitu ule.

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
(Alitetemeka sana pale)

‘’Sasa wakubwa mimi nimefanya nini ?mbona mnanifatili?’’aliuliza huku haja ndogo ikimtoka.

Wenyewe walibaki wakimshangaa tu huku wasimjibu kitu chochote,

‘’Mkuu embu ongea tumfanye nini huyu?’’mmoja aliuliza

Mkuu wao hakumjibu kitu na badala yake alimsogelea huku yule jamaa akirudi nyuma na alipomkaribia alimpuliza kama karatasi akajikuta akipeperuka angani na baada ya dakika mbili alijikuta akitokea kwao,Alijishangaa sana maana hakuamini yale yaliyotokea kule na hayo aliyofanyiwa,hicho ndicho kilichompa hofu sana na wakati akijishangaa alisikia sauti ikimueleza.

‘’Sikiliza wewe!leo umepona ila onyo kwako,uliyoyaona huku usimueleze mtu yeyote,tena sikiliza!Usimueleze mtu yeyote!!, sina mengi ila ni matumaini yangu umenielewa,huwasirudii mara mbili,sasa ukitaka kuona kitu gani nitafanya katika maisha yako,wewe fanya hivyo”Mara baada ya muda ile sauti ilikata katika masikio yake.

Kutokana na Sauti ile,ilimfanya aanze kukuna masikio yake,maana hakuelewa maana yake nini na ndipo alipoamua kutoka nje ya nyumba yao ili ajichanganye na watu walau apunguze mawazo yaliyokua katika kichwa chake.Wakati anatoka nje alianza kusikia sauti za watu wakilia,sauti zile zilimfanya aanze kua na wasiwasi sana maana hakujua nini sababu za watu hao kulia na ndipo aliposogea kwa watu waliokua karibu na maeneo ya nyumbani kwao ili awaulize kulikoni.

(Kwa shauku kubwa aliuliza)

‘’Enhe jamani za samahani nasikia kuna watu wanalia,wapi huko ??’’huyo kijana aliuliza

‘’Tulia dogo Elly,wenzio wanapofika maeneo yoyote kabla hawajaanza kuongea chochote,huwa wanasalimia ,kua na heshima mdogo wangu”mtu mmoja aliongea,Kutokana na majibu yale yalimkata usemi kidogo hasijue kitu gani cha kujibu .

(Kwa sura ya upole alijibu)

‘’Samahani sana kaka,si unajua maisha na kuchanganyikiwa, naomba unisamehe sana , Shikamoo !”alijibu Elly

(Huku akitabasamu mtu yule aliongea)

‘’Hayo ndio maneno mdogo wangu , sasa hapa ndio tunaweza kuongea sasa , Huko kwenye msiba ni kwao rafiki yako “alijibu yule mtu.

(Kwa sura ya mshangao ,Elly aliongea)

‘’Kwao rafiki yangu ? , Rafiki yangu gani huyo ?’’aliuliza Elly

‘’Usijifanye hujui bhana ,’’ aliongea yule mtu

‘’Kweli tena kaka , ni nani?’’ aliongea Elly

‘’Inawezekana hajui, wewe mueleze tu”alidakia mtu mwingine aliyekuwepo maeneo yale. Wakati huo maongezi yale yakiendelea, Mwili wa Elly ulikua ukizidi kupanda joto kwa kasi sana.

‘’ Ni hivi punguza presha , mama yake na rafiki yako Faluu amefariki dunia kwa kuchomwa na moto katika nyumba yake na watu wasio julikana kwa kisingizio cha uchawi’’ yule mtu aliongea.

(Kwa mshtuko mkubwa sana Elly aliongea)

‘’ Unasemaje wewe? Mama yake…! Na Faluu..! kafariki dunia kwa kuchomwa na moto, inawezekana vipi ?’’aliongea Elly

‘’Ndio hivyo bhana ! ‘’ alijibu yule mtu pale.

Kutokana na presha upande wa Elly kupanda , nguvu zilimuishia na pale pale alianguka na kupoteza fahamu…………..

Machozi ya Elly yaliwafanya watu wote watulie na kubaki wakimuangalia yeye, kwa maana aliwashangaza sana na kila mtu alijikuta akiwa na maswali sana katika ufahamu wake,ya kwanini Elly analia?

‘’Elly mwanagu mbona hatukuelewi?kulikoni?’’ mama mmoja alimuuliza.

‘’Mmmh, hamna mama’’ alijibu Elly huku akifuta machozi

‘’Hapana mwanangu unatuongopea sisi wakubwa wako au awepo mama yako? ,mbona unaonekana kama kuna kitu kinaendelea katika mawazo yako?’’aliongea yule mama.

Wakati akitaka kujibu,alitokea  mama yake pale, Elly alijikuta akisimama na kumfata mama yake mlangoni alipokua anaingia huku akilia…

‘’Mama yangu hapana! Mama mmh! Mama hapana!’’aliongea Elly huku akilia sana baada ya kumuona mama yake.

‘’Mwanangu kulikoni?mbona sikuelewi?nini kinaendelea? Nini kimekusibu mwanangu,embu niambie mwanangu’’ aliongea mama yake.

Wakati huo Elly akiwa anaongea na mama yake kitendo cha yeye kulia na kuanza kuongea yale maneno,kilifanya wale watu waliokua mle katika chumba alichokuwepo Elly kuzidi kupata wasiwasi maana walishindwa kumuelewa Elly nini anachokimaanisha..

‘’Elly embu ongea chochote basi unajua hapa tulipo unatupandisha presha tu’’aliongea yule kaka aliyekuwa amempeleka hospitali.. Lakini Elly aliishia kumuangalia tu huku akilia.

‘’Elly baba si uongee tu mwanangu ,embu sema chochote basi tunakusikiliza’’aliongea mama yake.

‘’Mama na ndugu zangu wote hapa.. mmh…’’aliongea Elly huku akitaka kuwaeleza nini kinachoendelea, lakini ghafla ilimjia ile sauti ya yule mtu kule porini

 ‘’Sikiliza wewe!leo umepona ila onyo kwako,uliyoyaona huku usimueleze mtu yeyote,tena sikiliza!Usimueleze mtu yeyote!!, sina mengi ila ni matumaini yangu umenielewa,huwasirudii mara mbili,sasa ukitaka kuona kitu gani nitafanya katika maisha yako,wewe fanya hivyo’’

Maneno haya yalimfanya ashindwe kuendelea kuongea nini alichotaka kuongea, watu walibaki wakimshangaa nay eye akiwashangaa..

‘’ Ndugu yetu mbona huongei sasa na sisi tunakusikiliza wewe hapo’’ aliongea mtu mmoja

‘’Ni kweli Elly embu sema kitu basi,ndugu zako tunakusikiliza ‘’alidakia mtu mwingine pale

‘’Mwanangu vipi mbona huongei sasa? Embu ongea mama yako na kusikiliza, sema kitu baba yangu’’ aliongea mama yake.

Katika kipindi chote hicho Elly hakuwajibu kitu chochote  zaidi ya kugeuka kwa kila mtu aliyekua anaongea wakati huo. Baada kama ya dakika 5 hivi alikuja yule muuguzi pale..

‘’Jamani saa hizi nafikiri mgonjwa wenu yuko salama, mnaweza kuondoka nae na ninaomba mpunguze sauti kidogo maana kuna wagonjwa wengine wamelala humu ndani’’ aliongea yule muuguzi.

‘’Sawa daktari asante sana kwa matibabu ya mtu wetu’’ aliongea yule kaka.

Baada ya yote hayo hakuwa na jinsi ilibidi waondoke pale hospitali na kuelekea nyumbani huku wakiwa wanataka sana kujua nini anachofikiria Ellyn a baada ya hapo watu wengine walipungua na kuelekea msibani na wengine walifatana kwao Elly huku wakiwa wanamuuliza maswali ya hapa na pale lakini ilikua ngumu sana kwa Elly kuyajibu.

Siku ile ilipita huku wakiwa bado hawajazika kwa lengo la kumsubiri mwanae Faluu ambaye walikua wakijua ameelekea shambani,lakini pia kutokana na hali iliyokua ikiendelea walianza kupata wasiwasi sana,siku ya tatu Elly alimuuliza mama yake..

‘’Mama hivi sababu ya kutokuzika mwili wa mama,mama yake Faluu ni nini?’’

‘’Wanamsubiri Faluu arudi,maana watu walisema alienda shambani’’ mama yake Elly alijibu.

Baada ya Elly kusikia hivyo,alijikuta akilia sana na asiwe na kitu chochote cha kuongea..

‘’Wewe Elly mwanangu,ndio nini sasa?mbona unalia?kuna nini kinaendeleaa?’’aliongea mama yake Elly

‘’Mama samahani naomba uniitie Mwenyekiti na wajumbe wakijiji’’aliongea Elly

‘’Mwenyekiti? Na wajumbe? Kuna nini?’’ aliuliza  mama

‘’Wewe naomba uniitie tu mama yangu’’ Aliongea Elly huku akilia tena kwa sauti saana na watu waliokua wakipita nje ya nyumba yao walikua wakisikia na kujikuta wakiingia ndani..

Nakutokana na majibu hayo,ilibidi mama awaite mwenyekiti na wajumbe wa kijiji ili waje kusikia  nini wanchoitiwa.Bila kuchelewa walifika pale ilikusikia sababu ya kuitwa,kulikua na watu wengi sana nyumbani kwa akina Elly..

‘’Enhe Elly tunakusikia kijana ..’’aliongea Mwenyekiti

‘’Mwenyekiti na ndugu zangu hapa,samahani sana kwa kuwapotezea muda ,nilichowaitia hapa nataka kuwaeleza wapi aliko Faluu’’aliongea Elly

(Watu kwa mshangaoo)

“Aaaaah,aliko Faluu!!!!’’

‘’Ndio ,juzi wakati natoka shambani juzi nilimkuta amelala barabarani,huku akiwa amepoteza fahamu, nilimuamsha lakini cha ajabu aliposhtuka alianza kutaja Mama! Mama! Mama! Na baadae akakimbia,nilimshangaa sana’’

“Enhe!ikawaje”aliongea Mwenyekiti.

‘’Nilimshangaa sana na baadae nikaendeleaa na safari yangu kuja huku nyumbani,nilipotembea mbele kidogo nikasikia sauti ya mtu anasema Wachawi! Wachawi            ! wachawi !,mimi nikatulia kufatilia sauti baada ya kusikia kwa makini ilikua nisauti ya Faluu,sikujua watu waliokua wamembeba na baadae ile sauti ilianza kupotelea Porini nikaanza kuifata’’aliongea Elly

‘’Mmh! Enhe! Ndio ikawaje?’’aliongea mwenyekiti.

‘’Baada ya kuingia porini kufika sehemu nikakutana na watu,wale watu sura zao zilikua ngeni sana katika macho yangu,tulipishana huku mimi nikiwa namtafuta Faluu,baada ya kumuita kwa muda mrefu nilisikia sauti yake ikiitika,lakini cha ajabu wakati nikifuatilia kule sauti ilikokua ikitokea nageuka nyuma nikakutana uso kwa uso na wale watu’’

“weeeeeee’’ watu walijibu

“enhe!! Ikawaje?’’aliongea Mwenyekiti

‘’wakaniambia Sikiliza wewe!leo umepona ila onyo kwako,uliyoyaona huku usimueleze mtu yeyote,tena sikiliza!Usimueleze mtu yeyote!!, sina mengi ila ni matumaini yangu umenielewa,huwasirudii mara mbili,sasa ukitaka kuona kitu gani nitafanya katika maisha yako,wewe fanya hivyo, na baadae yule mkubwa wao akanipulizia upepo nikajikuta natokea hapa nyumbani’’

Watu baada ya kusikia hivyo walishangaa na wengine walianza kulia, kwa maana mambo yale yalikua ni mapya kwao…

‘’Unaweza ukalikumbuka hilo pori ulilokuwepo?’’mwenyekiti alimuuliza Elly

‘’Ndio nalikumbuka sana’’Elly alijibu

‘’Basi jamani akina baba wote naomba mjiandae tuingie msituni’’aliongea Mwenyekiti………

Baada ya maneno mazuri kutoka kwa M/kiti,wanakijiji waliokuwepo katika eneo lile walitawanyika ili wakajiandae na kazi iliyokuwepo mbele yao kama Mwenyekiti alivyowaeleza.Kulitokea na minong’ono ya hapa na pale kutoka kwa wanakijiji wale huku kila mmoja wengine wakielekea katika eneo la msiba na wengine wakielekea majumbani kwao.Kwa namna moja ilikua ni udhuni sana kwa namna moja kutokana na tukio ambalo lilikua limemtokea kwa  Faluu.

‘’Sasa ,hivi tutakuta yule motto ni mzima kweli??,mbona kama mimi nakuwa na wasiwasi sana?’’ Mama mmoja alikua akimuuliza mwenzie,huku wakiwa wanaelekea katika msiba.

‘’Hata mimi Napata shida kidogo katika hili jambo,lakini kuna msemo unasema

(Hakuna kitu kinachopotea katika haki,huenda akakutwa ni mzima’’ yule mama mwingine alijibu

(Huku akivuta pumzi kwa nguvu,yule mama aliongea)

‘’Aaaaaaah,labda bwana,lakini Mungu atamsaidia’’

Waliendelea na maongezi yao na baada ya muda walifika msibani na taratibu nyingine ziliendelea pale katika msiba.

Baada ya Elly kubaki pale nyumbani kwao,alijikuta akipokea maswali mengi sana kutoka kwa watu waliokuwepo eneo la nyumba yao,wakitaka kujua zaidi nini na nini kiliendelea pale na namna alivyoathirika.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
61 Nyumba ya Wachawi Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni