Mtunzi: Denis Benard
SEHEMU YA TISA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
‘’Swali langu la kwanza,hapa wakati tunaongea mara ya kwanza upepo ulikuja paa ikaezuliwa na mvua ikanyesha na mpaka sasa juu kuko wazi na vitu vyetu vimelowa tunaishije? Na swali la pili siku ya kwanza nilipouliza kuhusu ndugu zangu hapa uliniambia wamesafiri na muda si mrefu watarudi,mbona sikuelewi?’’Faluu aliuliza.
(Mjomba alicheka )
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
‘’Kwanza kwa swala la mvua lisikupe shaka japo umelowa na vitu vimelowa,wakubwa walikuwa wamechukia,ila kwa kuwa umenieleza wewe mwenyewe utashuhudia kitakachojiri na kuhusu ndugu zako,sitapenda tena uniulize hilo swali katika kipindi chote tutakacho kuwa wote hapa nyumbani sawa’’ Mjomba aliongea na kuondoka.
Wakati mjomba akiondoka,lile paa liliokuwa limeezuliwa na upepo lilirudi na katika nyumba ya akina Faluu na mazingira yote yakawa kawaida kama zamani,kipindi hicho Faluu alikuwa na mawazo hasa kuhusu lile swali alililomuuliza juu ya ndugu zake pale nyumbani na alipokuja kutazama juu alishangaa kuona paa ya nyumba yao na kila kitu kiko sawa.Hali ile ilimstahajabisha sana na kujikuta akichunguza chunguza ili ajue imerudi rudi vipi pamoja na mabadiriko ya mule ndani.Muda wa kulala ulifika,wakati akiwa katika usingizi mzito alianza kusikia sauti kama mtu akiunguruma,sauti hiyo ilimfanya kukosa usingizi na hivyo ikabidi aamke.Wakati akiwa ameamka alianza kuifata na kuisikia vizuri ile sauti iliyokuwa ikiunguruma,Wakati akiwa ametoka katika chumba chake alishtuka baada ya kuona jitu kubwa sana likiwa ilinakula nyama huku likiwa limetapakaa damu,Faluu aliogopa sana nakushindwa kuvumilia na hivyo kujikuta akipiga kelele..
‘’Mama…mama…mama…’’
Lile jitu liligeuka huku likiwa limebeba ile nyama kwa bahati mbaya kumbe ile nyama ilikuwa nyama ya mtu na wakati akigeuka aliona vizuri kichwa cha yule aliyekuwa analiwa,kumbe alikuwa ni mjomba wake Faluu,Faluu alivuta pumzi huku nguvu zikiwa zimemuishia..
‘’Haaaaaaaaa,kumbe ni mjomba wangu…’’ aliongea Faluu aliongea
Baada ya zile kelele za Faluu na lile jitu la kutisha kumsikia,lilianza kumfuata Faluu huku Faluu alijikuta akishindwa kukimbia kutokana na namna alivyokuwa.Lile jitu liliendelea kumsogelea mpaka lilimkaribia ,ghafla likiwa linataka kumbeba alitokea mama yake Faluu nakupambana na lile jitu na baada ya kulishinda lilikimbia na kumuacha Faluu na mama yake pale huku mule ndani kukiwa kumetapakaa damu iliyotokana na kifo cha mjomba wake Faluu.Faluu na mama yake walijaa na simanzi sana.
‘’Sasa mama ni aina gani ya maisha ambayo mimi naishi katika hii nyumba? Na nitaendelea kuishi hapa mpaka lini mama yangu?’’ Faluu alimuuliza mama yake.
‘’Naujua ugumu unaopitia mwanangu,lakini hii ndio njia yako ya ushindi na ndiyo sehemu pekee itakayo kufanya wewe kuwa huru”mama aliongea.
‘’Ndio sehemu pekee itakayo nifanya mimi kuwa huru? Uhuru gani huo wakati mimi Napata shida? Kwanza ona hadi mjomba wangu kafariki?”aliongea Faluu huku akiwa analia.
‘’Mambo yote unayoyazungumza huko sahihi,lakini pia inabidi uwemwangarifu na mvumilivu maana ndivyo mafanikio yanavyohitaji na pia naomba usijifananishe wewe na mjomba wako sawa, maana kati yenu hamtembei katika njia moja’’mama aliongea.
‘’Kwani mama,embu naomba uniambie,kwanini mjomba amefanyiwa kitu hiki kibaya na kwa namna hii? Mtu analiwa kama ndege?’’ Faluu alimuuliza mama yake..
‘’Inaonekana mjomba wako hakuwaandalia hawa viumbe chakula chao,kwa hiyo limeamua kumla yeye mwenyewe’’ mama aliongea
‘’Daaah,inamaana mimi ndio chanzo cha haya?maisha gani haya sasa jamani!! Hapana “Faluu alijikuta akifikiria
‘’Mbona unashangaa sasa?”mama aliongea
‘’Hamna mama niko sawa tu”Faluu alijibu
Waliongea kwa muda mrefu na baadaye walijikuta wote wakiangaliana,baada ya kusogea mbele ya eneo walilokuwepo walijikuta wakiwa wakipigwa na butwaa baada ya kuona vipande vya nyama nyama kama kichwa na miguu ya mjomba wake Faluu yaliyoachwa na lile jitu lililokuwa likimla,Walianza kukusanya kusanya vipande vile huku Faluu akiwa anajaribu kujizuia kulia wakati tukio lile likiendelea,ila kutokana na simanzi aliyokuwa alijikuta akishindwa kujizuia kutoa sauti na hivyo akajikuta akipaza sauti yake..
‘’Mjoma wangu…ndio nini sasa mjomba”Alilia Faluu
‘’Shiiiiiiiiiiiiiiiiii,acha kutoa sauti bhana,hivi hujui kama saa hizi ni usiku’’Aliongea mama yake.
Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa Faluu maana japokuwa mama yake alikuwepo pale lakini alijikuta akihukosa uwepo wa mjomba wake pale nyumbani..
Kumbe kutokana na sauti ile aliyoitoa Faluu majirani wa karibu walimsikia na hivyo kuwafanya wasogee karibu ili wajue kinachoendeleaa,walipofika pale nje walianza kugonga kwa nguvu,huku Faluu na mama yake walibaki wanaangaliana..
‘’Embu nenda kawaone’’Mama aliongea.
‘’Mmmh,Sawa mama’’alijibu Faluu na baadaye alielekea Mlangoni kwaajili ya kuwaona hao watu waliokuwa wanagonga mlango.Alipofika mlangoni alijikuta akipigwa na butwaa baada ya kuwaona wale watu aliowakuta pale mlangoni kwa maana walikuwa ni wazee sana na hivyo kujikuta akitaka akukimbia lakini alipojaribu kufunga mlango ili akimbilie ndani,mlango ulikuwa mgumu kufunga na hivyo wale waliingia ndani..
‘’Kulikoni mbona unataka kufunga mlango,halafu kama unawasiwasi sana ?”Bibi mmoja alimuuliza.
‘’Aaah,hamna…..!’’Faluu alijibu huku akijilazimisha kutabasamu..
‘’Hamna nini?wakati unaonekana kama macho yako yapo juu juu?” bibi mwingine aliongea kwa makazo sana.
Muda huo ambao walikua wakijibizana ilikuwa saa kumi(10) alfajiri,
‘’Enhee!embu tuambie kulikoni mbona tumesikia sauti kama unalalamika?kulikoni ndugu yetu na mjomba wako yuko wapi?”Faluu aliulizwa..
Baada ya Faluu kusikia hivyo,alijikuta akishindwa kujibu chochote na badala yake alijikuta machozi yakimtoka huku akishindwa kujizuia..
‘’M..mmh…mmh,haaaaaa’’Faluu alikua akiunguruma tu bila kuwa na jibu.
Kutokana na hali aliyokuwa akionesha Faluu wale wazee walijikuta wakimtolea macho na kujikuta wakishindwa kumuelewa kile anachokimaanisha na hivyo kupelekea kukimbilia ndani kwa kasi ili wakajue nini kinampelekea Faluu kuwa katika hali ile.Walipofika mule ndani na kuiona ile hali ya mazingira walijikuta wakifurahi na kupeana pongezi..
‘’Safi sana!kumbe ndiyo haya yanayoendelea”aliongea mtu mmoja.
‘’Ndio hata mimi ndio nakumbuka,binafsi nilikua nasubiri kwa hamu sana swala hili,sasa tunafanyaje?”mzee mmoja alikuwa akiwauliza wenzie na katika kipindi hicho Faluu alikuwa akiwatazama tu..
‘’Huyu mototo tunaondoka naye leo,hatumuachi!!”alijibu mzee na muda huo walianza kuondoka naye huku Faluu akigoma…
Baada ya hapo waliondoka naye huku wakivutana,maana Faluu hakuwa tayari kutoka pale nyumbani,hivyo alijikuta akimuita mama yake..
‘’Mama!,mama yangu..! mama huko wapi sasa mama yangu?”Faluu aliita huku akiwa analia
Baada ya wale watu kumsikia analia huku anamwita mama yake,walianza kumcheka hadi wengine alikuwa wananguka chini kwa kukosa nguvu kutokana vicheko vyao..
‘’Muone huyu motto,mpuuzi kweli,eti mama..mama…mama yangu huko’’aliongea mmoja kwa kejeli huku akiibana pua yake.
‘’Hata mimi namshangaa sana huyu kijana,inamaana hajui kama mama yake alishafariki kweli?et wewe kijana au unauita mzimu?hahahahhah’’aliongea na mwishoni alicheka sana.
Kipindi chote hicho walikuwa wakitoka nje ya hiyo nyumba kutokana na ukubwa wa uzio wa nyumba hiyo,walichukua muda sana kutoka nje huku wakiendelea na maneno yao ya kashfa.Wakati wakiendelea na maneno yao,katikati yao alikuwepo kijana mmoja ambaye alikuwa ametulia na hakuwa anaongea kitu chochote wakati mengine yakiendeleaa.Wakati wakiwa wanaelekea getini ili watoke nje alijitokeza mbele yao na kuongea maneno..
‘’Embu muacheni kijana wa watu aende kwao,msimuumize kabisa’’aliongea huyo kijana.
‘’Wewe ni nani? Na unaongea kama nani? Wewe ni mfanyakazi tu hapa’’ mzee mmoja aliuliza.
‘’Mimi ndio nasema muacheni huyo kijana wa watu aondoke tena sasa hivi kabla sijakasirika’’aliongea tena yule kijana .
‘’Hahahahhaha, eti tena sasa hivi kabla sijakasirika’’ aliongea mzee mwingine huku akiwa anamsogelea yule kijana. Wakati akiwa anamsogelea yule kijana,yule kijana alianza kucheka sauti Fulani ya kutisha na watu wote walishtuka na kubaki wakimtazama,huku wakijaribu kujihami.
‘’Wewe umekuaje?”mzee mmoja alimuuliza.
Katika kipindi chote walichokuwa wakimuuliza, Yule kijana alikuwa akiendelea kucheka huku na ghafla katika mwili wa yule kijana alitokea mama yake Faluu na kuyaanzisha mashambulizi pale paleBaada ya kupambana sana,mama yake Faluu alifanikisha kumuua mzee mmoja pale na kwakuwa ndio kulikuwa kuna kucha ,wengine waliobaki walikimbia na kumuacha mwenzao akiwa amelala pale huku akiwa amekufa.Faluu alijikuta akitetemeka sana baada ya kuyaona yale yaliyotendeka pale .
‘’Mama sasa hii nini mama yangu?” Faluu alimuuliza mama yake.
‘’Kwani wewe unaona nini?mbona unakuwa na maswali ya ajabu?”mama alimueleza mwanawe huku akiwa ametapakaa damu katika mwili wake.Baada ya yote alianza kumla yule mtu aliye fariki.Lile swala lilianza kumuogopesha Faluu.
“Aaaah,mama sasa hiyo nini?si mtu huyo?mbona unafanya hivyo?acha bhana”Faluu alimwambia mama yake.Mama aligeuka na kumuangalia Faluu kwa macho Fulani ya kutisha,hali ambayo ilimpelekea Faluu kuogopa na kisha mama alicheka na katika mazingira yasiyotarajiwa alipotea na ule mwili wa marehemu.Ilikuwa ni siku ya historia kwa Faluu kwani hakuyategemea mambo yote yaliyotokea usiku kucha na hivyo kumpelekea kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu palepale.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi