Nyumba ya Wachawi (8)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mtunzi: Denis Benard
SEHEMU YA NANE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
‘’Huko sawa wakati mimi nikikuona tu kuna vitu naviona katika uso wako kama unavicha ?sasa sikiliza mimi mjomba wako nakupenda sana na sipendi yatokee mambo mabaya kwako sawa kua makini’’aliongea mjomba na baadae aliondoka
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
(Faluu alistaajabu sana na kumuuliza mjomba maswali)
‘’Sasa mjomba unamaanisha nini?mbona sikuelewi?” aliongea Faluu ,mjomba hakumjibu chochote na badala yake aliendelea na safari yake .Faluu alifanya shughuli zilizo muhusu pale na ilipofika usiku kama kawaida yake alitamani sana kuenda kushuhudia,lakini kila alipoyakumbuka maneno ya mjomba aliogopa sana.Zilipita siku mbili akiwa amesahau kila kitu kilichotokea siku wakati akiwa njiani anakwenda sokoni kununua mahitaji alikutana na yule aliyonana naye siku ile(Joyc),alishtuka sana kumuona na alijikuta mapigo ya moyo yakibadirika na yule binti alipomuona alimsogelea ili amuulize kitu,lakini kila alipomsogelea Faluu,Faluu alirudi nyuma akiwa ataki kua karibu kabisa na yule dada.
‘’Samahani kaka mbona kama sikuelewi’’Joyc aliongea
‘’Mmh,mimi sitaki usogee’’aliongea Faluu,neno lile lilimshangaza sana Joyc,wakati anarudi nyuma bila kuangalia nyuma yake kulikua na shimo kumbwa la taka lililokua limechimbwa pembezoni ya barabara,Joyc alipoliona alishtuka na kupiga kelele
‘’HAPANAAAAAAA……’’
Faluu alipokuja kugeuka alimkuta mtu akiwa anafanana kabisa na yule dada(Joyc)akiwa amesimama katika hilo shimo na kumsaidia Faluu,Faluu alipomuona alijikuta akimtolea macho tu…….
Faluu alijikuta akiangukia katika mikono ya huyo mtu aliyekua amesimama katika shimo lililokua nyuma yake na alipomuona yule na kumuona akiwa amefanana na Joyc akili yake iliishia na mawazo yake yaliishia kumuangalia tu na kutokua na jibu au neno lolote la kumueleza na mwishowe alijikuta kichwa chake kikizunguka mara amuone huyu aliyekua katika shimo na alipogeuka upande wa pili alikutana na Joyc wa ukweli akimshangaa.Joyc alijikuta akiwa na mawazo na kumshangaa Faluu.
‘’Lakini lile nyuma yake ni shimo lile,sasa inakuaje ameganda pale tena katika na hakuna kitu chochote kinachoendelea kibaya juu yake? Wewe Faluu wewe!!’’ Joyc aliongea.
Faluu alishtuka na kumuangalia na alionekana kuonesha sura ya uwoga sana na alipogeuka nyuma kumuangalia huyu mtu aliyekua amesimama upande wa shimo alikuta kapotea katika mazingira ya kutatanisha sana,alishtuka na kujikuta anakimbia kwa kasi kutoka katika eneo lile huku akipiga kelele.
‘’Mama!mama! mama!’’ Faluu aliongea huku akiwa anakimbia..
‘’Huyu naye vipi mbona kama simuelewi?’’ Joyc alijiongelea huku akimfuata kwa nyuma na kila Faluu alipogeuka na kumuangalia Joyc akimfuata alipiga kelele kwa nguvu sana…
‘’Mama! Mama! Mama !yangu nakufa!!!’’Faluu aliendelea kupiga kelele.
Kipindi chote hicho Joyc hakuchoka aliendelea kumfuata kwa nyuma ili ajue kilichomfanya amkimbie na kumuogopa yeye.Watu waliokutana nao barabarani walibaki wakiwashangaa na kutokana mwendo aliokua nao Faluu hakuna hata mmoja aliyebahatika kuongea naye,wakati Joyc akimfuata kwa nyuma watu walimsimamisha nakumuuliza kulikoni..
‘’Wewe Joyc vipi dada?, huku kijana si ndiye anayekaa kwa baba mtaa wa pili’’mama mmoja alimuuliza.
(Huku akipumua kwa nguvu)Joyc alisema
‘’Daah! Sijui hata niseme nini,lakini ndiye huyo huyo’’
‘’Sasa kimemkuta nini mpaka anakimbia hivyo??’’Yule mama aliendelea kumuuliza.
‘’Aaah,hata mimi sijui mama yangu,tulikutana tu barabarani,sasa aliponiona akaogopa sana na kuanza kurudi nyuma,ilikua ni karibu na lile shimo la mzee Kyopo,alipokua akitaka kudondoka katika lile shimo nilipiga kelele na alipogeuka ndiyo yakatokea haya unayoyaona’’aliongea Joyc.
‘’Mmmh, au huyo anayekaa naye ameshafanya yake nini?maana achelewi’’aliongea yule mama.
‘’Unamaana gani kusema hivyo?” Joyc aliuliza
‘’Wewe ni mototo haya hayakuhusu sawa’’aliongea yule mama na baadaye aliondoka na kumuacha Joyc palepale hakiwa na watu wengine.Joyc alibaki akimshangaa tu wakati akiondoka.
‘’Sasa anamaana gani kuongea hivyo kama anajua mimi ni mototo mdogo?wakina mama wengine bhana’’Joyc alikua akifikiria katika mawazo yake na baadaye aliamua kuishia hapo kumfatilia Faluu na kurudi nyumbani.
Kutokana na hayo yaliyomtokea,Faluu hakufanikisha kitu chochote kati ya vile alivyoagizwa na mjomba wake avifanye na hivyo kumpelekea kuogopa.Alipofika kwao alikimbilia ndani nakujificha katika chumba chake. Muda huo ilikua ni saa sita mchana, Wakati akiwa ndani amefunga mlango na madirisha akiwa hataki kitu chochote kibaya kimkute,Mwanga mweupe ulitokea katika chumba kile alichokuwamo Faluu na alipouona alianza kulia…
‘’Hiiii..,hiiii..,hiiiii… sasa nyie watu,sijui mzimu hata siwaelewi kabisa,nini lengo lenu katika maisha yangu??mbona mnanitesa?’’aliongea Faluu huku akilia.Baada ya kuongea hakuna sauti yoyote iliyomjibu na badala yake alianza kuhisi kama kuna mtu amemshika bega lake la kushoto. Kitendo kile kilimfanya awe na hamu ya kutaka kugeuke nyuma ili aone nini kinaendelea katika bega lake na ni nani huyo,lakini pia kuna mawazo mengine yalimjia kuwa asigeuke,ili asikutane na yakukutana,lakini kipindi hicho alikua akihisi kama maisha yake ndiyo yamefikia mwisho.Wakati akiwa katika mgongano wa mawazo ghafla alisikia sauti ikimueleza..
‘’Mwanangu mbona nimeshakueleza kuwa usiwe na shaka juu ya kila kitu kinachoendelea na nikakueleza tena kua mimi niko pamoja na wewe sasa mashaka yanatoka wapi?’’
Sauti hii ilimtoa hofu na kumfanya ageuke nyuma na alipogeuka alikutana uso kwa uso na mama yake huku akilia..
‘’Mama! kumbe ni wewe mama yangu’’ Faluu aliongea
‘’Ndiyo ni mimi mwanangu’’Mama alijibu
‘’Mwanao Napata shida sana mama yangu kama unavyoona,hii nyumba siielewi kabisa mama yangu,yanatokea mambo ya ajabu sana,ila ni matumaini yangu mambo yanayotokea kwangu unayaona’’aliongea Faluu
‘’Ni kweli mwanangu nayaona,ila sema inabidi uwe mvumilivu sana katika kuyashinda haya mambo sawa mwanangu’’aliongea mama
‘’Sawa mama nitajitahidi nifanye hivyo,lakini naomba nikuulize swali moja’’Faluu aliongea.
‘’Uliza tu mwanangu usiogope sawa’’Mama aliongea.
‘’Yule binti niliyekuwa naye kule karibu na lile shimo unamuonaje?’’ Faluu aliuliza
‘’Yule binti hana matatizo yoyote na wakati unamuona yule aliyekuwa katika shimo lile yeye alikuwa hamuoni,ulikuwa ukimuona wewe mwenyewe tu’’Mama aliongea
‘’Sasa itawezekana vipi hayo mambo mama yangu?’’ Faluu aliuliza.
‘’Ndiyo hivyo,ila sema ndoto yoyote utakayoota leo hakikisha unaimaliza mpaka mwisho maaana hiyo inaweza kuwa ukombozi wako sawa’’aliongea mama.
Waliongea muda mrefu sana na wakati wakiwa wakiendelea na maongezi yao,mjomba alirudi nyumbani na hivyo kumfanya mama aondoke pale ghafla huku Faluu akiwa bado anamaswali mengi katika kichwa chake ambayo yalikuwa yakihitaji majibu kutoka kwa mama.
‘’Mbona unaondoka wakati nikiwa nahitaji unijibu maswali yangu mama?’’ aliongea Faluu, japo maneno yake hayakuweza kumfanya mama arudi tena.
Mjomba alipoingia alianza kumtafuta Faluu huku na huku, akiwa anaita jina lake.Alipoingia katika chumba cha Faluu,Faluu alishtuka wakati huo mjomba akiwa anashangaa shangaa mule ndani..
‘’Mbona mazingira yanaonekana yako tofauti humu ndani?,ulikua na nani humu?’’ Mjomba aliuliza. Wakati akiuliza Faluu hakumjibu neno lolote,alibaki akimtazama tu.
‘’Unanitolea hayo macho eti,haya tangulia mbele huko twende’’ Faluu aliogopa na alipokua akitangulia mbele sauti ilisikika..
‘’Alikua na mimi hapa,kwani nini?’’…..
Walishtuka wote kwa pamoja na walipokuja kugeuka,walimkuta ni mama yake Faluu akiwa amesimama nyuma yao kumbe alikua hajaondoka muda ule.
‘’Kumbe ni wewe dada’’ Mjomba wake aliongea huku akitabasamu.
‘’Ndio ni mimi usikae unajichekesha hapa,cha msingi huyo ni mwanangu,sasa usilete michezo yako hapa’’mama yake Faluu aliongea na baadae alipotea katika yale mazingira.
‘’Ebu rudi hapa,hivi vile vitu nilivyokuagiza asubuhi umefanikisha?’’ Mjomba aliuliza.
Baada ya Faluu kusikia swali lile kutoka kwa mjomba alishtuka na kujikuta machozi yakimtoka kwani lilimkumbusha tukio lile lililotokea..
‘’Hapana mjomba sijafanya hata kitu kimoja kati ya yale uliyoniambia’’alijibu Faluu.
Baada ya mjomba kusikia vile,lile jibu la Faluu lilimkasirisha sana na kujikuta hali ya hewa ya mule ndani kubadirika na kwa mbali upepo ulianza kupuliza..
‘’Kwa maana hiyo unataka kusema leo hatuli siyo?’’Mjomba aliuliza huku macho yake yakiwa yamebadirika na kuwa mekundu.
Maneno ya mjomba yalifanya hali ya Faluu kuzidi kubadirika na nguvu zilimuisha na kutokana na upepo kuzidi paa ya nyumba yao iliezuliwa na eneo lile lilikua na baridi sana na muda mfupi baadaye mvua ilianza kunyesha katika nyumba yao tu Na kumuongezea hofu Faluu.
(Huku akiwa anatetemeka Faluu aliongea)
‘’Mjomba sasa haya yote yanamaana gani? Kwa maana mimi sikukusudia kabisa ‘’Faluu aliongea huku akiwa ananyeshewa na mvua tena mvua ya mawe.
‘’Unasema hukukusudia,unamaana gani kusema hivyo?’’ Mjomba alimuuliza Faluu.
‘’Mimi nimetoka asubuhi hapa nikawa naenda zangu sokoni kama ulivyoniagiza nifanye,wakati nikiwa njiani nilikutana na dada mmoja hivi,huyo dada namkumbuka alishawahi kunifanyia mambo ya ajabu,kwa hiyo baada ya kumuona niliogopa sana nikawa narudi nyuma,kumbe nyuma yangu kulikuwa na shimo kubwa sana na huyu dada wa niliyekuwa namkimbia aliliona nilipogeuka nyuma yangu nilikutana na dada mmoja uso kwa uso kama huyu niliyemkimbia mbele yangu akanisaidia nisidondokee katika lile shimo,ghafla nageuka tena sikumuona niliogopa sana ikabidi nikimbie nirudi nyumbani,kwa hiyo ndio hicho kilinichonikuta’’ Faluu aliongea.
‘’A aah,sawa kumbe ndiyo hivyo,basi haina tabu,lakini hawa wakubwa watakula nini??’’ Mjomba aliongea.
‘’Heee! Wakubwa ?? wakubwa gani tena’’aliuliza Faluu..
‘’Aaah,samahani wewe haya kuhusu’’alijibu mjomba huku akiondoka
‘
’Sasa mjomba mbona unaondoka’’aliongea Faluu huku akiwa anamshika mkono mjomba wake hasiondoke.
‘’Ndio kwani kuna nini?’’ Mjomba aliuliza.
‘’Naomba nikuulize kitu’’ Faluu aliongea
‘’Niulize tu usijali’’aliongea
‘’Swali langu la kwanza,hapa wakati tunaongea mara ya kwanza upepo ulikuja paa ikaezuliwa na mvua ikanyesha na mpaka sasa juu kuko wazi na vitu vyetu vimelowa tunaishije? Na swali la pili siku ya kwanza nilipouliza kuhusu ndugu zangu hapa uliniambia wamesafiri na muda si mrefu watarudi,mbona sikuelewi?’’Faluu aliuliza.
(Mjomba alicheka )
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni