Mtunzi: Maundu Mwingizi
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Simu ikaita kwa muda mrefu mpaka ikatakata bila ya kupokelewa, akajikuta anasonya peke yake ndani ya gari kama aliechanganyikiwa. Akawasha gari na kuweka ‘Gear’ ili aondoke ndipo sasa Simu yake ikaaita, akaitoa haraka na kuangalia ni nani aliekua akimpigia, alipomjua tu haraka akabonyeza kitufe cha kupokelea kisha akaweka simu sikioni na kuongea
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
“Hallow..”
“Niambie kaka, kwema?” ilikua ni sauti iliyojibu kutokea upande wa pili wa simu yake
“Kwema mzee, we nae hautulii kwako,” Alitania Suhail na kumfanya Msigwa nae acheke kwa sauti baada ya kuelewa kua rafiki yake alikua amewasili nyumbani kwake na hakumkuta nd’o maana anamtania kwa maneno yale
“Yaani we acha kaka utadhani miguu ilirambwa na Mbwa, haya niambie wapi hiyo?”
“Mimi nd’o natoka kwako hapa, nilikua nimekuja kwa ajili ya yale mazungumzo yetu, kama vipi niambe ulipo nikufuate”
“Mimi nd’o natoka Lamada Hotel, Ilala hapa”
“Basi usondoke nisubiri hapohapo nakuja sasa hivi,” Alijibu Suhail na kukata simu, haraka akaingiza gari barabarani kwa kasi ili amuwahi Lamada
*****
Meza nzuri ya duara iliyokerezwa vizuri kwa ubao imara wa mninga ilikua Imebeba vinywaji ghali huku ikiwa imevitenganisha viti viwili, Kimoja akiwa amekikalia Suhail na Kingine Msigwa huku wakitazamana baada kumaliza kusalimiana na kujuzana habari na mitikasi ya mjini, ilikua ni katika bustani ya maua iliyopo katika Hotel hiyo ya Lamada
“Kaka nimekuita ili niongee na wewe jambo moja la muhimu sana, jambo ambalo kwa muda mrefu sasa limekua likiyatesa maisha yangu na kunifanya nisione furaha ya maisha haya,” Suhail aliongea kwa utulivu mkubwa huku akimuangalia Msigwa usoni, Msigwa hakujibu chochote ikiwa ni ishara kwamba anaendelea kusikiliza kitu kilichomuamuru Suhail aendelee kuongea
“Kinachonitesa ni Siri nzito iliyokua moyoni mwangu, Siri ambayo niliamini kua sikupaswa kumwambia mtu yoyote nikihofia kua endapo itavuja nitapata tabu maana waswahili wanasema ‘Siri ni ya watu watatu endapo wawili kati yao wamefariki’ sasa kutokana na hali kua ngumu ikabidi niitoe Siri hiyo kwa mke wangu kipindi hicho tukiwa hatujafunga ndoa, haikusaidia kitu zaidi ya kuongeza matatizo ambayo sasa yananilazimu niitoe tena hiyo siri kwako wewe kama ndugu yangu na rafiki yangu wa karibu nikiamini kua wewe ndio msaada wangu wa pekee uliebaki.. Sasa kaka utaweza kuitunza siri yangu? Na je utaweza kunisaidia kweli?” Swali la Suhail lilimfanya Msigwa ashushe pumzi nzito sana kabla hajajibu
“Nina uwezo mkubwa sana wa kukaa na siri, hilo sina shaka nalo lakini hili la kukusaidia naogopa kulijibu haraka kwakua sijajua ni msaada wa aina gani uutakao, pia sijui kama utakua ndani ya uwezo wangu au Laa, ila ukweli utabaki palepale kua ni jukumu langu kukusaidia kama mtu wangu tuliotoka mbali sana”
“Sidhani kamamimi ninaweza kukuleta Mswada ambao najua hauwezi kuutekeleza, bila shaka unaweza kama utadhamiria”
“Haya tuendelee kaka, Lete maneno”
“Iko hivi kaka, We ni rafiki yangu wa kitambo tangu shule, tumeongea na kufanya mambo mengi kwa pamoja lako likiwa langu na langu likiwa lako. Je katika kipindi chote hicho ulishawahi kusikia kua nina mahusiano na msichana yoyote?”
“Ndio, ni Sharifa lakini uliniambia kua mlikubaliana kua msikutane kimwili mpaka mtakapooana”
“Sawa, sasa ile ilikua ni mbinu yangu tu ya uwongo kwa Sharifa lakini ukweli ni kwamba nilimkatalia tusifanye chochote kwakua nilikua nikijielewa hali yangu”
“Hali? Hali gani hiyo?”
“Kaka naomba unisitiri kwa hili, naumia moyoni kukueleza kua mimi ni Mbovu, siwezi kukutana na mwanamke na nimeshahangaika kwa wataalam kibao bila mafanikio”
“Eee bana eeh, pole sana kaka usikate tama unaweza kuja kupata mtaalamu na ukapona tu, sasa uliwezaje kuoa na kuishi na mkeo mpaka leo katika hali hiyo?,” aliuliza Msigwa kwa Fadhaa kubwa iliyomkumba
“Hilo sasa ndilo tatizo lililofanya nikutafute wewe kama jamaa yangu unifae na kunistiri aibu yangu hii..”
“Mnh, kivipi?”
“Mke wangu nilimueleza mapema hali yangu kabla sijamuoa akanikatalia katakata kuniamini, akataka mpaka kujiua akiamini kua nimepata mafanikio ndo nataka kumuacha kisanii, nilijaribu sana kumuelewesha akagoma, akaniambia nilazima tu tufunge ndoa kisha hayo mengine yataelewekea ndani ya Ndoa. Ilikua ngumu sana kumkubalia lakini mwishowe tukakubaliana kua tutafunga ndoa lakini wakati huo tutakua tunatafuta wataalamu, tukafanya hivyo baada ya Ndoa bila mafanikio sasa Mke wangu kawa kama mbogo aliejeruhisha, nyumba haikaliki, kelele ndo kelele, ugomvi kila siku mpaka sasa nimechoka mwishowe nikapitisha uamuzi wa kulitatua tatizo hili ila mtu pekee wa kulimaliza ni wewe?
“Kivipi sasa nilimalize mimi”
“Nahitaji ili mke wangu awe mtulivu ni lazima awe na mwanaume mwingine atakaekua anakidhi haja zake, Mwanaume huyo atatakiwa awe Muungwana, Msiri, Mstaarabu na makini katika kila nukta. Na kamwe sitakua na wivu wala usumbufu kwake kwakua mimi siwezi kutekeleza jambo hilo mwenyewe.. Mtu huyo mwenye sifa tajwa ni wewe kaka” Maneno hayo ya mwisho ya Suhail yalimshtua na kumshangaza sana Msigwa, hakika hakutegemea kabisa kukutana na jambo lile
“Suhail unasema?!,” Aliuliza Msigwa kwa Mshangao akiwa haamini alichokisikia
“Nadhani umenisikia vizuri kaka, naomba usiniangushe katika hali tafadhali” Msigwa alikaa kimya kwa Sekunde kadhaa kisha akaibuka
“Nisikilize kwa Makini Suhail, wewe ni rafiki yangu kama ndugu tu, nakupenda kama unipendavyo wewe lakini kwa hilo hapana, No! Siwezi kufanya huo upuuzi kamwe, hebu jaribu kujifikiria mara mbili yule ni mkeo iweje upange mipango hiyo ya ajabu kaka? Siwezi kukufanyia ushenzi na ukatili kiasi hicho.. haujafikiaubaya kiasi cha mimikukudhalilisha kwa kutembea na mkeo”
“Msigwa mbona unataka kupoteza uelewa ambao huo uko nao? Hakuna mke bila ya tendo kaka, pia ukumbuke ule sio kwamba ni ushenzi au ukatili utakaokua umenifanyia bali ni msaada mkubwa kwangu, utamfanya yule mwanamke atulie na kunipa heshma yangu katika jamii vinginevyo yakizidi ataweza hata kwenda kuwaambia wazazi wake na wangu kitu ambacho sitaki kamwe wakijue, nakuomba kaka nipo chini ya miguu yako unifae ndugu yangu”
“Hivi Suhail hata watu watakapojua si itakua aibu kubwa zaidi? Kwako, kwangu na kwa Sharifa mwenyewe!!.. na kwanini uogope wazazi kujua wakati wanaweza kua msaada kwa tatizo hili? Hata huyo Sharifa akijua kua nimekubali kufanya huo ujinga si atanishusha kabisa!,” aliongea kwa msisitizo Msigwa
“Sikiliza Msigwa katika vitu vilivyosababisha nikupendekeze wewe ni Usiri wako sasa nitashangaa utakaponiambia kua watu watajua, watajuaje sasa? Wakati mtakua huru wawili tu na nitawaacha muwe huru zaidi katika ile nyumba yangu ya Mbezi ambako hakuna waswahili kabisa, Pia Ondoa hofu kuhusu Sharifa nimekwishaongea nae kwa kina na akaridhia kabisa, na nilipokupendekeza wewe akawa hana pingamizi kwa kua ana kuamini kwa utulivu na umakini wako, hivyo kila kitu kipo tayari kaka,” Alidanganya Suhail lakini moyoni alijua kabisa kua hakua ameongea chochote na Mkewe
“Sikia kaka, kumbuka ni masiku kadhaa tu yaliyopita nimeachana na mke wangu, na ninatuhumiwa sana kwa kumuacha japokua ushahidi wa meseji ulionekana katika simu yake mwenyewe kua anafanya uchafu sasa hauoni kama ikija kuvuja nitaonekana nilimuacha mke wangu ili nipate kutimiza mambo haya?”
Ilichukua muda mrefu sana marafiki hawa wakiendelea kuwekeana hoja juu ya hoja lakini Msigwa aliendelea kukataa kabisa ikabidi sasa Suhail atumie nguvu ya pesa zake akimuahidi Msigwa kwamba atakua akimlipa pesa kama shukrani kwa kazi hiyo, na kwakua Msigwa anapenda sana pesa kiasi cha kujiongezea maadui maishani mwake akaanza kulegea japo hakuonesha kwa haraka hali ile
“Sasa kaka, naomba uende uniache nifikirie kwa kina jambo hili kwakua ni zito sana na ukizingatia umenishtukiza mno, kisha tutakaa tena siku nyingine tuzungumze zaidi,” Alimaliza mjadala kwa mtindo huo bwana Msigwa
“Ok poa kaka, ila nakusihi naomba usiniagushe wangu”
“Usijali kaka tutalipanga na kulifikisha mpaka mwisho”
Wakafikia muafaka na kupanga siku ya kuongea tena jambo hilo, Moyoni alianza kufurahi kuona Msigwa ameshalegea..
Lakini laiti kama angejua kinachojiri asingethubutu!!
*****
Siku hiyo alirudi mapema zaidi nyumbani tofauti na kawaida yake, mara nyingi hujichelewesha kurudi nyumbani mapema akihofia kukwazana na mkewe, Lengo kuu la kurudi mapema nyumbani ni kuongea na mkewe juu ya mpango wake alioubuni na ambao tayari ameshamdokeza muhusika namba mbili ambae ni Msigwa, na sasa ilikua ni zamu ya muhusika namba moja ambae ni Sharifa.
Siku hiyo nyumba ilikua kimya kama vile hakuna mtu alipofika getini akafunguliwa Mlango na Mlinzi akaingiza gari na kuiegesha sehemu yake kisha akaingia ndani akiwa na Shauku ya kuanzisha mazungumzo na mkewe japo bila shaka aliuona ugumu wa kuiwasilisha hoja yake. Alipofika ndani alipokelewa na Msaidizi wao wa kazi za ndani aliekua akinyoosha nguo zake, baada ya kupokelewa mizigo akaenda moja kwa moja mpaka ilipo ‘Seating room’ yake akamkuta Mkewe ameketi sofani akiangalia ‘Movie’ hizi za Kibongo, Akamsalimia
“Haujambo mamaa?”
“Sijambo,” alijibu Sharifa huku akiendelea kuangalia zake Tamthilia, Suhail akapitiliza zake chumbani akiwa hajua aanzie wapi.
Dakika ishirini baadae akatoka mpaka pale barazani akiwa amevaa fulana nyepesi ya rangi nyeupe na Bukta yake akamuita mkewe kisha akarejea chumbani akifutiwa na mkewe,
“Mke wangu nimekuita ili tujadili mustakabal wa Ndoa yetu, naona hali hii ya ugomvi na migogoro kila siku haifai kabisa hivyo nadhani tujadili suala la muhimu, tujikite zaidi katika kutafuta ufumbuzi na si mizozo ya kila siku,” Alianza kuongea Suhail baada ya kuwa wameshaingia chumbani na kuketi juu ya kitanda
“Ufumbuzi ndo kitu ninachokililia kila siku, lakini mwenzangu haujali”
“Mke wangu yatupasa kutafuta njia sahihi zinazowezekana kwa sasa, na si hizi ambazo zinaonesha kushindwa kufanya kazi kabisa”
“Zimeshindwaje kufanya kazi? Hautaki kwenda kwa wataalam kutafuta tiba, hautaki kuwashirikisha wakubwa watusaidie, sasa utajuaje kama jitihada zimeshindwa kuzaa matunda?”
“Mimi sihitaji tugombane mke wangu, nahitaji amani ya nafsi na familia nzima hivyo naomba na wewe uwe na dhamira kama yangu”
“Haya embu sema wewe unatakaje?”
“Hilo ndilo la msingi sasa..” Aliongea Suhail huku akijiweka sawa pale kitandani, huku akiyapanga maneno kabla hajayatoa kinywani “..Mke wangu mimi katika pitapita zangu huko kwa wataalam wa afya nikitafuta tiba ya matatizo yangu haya japo we unaona kama vile sijishughulishi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi