Vita vya Mapenzi (20)

0

SEHEMU YA ISHIRINI
TULIPOISHIA...
hata yeye alishangaa sana akaniambia kutakua kuna jambo tu hapo limejificha, hakuamini nilichomwambia kwakua simu inayonasibishwa na tukio hilo alikua nayo yeye.

akampigia simu Msigwa wakaongea kidogo tu lakini hawakuelewana ghafla wakaanza kujibizana vibaya na kutoleana maneno machafu

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
Sikufichi shemeji Nililia usiku kucha kama mwendawazimu lakini haikufaa kitu, rafiki yako aliendelea kusimamia maamuzi yake, Sikuondoka nikalala hapohapo nyumbani mpaka asubuhi ya leo ambapo wakaja dada zake, nao wakanitokomeza kwa maneno machafu kua ninajaza tu choo cha kaka yao nimekalia umalaya ndo maana nashindwa kuzaa, Msigwa akaniambia ameniacha rasmi, akanifungashia mabegi yangu akaniambia niondoke..

Nikampigia simu kaka akaniambia niondoke niende nyumbani kwa Shangazi hapo Ilala ila yeye yupo njiani anakuja Dar karibia afike” alipofikia hapo tena Specy akashindwa kujizuia akaanza kulia tena kwa uchungu huku akiingiza mkono katika pochi yake, akatoa Simu yake hiyo iliyoleta majanga ya ajabu na kuifungua katika sehemu ya meseji. akamuonesha Suhail zile meseji zinazoonesha kua alikua akiwasiliana na Msonjo..

Meseji ya kwanza ilikua ni ya Specy akimtumia Msonjo siku ya jumanne saa tisa mchana, ilisema hivi;

‘Sasa mpenzi fanya basi kesho tuonane tukale raha zetu, nimeli-Miss penzi lako tamu na la nguvu ulilonipa ile w’End.’

Meseji ya pili ilikua ni ya Msonjo akimjibu Specy, ilisema hivi;

‘Mnh tusije tukakamatwa bure, kwani huyo bwege wako hayupo?’

Meseji ya tatu ilikua ni ya Specy ikionesha amejibu hivi;

‘Wala usijali Honey, yule Pimbi hayupo amesafiri tangu jumamosi amekwenda Dodoma hivyo tutakua huru na kufanya tutakavyo, hata ukitaka uje kwangu poa tu’

Meseji ya mwisho ilikua ni ya Msonjo akijibu hivi;

‘Mnh kwako hapana, basi poa kesho saa tano tukutane Ilala pale Paradise Lodge’

Suhail alisoma meseji zile tata na kubaki mdomo wazi asijue aseme nini, kila alichokifikiria kilimgomea kichwani, mkasa ulikua ni waajabu na kushangaza

“Au baada ya kaka yako kuizima simu kuna mtu aliiwasha tena ndo akawa anajibizana na huyo kijana?,” Aliuliza Suhail

“Hapana, simu yangu hua ina ‘Security code’ hivyo baada ya kaka kuizima isingewezekana tena mtu mwingine yoyote kuiwasha, hata kaka mwenyewe asingeweza tena, na kaka anasema alipoizima aliifungia ndani ya kabati yake na ndo maana hata yeye amekalipinga suala hilo, Pia nilimpigia simu mtu wa tiGo aliyopo kwenye ‘systerm’ aniangalizie kama namba yangu iliwashwa saa ngapi tangu ilipozimwa siku ya jumanne, akaniambia haikuwashwa mpaka kufikia hiyo jana jioni ambapo alieiwasha alikua ni Msigwa” Suhail alichoka kabisa akajikuta ameyasahau mpaka yaliyokua yakimpeleka huko kwa Msigwa, akakohoa kidogo kisha akamwambia Specy kua inabidi waende kuongea na Msigwa ili wayamalize mambo hayo, japo Specy aligoma kabisa lakini Suhail alimbembeleza mpaka akakubali, na hivi alikua akiipenda Ndoa yake akakubali kishingo upande

Suhail akawasha gari na kuanza kuondoka eneo hilo huku kichwa chake kikiwa kimevurugwa kabisa na mkasa ule

****

Dakika kama kumi na tano tu akawa ameshawasili nyumbani kwa Msigwa akiwa yuko na Specyoza katika Gari yake, lengo lake likiwa ni kutafuta Suluhu baina ya Wanandoa hawa kwani pamoja na kwamba hakupenda waachane kwa tukio lenye utata kama lile lakini pia hata shida yake yeye iliyokua ikimpeleka kwa Msigwa ingependeza zaidi kama Msigwa angeitekeleza akiwa katika Ndoa yake. Specy alitaka kugoma kushuka ndani ya Gari lakini Suhail akambembeleza mpaka akakubali, wakashuka wote na kuanza kuelekea kule katika mlango mkubwa wa kuingilia ndani, hapohapo Msigwa akatoka huku akifuatiwa na dada yake, Msigwa hakua yule aliezoeleka siku zote, alikua ni kama Sheikh alielishwa nguruwe, hasira zilionekana kumjaa usoni, alipofika tu akawazua kwa mbali Suhail na Specy

“Kaka Suhail nakuheshimu sana ndugu yangu sitaki tuachane vibaya, naomba usiingie ndani mwangu na huyu mzoga, mwanamke Malaya mchafu sijapata kuona,” aliongea Msigwa mpaka povu likafurumia mdomoni

“Kaka tafadhali Shusha jazba kidogo tuongee, kumbuka mimi ni ndugu yako na nina haki ya kuongea na wewe katika kuwekana sawa, haupaswi kutoa maneno mach..” Kabla Suhail hajamalizia akakatizwa na dada yake na Msigwa aliekua ameshatoka nae nje na kusimama pale uani

“Kaka Suhail hebu haya mambo ungeyaacha kama yalivyo, Laiti ungeujua uchafu aliokua akiufanya huyu mbwa kwa kaka yetu sidhani kama hata ungekubali kuipakia hiyo najisi katika gari lako, Mtoe nje, Mtoe bana anatuletea kichefuchefu” Wakati dada yule akiendelea kutoa maneno ya kinyama na kishenzi huku akisaidiana na Msigwa mwenyewe, muda huo palikua na gari nyingine imewasili na kuegesha jirani na ilipokua imeegeshwa gari ya Suhail, mlango wa Gari hiyo aina ya Rangerover iliyokua imejaa vumbi ukafunguliwa akashuka Mwanaume mmoja asiefanana sana na gari ile kwa jinsi alivyokua amevaa.

Alikua amevaa kaptura ya jinzi, shati la draftidrafti, na miguuni amevaa Kandambili huku mkononi akiirusharusha funguo ya gari. Mtu huyu hakua Mzee wala kijana sana, alikua ni mtu wa rika la kati, kichwani kwa mbali alikua kama ana mchirizi wa Mvi uliokua ukianza kuukaribisha utu uzima, Ni bonge mwenye mwili uliojaziajazia ‘nyama uzembe’. Suhail hakumjua kwa haraka kua ni nani lakini alihisi kua Msigwa na Specyoza walimjua maana walishtuka sana kumuona. Mtu yule alikwenda kwa kasi mpaka pale uani ambapo Ngonjera ya maneno machafu na ya kebehi yalikua yakiendelea

“Wewe nilikuambia uende wapi?,” aliuliza mtu yule huku akimtazama Specy kwa hasira kidogo

“Kwa Shangazi”

“Sasa bado uko hapa unafanya nini? Au unaona raha unavyodhalilishwa na kuadhiriwa kama usiekua na kwenu?”

“Hapana kaka, nilikua nimekwishaondoka ndipo nikakutana na huyu hapa kaka hua ni rafiki wa karibu sana na Msigwa, nikamsimulia ilivyokua nd’o akaniambia turudi mpaka hapa aje aongee na Msigwa” Hapo ndipo Suhail akapata picha kua huyo mtu ndie kaka yake na Specy aliekua njiani anatokea Morogoro, aligundua hivyo kwakua Specy alikwisha mdokeza kua kaka yake wa Morogoro amemuambia aende kwa Shangazi yake na yeye yuko njiani anakuja Dar

“Aje aongee nini na mtu aliedhamiria kukufukuza?” Swali la bwana mkubwa yule safari hii halikupata nafasi ya kujibiwa na Specy kwani tayari Msigwa alitiririsha maneno

“Bwana Shemeji kwahiyo wewe unafurahia umalaya anaoufanya mdogo wako? Au na wewe unahusika? Au ulitaka nimuache tu hapa aendelee kufanya ukahaba wake ili mwishowe aje aniue kwa magonjwa Kisa ulinisaidia kupata kazi.”

“Msigwa unasema mimi nahusika na huu upuuzi wako? Sikiliza nikuambie kijana mimi kwanza sio shemeji yako tena kwakua umesema umeshamuacha mdogo wangu pili ukae ukijua mpango wako haramu ulioufanya umekosea njia nitaugundua tu, simu ya Specy haijahusika kufanya uovu wowote, hilo nina uhakika nalo asilimia zote kwakua nilikua nayo mimi, nimetafakari mara mbili na nimeshapata jibu kua hapa kuna mchezo unachezwa na nitaujua tu, Mimi ni Mtoto wa mjinikuliko wewe Bwa’mdogo nitakufuatilia mpaka mwisho na nitatekeleza wajibu wangu juu yako.

Wewe si ni mchafuzi katika vyombo vya habari eeeh! Haya Sasa kanichafue na mimi, umemdhalilisha Specy na umeidhalilisha familia nzima kwa huu mchezo wa ajabu uliotokea.. tutaoneshana, Specy twende tuondoke,” alimaliza kuongea bwana mkubwa yule akamchukua Specy na kuondoka nae, ikabidi Suhail akawafungulie mlango wa gari yake ili Specy atoe mabegi, walipomaliza tu Specy na kaka yake wakaingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi ya ajabu.. Lilikua ni tukio la aina yake.

Suhail akarejea mpaka pale waliposimama Msigwa na dada yake wakiwa kimya, Kilichomshangaza zaidi Suhail ni ile hali ya kutahayari iliyoonekana katika sura ya Msigwa, yaani ni kama vile anaejutia jambo Fulani lakini anajizuia kuionesha hali hiyo waziwazi,

“Kaka mimi nikuache kwanza upumzishe kichwa, nilikua nina shida kubwa iliyonileta kwako lakini kwa hali hii nimejikuta nimeambulia kazi ya ziada ambayo sikuifikiria kabisa,” aliongea Suhail baada ya kumsogelea Msigwa

“Oooh, No usijali kaka ni mambo ya kawaida tu, sidhani kama kuna haja ya kuchanganywa na ushenzi wa mtu mmoja. Kama ni jambo zito tukae tu tuongee,” alijibu Msigwa na kuzidi kuacha maswali mengi kichwani mwa Suhail

‘Hivi kweli umemfumania mkeo unaweza kua katika hali ya kawaida kama hii, unataka tuongee tu kilichoonileta! Mnh’ Mawazo yaliyokua katika mtindo maswali yalipita kichwani mwa Suhail huku akimuangalia Msigwa

Suhail hakuweza kuongea Mengi, akamuaga rafiki yake na kumuahidi kua angerejea tena siku nyingine kwa ajili ya mazungumzo yaliyompeleka pale, Baada ya hapo akaondoka zake na kurejea nyumbani kwake kupambana na Mchaka mchaka wa mkewe Sharifa..

*****

IKAPITA karibu mwezi mzima bila ya Suhail kuonana na Msigwa huku Suhail akiwa ameshakata shauri kua hapaswi tena kumtaka msaada jamaa yake huyo kwakua kwa sasa hana mke tena, aliamini kua zoezi lake lingetekelezeka vizuri endapo Msigwa angeendelea kua ni Mume wa Mtu, wakawa sasa wanapowasiliana wanajadiliana mambo mengine tu ikiwemo tatizo la Ndoa ya Msigwa, hapakua na jipya Msigwa alijiamini kufuatia ushahidi wa Meseji alioufumania katika simu ya mkewe hivyo aliendelea kuuamini msimamo wake.

Lakini sasa kutokana na ukweli kwamba haikua kazi rahisi kumpata mtu mwingine mwenye vigezo alivyovikusudia, akajikuta sasa anaanza kurejesha maamuzi ya kuongea na Msigwa japo aliiona harufu ya hatari ikimnyemelea lakini akapiga moyo konde akaamua kufanya kile alichodhani ni maamuzi ya kiume. Akaamua kumtafuta Msigwa ili sasa amfikishie ya moyoni, Hakua na haja ya kurefusha muda kwakua alikua Kariakoo katika moja ya ofisi zake akaiona haja ya kwenda haraka Magomeni kwa jamaa yake, akaingia ndani ya gari yake ndogo aina ya ‘Solano vheik’ na safari ya kwenda Magomeni ikaanza..

Japo ilimchukua muda mrefu njiani kutokana na msongamano wa magari barabarani lakini hatimae aliwasili. Bahati haikua yake kwani hakumkuta jamaa yake, wadogo zake wakamwambia kua aliondoka muda mrefu sana hivyo nae akaamua tu kuondoka, lakini kabla hajaondoka akatoa simu ili ampigie ajue ni wapi alipo ili kama kuna uwezekano aweze kumfuata, Hakutaka kulaza damu!

Simu ikaita kwa muda mrefu mpaka ikatakata bila ya kupokelewa, akajikuta anasonya peke yake ndani ya gari kama aliechanganyikiwa. Akawasha gari na kuweka ‘Gear’ ili aondoke ndipo sasa Simu yake ikaaita, akaitoa haraka na kuangalia ni nani aliekua akimpigia, alipomjua tu haraka akabonyeza kitufe cha kupokelea kisha akaweka simu sikioni na kuongea

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)