Mtunzi: Maundu Mwingizi
SEHEMU YA AROBAINI NA NNE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Haraka Ustadh akaukimbilia mlango na kuufunga kwa funguo kisha kuiweka funguo kwenye mfuko wa kanzu yake,
Hakuna mtu kutoka!
Vidume wale wakachakazana sana mpaka wakaishiwa nguvu
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Ikawa sasa hawana hata uwezo wa kusogeleana zaidi ya kutazamana kama majogoo tu! Lakini hali ya Mzee Sufian nd’o ilikuwa mbaya zaidi kuloko Takadir… Ghafla Komandoo Takadir akageuza macho yake na kuliangalia Bakuli lile lenye damu likiwa katika pembe ya nyumba ile, Akaangua kicheko cha nguvu na kusema “Suhail wewe ni mjinga sana, unatoa kafara ya damu ya mbuzi badala ya damu ya Mama au Baba yako..
Tazama sasa hatimaye leo unashuhudia kifo cha Sufian na kisha utashuhudia kifo chako mwenyewe kabla ya mimi kurejea budha leo hii nikiwa na Pete yao” Mzee Kusekwa na Mkewe wakatazamana kusikia damu yao nd’o ilipaswa kutumika kama kafara ya Pete ile ya ajabu, Familia nzima ikatazamana huku kila mmoja akiwa amebarizi kivyake kwa hofu na mashaka, ndipo tena wakamshuhudia komandoo akilisogelea Bakuli ili aichukuwe Pete, Suhail akiwa aliyejawa na woga akajikuta akikimbilia pembeni kumpisha Komandoo aliyekuwa akijongea kwa shida na tabu kutokana na mchoko wa mpamba
“NOOO SUHAIL, USIMRUHUSU ACHUKUWE PETE,” Alilalama Mzee Sufian akiwa hajiwezi kwa N’de wala Sikio, Suhail alimtupia jicho tu na kumpotezea kama hakumsikia,
Wakati sasa Komandoo Takadir amelifika bakuli lenye damu, aliachia tabasamu na kuingiza mkono wake ndani ya bakuli hilo, Suhail naye alikuwa amesimama jirani na meza ambayo juu yake kuna lile bakuli la maziwa, akaingiza mkono wake ndani ya bakuli lile huku akimtupia jicho Ustadh Chaullah aliyempiga ukope akimuashiria kufanya jambo fulani
Ghafla tabasamu la Takadir likayeyuka na nafasi yake kuchukuliwa na simanzi iliyochanganyika na hofu, akamgeukia Suhail na kumkuta akimalizia kuivaa Pete yake.. Kumbe pete haikuwa kwenye lile bakuli la damu kama ambavyo Takadar alidhani na badala yake iliwekwa kwenye bakuli la maziwa ikiwa ni hila na mpango kabambe uliosukwa na Ustadh Chaullah! Kuna siri kubwa ndani ya maziwa, Siri ya kiafya na kitabibu, hivyo siri hiyo ilipotumika kitaalam ilimfanya hata Takadir na ukomandoo wake wa kijini aamini kuwa ndani ya bakuli lenye damu ndipo ilipo Pete..
Sasa kabla Komandoo hajafanya lolote tayari Suhail alikwisha kibenjua kile kidubwasha cha maangamizi kilicho nyuma ya Pete ile na kumwelekezea Takadir palepale alipo, Ikatoka miale ya ajabu, miale ya moto iliyochanganyika rangi nyekundu, kijani, na nyeusi.. Ulisikika ukulele mkali kutoka kwa Komando Takadir mpaka hofu ikamjaa kila mmoja aliyekuwa akishuhudia tukio lile
Komandoo Takadr Al-Harabi alipatwa na maumivu yaliyochanganyika na ghadhabu zilizomtuma kumsogelea Suhail na kumuangamiza, lakini alikwishachelewa, hakupata nafasi ya kusogea japo hatua tatu, akateketea mpaka akabaki jivu tu.. Huo nd’o ukawa mwisho wake! hakuna aliyeamini.
Suhail akamkimbia Ustadh na kumkumbatia kwa faraja!
Wakati zoezi hilo linakamilika ndipo sasa Macho ya Mzee Sufian yakagongana na yale ya Fungameza aliyekuwa akimtazama muda mrefu
“Bwana Fungameza!” Aliita kwa mshangao wa hali ya juu Mzee Sufiani na kuacha taharuki ya aina yake,
“Sufiani? Ni wewe ama naota?” Mzee Fungameza alihoji akiwa haamini
“Ndiye mimi kaka, najuta kwa yote niliyokufanyia.. nisamehe sana.”
“Amaa kweli Malipo ni duniani akhera yaenda hesabu tu.. Leo umedhalilika mbele yangu, Yule mtu uliyenikarahisha, ukanidhalilisha na kuniahidi kuwa hakuna atakayekuweza wewe! hatimaye umewezekana… Haya Amanda yuko wapi?”
“Ni mkasa mrefu sana uliotokea kaka, ila kwa kifupi ni bora hata ningekuachia tu Amanda wako maana kuwa naye ndiko kulikonishusha kabisa hadhi yangu mpaka leo kuwa hivi.. na hatimaye naye akauawa kinyama na kiumbe huyo mshenzi aliyeteketea hapo sasa hivi.. ila nilibahatika kupata naye mtoto mmoja ambaye ndiye huyo Shekhia.”
“Khaaa! Amanda amekufa?.. Na huyu binti naye ni mtoto mwingine wa Amanda? Hii sasa ni aibu ya mwaka! Fedheha.. ila nilimkanya Amanda kuwa asipapatike na fedha za mtu asiyemjuwa lakini akanipuuza, hakujuwa kama anakikimbilia kifo, laity angejua anajiingiza katika mahusiano na Jini pengine angenisikiliza.. sasa maji yameshamwagika! Wanasema asiyesikia la mkuu, huvunjika guu!”
Kikapita kimya cha muda mfupi kabla ya Ustadh Chaullah kutupa swali
“Kwani mnajuana ninyi?” Ustadh alivunja hamu ya kila mmoja ya kutaka kujuwa endapo wanafahamiana vipi,
“..Ndio, tena sana tu! Enzi za uhai wa ujana wangu nilipata kuishi na mwanamke fulani aliyeitwa Amanda.. nilijidanganya kuwa tunapendana kumbe nilipenda peke yangu.. Nilijidanganya hivyo kwa jinsi mwanamke yule mrembo wa kipindi kile alivyowakataa wanaume wengi na kuangukia mikononi mwangu na hatimaye tukaishi pamoja na tujaaliwa mtoto wa kike ambaye ndiye huyu Sharifa.”
“Mungu wangu! Ina maana Shekhia na Sharifa ni ndugu? tena wa mama mmoja!” Aliropoka Suhail bila ya kutegemea, mara akaishiwa nguvu na kujikuta anaporomoka juu ya kochi kama kiroba…
Aibu iliyoje kwa kila Baba, Mama, Kaka, Dada, nk kushuhudia ndugu wawili wa mama mmoja kuwa ni wake wa mwanaume mmoja! halafu mnakuja kugundua hilo mkiwa nyote mu wajawazito!
Kilio kikazuka upya, kilio cha maumivu na fedheha!
Ustadh akawatuliza na kumtaka Mzee Fungameza aendelee kutoa kumbukumbu zake za muhimu
Ndani ya ofisi ya waziri wa ulinzi walisheheni vigogo wa Nchi hii, Alikuwepo Mhe waziri mkuu mwenyewe, Waziri wa fedha, IGP, Waziri wa ulinzi, Waziri wa nishati na madini, Kamanda wa Polisi kanda maalum, Naibu waziri wa fedha, Waziri wa mabo ya Nje, na Mkurugenzi wa usalama wa taifa. Pia walikuwepo maofisa wawili vijana wa Usalama wa taifa! Wote waliketi kwa kuizunguka meza moja ndefu iliyo katikati yao huku kila mmoja akiweka amekumbatia vitendea kazi vyao.. mwenye simu, mwenye laptop, nk
“Awali ya yote poleni kwa majukumu, na kwa usumbufu wa kuwaiteni ghafla japo yote ni katika majukumu ya kulijenga taifa..” Alianza kufungua kikaorasmi Mhe Waziri Mkuu “..Kikubwa kilichotujumisha hapa ni kuhusu usalama wa Nchi yetu, kufuatia uchaguzi mkuu ambao uko jirani kabisa kumezuka vikundi na mitandao ya wasaka uraisi ambao hufanya hila chafu na ikibidi hata hudiriki kuuwa ili tu kujiweka katika mstari mzuri wa ushindi..
Sasa kufuatia hali hiyo mambo yamekuwa makubwa inabidi sisi tulioitana humu, ambao tunaaminiana, tushirikiane kuwang’amua na kuwashughulikia wauuzi hawa wachache..” Wakati waziri mkuu akiendelea kutiririka, Mkurugenzi wa Usalama wa taifa Bwana Mlenda alikuwa akiwatembezea macho waheshimiwa wote ikiwa ni katika mbinu zake za kumgundua mhalifu
“…Kuna mtandao mmoja mkubwa unajiita Black Scopion umefikia hatua ya kuwashirikisha mpaka wauaji wa kukodisha kutoka nje na mitambo haramu ya Divier kwa ajili ya kufanikisha azma yao.. tumefanikiwa kumkamata muuwaji wao aitwaye Joram Ndege..” Neno Joram Ndege lilipokelewa kwa hofu na mashaka karibu na kila mmoja wao japo kwa namna tofauti..
Haraka Mkurugenzi wa usalama wa taifa Bwana Mlenda alishakibaini kitu kutoka kwa Mhe Sostenes Mitti(Waziri wa fedha)“… Ila kwa bahati mbaya pamoja na kumtesa sana awataje wenziwe hakukubali mpaka akatufia mikononi,” Alidanganya hapo Mhe Waziri Mkuu kama alivyoelekezwa na Bwana Mlenda ambaye muda huo sasa alikisoma kitu kingine katika macho ya Mhe Fortunatus Mwita(Waziri wa Nishati na Madini)..”
“Katika Laptop yake tumefanikiwa tu kujua hilo jina la kikundi chao na malengo yao ya kuukwaa uongozi kwa njia haram, tukagundua jinsi walivyomuuwa Yule mwanahabari baada ya kutofautiana naye, tukagundua kuhusu huo mtambo wenye kubumba meseji na kung’amua mawasiliano ya watu wengine kupitia simu zao..
Zaidi ya hapo mambo mengine yote yaliandikwa kwa mtindo wa kijasusi sana, kitu kilichozidi kututilia ugumu wa kuwajua wahusika na eneo ulipohifadhiwa mtambo huo.. mathalani hao viongozi wao wanajiita 5051-10s na 42&2c na kwamba siri zote zimo katika Laptop zao..Sasa hii kama taarifa tumeona tuwashirikishe nyote kutokana na umuhimu wenu ili kila mmoja atowe maoni yake.” Alihitimisha Mhe Waziri Mkuu na kuwatazama wajumbe wa kikao kwa macho ya kuhitaji kusikia chochote kutoka kwao
“Hili si jambo dogo.. ni jambo zito na bay asana hivyo si la kukurupuka, yatupasa tupate muda wa kutosha kila mmoja alichunguze ili tutakaporejea hapa kwa mara ya pili tuwe na pa kuanzia…” Aliongea Mhe Mitti, na kudakiwa na IGP “Mimi sikubaliani sana na Mhe Mitti japo ameongea kitu cha maana sana kuwa tunahitaji muda, ila inabidi kwa kupitia ushauri na maoni yetu hapo huenda ikawa ni mwanzo mzuri wa kuwajua hao mabazazi”
“Naogopa kuongea mengi kwa kuwa hata humu hatujafahamiana huenda ukakuta hao wahusika hata humu yumo mmoja wao hivyo naomba kushauri kitu hapa.. tuhakikishiane kuwa humu hakuna hata mmoja wao ndipo tuendelee,” Aliongea bwana Mlenda huku akipepesa macho yake kwa wajumbe alioanza kuwashitukia
“Tutahakikishiana vipi sasa? Kwa kutamka tu? Hiyo itakuwa Ngumu mtu kujitaja” Alijibu waziri mkuu na kuzua mjadala mpana mle ofisini
Mjadala ulichukuwa muda mrefu kidogo kabla ya Suluhu kupita kwamba.. kama yupo mwenye uwezo wa kung’amua majina yale ya mficho asaidie kabla hawajapambana.. Ndipo kijana mmoja kati ya wale wawili wa usalama wa taifa waliohudhuria akapita mbele na kuomba kutoa utaalum na uzoefu wake katika majina hayo ya mficho.. akaruhusiwa! Akavuta kijiubao kidogo kilichokuwa pembeni, akachukua na kalamu maalum ya kuandikia akaanza kuyanyambua majina yale
*****
“…Basi Sharifa akiwa bado mdogo ndipo huyu Sufian alipoibuka na kunipokonya mwanamke Yule niliyemjali na kumthamini, Pesa za Sufiani zikamhadaa Amanda, nilijaribu kupambana na Sufian nikiamini kuwa nitamshinda lakini kumbe nilikuwa natwanga maji kwenye kinu.. nikakumbana na madhila mazito mpaka nikanyoosha mikono, na sikuwaona tena mpaka leo hii..” Aliendelea kuongea Mzee Fungameza, huku mara kwa mara akitulia kidogo kupisha dukuduku lililomkaba kooni lipite maana angeendelea kuongea angevujisha machozi, kitu ambacho hakutaka kukiruhusu mbele ya wanawake, Akaendelea “…Kilichoniuma mimi ni jinsi nilivyopoteza muda wangu kwa Amanda..
Amanda aliingia Nchini kama mfanyabiashara lakini kiukweli hakuwa na dhamira ya biashara bali alikuja kumtafuta nduguye aliyezaliwa naye pacha! Nduguye huyo alipata kuniambia jina lake aliitwa Nadege Ndatabaye, kama ambavyo yeye aliitwa Amanda Ndatabaye.. tukiwa bado tuko katika jitihada za kumsaka huyo nduguye ndipo akapata ujauzito, ikamlazimu kusitisha kwanza biashara zake mpaka alipojifungua akiwa chini yangu kwa kila jambo, ndipo sasa alipoibuka huyu Suf..”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi