Mtunzi: Maundu Mwingizi
SEHEMU YA SITA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Lakini hali ilikuwa tofauti kwa Suhail Kusekwa ambaye nae aliwasili siku hiyo katika mji huo wa kihistoria kwa ajili ya kazi moja tu, kazi ya hiari iliyo ya lazima, nayo ni kumtafuta Shekhia mtoto wa mzee Shamhurish, japokuwa hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika Bagamoyo lakini hakuwa na hamu hata kidogo ya kutalii kwani akili yake ilikuwa imeshavurugwa na ndoto ya ajabu aliyoiota jana yake, Ndoto yenye dalili zote za kuashiria ujumbe wa kweli uliomfikia.
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Swali kubwa lililojenga kambi kichwani mwake ni Je wapi atampata Shekhia, na Je ni Shekhia Yule anaemjua yeye? Hakuwa na pakuanzia ukizingatia hakuwahi kufika Bagamoyo kabla ya siku hiyo,
Baada ya kuwasili katika stendi ya mabasi ya hapo Bagamoyo akitokea jijini Dar es Salaam, alianza kutoka nje ya stendi hiyo taratibu kama vile ni mwenyeji. Wakati akiendelea kutembea akielekea nje ya lango la kuingilia stendi hapo alikumbana na ghasia za hapa na pale kutoka kwa baadhi ya madereva wa Bodaboda kila mmoja akijitafutia riziki, Suhail hakushughulika nao akaendelea kutembea mpaka alipofika nje kabisa akawa anaendelea kuangalia mandhari ya Bagamoyo ambayo amekua akiyasikia tu na kuyasoma kwenye vitabu. Alipomaliza kuyaridhisha macho yake ndipo sasa akamuita kijana mmoja dereva wa bodaboda aliyekuwa amepaki upande wa pili wa barabara, na ndani ya dakika moja kijana Yule akawa ameshafunga breki mbele ya Suhail
“Mambo vipi afisa?,” alisalimia kijana Yule kwa ucheshi
“Poa kaka, Eee bana nataka unipeleke sokoni mara moja.”
“Hakuna noma ka’Mkubwa, ni sokoni palepale au?”
“Yeah ni hapo hapo sokoni” Akajibu Suhail huku akikaa katika pikipiki ile, nae dereva bila ajizi akapeleka kidole chake katika ‘stata’ na kuibofya, akatia ‘gia’ na safari ikaanza. Wakiwa njiani Suhail alikuwa akiangalia mazingira mazuri ya mji ule mpaka akajikuta anasahau shida zake, alijaribu kua anamuuliza maswali kijana Yule aliembeba ili azidi kuyafahamu mazingira ya mji ule lakini hakupata nafasi ya kengine itamrahisishia safari yake na kazi ya kumsaka Shekhia
“Kaka wewe ndie wa magomeni?,” aliuliza Suhail huku akimuangalia kijana Yule anaemuuzia mikufu
“Ndio mkubwa”
“Na mimi ni wa Ilala nadhani tuko karibukaribu” Jibu hilo la Suhail likawafanya vijana wale wote waangue kicheko kabla ya Yule kijana hajamfahamisha tena Suhail
“Iko hivi kaka hapa Bagamoyo pia kuna pahala panaitwa Magomeni wanapotoka watoto wa Kiswahili, hatuna maana ya magomeni hiyo ya Dar” Suhail ikabidi nae acheke tu, akajua kua amejichanganya, akaachana nao vijana wale baada ya kununua vidani viwili, akatoka mpaka nje ya soko akiwa sasa amepata mwanga kidogo akamuita tena dereva mwinginewa bodaboda akamtaka ampeleke sehemu inayoitwa Magomeni, haikua mbali sana kutokea pale sokoni, ni mwendo kama wa kilometa mbili tu akawa ameshafika, akateremka na kumlipa mwenye bodaboda kisha akaanza kutembea kwa miguu taratibu huku akitafutauelekeo. Baada ya mwendo wa muda mrefu akiendelea kutembea tu akatokea kwenye nyumba moja akawakuta wasichana kama watatu hivi wameketi katika kibaraza cha nyumba hiyo huku mmoja akimsuka mwenzie na mwingine aliekua amejifunga kilemba cha njano akiwapigisha stori tu wenzie, akawasogelea na kuwasalimu
“Wapendwa Asalamu alaykum”
“Waalyakum salaam,” wakaitika wote kwa pamoja kabla ya Yule msichana anaemsuka mwenzie kumkaribisha
“Karibu kaka”
“Haya nimeshakaribia, jamani mimi shida yangu maji ya kunywa tu”
“Wala usijali kaka yangu labda kama una jingine” dada yule msusi akamuagiza Yule mwenzao aingie ndani akamchotee maji Suhail, wakati anainuka Yule msichana kuendea maji ndipo Suhail akachombeza neon hapohapo
“Pia naomba niwaulize jamani”
“Uliza tu kaka”
“Mimi natokea Dar, hapa Bagamoyo si mwenyeji sana, namtafuta msichana mmoja anaitwa Shekhia” aliongea kwa umakini sana Suhail huku akiwatazama wale wasichana wanaosukana nywele lakini alishangazwa na hali ya wale wasichana baada ya kuwatamkia kile kitu maana waliacha kusukana kisha wakamuangalia kwa pamoja kabla ya msusi kutupa swali
“Shekhia yupi huyo?”
“Mtoto wa mzee Shamhurish”
“Mzee Shamhurish? Huyo hatumjui”
“Sasa mbona kama mlishtuka sana kusikia namuulizia Shekhia?”
“Tulidhani unamuongelea Shekhia Sufiani” jibu la msusi likamlipua moyo Suhail, akamkumbuka Shekhia S. Sufiani aliesoma nae chuoni
“Inaweza ikawa nd’o huyo, kwani huyo yeye ni wa wapi?” wasichana wale wakatazamana tena kisha kwa pamoja wakaangua kicheko wakati huo Yule mwenye kilembo cha njano akiwa ameshatoka na gilasi yake ya maji mkononi na kumkabidhi Suhail, wakati Suhail anakunya maji akamsikia Yule msusi akimuambia yule msichana alieendea maji ndani
“Haya shosti kuna ugeni hapo”
“Upi huo?”
“Huyo mkaka anamuulizia Shekhia”
“Shekhia?” Swali la dada mwenye kilembo cha njano japo lilielekezwa kwa msusi lakini haraka Suhail akamalizia funda la maji na kujibu
“Ndio Shekhia, jamani hebu niwekeni wazi kwani ana nini dada yule?” Swali la Suhail halikua na maana zaidi ya kuwazidishia siku za kuishi akina dada wale kwa kuwafanya wazidi kucheka, Suhail akabaki njia panda, ikabidi sasa nae aketi pale kibarazani na kuanza kuwadadisi wasichana wale. Baada ya muda mrefu wa udadisi ndipi dada mwenye kilemba cha njano akaanza kufunguka
“Ni simulizi ndefu sana iliyotokea hapa Bagamoyo, Shekhia alikua ni rafiki yangu zamani sana tulipokua shule ya msingi kwakua tulikua majirani na tulisoma shule moja, tukiwa bado wadogo kikatokea kioja cha mwaka kilichopelekea kifo cha maajabu cha mama yake mzazi, tangu hapo Baba yake akamkataza tena Shekhia kutokatoka nje kuja kucheza, ikawa tunakutania shuleni tu na baadae Shekhia kahamishwa shule na kupelekwa Dar japo kila wiki akawa anakuja pale kwao lakini akawa hachezi na sisi tena..” Kabla dada hajaendelea Suhail akamkatisha kwa swali
“Samahani kidogo, naona kama umeruka kitu, hicho kifo cha mama yake kilikua ni cha aina gani? Na wakati huo mlikua mkiishi wapi na akina Shekhia?”
“Tulikua tukiishi huko Mlingotini kama umewahi kupasikia.. siku moja Kilitokea kimbunga kikali kilichokua kama kilichotumwa vile, kikapita nyumba zote mpaka kwa akina Shekhia, kilipofika uani kwao kikamvaa mama yake na Shekhia akiwa anapika uani kwao kwao, cha ajabu waliokua jirani na nyumba hiyo wanadai ndani ya vumbi lile la kimbunga waliwaona watu kama watatu hivi, na kabla kimbunga hakijasambaa watu wale wakambeba mama Shekhia na kutoweka nae wao pamoja na kimbunga kile..”
Msichana yule akaweka kituo kidogo ili kuyapa uhuru mapafu yake kuvuta hewa mwanana itokeayo baharini, hakika habari ile ilikua ni ya ajabu na kutisha, Suhail alikua akizidi kuzizima ndani kwa ndani kwa uoga, alishaelewa kua Shekhia anaeongelewa hapo ni yule binti aliekutana nae kule chuoni lakini pia yawezekana ndie akawa mtoto wa Mzee Shamhurish, msichana mwenye kilemba cha njano akaendelea kusimulia huku wale wenzie wakiendelea kusukana nywele “..Basi bwana, nusu saa baada ya kimbunga kupotea watu wakiwa wamefurika uani kwa akina Shekhia wakishangaa muujiza huo ndipo tena ghafla ukadondoka mwili wa mama Shekhia ukiwa umeshaachana na roho yake ukitokea angani, watu wakatawanyika kila mmoja na njia yake.
Patashika ya nguo kuchanika, Ilikua ni tukio la ajabu sana japo kwa hapa bagamoyo matukio kama hayo ya kustaajabisha ni sehemu ya maisha yetu. Baadae wazee wakasogea tena pale, wakamstiri mama yule ili wamsubiri mumewe arudi lakini haikua hivyo, ilichukua kama siku mbili bila ya mumewe ambae ni baba yake na Shekhia kurejea hivyo viongozi wakaamua kwenda kumzika tu yule mama huku wakimchukua Shekhia kipindi hicho akiwa mdogo sana.
Mwezi mmoja Baadae ndipo yule Mzee alirejea, alipofika akapewa taarifa za tukio lile lakini cha ajabu hakuonekana kushtushwa sana na habari zile, ni kama vile aliekua akijua kila kilichotokea, alichokifanya akaenda kwa majirani tu kutoa shukrani zake kwa waliomsitiri mkewe, Akamchukua mwanae, na Baada ya muda hali ikatulia na kisa kikaanza kusahaulika. Ndipo hapo sasa Shekhia akapotelea Dar hatukujua tena Shekhia huko Dar anakaa kwa nani maana hata hapa hatukuwahi kuwajua ndugu zao kwa kua walikua wakiishi peke yao tu. Ila mpaka hivi tunaongea nadhani Shekhia yupo hapahapa Bagamoyo maana hua anaonekana mara mojamoja sana inasemekana amemaliza chuo ndo karejea.
Sasa Baada ya tukio lile la ajabu hata huyo Baba yake nae akawa haonekani kabisa. ila kama ukitaka kujua habari hizo kwa kirefu yupo babu yangu mimi kama ulishwawahi kumsikia Mzee Atrash Jamadu, yule ni kiboko anajua uganga wa kila aina, na yeye ndie anaejua siri kubwa ya akina Shekhia ila hua hasemi hovyohovyo, Nasikia ni watu wa hatari sana” maneno ya msichana yule yalimmaliza nguvu Suhail, akawa kama aliepigwa bomu la kutoa jasho mwilini, akiwa bado ameshangaa akatupiwa neno na yule msusi ambae aliekua kimya muda wote
“Upo hapo mkaka?, hii ndo bwagamoyo yakhee karibu sana, kama ulidhani umeopoa chombo basi umeopolewa” kisha kicheko cha kishangingi kikaunguruma
“Unaweza kunipeleka kwa huyo babu yako?,” aliuliza Suhail huku akimuangalia dada mwenye kilemba cha njano
“Ukafanye nini sasa?”
“Si umesema yeye ndio anajua mambo mengi zaidi?”
“Tena zaidi ya mengi lakini mimi siwezi kwenda huko saa hizi, kwanza ni mbali na pili ndio nimetoka huko sasa hivi nimekuja huku kwa rafiki yangu kusuka, labda nikusaidie kukuelekeza tu uende mwenyewe”
“Kwani ulisema ni wapi vile?:
“Panaitwa mlingotini, ni nyuma kidogo kabla haujafika huku Bagamoyo mjini, laity ungejua ungeshukia kulekule”
“Sikia dada naomba tu twende wote nitalipia Tax mpaka huko kwenu kisha itakurejesha tena mpaka hapa, na pesa ya Msusi nitakulipia”
“Mnh, kaka kwani we una jambo gani na Shekhia mpaka umekua makini kiasi hicho?”
“Aaah kawaida tu, kwakua tumeshakua marafiki nitakueleza tu muda ukiwadia, ila kwa sasa naomba ukubali twende tukamuone mzee” ilikua ni kama bahati ya mtende kwa Suhail kukutana na wasichana hawa waliompa maneno yaliyommaliza kabisa maana pamoja na uzito wa maneno ya msichana yule ameambiwa kua Mzee Atrash Jamadu ndio anajua Siri kubwa,
‘Ni siri gani hiyo?’
Ikabidi sasa Suhail atumie nguvu kubwa ya ushawishi pamoja na kutumia pesa ndipo dada yule akakubali kurudi huko Mlingotini kwa ajili ya kumpeleka Suhail, hawakua na sababu ya kuendelea kupoteza muda tena, wakainuka na kuwaaga wenzao kisha wakaanza kuondoka na kuelekea barabarani, walipofika tu haraka wakasimamisha Tax, wakapatana bei, na safari ikaanza huku Suhail akiwa kama mwendawazimu kwa habari alizozipata kuhusu Shekhia
*****
DAKIKA zipatazo ishirini na tano kwa mwendo wa teksi zilitosha kabisa kuwafikisha Mlingotini lakini kutokana na Miundombinu ya barabara kua si nzuri sana hivyo ikawalazimu washukie barabara kuu na kuanza kuanza kutembea kwa miguu kuelekea nyumbani kwa Mzee Atrash ambapo hapakua mbali sana kutokea barabarani hapo, Ndani ya dakika tano wakawa wanatazamana na Nyumba ya ‘Msumbiji type’ mali ya Mzee Atrash.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi