Vita vya Mapenzi (9)

0

SEHEMU YA TISA
TULIPOISHIA...
Shamhurish hakufariki kama unavyodhani wewe bali ilikua ni njia ya kuondokea huku Tanzania na kutokomea Yemen sasa Baada ya kumpata mtu wa kumpa pete yake tena mtu mwenye ni Mkwewe hivyo alipaswa aonekane hayupo tena katika Nchi hii kwa kufa au vinginevyo, hivyo hiyo ilikua ni kiini macho tu..”

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
Akashusha pumzi Mzee Atrash kisha akaanza kuhitimisha mazungumzo yake “..Kilichokuponza wewe ni Tamaa ya pesa za Shekhia kama ilivyomponza mama Shekhia kutamani pesa za Mzee Sufian Shamhurish, Pia kilichokuponza tena wewe ni Usaliti uliomfanyia Sharifa licha ya kwamba alikupenda, akakuamini, na kukutahamini kwa hali na mali kama ambavyo Mama Shekhia alivyomsaliti yule Mwanaume aliempenda, akamjali na kumthamini..

Vita vya Mapenzi vilivyotimka kipindi kile cha Nyuma sasa historia itajirudia kwako.. Na kinachoendelea kukuponza wewe ni Uongo kama huu uliokuja kunidanganya mimi hapa kua mnataka kufanya Biashara na akina Shekhia, haya sasa kaendeleeni na Biashara yenu ila ujue hii ndio Bagamoyo, pwani ya wajuvi wa mambo, haupaswi kuja ukavamia mji kwa mbinu za uwongo. Haya mimi nimemamaliza yangu naomba sasa kwa heshma na ta’adhima utoke nje waingie na wengine,” Alihitimisha Mzee Atrash na kumuacha Suhail akibubujikwa na machozi huku akiwa haamini kinachomtokea

“Mzee wangu naomba unisaidie, naomba unifae sina pa kukimbilie mie,” Suhail alikua akikongea na kulia kwa wakati mmoja kiasi cha kufanya sieleweke viozuri anaongea nini, lakini Mzee Atrash alisimama katika maamuzi yake akamuamuru Suhail atoke nje tena bila ya malipo, ila akamuambia anamkaribisha siku nyingine akiwa amejirekebisha tabia zake..

‘Afua mbili, Kufa na Kupona’ Suhail alijisemea kimoyomoyo, akainuka kishingo upande na kutoka nje ya nyumba hiyo huku akifuta machozi ili asigundulike na akina mama wale. Akatoka akiwa Kichwa chini mikono nyuma,

*****

Maneno ya Mzee Atrash yalimzidia uzito kichwani bwana mdogo Suhail, akawa kama aliyechanganyikiwa kabisa, akatoka mule ndani bila ya kujielewa, yaani njia nzima akawa anjisemea peke yake tu, kichwa chake mwenyewe lakini alihisi kikimzidia uzito kutembea nacho. Alipofika nje akawa anatoka na kile kinjia ambacho ni mfano wa barabara ndogo ili akaikute barabara kubwa asubiri gari la kurejea Dar es Salaam hakukumbuka tena kilichompeleka Bagamoyo ni kumtafuta Shekhia na kutafuta habari za Shekhia pengine angelizingatia hilo angesalimika lakini sasa amekua adui wa maamuzi yake mwenyewe, hakuona thamani ya kuendelea kuishi japo pia hakufikiria kuupoteza uhai, kila alipotembea hatua kadhaa aliiangalia Pete yake, hakua na kuifanya zaidi ya kutikisa kichwa na kuendelea kutembea kuelekea barabarani..

Dakika chache akawa amefika Barabarani, akawa anaangalia huku na kule kama ataona kituo maalum ambacho magari husimama kwa pale Mlingotini yakitokea Bagamoyo mjini kwenda Dar, ndipo ghafla alipatwa na mshtuko wa mwaka, moyo wake ukapiga tikitaka ndani ya kifua chake baada ya kushtushwa na Sauti nzuri nzuri iliomsemesha ikitokea kwa nyuma yake pale alipokua amesimama, ni sauti aliyoifahamu sana, na alipogeuka alithibitisha hisia zake kua alikua akitazamana uso kwa uso na Shekhia S. Sufian au Shekhia bint Shamhurish, nguvu zikamwisha kaanguka mpaka chini kama kiroba cha uchafu, akaanza kuhisi hali ya kupoteza fahamu lakini aliipigani nafsi yake kiume, akajikaza mpaka akasimama wakati Shekhia akimsogelea kwa furaha isiyo kifani,

“Suhail yaani mpenzi wako ulieyekua ukilala nae leo unamuogopa kamahujawahi hata kugusana nae?!, acha utoto wewe,” aliongea Shekhia huku akilizidisha lile tabasamu lake pana lililokua likiwachanganya vijana wengi kule chuoni.

Lakini kwa sasa Suhail hakuliona wala hakuhitaji kuliona. alipoinuka tu akaanza kutimua mbio kama mwendawazimu, Shekhia alijaribu kumuita kwa furaha ili ampunguze hofu aliyonayo lakini haikuwezekana, Suhail alikimbia umbali mrefu mpaka akawa hamuoni vizuri tena Shekhia, na hapo akaona haina haja ya kusubiri gari kubwa akasimamisha Tax iliyokua ikitokea kulia mwa barabara ambako ndiko njia ya kwenda Dar es salaam akaisimamisha na kuingia haraka huku akitweta akafunga mlango na kumuamuru dereva ageuze gari waelekee Dar es Salaam. Dereva hakubisha alitii amri akaanza kuendesha lakini hakugeuza gari yake kwa maana ya kuupata uelekea wa kurejea ambako Suhail alipataka

“We vipi mbona haunielewi, nimekwambia naenda Dar, sasa unaelekea huku wapi? Mimi siendi huko Bagamoyo,” alikaripia Suhail lakini kijana yule hakujibu wala hakujihangaisha japo kumtazama Suhail, aliendelea kuendesha gari yake mpaka hatua kadhaa ndipo akakata kona mkono wa kulia ikiwa ni njia kama ya pili hivi au ya tatu kutokea kwenye ile njia ndogo inayokwenda moja kwa moja mpaka Mzee Atrash, Sasa Suhail alipoona hamuelewi dereva yule akaamua kufungua mlango ili ashuke haraka kwa kua gari ilipunguza mwendo pale kwenye kona, alipojaribu kufungua mlango haikuwezekana, Mlango ulikua umepigwa “Lock” na dereva

Hakika Suhail alitamani hata amvae tu kijana yule lakini hakua na nguvu kabisa akabaki tu anamuangalia dereva yule ambae aliendesha gari yake kwa umakini mpaka katika nyumba moja hivi ndefu kwenda juu, ni kama ghorofa moja lakini ilikua ni chakavu sana kiasi cha kumfanya mpita njia ambae ni mgeni kuamini kua mule ndani hapakaliwi na watu na labda pengine ni Gofu tu la kuhifadhia taka. Lakini cha ajabu jingo hilo lilikua limo ndani ya uzio ambao ulionekana kusafishwa kwa kupaliliwa majani yaliokua yakiota pale na kufanya hisia kichwani mwa Suhail kua mule ndani kuna watu wanaishi,

Naam kulikua na watu wakiishi!

Dereva kasogeza gari mpaka getini ambapo bila ya kupiga honi mlango ukafunguliwa na kijana mmoja bila shaka ni mwenye asili ya kiarabu kutokana na nywele zake za singa na rangi yake ya ngozi. Gari ikaingizwa mpaka ndani kisha ikapakiwa upande wa kulia ambapo palikua na sehemu maalum ya maegesho ya magari, kijana yule aliefungua geti akasogea mpaka pale katika gari kisha dereva akatoa ‘lock’ ya milango na kumuamuru Suhail ateremke nae akatii bila shuruti

Maswali mengi yakawa yanapita kichwani mwa Suhail bila kuyapatia majibu, alijiuliza au labda ametekwa na majambazi kutokana na habari zilizoanza kuzagaa mjini kua yeye ni mfanya biashara tajiri sana kwa sasa, lakini hakutaka kuamini hivyo kutokana na kwanza huku Bagamoyo hakua akijulikana na mtu yeyote, Pili muonekano wa vijana wenyewe, hasa huyu aliefungua geti alikua akionekana kujawa na furaha isiyoeleweka ni ya nini. Akateremka kwenye gari ile akifuatiwa na dereva wake

“Karibu sana kaka, tulishaanza kuingiwa na hofu tukadhani hauji tena,” alisema kijana yule alieonekana kama mwarabu vile huku akimpa mkono Suhail, japo Suhail hakuupokea mkono ule wala hakuijibu salamu zaidi ya kuanza kulalama tu

“Ninyi ni akina nani? Na mmenileta humu kufanyaje?.”

“Khaa! Kwani we leo ulikuja Bagamoyo kufanyaje yakhee?,” aliuliza kijana yule huku akitabasamu kwa furaha na kumfanya Suhail azidi kuhamaki huku akiamini kua huenda sasa ameuvaa mkondo wa Mzee Shamuhurish

“Usiniulize swali juu ya swali, nimekuulizeni ninyi mmenileta humukufanya nini?,” aliongeaSuhail kwa jazba huku akiendelea kuyatilii mazingira ya mule ndani kama itawezekana kujaribu kuponyoka lakini alisalimu amri kua hakua na ujanja tena maana uzio ulikua imara madhubuti

“Nadhani ulikubaliana na Mzee kua leo utakua hapa kwa shughuli maalum, nadhani ndo umekuja hivyo hatuna haja ya kupoteza muda twendeni tu ndani” kijanayule alimalizia kauli yake na kumshika mkono Suhail kisha akaanza kuondoka nae na kuelekea ndani, Suhaila alikua kama aliyemwagiwa maji au kama vile mtuhumiwa anaekwenda kunyongwa kwa jinsi alivyoishiwa mbinu.

Hatua chache wakawa wameingia ndani ya jengo lile chakavu kwa nje lakini kwanda ilikua ni mfano wa ikulu ndogo kwa jinsi lilivyopendeza na kupambwa kiustadi sana, pia palikua na ngazi ambazo ziliashiria kua juu kuna ghorofa inaendelea lakini hawakuelekea huko bali waliendelea kutembea katika sebule ndefu ambayo iliwapeleka mpaka sehemu flani ambapo palikua na ngazi zikiashira kua zinaelekea chini zaidi ‘Underground’.

Muda wote huo hapakua na mazungumzo yoyote kati ya Suhail wala kijana yule wa Kiarabu, yule dereva yeye aliishia pale kwenye ngazi za kupandia juu. Hapakua na haja ya kuelekezana chochote wote wakaanza kwenda chini huku Suhail akiwa ameshikwa mkono, Hofu ikazidi kumuingia.

Safari ikaendelea!

Safari ya kwenda chini ilikuwa ndefu kiasi chake maana kila alipohisi kuwa sasa wanafika cha ajabu ngazi ziliendelea tu kwenda chini zaidi, ilikuwa ni kama dakika tano za kuteremka chini ndipo walipowasili sehemu nyingine iliyokuwa ni Tambarare!, ilikuwa ni sehemu iliyosafishwa na kutengenezwa vizuri sana kukiwa kumepambwa kwa mapambo yenye kufanana na yale waliyoyakuta kule.

Huku nakshi za milangoni zikiwa za rangi ya dhahabu, Ilikuwa ni kama nyumba ya kawaida tu ila iliyotengenezwa kwa uimara wa hali ya juu, hata hewa yake haikuonesha kuwa wapo sehemu ya chini ya ardhi, pia taa kubwa za umeme zilizo katika maumbo tofauti zilikuwa zikiwaka. Upande wa kulia tokea pale waliposimama akina Suhail palikuwa na Zulia kubwa jekundu huku kwa juu yake kukiwa na Sahani ya shaba, pia palikuwa na kabati kubwa la mbao upande wa kushoto tokea pale waliposimama, halafu kwa mbele yao palikuwa na Korido ndefu inayoonekana kuendelea kwenda ndani zaidi.. Korido ile ilitawaliwa na ukimya na hali ya giza kutokana kukosa taa, ilikuwa ni eneo la kuvutia sana lakini kwa Suhail ilikuwa ni eneo lenye kutisha sana.

Wakiwa eneo lile walisimama kama dakika mbili hivi ndipo wakaanza kusikia sauti za nyayo za watu zikisogea eneo lile zikitokea kule kwenye Korido ndefu, wote wakageukia upande ule lakini kutokana na giza lile hawakuweza kuona kinachowasogelea, lakini haikuwachukuwa hata dakika moja sauti za nyayo zilizidi kujongea na hatimaye wenye nyayo wakawasili. Lilikuwa ni kundi la watu kama tisa hivi, wakiwa wamevaa kanzu nyeupe huku wamejitanda vilemba vya rangi ya kijani wote kwa pamoja, walikuwa ni watu wenye asili ya ki-asia, Macho yalimtoka Suhail asijue cha kufanya,

Angefanya nini sasa!

Watu wale wakawasogelea akina Suhail wakawasalimu huku wakiwapa mikono na kuwakumbatia kwa furaha, bado lilikuwa ni tukio lisilo na majibu kwa Suahil, baada ya Salamu ile wote wakafuatana mpaka katika lile zuria jekundu kisha wakaketi kwa pamoja kwa kuizunguruka duara ile sinia. Haikuchukuwa dakika tano ghafla ukafunguka mlango usawa wa lile kabati kubwa lililokuwa upande wa kushoto, kwa harakaharaka usingeweza kutambua kuwa pale palikuwa na mlango kwa jinsi palivyonakshiwa kitaalamu

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)