Mtunzi: Maundu Mwingizi
SEHEMU YA KUMI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
CHA AJABU, Ilipofika kwenye mwezi wa sita ghafla hali ya Bi Mwajabu ikaanza kubadilika, kila siku lile tumbolake la ujauzito likaanza kuyeyuka mithili ya pulizo lililotoboka na hatimae ujauzito ukatoweka kabisa
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Ilikua ni tukio la ajabu sana sit u kwa familia ya Bw Kikoko bali hata kwa baadhi ya majirani na wakazi wa mkoani pale, habari zilizagaa mji mzima, kila mtu alisema lake. Walipomuhoji Bi mkubwa huyo akasema aliondoka akiwa mjamzito ila tyeye alikua na tumbo dogo lisiloonekana kiurahisi, Ikabidi sasa Kikoko ampeleke mkewe Hospitali lakini nako vipimo vikaonesha kua hana ujauzito kabisa.. wiki mbili baada ya tukio hilo Bi mkubwa(Bi Kapemba) karejea tabora, kilichowashangaza wengi mpaka mzee Kikoko mwenyewe ni kwamba Bi Kapemba alirudi na Ujauzito mkubwa wa miezi kama sita hivi, hakuna alieaminikua tukio lile linatokea dhahiri lakini huo ndio ulikua ukweli wa mambo, yaani Ujauzito umetoweka kwa Kwa Bi mdogo na ghafla umehamia kwa Bi Mkubwa, Sulahilo
lilizua zogo kubwa na hatimae wakaanza kushikana uchawi
Ndugu zake na Bi Mwajabu walienda kwa waganga wakaambiwa kua Bi Kapemba aliinyakua kichwawi mimba ya mwenzie na kuihamishia kwake kwa kua hakua na uwezo wa kushika ujauzito na hapo ndipo ikafahamika kua Bi Kapemba amefanyiwa hivyo na mizimu ya kwao Shinyanga, unaitwa MZIMU WA WAUFI, Ni mzimu mkali sana na wenye nguvu hivyo sasa yakaanza mapambano ya kimizimu kati ya Mzimu wa Waufi wa kwao na Bi kapemba na Mzimu wa WASWEZI wakwao na Bi Mwajabu Fundikira, mpambano ulikua ni mkali sana kila siku ndani mauzauza, ushirikina, vurugu, nk lakini hatimae mwaka 1980 Bi Kapemba akajifungua motto wa kiume, na kutokana na tabu, shida, na mkasa ho ndipo wakampa jina la MASUMBUKO, Japo Bi Kapemba ndie aliejifungua lakini Bi Mwajabu alisema hakika Yule ni mwanae na ni damu yake hivyo hatokubali kamwe..
Familia zilijaribu kukaa na kufanya suluhu ili kwakua mambo haya yanautata mkubwa waweze kuiyamaliza, ilikua ni suala gumu sana lakini hatimae waliridhiana kishingo upande huku kila mmoja akibaki na lake moyoni, inasemekana wakati Bi Kapemba alipokwenda Shinyanga Mizimu ya kwao iliinyakua kichwawi mimba ya Bi Mwajabu na kuihamishia kwake kisha wakampa sharti kua ni lazima atoe kafara ya damu haraka iwezekanavyo Laa sivyo watamchukua Masu wao na Pia walimtaka Bi kapemba kua Masu akifikisha miaka kumi ampeleke ili akaingizwe rasmi kwenye Ukoo wao chini ya Mizimu ya Waufi kwakua hakua damu yao lakini hakufanya hivyo….
Masu alikua amemtolea macho Mzee Kishindo aliekua akimpa mkasa mzima wa kuzaliwa kwake, ilikua ni stori ya ajabu na kustaajabisha sana
“Kwahiyo hakuna Dini ya Waufi mwanagu hiyo ni mizimu ya Waufi na kila wanachokufanyia ni kiini macho tu, hata Yule mchungaji na huyo sheikh wote si WAUFI bali unapokua unaongea na mtu yeyote anaonesha kutaka kukusaidia anakuja huyo hunudu na kujivisha umbile la huyo mtu kisha anajifanya nae ni Waufi”
“Mbona kwako wewe hua hatokei?”
“Nitakupa siri ya mizimu ya kwetu mimi”
“Sasa Baba nae aliamuaje?”
“Kikoko aliyakubali matokeo tu na anajua kila kitu sema anajaribu kujisahaulisha wakati wewe unaangamia” Masu akawa analia baada ya kuusikia Mkasa wake ule, Ikabidi sasa Mzee Kishindo akamkataze kulia
“Nilikuambia uwe na kifua, sasa unalia nini?”
“Mzee Kishindo mie nitakufa tu, sasa nitafanyaje mimi? Yaani kumbe Mama Masu hakua mama yangu halali??!”
“Hauwezi kufa japo huu mpambano ni mkali, unachotakiwa kufanya kwenda kwao na mama yako wa damu Bi Mwajabu Huko kipalapala tabora ili ukafanyiwe tambiko la kwenu, tambiko la Waswezi Laa sivyo utapotea kijana, ukiwa tayari nitakusindikiza”
“Kwahiyo tanafanyaje Mzee wangu?”
“Nitakusaidia, andaa nauli nitakupeleka mpaka Tabora kwenu, kwa mama yako”
Wakiwa katikati ya maongezi mazito ghafla walisikia sauti ya pikipiki ikija maeneo ya pale kwa Mzee Kishindo kisha mlio ukazima na baada ya muda kidogo mlango ukagongwa
Ngo! Ngo! Ngo!
Kabla hawajafanya lolote mlango ukafunguliwa akaingia Mzee Kikoko akiwa na Sheikh Jabu, baada ya Sheikh Jabu kugonganisha Macho na Mzee Kishindo hapo hapo Kikoko akamgeukia Sheikh Jabu
“Si nilikuambia kua huyu mshenzi ndie anaeleta fitna kwenye familia yangu?!!!”
******
MZEE Kikoko hakusubiri kugongewa kengere kama ishara ya kupata kibali cha kumvaa Mzee Kishindo na kuanza kumtembezea kichapo, ilikua ni kitendo cha kunusa na kutoa chafya, balaa kubwa kati ya wazee hawa ikaanza, tayari Kikoko alikua ameshasogelea na ameshamkunja shati Mzee Kishindo,
“Tafadhali Bw Kikoko niachie, hapa ni nyumbani kwangu utajiletea dhahma kubwa” alibwata Mzee Kishindo
“Sikuachii nataka nikuadabishe kidogo maana nilishakukanya kwa maneno ukaweka Nta masikioni” bada ya maneno yale hapo hapo Kikoko akamrukia kichwa mzee mwenzie, akamrushia ngumi, mara akamza ba kelbu la uso, Hakika Kikoko ni mzee mtata mwenye kila chembe ya ukorofi na shari, wakati huo kichapo kinaendelea Masu alikua ameshafika mlangoni kwa ajili ya kukimbia lile varangati lilikua likiendelea kuzizima mule ndani..
“Kikoko acha tafadhali” Sheikh Jabu alikua akijaribu kumuhami Mzee Kishindo asiendelee kupokea kichapo kutoka kwa Alwatani Kikoko ambae alikua ameshamgaragaza chini Mzee Kishindo, Kikoko aliendelea kumvugumizia makonde ya nguvu Mzee Kishindo, hakika ilikua ni hali ya hatari sana, baada ya purukushani kubwa pale chini hatimae Mzee Kishindo alifanikiwa kuinuka na kuponyoka kutoka katika mikono ya Kikoko, akatoka mbio akielekea Chumbani kwake
“Nitakuua mimi, unaleta ubwege wako hapa..” Kikoko aliendelea kutamba pale sebuleni kabla Kishindo hajatoka chumbani kwake kwa kasi ya ajabu, Alionekana kama Ng’ombe aliechanganyikiwa, hakika alikua amepandwa na ghadhabu, Mkononi akiwa ameshika kitu cha hatari sana, kitu chenye madhara, Naam ilikua ni mkia wa taa, Mkia wa taa ni hatari sana kwa mwenye kuujua hata ikiwa katika ugomvi mkubwa kiasi gani mtu akiutoa tu ule kila mwenye kuujua atakimbia kabisa, Ukichapwa na mkia ule kwanza utapata maumivu makali yasiyo ya kawaida na pia baada ya siku kadhaa utajishanga ukiugua tu hovyo
“Kishindo achaa tafadhali hiyo ni hatari” alipayuka Sheikh Jabu” Lakini Kishindo hakusikia ‘La Imam wala la mnadi swala’ Alikua amekasirika haswa! dakika chache tu akawa kaishamkaribia Mzee Kikoko na hapo hapo alianza kumcharaza kwa nguvu zote Mzee Kikoko, alimtandika mwilini hovyo hovyo, Kikoko alikua ameshahamaki hivyo kila alipojaribu kutaka kujihami ilikua ni sawa na kazi bure maana tayari Kishindo alikua ameshamtaiti vilivyo, Kipigo kilipozidi Kikoko Akaamua kutoka nduki kali lakini kutokana na Simenti laini iliyopo sebulaeni kwa Mzee Kishindo akaanguka chini ndipo sasa Mzee Kishindo akapata upenyo mzuri wa kumuadhibu Alwatan, Kikoko akawa anagaa gaa pale chini huku akipiga kelele lakini Kishindo hakua na hata chembe ya huruma aliendelea kutoa kiminyo utadhani anaua Nyoka,
Wakati hayo yakiendelea tayari Masu alishatoweka mule ndani, pia Sheikh Jabu alikua amekimbilia upande wa pili wa sebuleni akihofia kukaa karibu maana alijua bila shaka Mzee Kishindo atamgeukia na yeye na kumuadhibu pia, na kwa jinsi alivyoijua sumu iliyomo kwenye mkia wa taa hakutaka dhahma ile imkumbe,
Ghafla Kikoko akapata upenyo akachomoka na kutoka mbio mpaka nje ya nyumba ile, nae Sheikh Jabu akafuata mbio mpaka nje, Mzee Kikoko alikua kavimba mwili kwa kichapo cha mkia wa Taa
“Kama mwanaume kwanini ukimbilie mkia wa Taa?” Alipayuka kwa sauti Mzee Kikoko huku akiwa anatweta
“Pole Swahib wangu ila nilikukanya wewe, kua tukifika usifanye fujo hata kama tutamkuta Masu”
“Yule asingekua na ule mkia ningemdhibiti tu mimi ni mtoto wa mjini, we hukuona nilivyomuanzishia mpaka akahuma, halafu ananishambulia na silaha na wewe umekaa tu pembeni na kanzu yako mchinjo hiyo kama mtoto anaesubiri kutahiriwa..”
“Hilo ndo tatizo lako Bw Kikoko”
“Na hakyamungu usingekua swahiba wangu leo ningekutandika na wewe maana huna maana”
Baada ya malumbano na majibizano ya muda mrefu yale, Sheikh Jabu na Kikoko wakapanda pikipiki yao aina ya ‘Bata vuz’ kisha wakaondoka kwa kasi kuelekea nyumbani
*****
Nje ya Ofisi ya Birimuye Holding Ltd alikua amesimama Masumbuko Kikoko akiongea na kijana mmoja mfanyakazi mwenzie pale ofisini aliezoeleka kwa jina Shamsi, lengo la Masu ni kwenda kuongea na Boss wake Mr Kitale aweze kupatiwa kiasi kidogo cha fedha kwa kama mkopo ili akitumie haraka kwenda Tabora akisindikizwa na Mzee Kishindo ili akafanyiwe Tambiko na Zindiko kutoka katika Mizimu ya damu ya mama yake huko Kipalapala, Mizmu ya WASWEZI, Lakini Masu alishangazwa na taarifa alizopewa na Shamsi..
“Mbona sikuelewi Shamsi?” Alishangaa Masu
“Ndio hivyo Kaka, unajua mimi nimekulia uswahilini kama wewe, hayo mambo ya kishirikina ninayaelewa vema lakini hapa Ofisini kuna watoto wa Kishua tu hawayaelewi kabisa, wanachoamini wao kua wewe umechanganyikiwa hivyo wameamua kukusimamisha kazi kwa muda usiojulikana mpaka Boss atakapojiridhisha kua sasa umepona, na pia kama utaonekana hapo ofisini kwa kipindi hiki utaitiwa askari’
“Shamsi mbona nazidi kuchanganyikiwa ndugu yangu, sasa nitakimbilia wapi mie hapa nilikua nimekuja kuomba kukopa pesa kwa ajili ya nauli”
“Nauli ya kwenda wapi tena?”
“Si nimekudokeza kuhusu hilo suala la kwenda kufanyiwa tambiko huko Tabora”
“Sasa na wewe huna hata akiba nyumbani? Kwani inatakiwa kiasi gani?”
“Sio kama sikua na akiba, nilikua nayo kidogo lakini sasa nasikia Mzee Kikoko kamnyang’anya mke wangu kila kitu muhimu ikwemo na kadi za Benki na kwakua nitaenda na Mzee Kishindo hivyo nahitaji kama Tsh laki tatu tu zingenitosha kabisa” Masu alikua akitikisa kichwa kwa uchungu huku akiwa ameinamisha paji lake la uso chini kwa huzuni, kasha akamtupia swali Masu
“Sasa mwanzo uliniambia kua Mzee wako amewavamia pale kwa huyo Mzee Kishindo halafu akawaanzishia vurugu sasa huoni kua huyo mzee hatokua tena na nia ya kukusaidia?”
“Hayo nitaenda kuyajua hukohuko lakin kwanza niwe na pesa mkononi ili hata kama nitamshawishi na kumuomba radhi basi kazi itafanyika si unajua tena mkono mtupu haulambwi, Kwani humo ofisini yumo nani?”
“Aaah wamo tu kina Leylah, Hindu, nadhani na Yule dada mtata kutoka tabora”
“Ritha..??”
“Yeah Ritha, ila hao wote ndo wale wale wanamjaza Sumu Boss na kama wakikuona tu watampigia simu sasa hapo itakua shida kwako” Kikapita kimya cha muda mrefu kidogo kila mmoja akionakana kuzama katika dimbwi la mawazo, ndipo tena Shamsi akavunja ukimya
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi