Simulizi Mpya
Tidak ada notifikasi baru.

MZIMU WA WAUFU (4)


SEHEMU YA NNE
TULIPOISHIA...
Judith alipigwa na Butwaa na sasa badala amfariji mumewe yeye ndo akawa amechanganyikiwa mara mbili ya Masu mpaka Masu akawa sasa almanusura awe chizi,

“Mume wangu haiwezekani, hili jambo zito mie naenda kwa Mchungaji Jofrey kumueleza jambo hili”

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
“Hapana, acha tu”

“Siwezi kuacha, ni bora ukaombewa maana wamesema usiku wanakuja tena” Masu alikua akikataa kuombewa na Mchungaji kwakua yeye ni muislam japo Judith yeye ni mkristo na hata ndoa yao walifungia Bomani tu, Masu alijua kua endapo Baba yake atasikia kua ameombea na Mchungaji itakua kasheshe lakini kwa ushawishi aliopewa na Judith akajikuta amelainika, na Judith akaenda mpaka kwa mchungaji na kumueleza kila kitu, baada ya mchungaji kumsikiliza vya kutosha akakubali kua wafuatane mpaka nyumbani kwake na Judith ili mchungaji akamuhudumie Masu pale pale Nyumbani.. Walipowasili walimkuta Masu akiwa ameketi chini kabisa kwenye kapeti, Mchungaji akamshika mkono na kumuinua kisha akamkalisha kwenye Sofa lake dogo halafu akaanza kusema nae, lakini kabla hajaanza kuongea nae chochote Mchungaji akamuomba Judith awapishe wazungumze, Judith akatoka kasha Mchungaji akaanza..

“Pole sana Bw Masu”

“Ahsante Baba Mchungaji” Masu alikua akijibu kwa utiifu, kwakua maji yalikua yameshamfika shingoni ikabidi tu amtii Mchungaji japo sio dini yake hiyo “Kuna jambo nataka kukushauri kijana”

“Ndio Mchungaji..”

“Najua Hunudu anakusumbua sana mpaka unakosa raha” Maneno haya ya Mchungaji yalimshtua kidogo Masu akawa anajiuliza kua huyu mchungaji kamjuajea Hunudu? Lakini akajipa moyo kua huenda Judith kamsimulia kila kitu, akaendelea kumsikiliza bila ya kumjibu chochote “Lakini usimlaumu sana, hata yeye pia ametumwa na Viongozi wakuu wa Waufi hivyo inabidi atekeleze maalekezo aliyopewa, hata lile jicho lake Bovu alitobolewa na viongozi hao zamani kabisa alipokua akiambiwa atoe kafara ya damu akawa hataki, hata yeye nilimshauri kua akubaliane nao tu japo alinipinga sana hatimae akatobolewa jicho na kafara akatoa, sasa nawewe nakushauri mapema kabla hujaumia, Toa kafara hiyo wanayoitaka na utakua salama vinginevyo utaumia na kafara utatoa tu utake usitake” Masu alisimama ghafla kwa uoga baada ya kusikia maneno mazito kutoka kwa Mchungaji akawa hajitambui sasa, akaanza kusikia kizunguzungu akajikuta ameropoka

“Mchungaji sikuelewi kabisa”

“Utanielewa tu, hata mimi pia ni Mfuasi wa Waufi na ukiendelea kujidanganya kutukwepa utaangamia, Acha kabisa kutoa siri zetu kwa Mkeo na kwenye vijiwe vya kipuuzi, hakuna atakae kusaidia huko” Masu hakuamini maneno yale aliyokua akiyasikia kutoka katika kinywa cha Mchungaji, Mtumishi wa Mungu anaeaminiwa sana, akaona sasa hana ujanja, ni kweli anaangamia, akaanza kusikia anaishiwa nguvu, kizunguzungu kikamzidia na ghafla akaanguka chini kama kifurushi na kupoteza fahamu pale pale

BAADA ya Masu kuanguka chini na kupoteza fahamu, mkewe alishtushwa na mlio wa kishindo kizito uliotokea pale seating room ikabidi haraka akimbilie ndani kuangalia kuna kitu gani, alipofika pale ukumbini alipigwa na butwaa, akabaki kama Msukule au mwintunge kwa lugha ya kwetu baada ya kukuta Mchungaji akiwa amesimama anaendelea na maombi wakati huo Masu yuko chini amepoteza fahamu, Judith hakumuuliza kitu mchungaji akaenda mpaka pale chini huku akitetemeka akaanza kumtingisha na kujaribu kumuamsha lakini haikuwezekana, Judith akaanza kulia huku akimuuliza Mchungaji

“Imekuaje tena jamani Mchungaji”

“Mumeo ana mapepo, nimeyakemea sana yakamzidi nguvu na kumuangusha chini akapoteza fahamu” Mchungaji alikua akijibu kwa utulivu huku akijiamni sana lakini Judith alikua amechanganyikiwa sana akawa anaendelea kulia mpaka wapangaji wenzake wakasikia nao wakaja chumbani na kumkuta Judith akiwa amemuinamia Masu huku akilia wakati huo Mchungaji alikua amefumba macho akionekana yuko katikati ya Maombi, Kilichowashangaza wapangaji wenzao ni kile kitendo cha mchungaji kumuombea Masu wakati wanajua kua Masu ni muislamu, Lakini kwa hali ilivyokua wakashindwa kuhoji sana zaidi ya kujadili tatizo na kutafuta ufumbuzi mapema..

Baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya Judith, Mchungaji, na wapangaji wenzao wakakubaliana kumpeleka Masu hospitali haraka, hivyo mmoja kati ya wapangaji wale akaenda kutafuta Tax kisha akarudi nayo mpaka pale nyumbani wakambeba Masu mpaka kwenye Tax na safari ya kuelekea Hospitali ikaanza, Ndani ya Gari seat ya nyuma alikua amekaa Judith na Mchungaji wakiwa wamembeba Masu, na Seat ya mbelea alikua amekaa mpangaji mwenzie na Masu walikwenda mpaka Amana Hospital iliyopo Ilala na walipofika haraka mchungaji akaenda ndani kuongea na Dokta na baada ya muda wakaja manesi wakiwa na Machela zao, wakasaidizana kumtoa Masu kwenye Tax akiwa hajitambua na kumuweka juu ya machela kisha akapelekwa mpaka ndani kwa Dokta..

Baada ya kutoa maelezo Dokta akaanza kumpa huduma ya kwanza, na kisha akapelekwa Wodini kulazwa, wakiwa Wodini Judith akakumbuka suala muhimu kua alikua hajamuambia mtu yoyote juu ya tatizo lile, akafungua mkoba wake akatoa simu ya Masu kisha akaiangalia namba ya Mzee kikoko na kumpigia alipoweka simu sikioni alisikia ujumbe huu “Asante kwa kutumia mtandao wa Vodacom, simu yako haiwezi kukamilishwa kwa sasa tafadhali ongeza salio na upige tena” Simu haikua na salio, Akainuka na kutoka nje kwenda kutafuta vocha..

Baada ya kununua vocha na kuijaza katika simu ya Masu akampigia Mzee Kikoko

Akiwa nje ya nyumba yake kwa mke mdogo maeneo ya Shaikom akiendelea na shughuli zake za kupalilia majani huku akifagia fagia ndipo Mzee Kikoko akasikia kwambali kutokea chumbani kwake wimbo wa Jabari la Muziki Marijani Rajabu ukivuma na upepo akajua kua ni simu yake inaita, akatupa jembe na kwenda kuchukua simu, alipofika na kuiangalia aliona kua ni namba ya Masu akapokea kwa uchovu

“Hallo”

“Baba shikamoo” Kikoko akashtuka kusikia sauti ya mwanamke kutoka kwenye simu ya mwanae, haijawahi kuokea hata siku moja Masu akampa simu mkewe ampigie baba yake, japo tayari Kikoko alikua amekwisha ing’amua sauti ya Juddy lakini bado alishangaa tu maana hakua na mazoea ya kuiwasiliana na Mkwe wake huyo kwakua kwanza hampendi kuliko maelezo kutokana na suala la utofauti wa Dini kati ya Masu na mwanamke wake huyo, lakini akaitikia na kujiulizisha kama vile hajamjua..

“Marahaba, we nani?”

“Mie mama zani?”

“Mhuu kuna nini?”

“Baba, hali ya Masu ni mbaya sana, Masu anaumwa sana, amezidiwa na amepoteza fahamu hapa tumemleta Amana hospital”

“Amepoteza fahamu? Ilikuaje kwani?” Maneno haya ya Mzee Kikoko yalipenya sawia katika ngoma za masikio ya Mkewe mdogo aliekua Uani nae akaenda mpaka chumbani kusikiliza kinachoendelea, Mzee Kikoko alikua akimsikiliza Judith kwa makini sana kupitia simu yake nyeusi aina ya Nokia

“Leo Masu alikuja nyumbani akiwa anatetemeka sana huku akiwa kama amechanganyikiwa”

“Nikamuuliza kulikoni?, akaanza kunisimulia yaliyomkuta akaniambia kua alienda kule dukani kwa shekhe jabu akakutana na mzee mmoja ni rafiki yako wewe…”

“Anaitwa nani huyo mzee?”

“Anaitwa Mzee Kishindo..”Mzee kikoko kusikia jina la mzee kishindo sasa hofu ikamvaa lakini akajikaza

“Enhee ikawaje?”

“Masu akamuelezea huyo mzee kuhusu hii ndoto yake inayomsumbua, ndipo huyo mzee akampa maelezo mengi kuhusu hiyo ndoto yake na akamuambia kua yeye anakijua kinachomsumbua na akamuahidi kua atamsaidia, baaada ya Masu kuondoka pale dukani akiwa njiani ghafla akatokewa na yule kijana ambae hua anaemuta kila siku na kuanza kupewa vitisho..”

“Nini?Yaani huyo anaemtokeaga kwenye Ndoto akamuona njiani?”

“Ndio baba”

“Haya makubwa sasa..Ikawaje sasa?”

“Baada ya kupewa vitisho vingi wakamuacha, ndipo Masu akaja nyumbani akiwa amechanganyikiwa ndo mie nikaenda hapo jirani kwa Mchungaji Jofrey akaja kumuombea lakini wakati anamuombea mapepo yakapanda akapoteza fahamu ndio mpaka sasa tupo hospitali” Maelezo hayo yalimtoa jasho mzee Kikoko, hakuamini kila anachoambiwa..

“Hivi we mtoto ni Shetani?” Judith akapatwa na mshangao kusikia maneno hayo, ikabdi akae kimya kidogo

“Naongea na wewe, we ni Shetani? Aliekuambia ulete wachungaji kwa mwanangu ni nani? ”

“Lakini baba mie kosa langu ni nini wakati mtu alikua amepatwa na matatizo?”

“Aliekuambia kua Masu anatibiwaga na Wachungaji ni nani?”

“Lakini baba mie sikufanya kwa nia mbaya”

“Amaa kweli nimeamini Mchawi ni binadamu, Paka anatumwa tu, Kumbe wewe na Mzee Kishindo ndio mnanirogea mwanangu halafu mnajifanya kuwaleta hao wachungaji, sasa nakwambia hivi nataka Masumbuko apone Laa sivyo utakiona kilichomfanya kuku aanze kuota manyoa mkiani, Mie ndio Alwatan Kikoko” Baada ya mkwara huo mzito Mzee Kikoko akakata simu halafu akageuka nyuma ili aondoke ghafla akakutanisha macho na mkewe mdogo ambae alikua nyuma yake muda wote aliokua akiongea na simu

“Kwani kimetokea nini Baba Masu?”

“Naenda kwa Mama Masu..”

“Lakini hujaniambia kuna nini?”

“Tutaongea nikirudi” Kikoko akatoka ndani mule akamuacha mkewe huyu akiwa amesimama, cha ajabu huyu mwanamke akacheka kisha akasema kwa sauti ya chini

“Kama ni haki yangu Mungu atanilipia hapa hapa duniani”

Haraka haraka Kikoko akadandia baiskeli yake almaarufu kama Mkulima na kuanza kupiga pedeli kuelekea Mwasele kwa mkewe mkubwa mama Masu, Njia nzima alikua akimfikiria Judith kwa nini anampelekea mwanae wachungaji wakati anajua fika kua Masu ni muislamu, pia alikua akimuwazia Mzee Kishindo basi kwa kweli kichwa chake kilikua kimevurugika haswaa.. Baada ya kutembea umbali wa haja tu hatimae alikua amefika nyumbani kwake akateremka juu ya baiskeli na kisha akapita wima pale uani bila hata ya kusalimia

“Baba Masu kuna usalama kweli?” aliuliza mama Masu huku nae akisimama na kumfuata mumewe ndani

“Hakuna Usalama..”

“Kuna nini tena mbona hivyo?” wakati huo tayari baba Masu alikua ameshaingia chumbani na mama Masu nae alimfuata huko huko ndipo sasa Mzee Kikoko alipoanza kumsimulia Mama Masu kila kilichotokea mpaka mama Masu nae akabaki mdomo wazi

“Si nilikuambia Baba Masu, ile sio ndoto ya kawaida we ukawa unanipuuza?”

“Huu si wakati wa kulaumiana tena Mama Masu”

“Mguu umeshaota Tende ndo unakua muungwana sio, kwahiyo na huyo Mzee Kishindo na kamwambia nini sasa Masu?”

“Tena ngoja, umenikumbusha” Mzee kikoko akatoa simu yake na kumpigia Mzee Kishindo

“Asalamu alaykum Bwana Kikoko”

“Hakuna cha Salama leko hapa, hivi unanitaka nini na maisha yangu we Kishindo?”

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
63 Mzimu wa Waufu Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni