MY DIARY (37)

0
Jina: MY DIARY
Mtunzi: __

SEHEMU YA THELATHINI NA SABA
TULIPOISHIA...
Hapo alitulia tulii kama mtu aliyeaamia dunia ingine. Kimoyo moyo nikawa najisemeha kama amehamia dunia ingine na kuanza kuwaza ujinga sahuri yake mimi nipo kazini bwana acha nitafute hela. Ndio ni lazima nifanye kazi kwa utaalamu na utundu wa hali ya juu ili waendelee kusimuliana huko mjini ili niendelee kupata hela.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Wewe unafikiri mtu kutoa laki yake sa hivi kwa maisha haya ni jambo dogo. Nikashuka chini mpaka kwenye visigino na viwiko vya miguu. Nilivyofika kwenye unyayo akacheka nahisi nilimtekenya na hizi kucha zangu ambapo kipindi hicho zilitengenezwa rasmi kwa ajili ya kazi hiyo. Yaaani nilitamani huduma hiyo ndo ningekuwa namfanyia mchumba wangu Mark.Na nauhakika kuwa siku nikimfanyia lazima atanikataza kuwafanyia wanaume wengine, jamani hii kitu ni raha mwenye hela zake akajaribu ila usiende zile za vichoroni kwa watu waliovamia fani na wasio na ujuzi wowote.

Baada ya kumaliza zile sehemu za nyuma nilimwambia ageuke tuhamie sehemu za mbele. Mungu wangu kumbe mwanaume wa watu mawazo yake hayakuwepo hapo maana sehemu zake za siri zilikuwa zimesimama.Nikachukua lile taulo na kumfunika asije akasababisha na mimi nikaama kimawazo. Nikajipaka tena mafuta kwenye mikono yanu alafu nikachukua mkasi uliokuwepo hapo pembeni na kumgonga kwa nguvu magotini.Nia yangu iikuwa asikie maumivu ili mawazo yaamie kwenye maumivi hivyo yule jogoo aliyesimama tayari kwa kuwika arudishe kichwa chake bandani.Nikaanza kupitisha mikono yangu kwenye kifua chake na nikapanda juu kidogo na kufanya msisitizo kwenye mabega yake ya mbele na shingoni

Nikahamia kwenye sehemu za maziwa nikayachuachua na yenyewe ili yawe poa. Niliendelea hivyo huku nikihakikisha kila kiungo cha mwanaume huyo kinapata huduma. Badaye nilimwambia ainuke na kukaa kwenye kile kiti maalumu na nilimuuliza anajisikiaje? Yaani badala ya kunijibu swali langu yeye akanikonyeza yaani wanaume wengine bhana wewe acha tu. Yaani sijui ndo alishadata na mimi au ni mbwembwe tu baada ya kupewa huduma nzuri. Alafu huyu nahisi ndo ilikuwa ni mara yake ya kwanza nahisi alikuwa anasimuliwa tu habari zangu ndo akaja kujaribu. Na ndio maana hata nilivyomwambia afanyiwe na Waridi alikataa katu katu. Sikutaka kupoteza mda nilimuacha huko chumbani apumzike kidogo na mimi nikatoka na kwenda kwenye kile chumba kingine cha saloon.

Nikamkuta Waridi anapiga stori na mteja mwingine wa kike ambaye na yeye alitaka huduma hiyo ya massage. Mda ulikuwa umeenda sana lakini sikuwa na jinsi nikamwita Krish muhindi ambaye yeye alikuwa saloon ya kiume ambayo pia ni ya kwangu aje amfanyie huduma dada huyo.Ujue mimi nilikuwa na salooni mbili zilizofuatana moja ya kike na ingine ya kiume hivyo niliajiri watu wenye uzoefu na waliosomea mambo hayo.Siunajua tena Mark alinipa mtaji wa kutosha.

Krish alikuja kwa haraka kwa sababu yeye alishafunga ofisi hivyo ikabidi niingie ndani ili nimtoe yule mwanaume ambaye mimi nilikuwa nikimfanyia massage. Cha ajabu nilimkuta bado haja vaa hata nguo.Yaani hizi kazi zetu zilikuwa na changamoto nyingi sana.Ikabidi nimpe makavu live kuwa anipishe maana kulikuwa na mteja mwingine. Eti yule mwanaume akaniuliza hawezi kupata huduma ingine? Nilitamani nicheke lakini nilijikaza na kumuuliza sasa wewe si ulilipia laki ya full body massage sasa unataka huduma gani ingine.Akaniangalia na kuniambia si ni yale mambo ya kikubwa.

Nikamjibu kwa kifupi kuwa sisi hatutoi huduma hiyo. Ilimbidi avae nguo zake na kuondoka huku akilipia laki na nusu badala ya laki moja na aliacha namba zake za simu eti nimtafute baada ya kumaliza kazi. Yaani huyu baba ana bahati sana yaani angenikuta enzi zangu ningevikomba hivyo viela vyake vinavyomtia jeuri.

Yaani angemkuta Leah wa kipindi kile ningemchuna mpaka akome. Kwa bahati nzuri au mbaya siku hizi nimekuwa malaika tangia nikutane na Mark. Nakajisemea wacha tu nimvundikie Mark wangu ili siku akija akikute kimeiva na kuwa kitu piruuu kabisa. Siunajua tena kisipotumika mda mrefu kinajirudi na kujijenga utafikiri ndo kigoli.

Basi alitoka na kunipa nafasi ya kuandaa kile chumba na kuruhusu yule mteja na Krish waingie kupeana huduma. Walifanya yao na walipomaiza walitoka na mimi kufunga ofisi huku nikiamini kuwa Mark bado yupo mjini alikuwa ananitania tu. Nilijua Mark alikuwa ananirusha roho atakuwa hapa hapa mjini yupo mahali na marafiki zake wakiponda raha siunajua tena na yeye alivyokuwa akipenda starehe. Tuliondoka zetu na nilimpa nauli Waridi hivyo tukakubaliana kuonana kesho . Niliamua kwenda kwanza nyumbani ili nikaoge nile ndo nimtafute Mark.

Kama kawaida yangu nilipitia kwa muuza chipsi akanifungia chipsi kuku na nikaingia zangu ghetto. Kama kawaida muuza chipsi huyo hakuacha mautani yake eti ananipenda lakini anajua kuwa hawezi kunipata kwa sababu yeye nyota yake ni ya chipsi kupendwa na wanafunzi na mimi sio mwanafunzi hivyo hawezi kunipata kihurahisi. Unajua wanaume wamekuwa na mbinu nyingi sana unaweza kuona kuwa anafanya utani kumbe ndo mwenzio anamaanisha hivyo.Siunajua zile tena shemeji shemeji kulaaa huku anazima taa ukija kushituka unakuta tayari mambo yameshaharibika. Niliingia ndani nikaoga nikala kabisa huku nikiendelea kufungua zile zawadi zangu zilizobakia.

Kumbe alininulia mpaka nguo na viatu na mafuta mazuri na ile perfume ya kiss me ambayo huwa naipenda sana.Nilijikuta bila kutarajia nanyanyua simu na kumpigia na neno la kwanza nililomwambia ni LET ME LOVE YOU. Alicheka kwa sababu neno hilo alinambia mchana tukiwa pale saluni mara baada ya kukumbatiana kama vile wahindi baada ya kucheza zile nyimbo zao za kuchikuchi.Nikamuuliza yupo wapi lakini bado alijibu vile vile kuwa yeye yupo Dar.

Hapo nilkasirika maana usiku huo mimi nilikuwa na mizuka ya kuwa naye.

Nikamuuliza au huku Moshi ana mwanamke mwingine ambaye ndo amefikia?Bado aliendelea kujibu kwa kujiamini kuwa yeye yupo Dar na niache hisia zangu mbaya. Kwa hasira nilikata simu kuitupilia mbali, siunajua tena bila kudeka mapenzi hayanogi. Nilivyokata tu yeye akapiga sikupokea na nikaitupilia simu ile kitandani na nikaacha kabisa kufungua zile zawadi zake. Sijui kwa nini huyu mwanaume alizinyanyasa hivi hisia zangu. Haya ni mapenzi ganii ya kwenye simu wakati mwenzie mimi nilichoka kuvumilia.Ebu fikiria mwaka mzima mtu unamvumilia tu na kumtunzia wakati mimi kila siku napata vishawishi vya kutongozwa na wanaume wengi tena wenye hela zao.

Ujue ile kazi ya saluni hasa ile ya massage ilinisababishia niwe natongozwa sana na kuhongwa lakini bado niliamua kumtunzia Mark. Wakati mwingine nilijifariji kwa kale kamsemo kuwa mvumilivu hula mbivu lakini sikusahau kale ka msemo kuwa mvundika mbivu hula mbovu. Mark alipiga simu zaidi ya mara tatu lakini sikupokea kwa sababu aliniboa sana maana wewe huwezi toka Dar na kupanda ndege kuja Moshi eti kwa ajili tu ya kuniletea zawadi za happybirthday tu hiyo haikuniingia akili kwa kweli. Alivyoona nimegoma kupokea sms yake akatuma meseji iliyosema “LET ME LOVE YOU”(acha mimi nikupende). Eeeeh nilishangaa sana mbona hili neno alikuwa analipenda sana kwani lilikuwa na maana gani. Nikaamua kumjibu kwa kifupi kuwa ameniboa. Hapo hakujibu tena sms bali alienda kabisa hewani “am sorry baby” ndo lilikuwa ni neno lake la kwanza.Nikamwambia ajue mimi simuelewi kabisa na haya sijui ni mapenzi gani ya kihindi au kifilipino “baby am sorry alirudia tena na ndo neon lake kubwa alilokuwa akipenda kulitumia hasa mara baada ya kunivuruga. Yaani wewe ungekuwa una jua maana ya neno am sorry hata usingependa kulitumia kabisa nilimwambia Mark kwa sauti ya ukali.

Akaniuliza kwani lina maana gani? Am sorry maana yake unathibitisha wewe ni dhaifu na ndio maana unakosea kosea.Alicheka na kuniambia tena am sorry hapo ilibidi na mimi nicheke maana alijifanya haelewei kabisa. Alivyoona nimecheka akanambia basi atakuwa alitumii tena neno hilo ila anaomba yaishe.

Basi tukaanza kuongea mambo mengine siunajua tena biti na mikwara kwenye mapenzi ni muhimu la sivyo utaonekana huna wivu. Lakini ukweli utabaki pale pale huwezi kumpangia mwanaume ratiba zake au kumlinda. Kufanya hivyo ni sawa na kulinda bahari wewe unalinda bagamoyo mwenzako wanaogelea Zanzibar. Alinambia kuwa mwezi ujao atakuja kwa ajili yangu ili tuende Dar akanivishe pete. Yaani kusikia neno kuvalishwa pete nilinyanyua mkono wangu wa kushoto na kuuangalia vizuri kama kweli ulikuwa unastahili kuvalishwa pete.Hapo ikabidi nibadilishe na kuipotezea mada hiyo maana kuolewa sio jambo dogo.

Nikamuuliza mbona anapenda sana kutumia neno “LET ME LOVE YOU”.Akanambia analipenda tu na hakuna namna ingine acha anipende tu. Akanambia ameanza mikakaati ya kuandaa filamu ambayo itaitwa Let Me Love You ambayo pia anataka mimi nishiriki kama muhusika mkuu. Hapo nilifurahi kwa sababu moja ya vitu alivyoniahidi ni kuhakikisha kuwa ananiingiza kwenye tasnia hiyo ya filamu. Nikamuuliza kuwa hiyo ameshapata idea akanijibu kuwa hana idea yeyote zaidi ya jina hilo. Nikamwambia basi kama ni hivyo aache mimi nitunge stori ambayo itabeba maana ya jina hilo ambalo kwa kweli alipenda sana kulitumia.

Basi alikata simu na tukakubaliana mimi ndo nitunge stori hiyo. Kwani najua basi kutunga stori hata ya page moja. Hapo niliwaza sana lakini sikuapata picha hiyo stori iweje. Nilifikiria usiku wote huo lakini sikuwa na idea yeyote baadaaye niliona haina haja ya kujiumiza hizo ni kazi za watu waliopewa kipaji na mungu kutunga vitu. Hapo nikakumbuka kuwa kuna mwandishi mmoja ambaye stori zake huwa zinanigusa sana kwani huwa zinaelezea maisha halisi yanayotuzunguka stori hizo huwa nazifuatilia kwenye mitandao ya kijamii. Mwandishi huyo pia huwa anatoa ushauri wa mapenzi, uhusianao na saikolojia. Mimi huwa nampenda sana kwa sababu kuna kipindi aliwahi kunishauri sana kuhusu maisha ya mapenzi na hata ya kawaida pia. Mwandishi huyo alijulikana kwa jina la Eliado. Nilitaka kumpigia simu usiku huo lakini nikagundua kuwa mda ulikuwa umeenda sana hivyo nilala zangu na kupanga kuwa nitamtafuta kesho ili niweze kumshirikisha jambo hilo.

Nililala usingizi mzito sana siku hiyo kwa sababu nakumbuka nilikuwa nimechoka sana na sikuweza kushusha hata neti. Usiku nilishituka usingizini baada ya mbu kuning’aata na kunisumbua sana. Niliwachukia sana hao mbu kwa sababu walinikatisha ndoto yangu ambayo nilikuwa nikiota.Ndoto ilikuwa ikielezea jinsi harusi yangu na Mark itakavyokuwa. Ndoto ilikuwa tamu sana maana ilinipa taswira ya picha halisi ya maisha yangu ya mbeleni.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)